Je, huwa unafuatilia uwasilishwaji wa Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)?

JF Toons

Digital Art by JF
Feb 19, 2024
32
68
IMG_20240330_192231_881.PNG

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha za umma ili kuthibitisha matumizi yamefanywa kwa mujibu wa sheria na kanuni husika na kuna uwazi katika matumizi ya fedha hizo.

Ufuatiliaji wa uwasilishwaji wa ripoti hizi ni muhimu kwa wananchi ili kuhakikisha kuna uwajibikaji na wote waliohusika kwenye ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma wanachukuliwa hatua stahiki.
 
Professor Assad ndio alikuwa CAG alikuwa hana makando kando. Alifichua kila uozo. Ila pia nchi hii kuwa na CAG halafu uozo bado haufanyiwi kazi (yani hakuna uwajibikaji au uwajibishwaji) ni upuuzi mtupu.
 
Nchi hii viongozi wanawaona wananchi ni vinyesi vyao tu. Wanavihitaji vinyesi wakati wa vipimo tu. Hakuna haja ya kufatilia mambo yanayoumiza moyo na hayachukuliwi hatua,huo muda ni mara mia nikamtafuta mrembo monika aje anipunguzie nyege.
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha za umma ili kuthibitisha matumizi yamefanywa kwa mujibu wa sheria na kanuni husika na kuna uwazi katika matumizi ya fedha hizo.

Ufuatiliaji wa uwasilishwaji wa ripoti hizi ni muhimu kwa wananchi ili kuhakikisha kuna uwajibikaji na wote waliohusika kwenye ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma wanachukuliwa hatua stahiki.
Wakati mwingine unajiuliza huyu CAG motive ya ukaguzi hasa ni nini, kujua faida na hasara kwa maana ya cash...?

Ukiwauliza wanaofanya biashara ya maduka makubwa (supermarkets) watakwambia zipo bidhaa wanalazimika kuziweka dukani kwa sababu ni za kuvutia wateja waje dukani wanunue hizo bidhaa pamoja na bidhaa zingine, au kuwa-retain waje kila mara..lakin zenyewe peke yake hazina faida yoyote ya cash! ndivyo ambavyo ATCL inafanya au TRC inafanya, sisi tuna vivutio vingi vya utalii, huwezi kutegemea majirani wakuletee watalii wakati na wao wana vivutio kama vyako..TRC inafanya kazi kubwa ya kusafirisha mizigo mikubwa ambayo inasababisha uwepo wa nafuu ya bei mfano mafuta tofauti kama ingesafirishwa kwa barabara..hivi inahitaji maarifa ya pekee kwa CAG kujua mtazamo huu???

Pili, kwa hali ya sasa sidhani kuna uhitaji wa kuwa na CAG wakati hao anaopita kuwakagua wanaweza kabisa kupitia teknolojia kujua hiyo faida au hasara kwa wiki, mwezi, robo mwaka au hata kila siku...inasaidia nini kupoteza fedha nyingi kukagua taarifa za miaka miwili au mmoja nyuma? Hii si ni sawa na kufanya postmortem...mtu alishakufa, ukijua sababu za kifo atarudi???

Kuna wakati mmoja Profesa wa uchumi akiwa waziri wa fedha awamu ya tatu alipendekeza kuundwe MAMLAKA YA MATUMIZI itakayofanya kazi sawa na inavyofanya TRA..km wakati huo Bunge halikuona maana ya kuwa na mamlaka hii ya matumizi, pengine kwa sasa ni muhimu zaidi kuliko kuendelea na postmortem za CAG hakuna faida yotote ya uwepo wake ni kubebesha mzigo walipa kodi!
 
Mnakuwa na mkaguzi CAG kazi yake ni kuonyesha kasoro tu, nini chanzo cha kasoro aliyoiona hasemi, kasoro irekebishweje hasemi..bora CAG asiwepo kabisa.haya ndio madhara ya kukopi kopi kila kitu..kwa sasa hakuna haja ya kuwa na CAG.
 
Tamatizo kubwa wale walibainika kataika ripoti hizi tangu uhuru wa nchi hii hakuna aleiwajibishwa ,sasa no heri waache tu wale Kodi zetu na mikopo mabilioni wanayokopa kwa wazugu sisi lala hoi tutaishi kwa neema za mwenyezi mungu
 
Mnakuwa na mkaguzi CAG kazi yake ni kuonyesha kasoro tu, nini chanzo cha kasoro aliyoiona hasemi, kasoro irekebishweje hasemi..bora CAG asiwepo kabisa.haya ndio madhara ya kukopi kopi kila kitu..kwa sasa hakuna haja ya kuwa na CAG.
Pole sana uelewa wako mdogo sana au unacikiri nini kufanyike ili sasa wananchi wapaye chomvo kinacho jiyegemea amabcho kinaweza kuwapa taarifa za mapato na matumizi ya nchi yao, mana unataka ifutwe tu
 
Umuhimu wa hii ripoti ni kutujuza ni nani na nani ameongezeka kwenye list ya mabilionea wapya tu. Nje ya hivyo labda itakuwa ni sehemu ya burudani tu kama muziki au kipindi cha uswazi
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha za umma ili kuthibitisha matumizi yamefanywa kwa mujibu wa sheria na kanuni husika na kuna uwazi katika matumizi ya fedha hizo.

Ufuatiliaji wa uwasilishwaji wa ripoti hizi ni muhimu kwa wananchi ili kuhakikisha kuna uwajibikaji na wote waliohusika kwenye ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma wanachukuliwa hatua stahiki.
Sisi tumechagua Rais na Bunge, hao wataangalia maslahi yetu, sisi tuendelee na mambo mengine ya maendeleo
 
Back
Top Bottom