kali linux
JF-Expert Member
- May 21, 2017
- 1,996
- 5,055
Kuna ajali mbaya sana imetokea Mlandizi. Bus moja limegonga lori la mafuta na kusababisha moto, mwenye taarifa zaidi atujuze tafadhali.
Lakini hii Morogoro Road kwa nini serikali haijali? Barabara nyembamba saaana hasa kipande cha Mlandizi to Morogoro, barabara kila siku ina ajali na ndio lango la kuingilia na kutokea Dar.
====
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bw.Abubakar Kunenge, amezungumza na #ITVDigital ambapo amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu wawili katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya New Force, basi la Kampuni ya Sauli pamoja na Lori la mafuta, katika eneo la Ruvu, mkoani humo.
Kunenge amesema abiria walifanikiwa kutoka kwenye mabasi hayo isipokuwa abiria wawili ambao walikuwa wamebanwa kwenye moja ya mabasi hayo na wakati Jeshi la Zimamoto na Jeshi la Polisi wakiendelea na juhudi za kuwaokoa ndipo moto ukalipuka na kusababisha abiria hao kufariki dunia.