Ufafanuzi kuhusu kikokotoo cha mafao ya kustaafu

Yaani wewe ni POPOMA!

Nilitegemea utatoa mfano
Wa aliyekuwa kikokotoo Cha zamani alikuwa anapata ngapi mfano amestaafu na mshahara wa basic 1,500,000

Na huyu wa kikokotoo kipya atapata ngapi
Kwa basic hiyo hiyo...


Halafu uweke pension Kila mwezi
Huyu wa zamani anapata ngapi na huyu wa kikokotoo kipya atapata ngapi
Kwa muda Gani..

Vinginevyo wewe ni mpuuzi kama wapuuzi wengine...
Kwa kifupi wewe ni lipumbavu lenye uwezo wa kutumia mtandao
 
Kila siku nawaambia watu Pension sio Mtaji wala Akiba bali ni Kinga / Bima / Insurance ya watu wakizeeka / wakikosa nguvu kuweza kusukuma maisha yao mwezi kwa mwezi huku wakingojea siku zao za mwisho....

Pia ninachoogopa na huenda kikaja ni watu / wajanja kubinafsisha / kutengeneza Pension / Security Funds binafsi na kuwashauri watu wawekeze huko kutokana na returns kubwa zaidi na mwisho wa siku kupigwa kama waliopigwa na kina Bernie Madoff

Ila issue a maana zaidi ni kwamba wanachopata ni kwamba hakikidhi mahitaji na sio wao tu mbaya zaidi ni hata kizazi kinachokuja...;


Kwani hawajui kwamba sio mtaji,unaleta mawazo miaka ya 1960's nowadays watu wanafanyabiadhara wakiwa kwenye ajira,Kuna watu wanastaafu wakiwa na nguvu,wanataka kuongezeka pensheni zao kwenye investment zao Kwa ajili ya familia zao ww unawapangia Nn wafanye na pesa zao?
 
Kwani hawajui kwamba sio mtaji,unaleta mawazo miaka ya 1960's nowadays watu wanafanyabiadhara wakiwa kwenye ajira,Kuna watu wanastaafu wakiwa na nguvu,wanataka kuongezeka pensheni zao kwenye investment zao Kwa ajili ya familia zao ww unawapangai Nn wafanye na pesa zao?
Hio sio Pensheni waweke pesa Benki na hapo kutakuwa wala hakuna ulazima kwenye Sheria mwajiri wako kukuongezea hizo asilimia za ziada...

Narudia tena pensheni zilianzishwa kama Social Security na Sio Mtaji kwahio hawa unaosema wapo kwenye ajira na wanafanya biashara kuna mifuko tofauti ambayo wanaweza kuweka ambao wakitaka pesa zao wanaweza kupewa zote bila mfuko kuharibika / kufa...

Cha maana na kigezo ambacho kina-make sense ni watu kulalamika kwamba mtu anachopata kila mwezi hakikidhi mahitaji na wengine watakaokuja kesho watakuwa sio pensionable...; lakini issue ya kila mtu apewe chake chote sio sustainable
 
Inasikitisha kuona kuwa wengi wenu mnaojidai kutoa ufafanuzi wa kikokotoo kipya hamna guts kueleza ubadhirifu unaofanyika katika mifuko hiyo kwa mujibu wa ripotiza CAG. Pia hamjisunbui kueleza jinsi serikali inavyohujumu raia wake kwa kukopa mifuko Yao ya pension bila kurejesha
Badala yake mmekuwa mawakala wa serikali kutetea ukandamizaji wake kwa kuwashawishi TU watu wakubali kikokotoo.
 
Maelezo meengi! Halafu ni ujinga tu. Unafikiri jamii forums imejaa vilaza kama hao mnao wadanganya huko mtaani!!

Sababu ya hiyo mifuko kuishiwa hela ni kwa sababu ya wastaafu kulipwa pesa zao kwa kikokotoo cha awali, au ni kwa sababu hizo fedha zao mlikuwa mnazinafuja hovyo?

Ni kwa nini nyinyi wafanyakazi wa hiyo mifuko mnakopeshana mabilioni ya fedha za wastaafu, tena bila ya riba! Halafu hamzirejeshi kwa wakati? Kwa nini msiende kukopa benki kama ilivyo kwa wananchi wengine?

Kwa nini mnachukua fedha za wastaafu na kujengea miradi hewa? Kwa nini mnaruhusu serikali kuchukua hizo hela na kufanyia shughuli nyingine?

Kama hicho kikokotoo chenu kina tija; kwa nini hakiwahusu Wabunge na vigogo wengine wa ngazi za juu!! Au wao ndiyo wana uwezo mkubwa wa kutunza fedha zao hata baada ya kustaafu? Halafu ni nani aliyewapa mamlaka ya kumpangia matumizi ya fedha zake kama siyo kuendekeza wizi tu.

Hopeless kabisa wewe.
 
Ungeweka mifano halisi kwa mfano ungesema mtu aliyepata mzigo wa 400m kwa formula ya zamani mtu uyo kwa formula mpya anapata 100m

au yule aliyepata 200m kwa formula ya kale saivi anapata 50m ivo ungeelewa kirahisi na baada ya apo ungeongezea tu kusema sababu ya izo tofauti
 
Watumishi wa umma wengi sasa hivi wanafuatilia issue ya kikokotoo cha mafao yao ya baadaye.

Hata hivyo wapo watumishi wa umma ambao wapo kimya kuhusu kikokotoo labda kwa kuwa miaka yao ya kustaafu bado iko mbali saaana.

Wapo wengine wanaoongea kwa kuwa kikokotoo kipya kimewagusa kwa namna moja ama nyingine.

Kama Mwanazuoni wa Hifadhi ya Jamii, Naomba nifafanue baadhi ya mambo kuhusu kikokotoo cha mafao ya kustaafu.

Kikokotoo kipya cha:
1/580 × APE x PoS x 12.5 x 33%

Na kikokotoo cha zamani cha LAPF na PSPF yaani

1/540 × LAS x PoS x 15.5 x 50%

(LAS = Last Annual Salary na PoS = Period of Service)
APE = Annual Pensionable Emoluments
1/540 = Acrual factor
15.5=Commutation Factor
50%=Commutation Rate


Usipojifunza jinsi ya vikokotoo hivyo viliundwa utashindwa kuishawishi Serikali kipi kirekebishwe na kwa nini. Ni kama unakuwa unaongea kitu usichojua.

Kusema Serikali ikulipe pesa yako yote ni ujinga ujinga mkubwa saaana ambao watumishi wa umma wenye ujinga ndiyo watapromoti hoja hii.

Vikokotoo vyote hivyo vina uzuri na ubaya wake. Kama wewe siyo mchambuzi utashabikia tu lolote bila kujua vizuri matokeo yake.

Sheria za Kikokotoo cha PSPF na LAPF kilikuwa na mapungufu meengi sana. Bahati mbaya mapungufu hayo hakuna watalaam wanaoyadadavua sasa hivi.

Wanachama waliokuwa PSPF na LAPF kikokotoo chao kilikuwa na mapungufu kibao ukiacha upande wa Kiinua mgongo tu vipengere vingine vyote havikuwa vizuri.

Kikokotoo cha wanachama waliokuwa PPF, GEPF na NSSF kilikuwa hiki hapa:

1/580 × APE x PoS x 12.5 x 25%.

(APE = Annual Pensionable Emoluments na PoS = Period of Service/Contribution)

Makundi haya ya wanachama ambao ni zaidi ya 81% ya wanachama wote wa mifuko iliyokuwepo kwao kikokotoo kipya kimewaongezea mkupuo wa mafao waliokuwa wanapata kwa 8%. Yaani iko hivi:

1/580 × APE x PoS x 12.5 x 25%

Hapo kwenye asilimia 25 kwa kikokotoo kipya wao imekuwa 33% ambayo ni ongezeko la 8%.

Sasa watumishi wa umma wote wamepewa kikokotoo kimoja bila kujali wako idara ipi.

Zamani (2004 hadi 2018) waliokuwa Serikali kuu na serikali za mitaa yaa LAPF na PSPF walikuwa wakilipwa Mkupuo Mkubwa saaana kwa Kikokotoo hiki hapa cha 1/540 × LAS x PoS x 15.5 × 50% kwa sababu kikokotoo hicho cha Serikali Kuu kilizingatia Last Month Salary

Na wale wa sekta binafsi chini ya NSSF na PPF walitumia kikokotoo kilichozingatia Wastani wa Mshahara wa miaka mitatu.

Kwa hiyo tunafanyaje? Tuchukue kikokotoo cha serikali Kuu kiwe cha wanachama wote wa sekta binafsi na umma halafu mfuko uishiwe nguvu kulipa mafao baada ya miaka 5???

Au tuchukue kikokotoo cha sekta binafsi kilichokuwa kinatumika NSSF, PPF na GEPF kiwe cha wote na kiboreshwe kidogo from 25% to 33% na mfuko uweze kujiendesha kwa miaka mingi???? Kipi bora??

Maamuzi yaliyochukuliwa na serikali mwaka 2018 yalikuwa ya kuwatazama wanachama 81% waliokuwa mifuko ya NSSF, PPF, na GEPF ili wafanyakazi wote wafanane kwenye mafao ya uzeeni.

Yaani serikali ililenga kufanya pensheni ya kila mwezi na malipo ya Mkupuo yawe na usawa pamoja na watumishi wa umma waliokuwa na kikokotoo kikubwa kwa kutazama factors za uendelevu wa mfuko mpya wa PSSSF.

Mwaka 2014 hadi 2018 wastaafu wa serikali Kuu waliokuwa chini ya PSPF walikuwa wamefikia mahali Papaya sana hadi mafao yao yalikuwa hayapatikani tena kutokana na PSPF kushindwa kujiendesha kwa sababu ya madeni makubwa ambayo serikali ilikuwa inadaiwa tangu 1999.

Watu waliokuwa wanastaafu miaka hiyo 2014 hadi 2018 walikuwa wanaambiwa wasubiri. Walisubiri saaana mpaka Mwaka 2018 December mifuko ilipounganishwa zikachukuliwa fedha za LAPF na PPF kuwalipa wastaafu waliokuwa wamekaa mtaani bila mafao kwa zaidi ya miaka 2 hadi 3 bila mafao.

Ni bahati mbaya saaana kwamba tuna wanasiasa na wanachama wanaosahau mapema tulipotoka.

USHAURI MBAYA NI HUU

Kudai Kwamba wastaafu walipwe pesa zote (100%) na waendelee na maisha yao. Huu ni ushauri mbaya saaana kuishauri serikali.

Kwamba kwa nini wastaafu wawekewe pesa za kulipwa kila mwezi kidogo kidogo? Hili ni swali la kitoto litokanalo na kutojua maana ya Society Protection

Ukisikia mtumishi wa umma anadai hataki pensheni ya kila mwezi anaomba alipwe pesa zake zote aendelee na maisha yake ujue kuwa huyo siyo mtumishi wa umma. Ni Mjasiriamali.

Na Bahati mbaya watumishi wa umma asilimia 95 siyo wajasiriamali. Ni wategemezi wa mishahara ya kila mwezi.

Akilipwa pesa yote halafu ikaisha social economic crisis itakayotokea katika jamii ya wazee itazidi ile ya wazee wa East Africa Community waliovua nguo barabarani wakidai Pension ya kila mwezi.

Ukitaka kujua utamu wa pension ya kila mwezi kabla hujashauri utaratibu wa pension ufutwe, nakuomba ukawaulize waliostaafu miaka 10 iliyopita.

Waulize kama pesa kubwa ya kikokotoo kikubwa walicholipwa 2010 mpaka leo pesa ipo?

Kawaulize Tegemeo lao kuu la pesa ya kila mwezi ni wapi? Hawa wazee ukitaka ukosane nao ondoa utaratibu wa pension ya kila mwezi.

Waulize utamu wa pension na utamu wa kiinua mgongo ni kipi kitamu zaidi.

Kawaulize wazee waliostaafu 2010 kati ya Pension na Burungutu la pesa unayopewa ukistaafu ni kipi kiongezwe kiwe kikubwa?

Waulize kati ya Pension ya kila mwezi na kiinua mgongo(gratuity) wanashauri kipi kiongezwe?.

Ukiwauliza waliostaafu miaka 10 iliyopita wao wanaomba pension iongezeke iwe kubwa saaana.

Ukiwauliza wazee wastaafu Watarajiwa kipi kiongezwe, wao wataomba kiinua mgongo ndicho kiongezwe.

Hii inatokana na kwamba ni vigumu sana mstaafu mwenyewe tarajiwa kupendekeza alipwe nini kama hajafika huko uzeeni.

Wazee waliolipwa mafao kwa kikokotoo cha LAPF na PSPF miaka 5 iliyopita asilimia 90 yao tegemeo lao kuu kwa sasa ni pension ya kila mwezi pamoja na kwamba walilipwa kikokotoo kikubwa.

Hoja nyingine inayopotoshwa ni hii kwamba mstaafu analipwa pesa fulani na nyingine inabakia kwenye Mfuko kwa ajili ya kulipwa kidogo kidogo kama pension.

Huu nao ni uongo wa Mtaani umeshageuzwa kuwa kama ukweli.

Ukweli ni kwamba Hakuna pesa inayobakia kwenye Mfuko.

Mstaafu huwa analipwa pesa zote alizochangia yeye na Mwajiri wake (5% na 15%) halafu Mfuko unaongeza nyingine kutoka kwenye uwekezaji na kisha anaanza kulipwa pension kila mwezi. Hapo unasemaje kuna pesa imebakia PSSSF au NSSF.

Ukweli ni kwamba Mstaafu akishalipwa kiinua mgongo ambacho huwa mara nyingi ni zaidi ya hata michango yake yote anaanza kulipwa Monthly Pension ambayo mara nyingi huwa ni zaidi ya 40% hadi 50% ya mshahara wake (Net pay) aliyokuwa analipwa akiwa kazini.

Ukweli ni kwamba Pension hiyo atalipwa maisha yake yote yaliyoko mbele Hata kama akiishi miaka 50 au zaidi baada ya kustaafu.

Ndugu wafanyakazi wenzangu kama tunaomba mafao makubwa tuwe tayari kuongeza uchangiaji yaani badala ya kuchangia 5% au 10% ya mishahara yetu tukubaliane kiasi kiongezwe kiwe 10% au 15% na Mwajiri atuongezee 15% au 20%

Au pia kama tukitaka mafao makubwa tukubaliane mfumo wa pension ya kila mwezi uondolewe ili kila mtu akistaafu alipwe Kiinua mgongo kama wabunge na Madiwani halafu pension isiwepo.

Au tuchague mfumo wa pension kwa wote ambapo hakuna kuchangia chochote kila mwezi na kila mwananchi akitimiza miaka 55 au 60 anaenda HAZINA kuu ya Serikali kuchukua Kiinua mgongo chake bila kujali alikuwa mwajiriwa au Mjasiriamali.

Au tuchague kuwa na Mifuko mingi ya pension na kila mfuko ujipangie mafao utakayotoa chini ya Sheria za ushindani na serikali isiingilie lolote zaidi ya kuweka Sheria na sera za kuwalinda wateja wa Skimu hizo.

Imeandikwa na
FADEMO DIRECTOR.
Social Security Practioner with 19 years of Field Experience
Sijaona kosa la watumishi lililopelekea wapewe kikokotoo hicho. Hivi mimi nikistaafu nikapewa 400M zangu zote tatizo liko wapi?

Kwani hizo fedha za kununulia V8 mabilioni kwa mabilioni zinapatikanaje halafu za wasitaafu zinakosekana?

Jawabu zuri ambalo halina utata ni kwamba kipaumbele cha serikali ni kutengeneza masikini wengi na kuua wasitaafu kwa msongo wa mawazo ili fedha zao walizozitumikia zibaki huko mzichukue mkanywee juice ilihali ndugu wa wasitaafu wazisotee pasipo mafanikio.
 
Hio sio Pensheni waweke pesa Benki na hapo kutakuwa wala hakuna ulazima kwenye Sheria mwajiri wako kukuongezea hizo asilimia za ziada...

Narudia tena pensheni zilianzishwa kama Social Security na Sio Mtaji kwahio hawa unaosema wapo kwenye ajira na wanafanya biashara kuna mifuko tofauti ambayo wanaweza kuweka ambao wakitaka pesa zao wanaweza kupewa zote bila mfuko kuharibika / kufa...

Cha maana na kigezo ambacho kina-make sense ni watu kulalamika kwamba mtu anachopata kila mwezi hakikidhi mahitaji na wengine watakaokuja kesho watakuwa sio pensionable...; lakini issue ya kila mtu apewe chake chote sio sustainable
Siyo sustainable kwa nani kati ya msitaafu na mfuko?
 
Siyo sustainable kwa nani kati ya msitaafu na mfuko?
Kwa mfuko kusema kwamba makusanyo inakusanya na kila mtu akitaka chake anapewa chote palepale; je kuna wanaobaki kupewa mwezi kwa mwezi inakuwaje ?

Na vijana wakitoka ili wapewe chao kwa bahati mbaya pesa hio ikapotea huoni kwamba dhima nzima ya huu mfuko (kuhakikisha wanapata pesa uzeeni kila mwezi mpaka kifo chao inakuwa haina maana tena) ?

Point ni kwamba hili la mtu kuweza kuchukua chake saa yoyote tena chote kuna investment funds tofauti ambazo mtu anaweza kuweka..., lakini investment hio hatuwezi kuita Pensheni..., unless hatuoni tena faida ya kuhakikisha wazee, uzeeni wanapata blanket ya kuwakinga wakiwa hai mpaka siku wanakufa...

Hoja ya muhimu ni vipi wanaweza kuongezewa wanachopata kiweze kukidhi maisha yao ya kila siku....; Na hoja ya muhimu zaidi ni tunafanye kuhusu kesho ya hawa wengi ambao sio pensionable ?
 
Kwani wak
Kwa mfuko kusema kwamba makusanyo inakusanya na kila mtu akitaka chake anapewa chote palepale; je kuna wanaobaki kupewa mwezi kwa mwezi inakuwaje ?

Na vijana wakitoka ili wapewe chao kwa bahati mbaya pesa hio ikapotea huoni kwamba dhima nzima ya huu mfuko (kuhakikisha wanapata pesa uzeeni kila mwezi mpaka kifo chao inakuwa haina maana tena) ?

Point ni kwamba hili la mtu kuweza kuchukua chake saa yoyote tena chote kuna investment funds tofauti ambazo mtu anaweza kuweka..., lakini investment hio hatuwezi kuita Pensheni..., unless hatuoni tena faida ya kuhakikisha wazee, uzeeni wanapata blanket ya kuwakinga wakiwa hai mpaka siku wanakufa...

Hoja ya muhimu ni vipi wanaweza kuongezewa wanachopata kiweze kukidhi maisha yao ya kila siku....; Na hoja ya muhimu zaidi ni tunafanye kuhusu kesho ya hawa wengi ambao sio pensionable ?
Kwani wakipewa fedha zao zote hawawezi kuendelea kuwa nazo mpaka pale umauti utakapo wakuta?

Umesema habari za mfuko kukosa uwezo wa kuendelea kujiendesha,kwani muanzolishi wa huo mfuko ni mtumishi?

Aliyeuanzisha huo mfuko matarajio yake ilikuwa ni yapi na sasa anapata nini?
 
Watu wapewe chao,wafe wasife wapewe chao watajijuwa kwanza matumizi ya pensheni kwa mstaafu hayana hasara kwa serikali.Na kama kikokotoo ni kizuri kitumike Kwa watu wote kuanzia serikali kuu hadi serikali za mitaa,wanaolipwa kutokana na Kodi zetu.
Watakupiga mawe mkuu.

Kwa kusema wao wana wajali sana wanyonge
 
Sijaona ufafanuzi wowote uliotolewa hapa, zaidi ya kuwatukana wanaotaka kulipwa pesa yote. Ukipata nafasi pia tueleze kwanini serkali inakopa kwenye hii mifuko na hairejeshi kama ulivotupa mfano wa PSPF
Hakuna pesa inayo baki kwenye mfuko baada ya mstaafu, kulipwa kiinua mgongo. Tafuta contribution statement ya mstaafu angalia alicho lipwa Vs Contribution statement.
 
Kuwa mkweli, mifuko haiwezi kufa kama serikali itadhibiti ubadhilifu. CAG reprt zinaonesha wazi kuwa ni ubadhilifu tu ndio unaleta mifuko kuwa na hali mbaya.

To me nipe hela zangu nifie mbali. kama mtu hujui kuwa ulichopewa ndiyo basi ukakitumia vibaya bila kuinvest, KUFA!

all in alll una maoni mazuri.
nami nimeandika sasa hivi as below
Hakuna pesa inayo baki kwenye mfuko baada ya mstaafu, kulipwa kiinua mgongo. Tafuta contribution statement ya mstaafu angalia alicho lipwa Vs Contribution statement.
 
Umetumwa?

Ukishiba unajaamba sana

Wapeni fedha zao zote...roho mbaya tu.....nakibunda changu hapo NSSF isinge kuwa kujiongeza kupiga madebe Goma ningekukwa Lamadi majarubani
Hakuna pesa inayo baki kwenye mfuko baada ya mstaafu, kulipwa kiinua mgongo. Tafuta contribution statement ya mstaafu angalia alicho lipwa Vs Contribution statement.
 
Utumbo tu.
Expected pensioners ni proportion ndogo sana ya jamii.
Sasa serikali ndio inawajali sana hawa kuliko wasio watumishi (wakulima, wafanyabiashara), kiasi kwamba inataka iwatunzie pesa zao???

Serikali inazichukua hizo pesa, ikisingizia kuwantuzia, lakini inawekeza, na dividends haziwahusu wanachama. Si ujinga huo?

Inatengeneza taratibu za uendeshaji wa mifuko hiyo, taratibu zenyewe ni za kipigaji, na mifuko inaishiwa.

Mtoa mada unajua kabisa kuwa lengo kuu la hiyo mifuko sio welfare ya mtumishi, bali ni namna ya kumnyonga zaidi.

Kila mtu apewe chake.
Anayependa kuwekewa na serikali, awekewe, asiyetaka apewe akajue mwenyewe atakachofanya.

Vinginevyo kama ni lazima kwa watumishi wote, basi kikokotoo kitumike bila ubaguzi wa wafanyakazi wa kawaida, beki tatu, waziri au mbunge, wote watumie kikokotoo kimoja. Sheeeenzi sana!
Hakuna pesa inayo baki kwenye mfuko baada ya mstaafu, kulipwa kiinua mgongo. Tafuta contribution statement ya mstaafu angalia alicho lipwa Vs Contribution statement.
 
Kwamba mstaafu akishalipwa kiinua mgongo cha mkupuo, huwa habakizi kitu.
Anayolipwa kila mwezi faida ya uwekezaji?
Uko sahihi,
Hakuna pesa inayo baki kwenye mfuko baada ya mstaafu, kulipwa kiinua mgongo. Tafuta contribution statement ya mstaafu angalia alicho lipwa Vs Contribution statement.
 
Watu wapewe chao,wafe wasife wapewe chao watajijuwa kwanza matumizi ya pensheni kwa mstaafu hayana hasara kwa serikali.Na kama kikokotoo ni kizuri kitumike Kwa watu wote kuanzia serikali kuu hadi serikali za mitaa,wanaolipwa kutokana na Kodi zetu.
Chao wamesha pewa kwenye kiinua mgongo, kilicho baki kinatoka kwenye mfuko kama faida ya uwekezaji wa alicho changia, hakuna pesa inayo baki kwenye mfuko ya mwanachama baada ya kulipwa kiinua mgongo.
 
Back
Top Bottom