Kumezuka mtindo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya mikutano ya hadhara kwenye stendi za mikoa za mabasi. Leo katibu mkuu wa CCM ndugu Emmanuel Nchimbi ameongoza mkutano wa hadhara katika stendi ya mabasi mjini Babati mkoani Manyara. Jumatano tarehe 5 CCM wamepanga kufanya mkutano wa hadhara...
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amebaini upigaji na madudu yanayofanywa katika vituo mbalimbali vya mabasi hapa nchini.
Kupitia Ripoti Kuu ya Ukaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 iliyotoka hivi karibuni, pia amesema kuna uendeshaji...
Habarini Wanajamvi wenzangu
Gharama kubwa watanzania wanazolipa kila uchwao juu ya ajali za barabarani inaleta maswali lukuki. Pamoja na jitihafa za Jeshi la Polisi, bado kuna haja ya kama Taifa tukubali kufanya mageuzi makubwa katika matumizi ya teknolojia katika jeshi hili. Takwimu zilizopo...
Kutokana na ukuaji wa mjiji na majiji, wafanyakazi wengi wanaishi (kujenga makazi au kupanga) maeneo ya mbali kidogo (zaidi ya kilomita kumi) kutoka maeneo wanayofanyia kazi hali inayowalazimu uhitaji wa usafiri wa kwenda kazini na kurudi nyumbani. Kwa mfano katika jiji la Mwanza, wafanyakazi...
Huu mradi una maswali mengi ambayo binafsi ninakosa majibu. Tunajua na kutambua kwamba kuna gharama za uendeshaji wa mradi, ikiwemo kulipa mishahara wafanyakazi,mafuta, matengenezo n.k Lakini biashara yoyote ambayo ina wateja wengi kiasi kile, Nilitegemea mpaka sasa biashara hii ingekuwa imekua...
KITUO CHA MABASI MWENGE
Kipo chini ya manispaa ya Kinondoni
Ujenzi ulianza 1/7/2019 mpaka 30/11/2023
Ufadhili:fedha za ndani
Kitahudumuia : Daladala 100 na Bajaji 60 kwa wakati mmoja.
Gharama ya ujenzi : Billioni 15
Hongera sana Manispaa ya Kinondoni ,mmeonesha uthubutu.
STENDI YA MABASI YA...
Jiji la Mbeya, kama miji mingi inayoendelea nchini Tanzania, linakabiliwa na changamoto kubwa za usafiri. Bajaji, ambazo ni maarufu kwa kuwa nafuu na rahisi kupenya katika mitaa midogo, zimekuwa sehemu muhimu ya mfumo wa usafiri wa jiji hili. Hata hivyo, kuongezeka kwa idadi ya bajaji...
Mabasi mengi ya kwenda Mikoani huwa yanafungulia nyimbo za Injili kwanzia mwanzo hata mpaka mwisho wa safari.
Kitendo cha kufungulia nyimbo za Injili sio jambo baya lakini mara nyingi nyimbo hizo zinakuwa zimeegemea dini moja na kubagua nyingine kitendo ambacho kinachochea udini.
Vilevile...
Safari za mabasi za usiku zilikuwepo kitambo,Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani akazifutilia mbali.
Alijua akili zetu watanzania,madereva wetu hawana uwezo wa kuendesha usiku,kichwa kimejaa bange,pombe,madeni,michepuko huku unabeba roho za watu.
Watatumaliza
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Carolyne Nombo amesema wizara walitoa mwongozo wa mabasi ya shule na kwamba waliviachia vyombo vingine vya Serikali kuendelea na ukaguzi wa madereva hao kama wanavyofanya kwa madereva wengine na hawakuwahi kuwa na mfumo.
“Baada ya...
Kifo ni kifo lakini vifo vya wahanga wa ajali hii, looh! Mtu usemeje?
Watu wazima waliokuwa kwenye gari lile waliotoka salama, wanacho nini cha kumwambia nani leo?
"Kwa hakika mtu mzima aliyekufa na watoto wale akipambana kuwakoa alifanya yote yaliyokuwa sahihi."
Hawa watu ilikuwa muhimu...
Hizi ajali za barabarani za mfululizo za mabasi zinazomaliza maisha ya watu na kuwafanya maelfu kuwa walemavu ni kama zimekuwa jambo la kawaida sasa na kuzoelekana.
Inasikitisha sana kuona Waafrika hatuyapi maisha thamini na hadhi inayostahili. Ajali mfululizo za mabasi za aina hii zinazotokea...
Mambo vipi wakuu?
Nakumbuka kuna kipindi fulani miaka ya zamani kidogo serikali ilizuia buses zilizoungwa chassis zisioperate maana sio salama na ni kweli sio salama kabisa, ila sikuhizi kuna mtindo wa kuunga chassis na kuongeza tag axle kwenye bus kibao tu lakin kama imepotezewa vile...
Nakumbuka kulikuwa na utaratibu barabarani kwenye mabasi makubwa ya masafa marefu yanayotoka mkoa mmoja hadi mwingine, askari wanaingia kukagua mabasi na moja ya mambo waliyokuwa wanaangalia ni kama basi limezidisha idadi ya abiria.
Kutokana na hulka ya Watanzania tulivyo, tulikuwa tunakaushia...
Nimejiuliza hivi Wakandarasi wanaojenga vituo vya mabasi huwa wanachaguliwa kwa kuangalia vigezo gani?
Nasema hivyo kwa kuwa vituo vingi huwa vizuri vikiwa vipya tu baada ya muda changamoto mbalimbali zinaanza kujitokeza.
Vingine huwa vinakuwa vibovu au havikidhi vigezo kuanzia mwanzo kabisa...
Leo kupitia magazeti nimekutana na habari isemayo walipa kodi waongezewe kodi kwenye laini za simu, kama alivyopendekeza mheshimiwa asiyelipa kodi kwenye mshahara wake.
Mheshimiwa huyu ni mmiliki wa mabasi ya Shabbiby wa Gairo Morogoro japo anatambulika zaidi Dodoma huenda kutokana na Gairo...
Madereva wa mabasi ya mikoani pamoja na Costa hasa zile zinazofanya safari zake Moshi - Arusha wametishia kugoma kwa kile kinachodaiwa ni miundombinu mibovu iliyopo Stendi ya Bomang'ombe hasa barabara.
Barabara ya eneo hili lililopo Hai Wilayani Kilimanjaro limetawaliwa na mashimo mengi na...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.