Waziri Ummy: Tanzania yawa miongoni mwa nchi zilizoongoza duniani kwa unywaji wa pombe kali kwa Vijana Umri kati ya Miaka 15-19

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,960
18,515
Anaandika Ummy mwalimu Baada ya Report ya World Health Statistics 2023 ya WHO..

Taarifa zaidi kuhusu Kiwango cha Matumizi ya Pombe Tanzania na Magonjwa YasiyoAmbukiza.

Kwa mujibu wa World Health Statistics 2023 kiwango cha matumizi ya Pombe isiyozimuliwa (Pure alcohol - 100% ) nchini Tanzania kwa mwaka kwa kila mtu mwenye umri wa miaka 15 na kuendelea ni Lita 10.4. Wastani huu ukiwa ni wa juu zaidi wa wastani wa Africa (4.5 Lita); America (7.5 Lita); South East Asia (3.8 Lita); European Region 9.2 L.

Kwa kawaida Bia inayotumika (regular) huwa na kiasi cha kilevi (pure alcohol) cha asilimia 3 - 7; sasa piga hesabu lita 1 ya Pombe isiyozibuliwa ni sawa na chupa ngapi za Bia iliyozimuliwa. Halafu piga hesabu wanaokunywa Pombe nchini ni asilimia 20 ya watanzania wenye umri wa miaka 15 na kuendelea ambayo ni sawa na mtu 1 katika kila watu 5 ndio anakunywa Pombe. Then utapata jibu kama 10.4L ya Pure alcohol kwa mtu mmoja ni pombe nyingi au la?

Wajibu wetu ni kuwaeleza ukweli kuhusu Madhara ya Unywaji wa POMBE KUPITA KIASI. Unywaji wa POMBE KUPINDUKIA HUSABABISHA:
• Madhara kwa Ini
• Madhara ya Moyo na Mishipa ya Damu ikiwemo shinikizo la damu (hypertension), matatizo ya moyo kama vile kuziba kwa mishipa ya damu (atherosclerosis), na hatari ya kiharusi.
• Matatizo ya Afya ya Akili
• Kuathiri Mfumo wa Kinga
• Ugonjwa wa figo
• Ugonjwa kwenye kongosho na kuleta kisukari

Ninatoa rai kwa wananchi kupunguza unywaji wa Pombe kupita kiasi ili kujikinga na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza. Uamuzi ni Wako.
#KingaNiBoraKulikoTiba #AfyaYakoWajibuWako

20240425_110057.jpg
20240425_110043.jpg

Screenshot_20240425_110037_X.jpg
 
Kuna hii collabo kati ya energy drinks na double kick au kisungura.

Unakuta kijana amemix energy drink na double kick ,akipiga funda anaweka chupa ya pombe mfuko wa shati alafu anawasha bodaboda anasepa zake kufuata abiria.

Akikaa tako Moja haligusi popote (anakaa upande) alafu mguuni ana malapa.

Njiani akipishana na magari anahisi anaendesha greda alafu magari anayaona kama makopo ya plastick.

Collabo ya bodaboda na visungura vilivyomixiwa na energy drinks inaua sana vijana kwa kweli.

RIP vijana wa Arusha,Chugastan Republic.
 
Back
Top Bottom