DOKEZO Je, Chuo cha Tabora Polytechnic kilichopo Tabora mjini kimeuziwa taarifa za wanafunzi na Ndono Sekondari?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Waulizeni vizuri watoto zenu.

Wengi wao hupendelea kwenda chuo hivyo wakati mwingine hufanya application pasipo wewe kujua. Kumbuka hao jamaa wanafanya matangazo Sana.

Pia Wanafunzi Ni Kama nyumbu.
 
kuna mfumo unatumika kupata majina na namba zao kwa wanafunzi walio maliza form four. ukinipa jina la shule uliyo maliza pamoja na mwaka nitakupatia majina ya uliohitimu nao pamoja nawewe ukiwemo. mbona ni kitu cha kawaida.
 
  • Mshangao
Reactions: G4N
Wazazi wa Wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne 2023 wamepokea ujumbe mfupi wenye taarifa halisi za Watoto kutoka Chuo cha Tabora Polytechnic kilichopo Tabora Mjini.

Ujumbe huo ulisomeka kuwa,
Mkuu wa chuo cha Tabora Polytechnic kilichopo Tabora Mjini anakutangazia nafasi za masomo mzazi wa ......... Mwenye namba ........2023 katika kozi zifuatazo( kozi zimeorodheshwa kulingana na mchepuo aliofaulu mtoto husika kama ni Art au Science)
View attachment 2946641
Mara baada ya mmoja wa watu wangu wa karibu kupata ujumbe huo, alishtuka kwani hajawahi kuwasiliana na hicho chuo kwa namna yoyote kwamba watakuwa wamepata namba za simu kutoka kwake mwenyewe.

Ndipo alipochukua hatua za kumtafuta mzazi wa aliyekuwa rafiki wa mwanaye shuleni hapo ili kuona kama naye katumia ujumbe huo. Mzazi huyo alithibitisha kuwa naye katumiwa ujumbe kama huo kwa jina la Mwanaye.

Akaamua kupiga namba inayoonekana kwenye ujumbe ili ahoji wamepata wapi namba ya simu ya mzazi wa mtoto husika, majina matatu na namba sahihi ya mtihani ya mtoto huyo.

Ndipo alipojibiwa kuwa kuna mawakala ambao huzunguka mashuleni, kukusanya/ kununua taarifa hizo za wanafunzi na kuwauzia wao hapo chuoni kupit8a Mkuu wa chuo, kisha wao huwatumia wazazi wa watoto jumbe za kiwajulisha uwepo wa kozi ili kuwaaloka wakasome hapo.

Jambo hili ni baya sana ambalo linaonekana kufanywa na Shule ya Sekondari Ndono kuuza taarifa nyeti za wanafunzi wao na namba za simu za wazazi wao.

Jambo hili linakiuka sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi za watu.

Na Tabora boys pia ni kesi hiyo hiyo. Hiki chuo kichunguzwe pamoja na shule tajwa. Wanatibua sana Wazazi huku mitaani. Ni wapumb*vu sana.
 
kuna mfumo unatumika kupata majina na namba zao kwa wanafunzi walio maliza form four. ukinipa jina la shule uliyo maliza pamoja na mwaka nitakupatia majina ya uliohitimu nao pamoja nawewe ukiwemo. mbona ni kitu cha kawaida.
huo mfumo nani castodian? Anaruhusiwa kuzitumia hizo taarifa katika mazingira yapi? Haya ndio mambo yanayohojiwa mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
huo mfumo nani castodian? Anaruhusiwa kuzitumia hizo taarifa katika mazingira yapi? Haya ndio mambo yanayohojiwa mkuu.
Kwani ndugu, ulipopewa jina Kuna conditions ziliwekwa za mazingira yapi na watu gani wanaruhusiwa kutumia jina lako?
Uliposajili namba yako ya simu, Kuna conditions ziliwekwa za mazingira yapi na watu gani wanaruhusiwa kutumia namba yako ya simu?
Ulipoingia shule, ukapewa namba ya mtihani, Kuna conditions ziliwekwa za mazingira yapi na watu gani wanaruhusiwa kutumia namba yako ya mtihani?
Kama hizo conditions hazijawekwa, unaanzaje kulaumu taasisi zinazotumia majina na namba za simu kutangaza nafasi za masomo?
Andaa conditions kwanza, nenda kwa mwanadheria, then toa matangazo, Kisha Anza kulaumu na kuwachkulia hatua wale watakaotumia jina na namba zako kinyume na matakwa yako

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Watanzania mtaacha kutapeliwa mpaka lini?
Mbona kila siku tunatumiwa sms kuwa umeshinda hujiulizi namba wamepata wapi.
Kama umetumiwa sms hiyo achana nao kama hukiamini chuo utatapeliwa.
 
Shida sio kuuziwa taarifa. Hawa jamaa wazinguaji kinoma..., matapeli balaa. Kuna kingine kipo singida kinaendeshwa na dada ake na mwenye chuo hiki. Kinaitwa city college wamepangisha pale jengo la walimu(cwt) mitaa ya mwenge. Ni matapeli kinoma. Wanakupokea ukitaka kusoma kozi yeyote hata kama haipo hapo(haijasailiwa), we lipa tu pesa Ako ndo utajua hujui.

Wanaokota walimu na wanatapeli. Hakuna mwalimu alipita pale bila kutapeliwa. Mwanafunzi anawaza kwenda pale akasema nataka nisome umeme. Wanaitikia sawa kozi ipo na inafundishwa wakati hamna chochote. we lipa tu pesa Ako ndo utajua. Watakuzungusha wee... Mwisho wa siku watakushauri ubadilishe kozi. Wanazulumu mpaka wamama ntilie.

Wanaweza wakaleta mwanafunzi wakamuungashia kwa mama ntilie wakati huo mwanafunzi amelipa ada. Wanampanga ma ntilie mhudumie dogo tutakulipa Hela Ako. Akikubali imekisha hyo.. hawatamlipa. Wanaweza kuwandanya wanafunzi.., kozi imesajiliwa mpaka level 3 mfano Kozi ya ICT kumbe kozi imesajiliwa level 2. Hawa jamaa ni matapeli ogopa.
Hiki chuo Cha Tabora polytechnic (T.P.C) a.k.a Musoma utalii,hawajaacha utapeli,juzi Kuna mwanafunzi Mmoja ametapeliwa 380,000/= na mwalimu Mmoja anaitwa Kizwalo,mbaya zaidi inaonesha baadhi ya viongozi unashiriki huu utapeli,Yaani kile chuo ni utapeli kwa kwenda mbele.
 
Wazazi wa Wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne 2023 wamepokea ujumbe mfupi wenye taarifa halisi za Watoto kutoka Chuo cha Tabora Polytechnic kilichopo Tabora Mjini.

Ujumbe huo ulisomeka kuwa,
Mkuu wa chuo cha Tabora Polytechnic kilichopo Tabora Mjini anakutangazia nafasi za masomo mzazi wa ......... Mwenye namba ........2023 katika kozi zifuatazo( kozi zimeorodheshwa kulingana na mchepuo aliofaulu mtoto husika kama ni Art au Science)
View attachment 2946641
Mara baada ya mmoja wa watu wangu wa karibu kupata ujumbe huo, alishtuka kwani hajawahi kuwasiliana na hicho chuo kwa namna yoyote kwamba watakuwa wamepata namba za simu kutoka kwake mwenyewe.

Ndipo alipochukua hatua za kumtafuta mzazi wa aliyekuwa rafiki wa mwanaye shuleni hapo ili kuona kama naye katumia ujumbe huo. Mzazi huyo alithibitisha kuwa naye katumiwa ujumbe kama huo kwa jina la Mwanaye.

Akaamua kupiga namba inayoonekana kwenye ujumbe ili ahoji wamepata wapi namba ya simu ya mzazi wa mtoto husika, majina matatu na namba sahihi ya mtihani ya mtoto huyo.

Ndipo alipojibiwa kuwa kuna mawakala ambao huzunguka mashuleni, kukusanya/ kununua taarifa hizo za wanafunzi na kuwauzia wao hapo chuoni kupit8a Mkuu wa chuo, kisha wao huwatumia wazazi wa watoto jumbe za kiwajulisha uwepo wa kozi ili kuwaaloka wakasome hapo.

Jambo hili ni baya sana ambalo linaonekana kufanywa na Shule ya Sekondari Ndono kuuza taarifa nyeti za wanafunzi wao na namba za simu za wazazi wao.

Jambo hili linakiuka sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi za watu.

Kuna vyuo vya afya vya binafsi viko juu ya sheria.Pesa inawaweka juu ya sheria na hawagusiki.
Mfano wa vyuo hivyo ni hicho ulichotaja,na vingine vimejaza mabango nchi nzima.
Vyuo vinawatu wanasaka mitihani kwa udi na uvumba ili waendelee kuwa na idadi kubwa darasa lenye zaidi ya watu 300 huku idadi ya wakufunzi ikiwa ni ndogo.
Hivi vyuo vimeshakuwa sugu kama chama tawala.
 
Watanzania mtaacha kutapeliwa mpaka lini?
Mbona kila siku tunatumiwa sms kuwa umeshinda hujiulizi namba wamepata wapi.
Kama umetumiwa sms hiyo achana nao kama hukiamini chuo utatapeliwa.
Mm siku hz wale wa tuma kwenye namba hii narudisha sms ya tusi tu, nshachoka mie.
 
Kwani ndugu, ulipopewa jina Kuna conditions ziliwekwa za mazingira yapi na watu gani wanaruhusiwa kutumia jina lako?
Uliposajili namba yako ya simu, Kuna conditions ziliwekwa za mazingira yapi na watu gani wanaruhusiwa kutumia namba yako ya simu?
Ulipoingia shule, ukapewa namba ya mtihani, Kuna conditions ziliwekwa za mazingira yapi na watu gani wanaruhusiwa kutumia namba yako ya mtihani?
Kama hizo conditions hazijawekwa, unaanzaje kulaumu taasisi zinazotumia majina na namba za simu kutangaza nafasi za masomo?
Andaa conditions kwanza, nenda kwa mwanadheria, then toa matangazo, Kisha Anza kulaumu na kuwachkulia hatua wale watakaotumia jina na namba zako kinyume na matakwa yako

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
TAPEL JINGINE HLI HAPA
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Back
Top Bottom