Ni sahihi Rais kutajwa kwenye kila kitu?

😂 😂 😂 kuna jamaa mkewe kazaa mtoto wa kiume kaanza kwa kumshukuru mama Samia kwa uongozi bora
Screenshot_20240329_090857_WhatsApp.jpg
 
Hii ilikuwepo hata enzi za Mwalimu Nyerere ikaja kupotea enzi za "Rukhsa" na Ben, Kikwete mwenyewe alikuwa hamaindi sana kusifiwa sifiwa.

Nadhani ni Nyerere Mwendazake na huyu Bibie.
Huyu bibie ni too much
 
Kwanza namshukuru Rais Dr. SSH kwa kuruhusu JF iwepo.

Huu uchawa wa kusifia Rais kiboya umeanza enzi za Jiwe sasa ni muendelezo tu. Yeye alihodhi mamlaka yote na kudissolve mamlaka zingine zote. Rais wa sasa dkt. SSH nae anapenda hizi sifa hafanyi lolote kutokomeza huu uchawa.
 
Kama uwezo wako ni mdogo na utendaji wako ni mbovu unadhani utafanya nini ili kuendelea kubaki kwenye nafasi yako kama sio kumsifia Rais hata mkeo akikupikia chakula kitamu?
 
Huko bungeni Sasa.
Shule imejenga matundu mawili ya vyoo kwa gharama ya milioni Mia tano lkn utasikia MTU akisema, tunamshukuru Fulani kwa kutuletea hela na sisi si Haba tumefanya ubadhirifu wa kutosha.
Kidumu chama Cha majizi.
 
Bungeni ndio kisanga
 
Habari wanajukwaa.

Kumeibuka mtindo kila mtu anapopata nafasi ya kuongea kumsifia Rais hata kwa yale ambayo Rais hausiki wala hayajui.

Mfano Mrisho Ngasa alipoalikwa Kwenda Ivory Coast kama Legendary kipindi cha AFCON alipohojiwa alianza kumshukuru Rais Samia.

Binafsi yangu naona hii ni aina mpya ya Uchawa kwa Rais.

Mtoto wa Lowasa alifikia kusema bila ya Samia yawezekana Lowasa angekufa mapema, hii ni kama kumpa Samia mamlaka ya kimungu ilihali ni binadamu.

Swali langu kwenye wana Jamii Forum ni sawa kwa Rais kushukuriwa, kutajwa na kutukuzwa kwenye kila jambo?
Inategemea uwezo wa kiakili alionao huyo Rais, kama ni rais mpumbavu na mjinga mjinga anaweza akawa sehemu ya kutengeneza mazingira ya kutaka kusifiwa na kila mtu au kutajwa tajwa kila mahali kila mara.
 
Marais husifiwa ila kwa mama imekuwa too much
 
Back
Top Bottom