Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,197
- 4,120
Wazazi wa Wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne 2023 wamepokea ujumbe mfupi wenye taarifa halisi za Watoto kutoka Chuo cha Tabora Polytechnic kilichopo Tabora Mjini.
Ujumbe huo ulisomeka kuwa,
Mkuu wa chuo cha Tabora Polytechnic kilichopo Tabora Mjini anakutangazia nafasi za masomo mzazi wa ......... Mwenye namba ........2023 katika kozi zifuatazo( kozi zimeorodheshwa kulingana na mchepuo aliofaulu mtoto husika kama ni Art au Science)
Mara baada ya mmoja wa watu wangu wa karibu kupata ujumbe huo, alishtuka kwani hajawahi kuwasiliana na hicho chuo kwa namna yoyote kwamba watakuwa wamepata namba za simu kutoka kwake mwenyewe.
Ndipo alipochukua hatua za kumtafuta mzazi wa aliyekuwa rafiki wa mwanaye shuleni hapo ili kuona kama naye katumia ujumbe huo. Mzazi huyo alithibitisha kuwa naye katumiwa ujumbe kama huo kwa jina la Mwanaye.
Akaamua kupiga namba inayoonekana kwenye ujumbe ili ahoji wamepata wapi namba ya simu ya mzazi wa mtoto husika, majina matatu na namba sahihi ya mtihani ya mtoto huyo.
Ndipo alipojibiwa kuwa kuna mawakala ambao huzunguka mashuleni, kukusanya/ kununua taarifa hizo za wanafunzi na kuwauzia wao hapo chuoni kupit8a Mkuu wa chuo, kisha wao huwatumia wazazi wa watoto jumbe za kiwajulisha uwepo wa kozi ili kuwaaloka wakasome hapo.
Jambo hili ni baya sana ambalo linaonekana kufanywa na Shule ya Sekondari Ndono kuuza taarifa nyeti za wanafunzi wao na namba za simu za wazazi wao.
Jambo hili linakiuka sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi za watu.