CAG Kichere: Licha ya kupewa Ruzuku ya Tsh. Bilioni 31.55, ATCL imepata hasara ya Tsh. Bilioni 56.64, ongezeko la 61% kutoka hasara ya Mwaka 2021/22

Yaani haya mambo ungeweza kuweka video clip ya kilichotokea mwaka jana na mwaka huu itakuwa yaleyale....; Hakuna Jipya Wizi Mkubwa , Brah.., Brah.., Brah za hapa na Pale baada ya hapo Business as Usual..,

To be repeated Next Year...
 
Sasa matokeo ya uwasilishwaji huo niyapi? Naona kama vile wanakamilisha tu utaratibu lakini wizi upo palepale kila mwaka.
Na mimi nimejiuliza hivyo hivyo.

Kwa jinsi wasivyochukua hatua zozote baada ya hiyo ripoti kusomwa ni bora isifanywe kama vile ni tukio muhimu.
Watoe tu hiyo ripoti kwenye gazeti la serikali, anaetaka kusoma jinsi tunavyoibiwa asome asietaka aache.

Huu unaofanywa ni upuuzi wa kusomewa wizi wa wenye nyadhifa bila hatua zozote kuchukuliwa. Hii imekuwa kama ripoti ya wezi kuringishia wizi wao.
 
Yaani haya mambo ungeweza kuweka video clip ya kilichotokea mwaka jana na mwaka huu itakuwa yaleyale....; Hakuna Jipya Wizi Mkubwa , Brah.., Brah.., Brah za hapa na Pale baada ya hapo Business as Usual..,

To be repeated Next Year...

Yes , kuwe na comparison reports .

Implementation and action taken after CAG report submission for the FY 2021/2022.

Ndio utajua hata kufuatilia hayo mambo ni waste of time

Ile story ya nuhu vipi, nasikia waafrica mlilaaniwa baada ya kumchungulia baba yenu akiwa uchi, kuna unwell ?
 
Naamini juu ya watoto wa Nuhu kuwa mmoja aliona utupu wa baba yake ila siamini kuwa huyu mtoto ndiye chimbuko la Waafrika. Hiyo imetumika tu kuwa undermine na kuwa discriminate Waafrika

Apart from bible , toa evidence kuwa kuna mtu aliitwa nuhu aliexist, na toa evidence pia ni kweli kuna mtoto alichungulia huo utupu?
 
Bora huyu anapokea ripoti na tunajuwa ubovu na ufisadi wote. Kuliko DIKTETA Magufuli yeye aliposomewa ripoti ya upotevu wa Tsh 1.5 Trillion akamfukuza kazi CAG Prof Assad.

Bahati mbaya Bunge ndilo lenye kuchukua hatua. Ila Bunge lenye UTAAHIRA aliloliacha Magufuli unategemea lifanye nini? Bunge lina wabunge 99.999% wa CCM.

Simtetei Samia kwa kutochukua hatua kwenye ropoti ya mwaka 2021/22 kama tulivyotarajia. Nchi hii inaendeshwa kwa Katiba na utawala wa Sheria. Rais hawezi kusomewa ripoti leo halafu kesho aseme kamata fulani na fulani peleka Mahakamani. Tutakuwa tuarudia UHAYAWANI uleule wa Magufuli aliyejaza watuhumiwa magereza lakini hakuna hata kesi moja aliweza kuimaliza hadi anakufa.

Upo utaratibu nankuna vyombo vya kufanya hayo mambo. Na mwenye majukumu makubwa ni Bunge.

Katiba inaruhusu Wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kama maagizo ya CAG hayatekelezwi. Kura zikipigwa na wakashinda wanaosema hawana imani basi Rais anavunja cabinet.
Magufuli na mapungufu yake atabaki kuwa Rais Bora Tanzania
Kwa Sasa nchi hata haieleweki inaenda wapi
 
Back
Top Bottom