Kocha wa Simba Benchikha awasilisha barua rasmi ya kuomba kuondoka mwishoni mwa msimu

Sijui nani alimshauri kwenda Simba, kashusha CV kwa kiwango cha kutisha!
Kabla ya kuangalia pesa ni vyema kujiridhisha kwanza mazingira ya kazi unayoenda kuifanya.
Kashusha CV kivipi
Kwani hajawahi kushika nafasi ya 2 au 3 kwenye ligi?
Hajawahi kuishia robo fainali CL?
 
Simba ni ya benchika, mpk itakapo chukua ubingwa wa Africa msimu ujao ndo mtakubali, msichokijua ni kuwa benchika amekuja simba kimkakati na asingeweza kuchukua kombe coz simba ilikua mbovu, ngojeni dirisha la usajili lifunguliwe ndo muone.
Hilo dirisha lilipofunguliwa alisajili kina Pa Omary Jobe
 
Baada ya Kuona anafundisha timu yenye wachezaji wenye vichwa vigumu kumuelewa atimaye kocha la makombe limeamua litumie njia mbadala kujiondokea baada ya kudai linaondoka kutokana na matatizo ya KIFAMILIA🤣🤣
Ikumbukwe ni majuzi tu baada ya kutandikwa na yanga alikiri mwenyewe kuwa tokea aanze kudundisha soka ajawai kukutana na timu yenye wachezaji wenye vichwa vigumu kumuelewa Kama wa Simba, Sasa kaamua kuchomoka kiaina kaona CV inaporomoshwa kwa Kasi ya kimondo!
ukiachana na kibu kama lile bichwa la saidoo linaelewa kitu kweli!!!
 
Simba ni ya benchika, mpk itakapo chukua ubingwa wa Africa msimu ujao ndo mtakubali, msichokijua ni kuwa benchika amekuja simba kimkakati na asingeweza kuchukua kombe coz simba ilikua mbovu, ngojeni dirisha la usajili lifunguliwe ndo muone.
Mbona unalazimisha mtu abaki kilazima? Mtu kaishaandika barua ya kuomba kuondoka bado unalazimisha kuwa Simba ni ya Benchikha
 
Sijui nani alimshauri kwenda Simba, kashusha CV kwa kiwango cha kutisha!
Kabla ya kuangalia pesa ni vyema kujiridhisha kwanza mazingira ya kazi unayoenda kuifanya.
CV yake ime base kwenye mashindano ya confederation cup ambayo Simba wanayananga kuwa mashindano ya losers. Mara ya mwisho kuchukua kombe la ligi kuu ni mwaka 2007.
Sio kocha wa mashindano ya mbio ndefu huyu na ndio maana kapata dodo la super cup mbili ila hana CV yeyote kwenye klabu bingwa wala ligi kuu. Sijui hizo sifa za CV kubwa anapewaga kwa kipi zaidi
 
Simba kwa sasa uongozi ndio tatizo linapoanzia, wale kina Try Again ndio wamefeli hawa wengine huku chini wanafelishwa na mipango mibovu ya uongozi, kila siku kubadilisha makocha mpaka lini?
 
Mpaka Simba ije kukaa sawa kwa kubadilisha makocha Kila mara Kama vile unabadilisha boxer za kuvaa yanga watakuwa washatwaa ndoo mara 10 mfululizo, wanadhani kubadili makocha Kila msimu ndio suluhisho la matatizo yao!
 
Ni official news ndio kwasababu waandishi mbalimbali wameripoti hii taarifa. Kwasasa subiria mechi za ligi kuu ziishe usikie taarifa kwa umma kutoka kwa klabu yako ya Simba.
Haya endeleeni kujifariji
 
Simba wamemfedhehesha sana kocha huyu ambaye nyota yake ilikuwa inapanda. Sasa hivi hapo alipo, ana mfadhaiko mkubwa sana wa moyo anaomba msimu uishe haraka ajiondokee akaanze upya Simba imapaka matope mengi sana kwenye rekodi yake.


Ndani ya kipindi cha miaka minne January 2021 Simba imeshafukuza makocha wangapi na mafanikio yake ni yapi?
 
Back
Top Bottom