Tabutupu
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 13,113
- 18,329
Kume kuwa na utaratibu wa ajabu kwa awamu hii kutaka kuita kila mradi jina la Rais, na mbaya zaidi hakuna sheria wala utaratibu wa kufuata.
Sasa hivi nasikia uwanja wa Arusha wanataka uitwe Samia.
Miaka ya nyuma ilikuwa ni mwiko kuita kitu chochote kwa jina la Rais aliyeko madarakani, ilikua ni heshima anayo pewa mtu akistaafu.
Baadae tutakuja kuchabganyana tuu maana viwanja vya ndege vitaitwa samia, viwanja vya mpira samia, malls samia, miradi ya NHC samia.
Tatizo sio Rais tatizo ku a mwanya upo sehemu watu wanautumia kujiweka karibu na Rais kwa kujipendekeza.
Ni vyema kama taifa tuwe na sheria na taratibu za kuita maeneo ambayo yanatoa huduma za jamii.
Kuna ukakasi mkubwa sana katika hili toka awamu ya 5.
Kuna nchi walifika wakati wakafuta majina yote ya viongozi kwenye sehemu za kutolea huduma.
Na hii ni kutokana na mitazamo tofauti waliyo nayo wananchi juu ya hao viongozi.
Napendekeza itungwe sheria na bunge lihusishwe.