covid 19
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 5,010
- 11,025
Fuatilia yanayojiri wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya CAG na TAKUKURU kwa mwaka 2022/23, Ikulu ya Chamwino, Dodoma, leo Machi 28, 2024.
View: https://www.youtube.com/watch?v=6yQwHaO3rEA
MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA TAKUKURU CP SALUM RASHID HAMDUNI
View attachment 2946700
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), CP Salum Rashid Hamduni anawasilisha Taarifa ya Utendaji kazi wa TAKUKURU kwa Mwaka 2022/2023, Ikulu Mkoani Dodoma, leo Machi 28, 2024.
Amesema walifanya tathmini ya Miradi 1,800, walibaini Miradi 171 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 143.3 ilibainika kuwa na utekelezaji hafifu na hivyo kuanzisha uchunguzi.
Akizungumzia tatizo la Ujenzi wa Vituo vya Mafuta katikati ya Makazi ya Watu linaongezeka, CP Salum Rashid Hamduni, amesema walifanya Uchambuzi kuhusu Mfumo wa Uzingatiaji wa taratibu za Ujenzi wa Vituo vya Mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambapo Vituo 38 vilihusika.
Asilimia 79 ya Vituo vilivyochambuliwa vilizingatia Sheria kwa kuwa na Vibali vya Ujenzi kutoka Halmashauri ambapo Ujenzi umefanyika, Asilimia 21 ya Vituo havikuwa na leseni wakati zoezi la Ufuatiliaji linafanyika.
Pia, walibaini Ongezeko la maombi ya Ubadilishwaji wa Matumizi ya Ardhi kutoka Matumizi ya awali na kuwa Matumizi ya Vituo vya Mafuta, pamoja na tatizo la Ujenzi wa Vituo vya Mafuta katikati ya Makazi ya Watu linaongezeka na kuleta Changamoto ya Usalama wa Watu waishio karibu.
Huyu CAG nae ameenda kumshukuru mama anaupiga mwingi.