Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Prof. Mohamed Janabi amesema kila siku takriban Wagonjwa 150 wa Figo wanasafishwa Damu hospitalini hapo na 90% wamegundulika kuwa na Kisukari na Shinikizo la Damu
Amesema kama watu wasipochukua hatua za...
AFRIKA KUSINI: Mahakama ya Juu imetoa uamuzi unaomuondoa Jacob Zuma, Rais wa zamani wa taifa hilo katika orodha ya Wagombea katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Mei 29, 2024
Kwa mujibu wa nyaraka za Mahakama, imeelezwa kuwa Zuma amepoteza sifa za kushiriki Uchaguzi kutokana na Kifungo cha...
DODOMA: Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imewasilisha Bungeni Bajeti ya Tsh. 3,326,230,419,000 kwaajili ya matumizi ya Wizara, Vikosi vya Ulinzi kutoka Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mwaka 2024/25.
Kwa mujibu wa Hotuba ya Bajeti iliyowasilishwa na Waziri...
Kama leo imetokea umepata nafasi ya kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, ukangalia hali ya masuala ya Kisheria nchini pamoja na mfumo wa utoaji Haki, utaanza na mabadiliko gani ili kuongeza Haki na Uwajibikaji nchini?
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena L. Tax amesema Migogoro ya ardhi inayohusisha maeneo ya Jeshi inapaswa kutatuliwa kwa mashauriano kwa kufuata Sheria zilizopo na si Kisiasa
Akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2024/25 amesema, maeneo ya Jeshi ni maalum kwa...
DR-CONGO: Serikali imesema jaribio la Mapinduzi lililozimwa mwishoni mwa Wiki iliyopita liliongozwa na Christian Malanga, Mwanasiasa mwenye uraia wa Congo lakini makazi yake yapo Nchini Marekani akiwa na kundi la Wanajeshi walioasi.
Msemaji wa Jeshi la DRC amesema takriban Watu 50 akiwemo Mtoto...
Mikoa ya Arusha na Manyara imetajwa kuwa na Kiwango kikubwa cha Ukeketaji nchini Tanzania ikiwa na Wastani wa 43% ya Vitendo hivyo ikifuatiwa na Mikoa ya Mara 28%, Singida 20% na Tanga 19%
Mikoa mingine Dodoma (18%), Iringa (12%), Morogoro (10%), Kilimanjaro (9%), Njombe (7%) Pwani (5%) na...
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imesema hadi kufikia Aprili 2024, kulikuwa na Vituo 3,862 Vilivyosajiliwa kwa Kulelea Watoto 397,935 (Wakiume 175,517 & Wakike 222,418) na Vituo 206 vya Kijamii vyenye Watoto 11,675
Idadi hiyo ni ongezeko la Watoto 225,003 sawa na...
Siku ya Shinikizo la Damu Duniani huadhimishwa Mei 17 ya kila mwaka ikiwa na lengo la kuongeza ufahamu utakaosaidia Kuzuia, Kugundua hali na Matibabu ya Shinikizo la Damu.
Shinikizo la Damu huathiri mtu mzima 1 kati ya 3 duniani kote huku likisababisha matatzo mengine kama Kiharusi, Mshtuko wa...
Nadhani kila Mkoa nchini Tanzania una alama yake au kitu fulani maarufu sana kinachutambulisha Mkoa bila hata kuambiwa ukiona unajua tu hii kitu ya mkoa fulani.
Twende kazi wadau, nini kinautambulisha mkoa wako?
Kwa mujibu wa taarifa ya Madeni iliyopo katika tovuti ya Shirika la Fedha Duniani (IMF), imeonesha takriban nchi 47 kutoka Afrika zimeendelea kuwa na Madeni katika taasisi hiyo ya Fedha ambapo hadi hadi kufikia Mei 16, 2024 Nchi 10 zilikuwa na Deni la takriban Tsh. Trilioni 72.3.
Aidha, Nchi...
“Ukikuta kijana ameingia ndani kwa kuvunja dirisha ujue kuna mambo mawili ameyadhamiria. Jambo la kwanza amedhamiria kuiba na jambo la pili amedhamiria kuua na jambo la tatu amekubali kuuawa. Naomba nisisitize, jambo la tatu amekubali kuuawa, naomba nirudie, jambo la tatu amekubali kuuawa...
Klabu zinazoshiriki Ligi Kuu zimeombwa kuunga mkono hoja iliyowasilishwa na Klabu ya Wolverhampton Wanderers inayopendekeza azimio la kupiga Kura ya kufuta Matumizi ya 'VAR' kuanzia Msimu ujao
Pendekezo hilo ambalo linadaiwa kupingwa na Bodi ya Ligi Kuu linatarajiwa kusikilizwa Juni 6, 2024...
Kila mwaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) huwa inatoa Ripoti ya Taarifa ya Utendaji Kazi ambayo hukabidhiwa kwa Rais kwaajili ya hatua mbalimbali. Lakini Ripoti hiyo haiwekwi wazi kwa Umma kutokana na kubanwa na Sheria ya Kupambana na Rushwa ambayo haijaweka takwa hilo
Je...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.