CAG Kichere: Licha ya kupewa Ruzuku ya Tsh. Bilioni 31.55, ATCL imepata hasara ya Tsh. Bilioni 56.64, ongezeko la 61% kutoka hasara ya Mwaka 2021/22

Kuna utawala wa sheria. Siyo kila kitu atafanya Rais Samia. Kwanza anachotoa CAG ni hoja za kiukaguzi wala siyo ropoti ya wizi. Hicho hamkijui. Mnataka kila hoja ya ukaguzi iende jela.

Hao wenye hoja za ukaguzi wanapaswa kujibu. Baada ya hapo Kamati ya hesabu za bunge itazifuatilia na kisha.

Zile ambazo hawataridhika ndiyo zinakwenda TAKUKURU. Na hao TAKUKURU wanakusanya ushahidi wao na kisha wanapita kwa DPP kwa ajili ya kupeleka Mahakamani.

CAG query isn't fraud but a mere symptom
Na ikifika kwa dpp ndiyo kwishney,dpp anapigiwa tu simu moja kesi inatupiliwa mbali,sioni faida ya dpp, naye ni hasara kubwa tu kwa taifa.
 
Zambia wapinzani wameingia ikulu.
Senagal kijana mdogo wa upinzani waliyekua wamemfunga jela anakaa ikulu.
Ipo siku watu watachoka na hii Hali ya CCM kushindwa kusimamia Mali ya wanànchi.
 
Bora huyu anapokea ripoti na tunajuwa ubovu na ufisadi wote. Kuliko DIKTETA Magufuli yeye aliposomewa ripoti ya upotevu wa Tsh 1.5 Trillion akamfukuza kazi CAG Prof Assad.

Bahati mbaya Bunge ndilo lenye kuchukua hatua. Ila Bunge lenye UTAAHIRA aliloliacha Magufuli unategemea lifanye nini? Bunge lina wabunge 99.999% wa CCM.

Simtetei Samia kwa kutochukua hatua kwenye ropoti ya mwaka 2021/22 kama tulivyotarajia. Nchi hii inaendeshwa kwa Katiba na utawala wa Sheria. Rais hawezi kusomewa ripoti leo halafu kesho aseme kamata fulani na fulani peleka Mahakamani. Tutakuwa tuarudia UHAYAWANI uleule wa Magufuli aliyejaza watuhumiwa magereza lakini hakuna hata kesi moja aliweza kuimaliza hadi anakufa.

Upo utaratibu nankuna vyombo vya kufanya hayo mambo. Na mwenye majukumu makubwa ni Bunge.

Katiba inaruhusu Wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kama maagizo ya CAG hayatekelezwi. Kura zikipigwa na wakashinda wanaosema hawana imani basi Rais anavunja cabinet.
Ni USA au bongoland unasema mkuu?
 
Wewe bora dingi wako angevaa condom kipind anamnyadua maza wako kuliko kutuletea kubwa jinga kichwa kubwa akili ndogo
Kwanini usingemleta mama yako sasa kwa dingi wangu atombwe bila kondom?
 
Na ikifika kwa dpp ndiyo kwishney,dpp anapigiwa tu simu moja kesi inatupiliwa mbali,sioni faida ya dpp, naye ni hasara kubwa tu kwa taifa.
Unaweza ukaweka kesi japo 3 za ufisadi ambazo DPP alipigiwa simu? Na nani alimpigia?
 
Bora huyu anapokea ripoti na tunajuwa ubovu na ufisadi wote. Kuliko DIKTETA Magufuli yeye aliposomewa ripoti ya upotevu wa Tsh 1.5 Trillion akamfukuza kazi CAG Prof Assad.

Bahati mbaya Bunge ndilo lenye kuchukua hatua. Ila Bunge lenye UTAAHIRA aliloliacha Magufuli unategemea lifanye nini? Bunge lina wabunge 99.999% wa CCM.

Simtetei Samia kwa kutochukua hatua kwenye ropoti ya mwaka 2021/22 kama tulivyotarajia. Nchi hii inaendeshwa kwa Katiba na utawala wa Sheria. Rais hawezi kusomewa ripoti leo halafu kesho aseme kamata fulani na fulani peleka Mahakamani. Tutakuwa tuarudia UHAYAWANI uleule wa Magufuli aliyejaza watuhumiwa magereza lakini hakuna hata kesi moja aliweza kuimaliza hadi anakufa.

Upo utaratibu nankuna vyombo vya kufanya hayo mambo. Na mwenye majukumu makubwa ni Bunge.

Katiba inaruhusu Wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kama maagizo ya CAG hayatekelezwi. Kura zikipigwa na wakashinda wanaosema hawana imani basi Rais anavunja cabinet.
Ubwa
 
Fuatilia yanayojiri wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya CAG na TAKUKURU kwa mwaka 2022/23, Ikulu ya Chamwino, Dodoma, leo Machi 28, 2024.


View: https://www.youtube.com/watch?v=6yQwHaO3rEA

MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA TAKUKURU CP SALUM RASHID HAMDUNI

View attachment 2946700

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), CP Salum Rashid Hamduni anawasilisha Taarifa ya Utendaji kazi wa TAKUKURU kwa Mwaka 2022/2023, Ikulu Mkoani Dodoma, leo Machi 28, 2024.

Amesema walifanya tathmini ya Miradi 1,800, walibaini Miradi 171 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 143.3 ilibainika kuwa na utekelezaji hafifu na hivyo kuanzisha uchunguzi.



Akizungumzia tatizo la Ujenzi wa Vituo vya Mafuta katikati ya Makazi ya Watu linaongezeka, CP Salum Rashid Hamduni, amesema walifanya Uchambuzi kuhusu Mfumo wa Uzingatiaji wa taratibu za Ujenzi wa Vituo vya Mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambapo Vituo 38 vilihusika.

Asilimia 79 ya Vituo vilivyochambuliwa vilizingatia Sheria kwa kuwa na Vibali vya Ujenzi kutoka Halmashauri ambapo Ujenzi umefanyika, Asilimia 21 ya Vituo havikuwa na leseni wakati zoezi la Ufuatiliaji linafanyika.

Pia, walibaini Ongezeko la maombi ya Ubadilishwaji wa Matumizi ya Ardhi kutoka Matumizi ya awali na kuwa Matumizi ya Vituo vya Mafuta, pamoja na tatizo la Ujenzi wa Vituo vya Mafuta katikati ya Makazi ya Watu linaongezeka na kuleta Changamoto ya Usalama wa Watu waishio karibu.

MDHIBITI NA MKAGUZI MKUUU WA HESABU ZA SERIKALI, CHARLES KICHERE
Ukaguzi umebaini MSD ilitoa zabuni ya ununuzi wa vifaa vya maabara ambavyo ni vipimo vya COVID 19 kwa kampuni ambayo haikuwa mtengenezaji wa vifaa hivyo kinyume na makatwa ya zabuni, pia ilinunua vifaa hivyo bila kufuata ushauri, baada ya kufika kwa vifaa hivyo wataalamu walibaini havifai kwa matumizi yetu na tayari MSD ilikuwa imelipa fedha zote.

Mashirika ya Umma yanayojiendesha kibiashara yamepata hasara. Mwaka 2022/23, ATCL imepata hasara ya Tsh. Bilioni 56.64, sawa na ongezeko la 61% kutoka hasara ya Mwaka 2021/22 iliyokuwa Tsh. Bilioni 35.24. Ikumbukwe kuwa Shirika hili lilipokea ruzuku ya Tsh. Bilioni 31.55 kutoka Serikalini.

Shirika la reli limepata hasara ya Tsh. Bilioni 100.70 licha ya kupewa ruzuku ya Tsh. Bilioni 32.81 kutoka Serikalini.

TANOIL imepata hasara ya Tsh. Bilioni 76.56, ongezeko la Bilioni 68.72 kutoka hasara ya mwaka 2021/22.

Shirika la Posta limepata hasara ya Tsh. Bilioni 1.34.

NHIF umeendelea kupata hasa kwa mwaka wa 5 mfululizo ambapo mwaka 2022/23 umepata hasara ya Tsh. Bilioni 156.77. Hata hivyo, NHIF imeikopesha Serikali Bilioni 208 ambazo hazijalipwa hadi sasa.


View attachment 2947166
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2022/23 kutoka kwa Charles Kichere Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Machi, 2024.
View attachment 2947196
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Utendaji Kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa Mwaka 2022/2023 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo CP. Salum Hamduni Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 28 Machi, 2024.​

Kuna Jambo watu hawa taki kusema, kuna Ndege ililetwa Kwa aijili ya kufanya biashara , lakini sasa hivi inafanya safari za sirikali au Kwa maelekezo ya sirikali , matokeo yake hakuna mrejesho wa uwekezaji uliofanyika zaidi ya gharama juu ya gharama.
 
Lazima litaenselea kupata hasara ya mabilioni kila mwaka.

Mheshimwa akitaka kusafiri na mojawapo ya ndege za abiria anaichukua, abiria wanaahirishiwa safari unategemea Shirika lipate faida!

Unanunua nfege kubwa ya abiria unasafirisha abiria nusu ama chini ya hiyo idafi kwenda mataifa ya nje unategemea shirika lipate faida!

Inanunua ndege kubwa ya mizigo wakati mizigo ya kudafirisha nje ya nchi kwa ndege ni midogo unategemea shirika lipate faida!
 
Hizo pesa tunazopoteza kwenye ndege zingeweza kufanya ishu zenye faida sana kwa nchi. Kama kujenga miradi ya umwagiliaji na kuajiri maelfu ya vijana. Hii miradi ya kufanya ili kujionyesha imeziumiza nchi za Kiafrika toka zinapata Uhuru.
 
Haya mambo haya ni kama kuna kadalili cha kwenda kubinafsisha embu ngoja tuone. Hivi ni mashirika mangapi ya ndege duniani yamepata faida mwaka huu.
 
Ngoja watu waendelee kuiba mpaka ndege zote zisimame na shirika liwe na madeni yasiyolipika ndiyo tutaanza kutafuta mwendeshaji shirika anaeweza.
 
Hatuitaji ubora, tunahitaji uwajibikaji


Nasikia waafrica mnalaana ; wakati wa nuhu mlimchungulia baba yenu akiwa uchi, kisha akawalaani, nasikia ile laana inawala hadi leo !

Eti ni kweli ?
Ni kweli
Angalia muendelezo hata humu jf
Ni CHAPUTA na Mipalange.....na mambo ya hivyo.....
 
naona report iandaliwe na wakuu wa mikoa kwa kushirikiana na ras na maded ili kupunguza gharama ya uendeshaji. report ya mwaka uliopta iliichafua sana chama kwenye upigaji wa halmashauri na ilitokea hadi haja ya kukaa na kuangalia namna gani isijirudie. ikumbukwe mwenyekiti anaelekea kwenye maigzo mengne ya uchaguzi hvyo hataki sifa mbaya sijui ameshndwa kusimamia serikali n.k. hvyo halmashauri zitasemwa vizur haijarish nin kimetokea hadi pale maigzo yatakapoisha. ripot hii inaenda kusifiwa bungeni kama sehem ya usimamizi imara na kuvunja rekodi duniani. safari hii tutajua hadi ripot za eac countries na nchi kubwa kubwa duniani namna tulivyowapita kwa nidhamu ya matumizi ya hela.
 
NHIF imekuwa inashindwa kuhudumia wateja wake kutokana na Ufisadi, serikali kukopa hovyo, kukopesha hovyo na wizi wa viongozi wake na sio michango ya wateja wake kuwa kdg!
 
Back
Top Bottom