Spika Ndugai: Mbowe alikuwa Ulaya sasa katumwa na watu wake anapotosha kuhusu ripoti ya CAG

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Spika wa Bunge Job Ndugai, amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya CAG na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne, kwa kuwa inapotoshwa huku akimtaja Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuwa mmoja wapo

Ndugai.jpg

Spika wa Bunge Job Ndugai amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya Mdhibiti na Mkuguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne badala ya mkutano wa tano, kwa kuwa inapotoshwa.

Akizungumza leo Jumatatu Aprili 12 2021, Ndugai huku akimtaja Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amedai kuwepo upotoshaji wa ripoti hiyo.

Kauli ya Spika imekuja siku moja baada ya Mbowe kuhutubia kupitia mitandao ya jamii, ambapo pamoja na mambo mengine alilituhumu Bunge kwa vitendo vya rushwa.

“Watu wanabeba tu mabilioni yameibiwa sasa huyo rafiki yangu Freeman Mbowe alikuwa Ulaya huko sasa katumwa na watu wake huko anapotosha mambo,” amesema.

Amesema sio watu wengi wenye uelewa wa kuchambua taarifa za kihasibu na hivyo kunaweza kukawa na ujenzi wa kituo cha afya wa Sh 500milioni lakini Sh 499milioni zimetumika vizuri kabisa.

Hata hivyo, amesema lakini kati ya fedha hizo Sh1milioni ikikosa kiambatanisho fulani ni kawaida wakaguzi wanahoji fungu zima la Sh 500milioni.

Amesema kwa hiyo unaposoma mtaani unaona sh 500 zimeibwa lakini kumbe pale ni Sh milioni moja ndio hazina risiti.

Amesema kamati hizo zitaanza mapema kuchambua ripoti hizo ili waangalie ratiba yao na kuwaelimisha watu kuhusiana na ripoti ya CAG ambayo ni taarifa nzuri lakini baadhi ya watu wanabeba na kupotosha tu.

Mwananchi
 
Dodoma. Spika wa Bunge Job Ndugai amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya Mdhibiti na Mkuguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne badala ya mkutano wa tano, kwa kuwa inapotoshwa.

Akizungumza leo Jumatatu Aprili 12 2021, Ndugai huku akimtaja Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amedai kuwepo upotoshaji wa ripoti hiyo.

Kauli ya Spika imekuja siku moja baada ya Mbowe kuhutubia kupitia mitandao ya jamii, ambapo pamoja na mambo mengine alilituhumu Bunge kwa vitendo vya rushwa.

“Watu wanabeba tu mabilioni yameibiwa sasa huyo rafiki yangu Freeman Mbowe alikuwa Ulaya huko sasa katumwa na watu wake huko anapotosha mambo,” amesema.

Amesema sio watu wengi wenye uelewa wa kuchambua taarifa za kihasibu na hivyo kunaweza kukawa na ujenzi wa kituo cha afya wa Sh 500milioni lakini Sh 499milioni zimetumika vizuri kabisa.

Hata hivyo, amesema lakini kati ya fedha hizo Sh1milioni ikikosa kiambatanisho fulani ni kawaida wakaguzi wanahoji fungu zima la Sh 500milioni.

Amesema kwa hiyo unaposoma mtaani unaona sh 500 zimeibwa lakini kumbe pale ni Sh milioni moja ndio hazina risiti.

Amesema kamati hizo zitaanza mapema kuchambua ripoti hizo ili waangalie ratiba yao na kuwaelimisha watu kuhusiana na ripoti ya CAG ambayo ni taarifa nzuri lakini baadhi ya watu wanabeba na kupotosha tu.
 
Ndugai yuko sahihi.

Mbowe amechambuliwa huko ulaya taarifa ya CAG akameza anakuja kujiropokea hapa Bongo.

Kwa tunaojua mambo ya kihasibu hatushangai na hua hatukurupukii taarifa ya CAG maana mkaguzi asipoelewa kitu basi hukibeba kama kilivyo kwenye report yake.

Ndio maana cases nyingi ambazo hua CAG anataja, watuhumiwa wakiitwa kwenye kamati za Bunge hua majibu yanatolewa na baadae zinaonekana hazina msingi.

Sasa Mbowe ametafsiriwa report na wazungu huko anakuja kujiropokea tu hapa.
 
Sasa amejuaje kama inapotoshwa wakati yeye hajaisoma, hajui chochote na hao wabunge wanaounda LAAC na PAC hawajaichambua?

Ndugai ni Speaker wa HOVYO sana kuwahi kutokea katika historia ya Bunge letu tukufu. Ameiharibu sana taswira ya Bunge na sasa kila zuzu yeyote anatamani kuingia kule
 
Ripoti ipo wazi inajitosheleza watu wengi wana ufahamu wa kusoma,kuielewa na siyo mpk hizo kamati ndo zitutafsirie.....Kwani imetumika lugha ya kiispaniola????.......Tumeshajua tumepigwa mchana kweupe.
mangi hizo ni audit queries na opinions sio final conclussion.
 
Ukisikia yowe ujue imepiga panyewe, hapa ndio ninapomkubali Mbowe huwa anapiga panyewe.

Ila kwa kweli Tanzania imepatikana spika wa bunge hana tofauti na Polepole wa Lumumba.

Halafu na rais ndio alikua tapeli na mwizi.. Asante Mungu kutupumguzia hizi ghasia.
 
Back
Top Bottom