Ni sahihi Rais kutajwa kwenye kila kitu?

Ndata

JF-Expert Member
Mar 2, 2017
226
321
Habari wanajukwaa.

Kumeibuka mtindo kila mtu anapopata nafasi ya kuongea kumsifia Rais hata kwa yale ambayo Rais hausiki wala hayajui.

Mfano Mrisho Ngasa alipoalikwa Kwenda Ivory Coast kama Legendary kipindi cha AFCON alipohojiwa alianza kumshukuru Rais Samia.

Binafsi yangu naona hii ni aina mpya ya Uchawa kwa Rais.

Mtoto wa Lowasa alifikia kusema bila ya Samia yawezekana Lowasa angekufa mapema, hii ni kama kumpa Samia mamlaka ya kimungu ilihali ni binadamu.

Swali langu kwenye wana Jamii Forum ni sawa kwa Rais kushukuriwa, kutajwa na kutukuzwa kwenye kila jambo?
 
Na Mrisho Ngassa naye yumo ??!!
Duh ๐Ÿ™„ ! ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ™
 
Katiba yetu unampa uwezo wa Kimungu.
Lakini Katiba hii ipo tangu mwaka 1977

Hii maneno ilikuwa haiko kama hivi

Hii imeanza miaka ya hivi karibuni.

Kwanini imekuwa hivyo hata mimi sielewi mantiki yake ni nini?

Lakini nadhani wenyewe wanajua ni kwanini wanafanya hivyo ila wengine huwa hawajui ila wanafuata mkumbo tu
 
Lakini Katiba hii ipo tangu mwaka 1977 !
Hii maneno ilikuwa haiko kama hivi !
Hii imeanza miaka ya hivi karibuni. !
Kwanini imekuwa hivyo hata mimi sielewi mantiki yake ni nini !!
Lakini nadhani wenyewe wanajua ni kwanini wanafanya hivyo ila wengine huwa hawajui ila wanafuata mkumbo tu !!
Hii ilikuwepo hata enzi za Mwalimu Nyerere ikaja kupotea enzi za "Rukhsa" na Ben, Kikwete mwenyewe alikuwa hamaindi sana kusifiwa sifiwa.

Nadhani ni Nyerere Mwendazake na huyu Bibie.
 
๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ

IMG-20240329-WA0147.jpg
 
Wengi wanaofanya hivyo ni wale wanaojikomba ili waendelee kubaki kwenye madaraka au waonekane ili wapate uteuzi na kundi la pili ni wale wenye nidhamu ya woga wakidhani wasiposema hivyo wataonekana hawana adabu ama hawana shukrani.
Hawa wote ni wagonjwa wa akili wanahitaji tiba.
 
Wengi wanaofanya hivyo ni wale wanaojikomba ili waendelee kubaki kwenye madaraka au waonekane ili wapate uteuzi na kundi la pili ni wale wenye nidhamu ya woga wakidhani wasiposema hivyo wataonekana hawana adabu ama hawana shukrani.
Hawa wote ni wagonjwa wa akili wanahitaji tiba.
Nakubaliana na wewe
 
Back
Top Bottom