Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

Roma aliendesha gari kama kichaa , uzuri ni kwamba barabarani hakukuwa na magari mengi , alitumia dakika chache tu kufika ndani ya Kibaha na kukunja kushoto barabara ya vumbi kama vile alikuwa akielekea Bagamoyo nyuma ya kiwanda cha kuunganisha magari na akasonga mbele.

Alikuja kusimamisha gari yake mita mia moja kutoka kilipokuwa kilipo kiwanda hiki cha kuunganisha magari na kisha alisimama huku akiangalia eneo ambalo watu hao walimwelekeza , bado hakuwa akiona nyumba yoyote hivyo alishindwa kusogea mbele, baada ya kusimamisha gari kwa dakika kama kumi hivi simu yake ilianza kuita.

“Mr Ramon tumehakikisha umekuja peke yako , unaweza kusogea mbele mita mia nne kutoka ulipo kisha kunja kulia utaona nyumba yenye geti jeusi na simamisha gari yako hapo”.

Roma bila ya kujiuliza , aliendesha gari na baada ya kusogea umbali unaotakiwa kama alivyokuwa amepewa maagizo , aliona barabara ya vumbi iliokuwa ikikunja kulia , alichukua Barbara hio na kusimamisha gari mara baada ya kuona ukuta mrefu ambao ulifanya usiweze kuona ndani ya ukuta huo ndani kuna nini , baada ya kushuka tu kwenye gari ni kama walikuwa wanamsubiri kwani kijana mmoja mwenye koti jeusi alievalia kofia ya chepelu alimyooshea Roma bastora na kumuingiza ndani ya jumba hili.

Roma aligundua kuwa hiii sio nyumba bali ni Godauni , kwani ndani hapa kulikuwa na magari yale ya kuchimbia barabara yakiwa katika hali ya uchakavu na baadhi ya mavyuma mengi makachakavu.

Walimwigiza kwenye jumba lililokuwa mbele ,upande wa kushoto huku vijana watatu wakionekana ndani ya eneo hilo wawili walikuwa na siraha za moto na mmoja aliekuwa anavuta sigara ndio hakuwa na siraha lakini alionekana kuwa ndio kiongozi , Roma alianza kuangalia mmoja mmoja kwa hasira.

“Edna yuko wapi ?”

“Tuliza wenge wewe fala”Aliongea huku akimsukumia ndani ya chumba na hapo ndipo alipomuaona Edna akiwa amefungwa kwenye kiti , kitendo cha Edna kumuona Roma ni kama vile hakukitarajia, Roma alimwangalia namna mwanamke huyo alivyokuwa ametawaliwa na machozi usoni na kumuonea huruma, lakini baada ya Roma kugeuka upande wa pili aliweza kumuona mtu mwingine na huyu alikuwa ni baba yake Edna wote wakiwa wamefungwa.

Mbele ya Edna kulikuwa na kijisturi ambacho kilikuwa na makaratasi na karamu , huku pembeni kuna jambazi mmoja aliekuwa amekaa kwenye matofari matatu yaliokuwa yamepangwa kwa ustadi.

Roma hakuweza kutambua sura hata moja , alisukumiwa na kwenda kufungwa karibu na baba yake Edna miguuni na mikononi kwenye kiti.

“Mnataka nini kwa Edna , nishakuja mfungueni sasa”

“Tushakuambia tuliza wenge, wewe hata haunathamani kwetu , umeitwa hapa kwa ajili ya kufa, na Edna ameletwa hapa kwa mpango mwingine”Roma hakuelewa kinacho endelea lakini alikuja kuelewa baada ya kuona bwana mmoja hivi aliekuwa amekalia tofali alikuwa akimlazimisha Edna kutia saini kwenye makaratasi yaliokuwa yapo mbele yake.

“Mrembo acha kutupotezea muda tia saini umuokoe baba yako , nitahesabu mpaka nne maana umetusumbua sana , usipo fanya kile tunachotaka hii itamuhusu baba yako”Aliongea bwana huyu huku akionekana hana hasira hata kidogo.

Edna alimwangalia baba yake na kisha kugeuza macho kwa Roma na kisha kuziangalia karatasi zilizokuwa mbele yake , karatasi zilizokuwa zikimtaka kutia saini ili kuruhusu asilimia sitini ya hisa za kampuni yake kwenda kwa mtu mwingine.

“Hapana sipo tayari , nitailinda kampuni hata kwa kifo”

“Mojaaa.. , mbilii , tatuu.. nne”.

“Paaah!!”Ulilia mlio wa risasi uliomfanya Edna afumbe macho , kwani hakuwa tayari kushuhudia baba yake akipigwa risasi, jambo hili hata kwa Roma lilimshangaza sana , hakuamini kama Edna yupo tayari kumuona baba yake akifa ili tu alinde kampuni.

“Mamaa... isiiiii... nakufaa Edna ”Ilikuwa ni sauti ya mauimivu iliomtoka mzee Adebayo , kwani alikuwa amepigwa risasi ya paja na damu zilikuwa zikimtiririka.

“Risasi itakayofutia itatua kwenye kichwa cha baba yako , nadhani unatuona kama tunatania , weka sahihi yako pumbavuu”

“Edna wape wanachotaka wata.. niua baba yak..o”

Edna alimwangalia baba yake kwa uchungu huku akitoa machozi.

“Nisamehe baba sipo tayari kufanya kama wanavyotaka , watuue tu wote”Aliongea Edna na kuwafanya majambazi hawa kushangaa lakini sio majambazi tu hata Roma alikuwa akishangaa.

Roma japo yeye alionekana kufungwa lakini ni kama amepumzika kwani hakuwa na wasiwasi kabisa.

“ Kama ndio unavyotaka basi hatuna namna tutafanya kile ambacho unataka , na nakuambia baba yakoo atakufa lakini pia kusaini utasaini”Aliongea jambazi kiongozi na kisha alinyanyua bastora yake na kumlenga baba yake Edna , huku Edna akifumba kwa mara nyingine macho kwani hakuwa tayari kushuhudia kifo cha baba yake.

“Nitahesabu upya mpaka tatu , kama utashindwa kutia saini hizo karatasi basi sitakuwa na jinsi kukupa kile unachotaka.. moja , mbili ….. , tatu”Edna hakutia saini na jambazi liingiza kidole kwenye Triga..

“Stop nipo tayari kusaini ,.. nitasaini muacheni baba yangu”Aliongea Edna na kuwafanya majambazi hawa watabasamu na jambazi lile kiongozi lilimpa ishara jamaa aliekuwa karibu na Edna amsogezee karatasi.

Edna aliangalia karatasi zile huku akitoa machozi , alichukua kalamu huku akiwa anatetemeka mno , hakuamini anakwenda kuachia hisa asilimia Sitini na kubakiwa na asiliamia therethini tu za umiliki ndani ya kampuni yaie kitendo ambacho kitamfanya kukosa kauli ya mwisho ndani ya kampuni.

“Hapana ngoja nimuokoe baba , pesa zinatafutwa tu na hata mama atanielewa , huyu ni baba yangu siwezi kumuangalia akifa mbele yake sitokuwa na furaha”Aliwaza Edna

“Fanya haraka”Aliongea jambazi kiongozi na Edna aliangalia karatasi zile na kisha kama mtu alieghaili aliweka kalamu chini na kisha akanyanyua uso wake na kumwangalia Roma kwa huzuni.

“Kabla sijasaini nataka mnihakikishie jambo moja”Aliongea Edna

“Ongea”

“Mtamuachia mume wangu akiwa hai maana hahusiki kwa chochote katika hili”Wale majambazi waliangaliana na kisha kiongozi alitoa simu na kusogea pembeni , alionekana hakuwa na maamuzi ya mwisho juu ya ombi la Edna.

Roma alishangazwa na maamuzi ya Edna na kujikuta kuna kitu flani kipya kiliingia ndani ya moyo wake juu ya mke wake huyu wa mkataba.

“Bosi anataka tumuahidi Roma awe huru”

“Acheni upumbavu , mdanganyeni tu akishasaini mpigeni Roma risasi sitaki huyo mwanaharamu aishi tumieni akili”Ilisikika sauti upande wa pili.

“Sawa bosi”

Jambazi kiongozi alirudi na kumwambia Edna kuwa wapo tayari kutii ombi lake , lakini kwa Edna hakuwa mpumbavu alikuwa anajua kabisa watu hao watamuua Roma akishafanya kile wanachotaka.

“Kama mpo tayari nataka mumfungue yeye na baba yangu waondoke na mimi ndipo nitasaini.. siwezi kuwaamini”Aliongea na wakaangaliana lakini awamu hii kiongozi aliona afanye maamuzi bila ya kumshirikisha bosi wake, alimpa ishara jamaa aliekuwa ameshikilia bastora amfungue miguu Roma na baba yake Edna kisha awatoe nje.

“Wakishafika mbali na nikithibitisha wako mbali nitasaini Roma naomba umepeleke baba hospitalini ukitoka”

“Sawa Mke wangu nitafanya hivyo na Asante kwa kunipenda Mumeo”Huku akimkonyeza

Baada ya majambazi kukubaliana na matakwa ya Edna jambazi mmoja aliekuwa na bastora alimsindikiza baba yake Edna na Roma nje , baba yake Edna alikuwa aivuja damu japo sio sana , alikuwa akijikaza kwa maumivu.

Majambazi waliobaki baada ya kutoka walisubiria simu ya Roma iwapigie ili kumthibitishia Edna kama ashafika mbali na yuko salama lakini walikuja kushituka baada ya mwili kutua ndani ya chumba hiki walichokuwepo kwa nguvu kiasi kwamba kutoa mlio , baada ya wao wote kuangalia kwa umakini ndipo walipogundua ni mwili wa mwenzao.

“Kioba!”Aliiita jambazi mkuu kwa hamaki na ile anainua macho alimuona Roma akiingia , tena awamu hii alikuwa akijiamini kiasi kwamba utadhani yeye ndio aliewaagiza hao vijana, Mwenzao alikuwa tayari ashakufa tena kifo chake kilionekana kuwa cha kikatili mno kwani shingo ilikuwa imelegea sana.

“Katika maisha yangu nina sheriia tatu ambazo nimeziweka kwa mtu yoyote kutozivuka , moja sipendi kutishiwa Amani , pili sipendi watu wanaotumia ngao watu wengine kutimiza mambo yao, tatu kwangu neno Onyo ni mara moja ukirudia ni kifo na nyie makossa yote mnayo”Aliongea Roma kwa sauti ya upole kabisa na hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo na isitoshe hakuwa na siraha ila jambazi mmoja alikuwa na siraha.

“Mpige risasi unasubiri nini?”Aliongea jambazi yule kwa pupa na yule mwingine akainua Risasi ili kumpiga Roma , lakini kufumba macho na kufumbua , Roma tayari alikuwa ashamfikia na kilichosikika ilikuwa ni

“Crak’

“Mamaaa.. nakufaaa”

Ulikuwa mlio wa mvunjiko wa mfupa wa mkono uliokuwa umeshika Bastora lakini Roma hakuishia hapo tu alimshika shingo na kichwa na kukizungusha na mifupa yote ya shingoni ikakatika huku kichwa kikigeukia mgongo kitendo ambacho kilimfanya hadi Edna afumbe macho , kwani alishuhuidia Roma akiua kikatili mno mambo ambayo hakuwahi kuwaza atayaona laivu.

Jambazi mwingine baada ya kuona mambo sio kama alivyodhania , alikimbilia chuma na kulinyanyua huku akimtishia nalo Roma , na kwa Roma wala hakujali kwani alizidi kumsogelea huku jambazi hili lilikianza kutetemeka , kwani hakuwahi kukutana na aina ya mtu ambaye alikuwa akiua kama anaua kuku tema kikatili kwa namna alivyoshuhudia.

“Huyu sio mtu , ni shetani inabidi nipate upenyo wa kukimbia”Liliwwaza Jambazi hili

Jambazi alimrushia Roma lile Chuma lakini Roma alilikwepa halafu akalidaka na kulivuta kwa nguvu kitedo ambacho Jambazi alivutwa nalo kwani alikuwa amelishikilia kwa nguvu na baada ya kumsogelea Roma alipigwa teke la mguuni lililomfanya kuhisi maumivu makali mno na kutoa ukulele.

“Leo utaniambia bosi wako ni nani, aliekutuma kumteka mke wangu”Aliongea Roma huku macho yake yakionekana sio ya kawaida hata sauti yake pia sio ile iliokuwa ikizoeleka , aliongea kama roboti.

Alimshika yule jambazi na kama vile anavunja paja la kuku alimshika mguu kwenye Goti na kulipindisha kiasi ambacho mguu ule ulitoa sauti kubwa ya viungio kupishana na mguu ule kugeukia mbele.

“Mamaaaa.. nakufaaa….”Ulikuwa ni ukululele wa aina yake

“Sema nani kawatuma la sivyo naendelea na mguu wa pili?”

“Nasema .. nasemaa”

“Okey ! nadhani uanze kuaongea sasa”

“Alietutuma ni Jose na Baba yake Edna”.Roma ni kama hakuwa ameelewa vizuri .

“Ongea vizuri ueleweke au unataka niendelee..”

“Huyu mzee eliekuwepo hapa na Jamaa anaefahamika kwa ina la Jose ndio alietuagiza , ila huyo Jose anasema pia ana bosi wake alietoa kazi hio”Baada ya kuongea vile lile Jamaa ni kama Edna hakuwa akimuamini , alinyanyua karatasi zilizokuwa mbele yake na kuzisoma na alijikuta akiishiwa nguvu mara baada ya kuona karatasi hizo zilikuwa na jina la baba yake , inamaana muda wote alitakiwa kusaini ili kuruhusu hisa ziende kwa baba yake.

Roma aliona maelezo hayo yanajitosheleza , alichukua lile chuma na bila hata ya huruma , alimchoma nalo Shingoni kiasi cha kufanya Damu imrukie na kumchafua kwenye nguo mpaka usoni Roma aligusa ile damu usoni na kisha kuinusa.

“Mwamba ana damu inanuka vibaya huyu” Aliwaza

Na huo ukawa ndio mwisho wa majambazi yote matatu yaliokufa kikatili mno na kwa mtu yoyote angeshuhudia maiti hizo hakika angeishia kusema Roma ni Shetani..

Lakini wakati anamaliza mara mlango ulisukumwa na mtu anaechehemea huku akiwa na bastora mkononi na huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni baba yake Edna.

“Edna Saini hizo karatasi kabla sijaachia Risasi”Aliongea mzee huyu huku akionekana ni mwenye kuvumilia maumivu kwani hadi mikono ilikuwa ikimtetemeaka.

“Baba .. siamini kama unaweza kwenda mbali kiasi hiki….”

“Kimya mpumbavu wewe mimii sio baba yako , saini karatasi hizo kabla sijakutandika risasi ya kichwa na huyu muaaji mwenzako hapa”Aliongea huku Roma akimwangalia mzee huyu na kisha akatabasamu.

“Mzee bora ungekimbia baada ya mimi kukuacha kule nje , ila nimekupa nafasi ili hali najua ulikuwa kwenye huu mpango ila ukajileta mwenywe hivyo sina budi ya kukupeleka kuzimu”Aliongea Roma na kumfanya Edna ashangae kuona Roma alikuwa ashajua kuwa baba yake alikuwa akihusika , alishangazwa na uwezo wa Roma na kujiuliza maswali mengi.

Baba yake Edna alimwangalia Roma na kisha akaangalia namna Roma alivyoweka mguu wake kwenye kichwa cha jambazi linalovuja damu shingoni na kutikisika kama kuku bila wasiwasi kama vile kaweka mguu kwenye tofali , mzee huyu alijikuta mwili wake ukipatwa na ubaridi ambao hakuelewa alijiuliza huyu matu ni binadamu au mnyama.

“Baba naomba uweke hio siraha chini nitaacha hili lipite ,, licha ya kwamba sitokuja kusahau”

“Tulia Edna .. mmeninyanyasa sana wewe na mama yako kiasi cha kunifanya nionekane mwanaume bwege ndani ya macho ya walimwengu , leo nalipiza maumivu mlionisababishia kwa miaka mingi”Aliongea huyu mzee na hakuwaza tena alivuta triga yake kwa dhumuni la kuua , lakini kabla hajatimiza azima yake alijikuta akipigwa na chuma mikononi na Siraha ile kwenda chini.

“Kitendo cha kurudi hapa ndani umejitafutia kifo chako”Aliongea Roma na kumpiga teke sehemu iliokuwa na Jeraha na kumfanya mzee huyu apige yowe , lakini Roma hakuishia hapo tu , alimkanyaga kwenye kigoti cha mguu na kusababisha mfupa wa mguu uvunjike , yote hayo aliokuwa akiyafanya hakumuwazia Edna alikuwa kwenye hali gani.

Roma alimvunja mzee Adebayo miguu yote na hapo ndipo alipomgeukia Edna ambaye muda wote alikuwa kwenye mshituko kiasi kwamba hakuwa hata akiongea kwani alikua ni kama mtu aliekuwa amezimia huku anaangalia , ile Roma anamfungua Kamba Edna alizimia palepale.

Baada ya lisaa limoja Roma alifika Kigamboni na kumtoa Edna kwenye gari na kuingia nae ndani huku Bi Wema akiwa kwenye mshangao kwani alimuona Wema akiwa na damu mwili mzima.

“Nini kimetokea Roma?”Aliuliza bibi huyu huku akionekana ni mwenye wasiwasi.

“Kuna wapuuzi wanajifanya wajanja , wamemteka mke wangu na mimi nimelipiza kwa kuwaua”Bi Wema macho yalimtoka.

“Umesema umewaua?”

“Ndio wamekufa , mwingine ni baba yake Edna nimemvunja miguu ili akampe taarifa anaeshirikiana nae”Huku akimpandisha Edna juu kweye chumba chake akifuatiwa na Bi Wema .

Roma ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuingia kwenye chumba hiki cha mke wake , kilikuwa ni chumba kikubwa kilichokuwa kinapendeza sana kuitwa chumba cha mwanamke CEO mkubwa ndani ya ulimwengu wa wafanya biashara duniani.

“Bibi atazinduka huyu baada ya muda alikuwa kwenye mshituko”

“Unajuaje Roma wakati mtu yupo mahututi tumepeleke hospitalini”.

“Haina haja Bi Wema, Atazinduka”Aliongea Roma na kisha akatoka akimuacha bibi huyu kwenye mawazo , hakuweza kujua Roma ni mtu wa namna gani kwani alionekana kujiamini mno.

Baada ya kutoka ndani ya chumba chake aliingia bafuni na kuoga na baada ya kumaliza alichukua simu yake na kumpigia Doris na kumwambia ashamuokoa mke wake na yeye yuko salama baada ya kukata simu alitafuta namba ya Rose.

****

Ilikuwa ni muda wa usiku saa tisa kamili ndani ya chumba kikubwa anacholala mheshimiwa Rais Senga , akiwa amepumzika na mke wake mara simu yake kubwa ya I phone ilianza kuita mfuliulizo kiasi cha kumuamsha na kushangaa ni nani anampigia muda huo kwani sio kawaida yake , na mara nyingi akipokea simu usiku sana huwa ni za dharula na kuna tatizo kubwa ambalo wasaidizi wake wameshindwa kulitolea maamuzi, aliangalia jina la mpigaji na kujikuta usingizi ukimuishia jina kwenye kioo lilionekana limeandikwa Senior(Mkubwa kazini).

“Mheshimiwa kuna nini? , maana sio kawaida kunipigia muda huu”.

“Senga ulinihakikisha kuwa Edna atakuwa salama ndani ya taifa lako , lakini nini hiki kinaendelea ndani ya nchi yako”

“Naomba upunguze jazba Senior nini tatizo?”

“Vijana wangu wamenitumia ripoti kwamba Edna alitekwa”

“Nini..!! , unahakika na hio taarifa Senior?”

“Nina uhakika na vijana wangu wangu Senga , nimewapa kazi hio moja tu ya kumlinda Edna kwa siri”

“Vipi hali ya Edna kwa sasa??”.

“Ni bahati kwamba sasa hivi ana mume , kwa hilo namsifia sana , yule mtoto ana akili sana kachagua mume bora”

“Unamaanisha Roma ni mume bora kwa Edna?”.

“Ndio Senga mchunge sana huyo kijana sio mtu wa mchezo mchezo na ni mtu katili kuwahi kutokea katika huu ulimwengu hakikisha unakuwa upande mzuri na yeye kukusaidia kwenye mpango wako, mimi yangu ni hayo tu na nikwambie Senga haupo makini kabisa Edna anatekwa huna habari , mimi niliopo ng`ambo ya pili ya nchi yako nimepata taarifa kabla yako , nimekasirishwa sana na jambo hili ,Usiku mwema nadhanni tutaongea Zaidi juu ya mipano yetu siku tukionana”Aliongea Senior na kisha kukata simu.

“Who is this Guy?”Alijiuliza mheshimiwa Senga huku akiwa ni mwenye kushangaa Senior anamfahamu Roma.

“ My guess was right he is not normal , there is more hidden info about him , I have to dive deep to discover more details”

ITAENDELEA JUMATATU WADAU
 
SURA YA KUMI NA MBILI

Ilikuwa ni muda wa asubuhi ya saa mbili Roma alionekana akiendesha gari kwa spidi akielekea maeneo ya Mbagala , baada ya kuupiga mwendo kwa madakika kadhaa alikuwa mbele kabisa ya nyumba ya Rose , alipiga honi na mlinzi alifungua na Roma akaingia ndani na kwenda kugesha gari , baada ya kutoka aliingia ndani ya jumba hili ambalo lilikuwa kimya mno kwani Rose alikuwa akiishi yeye peke yake.

“Bebi karibu”Aliongea Rose huku akiwa ni mwenye mshangao mkubwa sana kumuona Roma asubuhi asubuhi , alihisi kuna tatizo.

“Asante , nimekuja nina mazungumzo na wewwe ya muhimu sana”Aliongea Roma na kumfanya Rose ashangae huku akivua aproni na kuiweka kwenye sofa kwani alikuwa jikoni na alionekana alikuwa akiandaa kifungua kinywa.

“Kuna nini mpenzi ,kuna kilichotokea?”.

Roma alitoa cheni flani hivi yenye kidani cha kichwa cha Tembo na kumrushia Rose na akakiokota.

“Umeitoa wapi hii Roma? .. hiki ni kidani kinachowakilisha kundi langu”

“Vijana wako jana wamehusika kumteka mke wangu na nimewaua wote”Aliongea Roma na kumfanya Rose ashangae.

“Usijifanye hujui hili jambo Rose ?”

“Bebi Calm Down sijui chochote juu ya hili swala na sijatoa ruhusa yoyote , itakuwa ni Ramso”

“Kama hujui swala kama hili naamini hauko makini na kundi lako na wanafanya mambo ya kiholela kuhatarisha maisha ya jamii ,Rose sipo radhi kuona mtu yoyote ndani ya familia yangu anaguswa na mtu yoyote yule na nipo tayari kuua , hivyo naomba uwaweke vijana wako under control”Aliongea Roma na kisha kukaa chini ya sofa.

“Baby Am sorry”.

“Usijali nishakusamehe kipenzi , ila hakikisha maswala kama haya hayajitokezi hususani kwenye familia yangu”

Roma aliandaliwa chai na mchepuko wake Rose na baada ya kushiba waliagana na yeye akaondoka huku akielekea kazini.

Baada ya Roma kuondoka Rose alijiandaa na kutoka kisha akaelekea ofisni kwake.

“Zonga mpigie simu Ramso sasa hivi” afike ofisini kwangu”

“Sawa madam”

Baada ya madakika kadhaa Ramso aliingia na alionekana kuwa na wasiwasi sana kwani macho yake yalionesha, huku jasho likiwa linamtoka,Rose macho yalikuwa yamebadilika hakuwa yule mrembo anaeonekana kuwa mpole ila huyu alionekana kuwa katili.

Aliinuka kwenye kiti chake na kisha alimsogelea Ramso huku mkononi akiwa na kisu kikali kinachowakawaka kwa kung`aa ,, kisu aina ya Sime kama zile za wamasai huku kikiwa na alama ya Tembo katikati.

Ilikuwa ni kitendo cha fasta sana Ramso alitoa mguno wa maumivu baada ya kuchomwa na lile bisu kwenye paja la mguu wa kulia damu kuanza kutoka mfululizo .

“Hio ndio adhabu yako ya kufanya mambo bila ruhusa yangu”Aliongea Rose na akakivuta kisu kile na Ramso akadondoka chini kwa maumivu huku Rose akifuta damu kwenye kisu chake na kitambaa cheupe na kukitupia kwenye Dustbin.

“Anza kunieleza kwanzia mwanzo nini kilitokea”Aliongea huku akionekana sio mwenye utani hata kidogo.

“Nisamehe madam sitorudia tena”

“Achana na msamaha wako wa kipuuzi nieleze nini kilichotokea mpaka ukaenda kumgusa mke wa Roma”

Ramso alieleza kwa wasiwasi namna hali alivyofuatwa na marasta na kutaka atoe vijana kwa kazi alioiita maalumu kwa malipo makubwa.

“Nitamaa ya pesa tu boss nisamehe”.

“Ole wako lijirudie, siku nyingine hiki kisu kitaingia kwenye koo lako unaweza kwenda”

“Asante bosi kwa kunisamehe niakutii kwanzia sasa”Aliongea Ramso na kisha alitoka.

Rose alirudi kwenye tarakishi yake na kisha aliwasha na kuandika jina la Edna Kwenye mtandao wa Google na kisha maelezo kutoka Wikipedia yalitokea na kuanza kuyasoma.

“Edna Adebayoo mwanamke wa kwanza kutoka Tanzania na Afrika na kuingia kwenye Top 20 ya wanawake matajiri duniani , anatajwa kuwa mwanamke mwenye ushawishi mkubwa katika medani za kibiashara ndani ya Afrika,utajiri wa Edna ni Dola bilioni tano za kimarekani akishika nafasi ya kumi duniani kama matajiri wenye umri mdogo.”.

Rose alisoma taarifa hio na kujikuta akivuta pumzi , ndio alikuwa anafahamu sasa mke ambae Roma alikuwa amemuoa , aliona hana nafasi ya kuweza kushindana na mrembo Edna kwani alikuwa amemzidi kila kitu.

“Sina ninachomzidi , ninatakiwa kuridhika na nafasi niliokuwa nayo kwenye maisha ya Roma”Aliiwazia Rose huku akimuangalia mrembo Edna picha yake ikimuonesha kupokea tuzo kama moja ya CEO wanawake waliokuwa wamefanya vizuri katika maswala ya uongoz ndani ya kampuni.

“Nilijua tu Roma sio wa kawaida na ndiio maana nimetokea kumpenda , kwa jinsi alivyoniokoa kutoka kwa wale watu waliotumwa na baba yangu inanifikirisha mpaka sasa na kutaka kumjua Zaidi na Zaidi”

****

Wakati hayo yakiendelea upande wa hospitali ya Aghakani katika wodi ambayo ilikuwa ikitumika kuhudumia wagonjwa wenye hadhi ya juu yaani VIP alionekana Abuu akiingia ndani ya wodi hii huku akiwa ametangulizana na wasaidizi wake , bwana huyu alionekana hakuwa na furaha hata kidogo katika uso wake.

Baada ya kuingia ndani ya wodi aliokuwa amelazwa mzee Adebayo alimsalimia na kisha alikaaa kwenye kiti, huku mzee huyu akimwangalia kijana huyu kwa wasiwasi.

“Abu yule mtu ni katili sijawahi pata ona , inakuwaje binadamu anaua bila ya kuwa na wasiwasi hata kidogo”Aliongea mzee huyu kwa pupa.

Na baada ya kuona huyu mzee anaropoka aliwaruhusu walinzi wake na wahudumu watoke nje ili kubaki na mzee kwa ajili ya meongezi.

“Nini kimetokea mzee?”.

“Nikama unavyo ona Abu, yule kijana sio wa mchezo ni katili na muuaji amenifanya kuwa kilema wa maisha”Aliongea kwa hali ya simanzi.

“Hata kama ni mkatili vipi mzee , siwezi kuruhusu aendelea kuwa na Edna ilihali nimefight kwa ajili yake kwa muda mrefu”.

“Hata mimi sijakata tamaa Abuu , lazima yule mwanaharamu nimkamate na kumrudishia haya alionifanyia , ila nakutahadharisha tu kwamba yule kijana sio wa kawaida na tunapaswa kuwa makini”Abuu baada ya kuona hana la kufanya hapo ndani aliaga na kuondoka huku akiwa ni mwenye mawazo , alikuwa akiwaza ni namna gani ya kumdhibiti Roma , hata yeye alikuwa ashajua Roma hakuwa mtu wa kawaida , kwani alikumbuka siku aliyokwidwa na mwanaume huyo na kuning`inia hewani.

Wakati akiwa anatoka simu yake ilitoa mlio na kuonesha ilikuwa inaita , baada ya kuona jina la mpigaji alisimama na kisha akapokea.

“ Ndio baba!”

“Sawa nakuja”.

Abuu alliongeza mwendo na kisha alitoka ndani ya hospitali na ndani ya madakika kadhaa alikuwa ndani ya eneo walilokuwa wakiishi matajiri Masaki.

Baada ya kufika nje ya geti kubwa alifunguliwa na kuingiza gari ndani na kisha aliliegesha na kuingia sebule ndani ya jumba hili ambalo lilionekana lilikuwa la kifahari , baada ya kuingia mtu wa kwanza kumuona ni msichana mmoja mrembo aliekuwa amejiachia kihasara hasara akiwa na simu yake kubwa akionekana ni mwenye kuchat eneo la Sebuleni..

“Queen mzee yuko wapi?”

“Kwenye ofisi yake”Aliongea mwanadada huyu pasipo ya kugeuka , alionekna kuwa ni wale wanawake waliokuwa na maringo. Ila Abuu hakujali alipandisha ngazi kuelekea juu na ndani ya dakika chache alikuwa ndani ya ofisi iliokuwa kubwa , huku ikiwa na mavitabu mengi na makabrasha mbalimbali , huku mbele yake kukiwa na masofa na meza kubwa iliokuwa na tarakishi kubwa ya kampuni ya Apple , huku nyuma ya tarakishi hio akiwa mzee Alex

Baada ya mzee huyu kumuona Abuu amefika alitoka alipokuwa amekaa na kisha alimsogelea Alex na kisha alimramba kibao.

“Abuu mbona siku hizi umekuwa na uwezo mdogo wa kufikiria”

“Nisamehe baba , ni kwamba sikuwa na taarifa sahihi zinazomuhusu Roma na ndio maana mpango wangu umefeli”

“Acha sababu zako za kipuuzi , unajua ni vitisho gani napokea kutoka kwa The Doni , kwanini hili swala unalifanya lichikue muda mrefu hivi”Abuu hakuwa na majibu , alifokewa mno.

“Nakupa siku kumi kwanzia leo swala hili uwe ushalifanyia kazi , sitaki uzembe tena ukishindwa nakutoa kwenye nafasi yako”Aliongea mzee huyu kwa hasira na Abuu alitoka huku hasira juu ya Roma zikiongezeka Zaidi.

“Roma nitakuua kwa nmna yoyote ile hata kwa kukodi watu kutoka nje ya nchin siwezi kudhaliliska kiasi hiki” .

Baada ya kutoka ndani ya jumba hili moja kwa moja alipanga kwenda ofisini kuendelea na kazi huku akiendelea kufikiria namna ya kumdhibiti Roma na hatimae Edna , dakika chache alikuwa nje ya ofisi yake huku katibu muhtasi akimwangalia kwa wasiwasi.

“Kuna nini?”

“Mgeni”Alijibu na kufungua mlango na kisha akaingia na kumkuta mgeni akiwa amekaa kwenye kiti chake cha mzunguko akiwa hana habari, na mgeni huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Roma .

Abuu alimtazama Roma kwa hasira kali mbo na alitamani awe na siraha ammalize pale pale , lakini siraha hio hakuwa nayo.

“Nani kakuruhusu kuingia kwenye ofisi yangu bila ruhusa”

“Nimejiruhusu mwenyewe kwani vipi?”

“Kuwa na heshima kwenye ofisi za watu bwana , toka kwenye kiti changu”

“Ninatoka lakini leo nimekuja kukupa onyo kwa mara nyingine ya pili na unabahati sana kwani huwaga sitoagi onyo mara mbili , mimi sheria yangu ni onyo mara moja ukirudia ni kifo , sasa nakuambia hivi mimi Roma Ramoni ikitokea siku muda na saa yoyote umemsumbua Edna mke wangu, anza ktubu dhambi mapema angalau nikikupelekka kwa father God uingine peponi”Aliongea na kisha akanyanyuka na alivyomfikia Abuu alipiga teke lililomfanya abuu atoe kulele maana ni kama amegongwa na chuma.

“Hakikisha unatii hiki nilichokuambia siku ya leo , ukifanya ujinga nitahakikisha unafia kwenye hiko kiti”

Roma alifungua mlango na kisha kutoka nje lakini ile anakaribia mapokezi uso kwa uso na Edna aliekuwa anaonekana kama vile hakijatokea kitu jana yake kwani alikuwa na uso ule ule wa kikauzu na mwendo wa kujiamini akiwa ametangulizana na Sekretari wake.

“Huyu mwanamke ni ngangari bwana” Aliwaza Roma

SEHEMU YA KUMI NA TATU

Edna ni kama hajamuona Roma , kwani Zaidi ya kutingisha kichwa kama salamu alimpita na alionekana alikuwa ndani ya eneo hili kwa aili ya kuonana na Abuu.

Roma hakujali sana, na yeye alichapa raba kwani kilichokuwa kimemleta eneo hilo alikuwa ashakimaliza , aliingia kwenye lift na ndani ya dakika chache alikuwa akitoka na gari yake .

Alipiga mwendo mpaka alipokuja kuibukia ndani ya Samora ambayo kampuni ya mke wake ilipo , lakini muda huu kulionekana kukiwa na foleni kidogo kiasi cha kufanya magari yasimame.

“Boss nunu magazeti”Ilikuwa ni sauti ya kijana mdogo iliomshitua Roma aliekuwa akisikiliza mziki kwenye gari yake na kisha akashusha kioo na kumhurumia kijana huyo na kuona ngoja anunue , alilipa pesa na kupata gazeti lake.

“Asante bosi” Roma aliitikia kwa kichwa na kisha alianza kufunua gazeti hilo kwa mbelle , na hapo ndipo alipopigwa na mshangao kwani mbele kabisa ya gazeti hili kulikuwa na picha ya Abuu na Edna na kichwa kikubwa cha habari.

“KAMPUNI YA VEXTO NA JR WASAINI MKATABA WA KUSHIRIKIANA KATIKA UJENZI WA BARABARA YA MWENDO KASI KUTOKA MBAGALA KWENDA CHAMAZI”

Roma alisoma kichwa hiko na kufungua ndani kupata habari kamili na hapo ndipo alipokuja kugundua kuwa mke wake Jana alikuwa na miadi na Abuu kwa ajili ya kusaini mkataba huo , kwani ndani ya gazeti hilo ilionesha kuwa mkataba huo ulisainiwa jana yake ndani ya hoteli ya Serena.

“Sasa mke wangu walimteka vipi?”Alijiuliza Roma na kisha kuendelea kuendesha gari kwani magari yalikuwa yashaanza kusogea na ndani ya dakika chache alikuwa ndani ya jengo hili la kampuni huku akiwa amechelewa sana kwani muda huo ilikuwa yapata saa tano za mchana.

“Roma!”Ilikuwa ni suati ya uchangamfu kutoka kwa mrembo Doris ndio iliomwita Roma na kumfanya bwana huyu ageuke na hii ilikuwa ni ndani ya ofisi ambayo Roma alikuwa akifanyia kazi.

“Niambie mrembo , unaonekana kuwa mzuri Zaidi kuliko jana”

“Hahaha.. mnafiki sana wewe unanisifia huku unasema mkeo ndio mzuri kuliko wanawake wote”

“Hehe.. hilo ni kweli”Aliikuta akipigwa ngumi na Roma akajifanya kuumia na kitendo hiki kilifanya baadhi ya wafanyakazi hapa ndani washangazwe na ukaribu wa ghafla wa Roma na Doris ila hawakutaka kuuliza kwani Dorisi alikuwa mkubwa wao kikazi na nafasi ndani ya kampuni.

“Hawajakuumiza popote , jana ilikuwajje?”

“Doris hayo tuyaache tutaongea tukienda kupeana mambo tena au unaonaje mimi niko kamili gado na nikama wameniongezea nguvu na nataka nikazitoe kwako”Huku akitabasamu na kumfanya Doris aone aibu za kike.

“Jishaue tu mwanaume nani kakuambia tutafanya tena”Aliongea na kisha akaondoka .

“Hey! Handsome uko poa?”

“Niko poa Recho mrembo”

“Mh! Umechelewa unakua hapa ofisni kama kwako vile?”

“Sio hvyo mrembo , nilikuwa na Dharula”

“Mh! Haya bhana ila wewe na Doris kuna kitu kinaendelea ila sisemi”Roma alitabasamu na akaachana na Recho na kisha akatafuta gemu lake la Zuma na kuanza kucheza mpaka muda wa chakula na kuungana na Doris na Recho.

****

Usiku Edna alirudi mapema sana , na kusalimiana na Roma ambae alikuwa yupo sebleni akiongea na Bi wema , baada ya kusalimiana nao moja kwa moja aliingia kwenye chumba chake.

Mrembo huyu alikuwa ni mwenye mawazo ya hapa na pale lakini alichokuwa akiwaza kikubwa ni juu ya Roma , picha ya matukio yaliotokea kule kibaha hakuwa akiyaamini kabisa kwamba mtu aliekuwa ameyafanya ni Roma , mwanaume ambae alimdhania kuwa mbeba mizigo tu mpaka kufanya maamuzi ya kuolewa naye , huku akiamini kwamba atamfanya mwanaume huyo kuwa bwege , lakini matokeo yake yakawa tofauti.

Edna kuna vitu vingi vilikuwa vikipita kwenye kichwa chake kwa wakati mmoja , alikuwa akiwaza namna siku alivyoweza kuamka akiwa ndani ya chumba cha Roma mpaka siku ambayo alikutana na kwa mara nyingine ndani ya hoteli kwa ajili ya kumuomba ndoa.

“Anaonekana sio mtu wa kawaida kwa muonekano wake”Aliwaza.

Wakati akiendelea kuwaza mara simu yake ilipata uhai , aliinua na kuangalia jina na kukuta ni jina la Mheshimiwa , alipokea haraka na kisha aliweka sikioni.

“Hello Mheshimiwa habari za jioni”

“Nzuri sana Edna , unaendeleaje ?”

“Naendelea vizuri mheshimiwa”

“Nafurahi kusikia hivyo Edna , sasa nimekupigia simu kukuomba wewe pamoja na mume wako kuhudhuria chakula cha jioni Ikulu nina mazungumzo pia na wewe”Edna alibabaika , hakujua kuwa mheshimiwa Raisi alikuwa akijua kuwa tayari ashaolewa , alishangaa ila aliona Raisi ni mtu mwenye kujua mengi hivyo swala lake lilikuwa rahisi sana kulifahamu.

“Sawa mheshimiwa , sikujua kuwa unafahamu kama nishapata mume”

“Hahaha..Edna wewe ni mtu mkubwa sana kwenye taifa hili kila unachokifanya lazima nipate taarifa zako hususani kwa jambo muhimu kama lako”Edna alitabasamu na kisha waliagana na mheshimiwa huku akivuta pumzi.

Baada ya kukaa kwenye chumba chake cha kujisomea kwa muda hatimae ilikuwa saa mbili za usiku na alishuka kwa ajili ya chakula cha usiku baada ya kuitwa na Bi wema.

Mezani Roma alikuwepo na alikuwa tayari ashaanza kula huku Bi Wema akiwa ameachia tabasamu akimwangalia Roma jinsi anavyokula , ilionyesha alikuwa akifurahishwa na hamu ya kula aliokuwa nayo Roma.

“My Wife Bi Wema ni mtaalamu sana Sidhani kama unamfikia likija swala la mapishi”Aliongea Roma huku akijilamba midomo wakati huu akiwa ameshikilia paja la kuku na Edna alimwangalia mwanaume huyu kwa mtazamo wa maswali mengi.

“Huyu namtambulishaje kwa mheshimiwa kesho huyu , si ataenda kunitia aibu”Aliwaza Edna huku akianza kupakua chakula chake pasipo kumjibu Roma.

“Edna hajawahi kupika, hajui chochote kuhusu mapishi”Aliongea Bi wema na kumfanya Roma ashangae.

“Kwa hio Bi Wema unaniambia nimeoa mke jipu , maana mke ni upishi na mengineyo”Aliongea na kumfanya Edna akareke.

“Mr Roma licha ya kwamba Edna hajui kupika ila yupo vizuri kwenye mambo mengi”

“Bi wema naona unamsifia mke wangu , hayo mambo mengi anayoyajua ni kama yapi?”

“Edna licha ya kuwa mkimya ila ana roho nzuri , lakini pia ni mchapakazi mzuri huoni hata kampuni imekuwa kubwa baada ya kupewa uongozi wa juu”.

“Bi wema sawa , lakini hilo swala halihusiani na yeye kuwa mke akiwa nyumbani”

“Ndio hivyo , lakini naamini atajifunza kwani ashakuwa mke sasa”.

“Bi wema sitojifunza , kwanza sinampango wa kumpikia mwanaume anaekula kama mbuzi mimi”Aliongea Edna kwa hali ya kukereka ila kwa Roma ni kama hajamsikia kwani alivuta bakuli na kuongea wali kwenye sahani yake.

“Usiseme hivyo Edna ,Roma ni mumeo”.Edna hakutaka kuongezea neon aliendelea kula.

Baada ya Roma kumaliza kula alipandisha ngazi kuelekea uu huku akiwaacha wanawake watoe vyombo , baada tu ya kuingia kwenye chumba chake alibadilisha mavazi na kuchukua ufunguo na kushuka chini.

“Mke wangu natoka kidogo”Aliongea Roma na kuanza kupiga hatua kuelekea mlangoni.

“Kesho jioni kuna mahali tunapaswa kwenda pamoja ujiandae”Aliongea Edna na Roma aligeuka na kisha kutabasamu.

“Okey my Wife Usiku mwema”Aliongea Roma na Edna hakujali Zaidi kwani alipandisha ngazi kupanda juu chumbani kwake huku Bi wema akiwa anamuangalia.

Roma kama kawaida , alikuwa akiwaza kutafuta kitumbua cha kupunguza kichupa usiku huo , alianza kumfikiria Rose , lakini wazo hilo alilitupilia mbali , aliendelea na kumfikiria Dorisi na kuona pia wazo hilo sio zuri.

“Ngoja niende New Afrika hoteli pale sikosi warembo”Alijiwazia Roma wakati akiwa anapita daraja la kigamboni.

Dakika chache mbele alikuwa akiegesha gari yake mahali maalumu ndani ya hoteli hii kubwa ndani ya jiji la Dar na kisha alishuka na kuingia ndani na moja kwa moja alienda sehemu ya Bar iliokuwa ndani ya hoteli hii.

Baada ya kuingia ndani ya hili eneo , kwanza alitabasamu baada ya kuona ni sehemu iliochangamka , lakini jambo ambalo lilimfanya kujisikia vibaya ni kwamba ndani ya hili eneo lilionekana kuwa na watu waliokuwa wawili wawili au Zaidi , kuna waliokuwa na wachumba zao , lakini pia kuna waliokuwa wakipiga stori wakiwa jinsia moja ,Roma aliangaza upande wa kulia kushoto na alijikuta akivutiwa na upande wa kushoto baada ya kumuona mwanamke mmoja alieonekana kuwa peke yake.

Roma alipiga hatua kuelekea upande ule na kumfikia yule mwanamke na alikiri ni mrembo mara baada ya kumuona kwa ukaribu , mwanamke huyu hakuonekana kuwa mkubwa sana kimakadirio Roma alimuona kuwa na miaka isiozidi therethini , alikuwa amevalia gauni refu la maua maua rangi ya njano na nyeupe huku akiwa ameifunga mkanda mkubwa kwenye kiuno , alikuwa na nywele alizokuwa amenyoa na zikawa fupi kiasi huku zikiwa zimepakwa rangi nyeusi na kuonesha mawimbi na kufanya kuzidi kumfanya mwanamke huyu kuzidi kiuonekana kuwa mrembo.

“Niambie mrembo , Uko peke yako?”Aliuliza Roma kabla ya kuketi na mwanake huyu alimwangalia kwa macho yake makubwa ya gololi, wakati haya yakiendelea baadhi ya watu walikuwa wakimwangalia Roma ni kama walionekana walikuwa wakimfahamu huyu mwanamke , lakini kwa Roma hakujai Zaidi kwanza mwanamke aliekuwa mbele yake hakuwahi kumuona na pia alikuwa mrembo.

“Niko peke yangu , Unaweza kukaa”Aliongea huyu mwanamke kwa sauti Fulani hivi ya kupendeza na kumfanya Roma Atabasamu.

“Inakuwaje mwanamke mrembo kama wewe unakaa peke yako?”

“Nimejisikia leo sihitaji kampani kwani nina mengi ya kufikiria”.Aliongea huku akinyanyua glasi yake iliojaa wine ya gharama ya juu kabisa iliokuwa na jina la Abreu.Roma alitabasamu huku akiangalia chupa ya Wine.

“Hio ni moja ya Wine ya bei ghali sana duniani , imetengengezwa na David Abreu”Aliongea Roma na kumfanya mrembo huyu amwangalie na kisha akatabasamu.

“Umepatia , inaonekana ni mpenzi wa hii wine , mpaka unamjua mtengenezaji”

“Ndio ni moja ya Wine ninazozipenda”Aliongea Roma na akaja mhhudumu kwa ajili ya kuchukua aina ya kinywaji atakachotumia.

“Nipe kama ya huyu mrembo”Aliongea Roma na kisha mhudumu akaileta ndani ya dakika kadhaa huku Roma akiendelea kumpigisha stori mrembo huyu , muda ulizidi kusogea kwa mrembo huyu alionekana kuanza kulewa , ila kwa Roma hakuwa ni mwenye kuongekana kulewa

“Unamawazo gani mrembo , mpaka yakakufanya ujitenge siku ya leo?”

“Kuna mshenzi kaniboa leo , na sitaki hata kumsikia tena kwenye maisha yangu”

“Pole ni mume au Boyfriend?”

“Sio mume wala sio Boyfriend .. sijui haa nimuweke vipi , ila amenikera sana leo”Aliongea mrembo huyu.

“Atakuwa mchepuko”Aliwaza Roma

“Unaonaje tukichukua chumba mrembo nikakuusahaulisha na ya dunia”.

“Utaweza kunisaulisha kweli , unaonekana mdogo mno”Roma hakutaka kuongea Zaidi , aliona hapa ni vitendo pekee ambavyo vingefanya kazi , alichokifanya ni kumuambia huyo mwanamke anyanyuke amfuate na mwanamke huyu alimwangalia Roma na kisha akanyanyuka kivivu na kumshikilia Roma kilevi na wakatoka ndani ya hilo eneo huku Roma akiacha Hela zilizokuwa kwa mfumo wa Dola na kuondoka.

Masaa machache mbele mwanamke yule mrembo alionekana kutoa maneno ya kila aina yasio kuwa yanaelewweka na yale ambayo hayakuwa katika mpangilio mzuri ,,alionekana alikuwa kwenye ulimwengu mwingine kabisa.

“Naomba tupumzike wewe mwanaume utaniua”Aliongea huyu mwanamke na Roma hakutaka kusikiliza Zaidi kwani alikusanya miguu ya mwanamke huyu na kuiweka kichwani na kuendelea kukata kiuno na ndani ya lisaa limoja na nusu , alitua mzigo na kulala pembeni huku akihema.

Upande wa yule mwanamke , alionekana kumwangalia Roma pasipo kummaliza kwani magoli aliofunga usiku hio hayakuwa na idadi , alikumbuka vyema muda ambao walianza kufanya tendo hilo ni Zaidi ya masaa mawili.

“Sijawahi kukutana na mwanaume anaeweza kuto**mba muda mrefu kama huyu”Aliongea huyu mwanamke na akapitiwa na usingizi.

Asubuhi kulivyokucha huyu mwanamke aliangalia pembeni na kujikuta akiwa peke yake na Roma hakuwepo, wakati akiendelea kuwaza yaliotokea usiku , simu yake ilianza kutia mfululizo aliangalia jina na kisha akapokea .

“Kuna nini Grace?”

“Mheshimiwa Angalia mtandaoni kuna habari zako”Ilikuwa ni sauti ya wasiwasi ya upande wa pili ikiongea.

Huyu mwanamke mrembo akiwa uchi aliangia Instagram na kuangalia kuna nini mtandano”

“MBUNGE NA NAIBU WAZIRI WA SANAA NA MICHEZO NEEMA LUWAZO AONEKANA NA MWANAUME KWA MARA YA KWANZA WAKILA BATA”Huku kichwa hiko kikiambatana na mapicha , picha ya kwanza ilikuwa ni ya Roma japo haijaonekana vizuri , ila kwa mtu anaemjua Roma angejua ni Roma na picha ya mpili ilikuwa ni ya mrembo huyuy Neema Luwazo ambaye ni Naibu wazri wa Sanaa na michezo.

SEHEMU YA KUMI NA TANO.

Saa kumi na mbili na nusu Roma alinyanyuka na kujivuta kisha akashuka chini kwenye chumba cha mazoezi kwa ajili ya kupasha mwili joto , wakati akiendelea kuchukua mazoezi , alikuwa akikumbuka vyEma usiku wa jana alivyoumaliza na yule mwanamke ambaye hakuwa akimjua hata jina Zaidi ya kumnyandua.

“Nadhani hatutaonana tena”Aliwaza Roma

Saa moja kamili Roma alikuwa ashamaliza kila kitu na alikuwa mezani akinywa chai yeye pamoja na Edna kwa ajili ya kuelekea kazini.

“Wife mbona unaniangalia hivyo”

“Hivi Roma tokea uanze kazi umefanya nini ndani ya kampuni?”

“Sina nilichofanya Zaidi ya kucheza gemu mke wangu , sijui cha kufanya kama vipi nipe kazi hata ya ulinzi nifanye hio kuliko ya kukaa kwenye meza”Edna alishangaa ila hakuongea kitu , aliendelea kunywa chai na alimaliza wa kwanza akimuacha Roma.

“Usisahau leo kuna sehemu tunapaswa kwenda, nitamwagiza Suzzane akuletee nguo za kuvaa”Aliongea Edna na kumfanya Roma ashangae.

“Mke wangu nguo si ninazo kuna ulazima gani wa nguo zingine?”

“Fanya kama nilivyokuambia ,acha maswali mengi”Edna hakutaka kuongea Zaidi na Roma alimuaga Bi Wema na kisha ndani ya Sekunde chache Roma alisikia mngurumo wa Gari ukipotelea nje ya geti.

Roma na yeye baada ya kumaliza kunywa chai , alitoka na kuingia kwenye gari yake kuelekea kazini.

“Nikifika nipakue mtandaoni Gemu lingine lile limenichosha sina ninachojua mimi kuhusu kazi za kukaa ofisini najua kurudha ngumi tu na kuua”Aliwaza Roma huku akikanyaga pedeli kuelekea kwenye kampuni.

Roma alifika na siku hii Recho alionekana kuchelewa kufika kazini kwani Roma hakumkuta,wakati Roma anawasha Tarakishi yake kwa ajili ya kupakua gemu , mara aliingia Doris akiwa ni mweye kununa , baada ya kumfikia bila hara ya salamu alimpa Roma Tablet alioishika mkononi na Roma aliichukua na kuangalia baadhi ya picha zake zikiwa mtandaoni.

“Huyu mwanamke kumbe alikuwa waziri , mbona mdogo hivi”Aliongea Roma kwa sauti na kumfanya Doris azidi kufura kwa hasira.

“Usiniambie huyu ni wewe kweli?”

“Bebi Doris ni mimi ndio, si unaniaona kabisa hapo kuna kipi cha kuficha sasa”Aliongea Roma na kumfanya Dorisi azidi kushangaa inakuwaje huyu mwanaume hata kujitetea hafanyi , maana kwa alivyokuwa anawajua wanaume lazima wangeanza kutoa sababu ila kwa Roma yeye alikiri.

“Bebi Doris huyu mwanamke alikuwa mrembo ila sikumdhania ni Mbunge”Doris alimwangalia Roma kwa hasira na kisha bila ya kusema neno aliondoka na Roma hakujali , aliendelea kupakua gemu lake kwa aili ya kuendelea kucheza.

Ndani ya ofisi ya CEO Dorisi aliingia na kumkuta Edna akiwa anaendelea na kama kawaida yake mwanamke huyu kwa uchapaji kazi , baada ya Dorisi kumfikia.

“Bosi umeona taarifa ya Roma inayozagaa mtandaoni?”

“Hapana sijaona”Aliongea Edna na Doris alimkabidhi Edna ile tablet na Edna aliangalia kwa muda huku uso wake ukijikunja kiasi.

“Kumbe alivyoniaga anatoka kidogo alienda kukutana na huyu kimada , mwanaume Malaya huyu”Alijiwazia Edna na kisha alimrudishia Doris Tablet yake.

“Hii sio nzuri kwa image ya kampuni Edna”

“Doris haya ni mambo binafsi ya Roma na wala hayahusu kampuni hivyo swala hili achana nalo na kaendelee na kazi”Aliongea Edna na Dorisi aliondoka huku akionekana ni mwenye hasira kweli .

Baada ya Dorisi kuondoka Edna alijikuta akivuta pumzi na kuangalia mlango aliotoka Edna.

“Maskini hata Dorisi kashaingia kwenye mtego wa huyu mwanaume”Aliwaza na kisha akanywa kahawa kidogo na kuendelea na kazi.

*****

Upande mwingine ndani ya mji wa Mheshimiwa Mstaafu sehemu iliokuwa ikifahamika kama Village G alionekana mheshimiwa Raisi mstaafu bwana Kigombola Hamisi Hamisi akiwa ameketi kwenye sofa za bei ya hali ya juu kwenye jumba lake hili la kifahari ndani ya kijiji hiki , muda huu ilikuw ni asubuhi ya saa nne akiangalia runinga huku akipata chai yake taratibu.

Wakati mzee huyu mwenye mvi zilizoacha uwararaza akiendelea kuangalia runinga mara aliingia moja ya Sekretari wake na kumsogelea.

“Mheshimiwa kuna taarifa hapa nataka kukutaarifu juu ya Madam Neema”

Mheshimiwa alichukua ile simu ya Iphone kiana huyu aliokuwa ameishikilia na kuanza kuangalia picha zilizokuwa zimetumwa kwa njia ya Watsapp , Moja ya picha hizo zilimuonesha Roma akiingia ndani ya chumba na Neema huku wakiwa wameshikana viuno.

Mzee huyu mara baada ya kuona picha hii alionekana kukunja sura kwa hasira kali na kisha alichukua kikombe kilichokuwa na chai mbele yake na kunywa kidogo na kisha alimgeukia huyu bwana.

“Erick nataka taarifa zote za huyu mwanaume kwenye hizi picha kabla ya saa saba mchana”

“Sawa mheshimiwa”

Neema Luwazo kwa wale wasio mfahamu ni kwamba mwanamke huyu ni moja ya wanawake maarufu sana ndani ya ulingo wa siasa , moja ya sifa kubwa iliomfanya mwanamke huyu kuwa maarufu ni uzuri wake aliokuwa nao.

Kabla ya neema kujiingiza katika siasa alikuwa ni msanii na mwigizaji mkubwa sana lakini pia ashawahi kushinda shindano la umiiss miaka kadhaa iliopita.

Kipindi cha uongozi wa mheshimiwa Kigombola ndio kipindi ambacho Neema kwa mara ya kwanza alipata uteuzi na kuwa mkuu wa wilaya ndani ya jiji la Dar es salaam , uteuzi ambao ulianza kufanya watu wahisi kuna kitu kinachoendelea kati ya mheshimiwa Kigombola na Neema.

Licha ya tetesi hizo zilizokuwa zikisambaa mtandaoni , hakukuwa na ushahidi wowote wa kuthibitisha taarifa hizo na hata pale Neema mwenyewe alivyoulizwa alisema.

“That is just Groundless Rumors na siwezi kuzungumza lolote kwani sipo kama watu wanavyonifkiiria , nimefikia hapa kutokana na juhudi zangu mwenywe”Hilo ndio jibu ambalo alilitoa Neema miaka kadhaa nyuma , lakini jibu hili pia lilionekana kuwa na mashiko kwani licha ya mwanadada huyu kuwa mkuu wa wilaya , lakini pia alisifika kwa kuwa na mali nyingi sana ambazo alirithi kutoka kwa wazazi wake miaka kadhaa baada ya wao kufariki katika ajali ya ndege.

Utajili wa Neema ulikuwa ni kiasi cha dola za kimarekani milioni 570 wakati akiwa anarithi mali zote za wazazi wake kama mtoto wa kipekee alieachwa duniani.

Baada ya miaka kadhaa ya kufanya kazi Neema alizidi kujizolea umaarufu mwingi kutokana na uchapakazi wake , lakini pia uzuri wake uliopitiliza lakini pia utajiri aliokuwa nao ambao ulizidi kuongezeka miaka hadi miaka.

Katika kipindi chote hiko cha kuwa mkuu wa wilaya ,Neema hakuwahi kuhusishwa na mwanaume yoyote yule kutoka nae kimapenzi jambo ambalo lilifanya mashilawadu wengi kila siku kuandika makisio yao ya hapa na pale , lakini tetesi hizo zilikuja kukoma mara baada ya Neema kubeba ujauzito na pale alipohojiwa juu ya baba wa mtoto ndipo alipoweka wazi kuwa baba wa mtoto ni mheshimiwa Kigombola na kipindi hiki mheshimiwa kigombola alikuwa kwenye muhula wa mwisho wa uongozi wake.

Kwanzia hapo , ndipo ilipofahamika Rasmi kuwa Neema ni chombo ya wakubwa na watu wengi walijiweka mbali na mwanamke huyo , hakuna mtu alieweza kumsogelea na kumtongoza Neema jambo ambalo lilimfanya mwanamke huyu kuwa mpweke kiana licha ya kuwa na mahusiano na mheshimiwa.

Baada ya uongozi wa Senga , Neema ndipo alipopata ubunge wa viti maalumu na kuteuliwa kuwa naibu waziri wa Sanaa na michezo , kipindi hiki mtoto wa Neema wa kike afahamikae kwa jina la maarufu la Donyi alikuwa na miaka minne tayari.

Upande wa mheshimiwa Kigombola alikuwa amekufa na kuoza juu ya Neema , alikuwa haambiwei chochocte kuhusu Neema na kutoka na mapenzi yake juu ya mwanamke huyo , alikuwa ameweka watu ambao walikuwa wakimchunguza mienendo yake kwa siri.

Upande wa Neema licha ya kuzaa na mheshimiwa , hakuwa na mapenzi yoyote kwake na kuna tukio ambalo lilimtokea Neema na kumfanya aombe msaada wa Mheshimiwa na hapo ndipo ulipoanza mwanzo wa kulala na mheshimiwa mpaka kupata mtoto Donyi na yeye alimchukulia Kigombola kama ‘stepping stone’ kwenye carear yake ya kisiasa.

Sasa hii ndio maana siku Roma wakati anamsogelea Neema watu wengi walikuwa wakimshangaa kwa ujasiri wake wa kutoogopa kuonekana na chakula ya wakubwa , ila kwa upande wa Roma hakuwa akimjua kabisa Neema kwani hakuwahi kukaa na kuanza kufatilia siasa za Taifa la Tanzania.

*****

Ni muda wa saa kumi na mbili na Nusu za jioni Roma alieonekana kupendeza sana kwa suti nyeusi ya bei ghali , iliochangamshwa na tai , huku chini akiwa na kiatu kikali cha kampuni ya Louis Vuitton pamoa na Saaa ya Rolex mkononi , hakika ungemuona Roma usingemdhania ni yule wa siku kadhaa zilizopita aliekuwa akibeba mizigo.

Dakika chache mbele za Roma kusubiri chini ya eneo hili la Sebuleni akiwa na Bi Wema mara hatua za viatu zilisikika zikishuka kutoka juju na hapo ndipo Roma alipogeuza macho yake na kumuona mwanamke mrembo kama malaika akishuka , huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni mrembo Edna.

Edna alikuwa akivutia haswa , muonekano wa mavazi yake jioni hii ulimfanya Roma kupagawa , bwana huyu alikuwa ameona wanawake warembo ila kwa Edna alikiri alikuwa mzuri tena Zaidi ya mzuri , kila kiungo cha mwanamke huyu katika mwili wake kilikuwa kimepangwa kimpangilio ili kuleta radha ,Edna alikuwa amevalia kigauni flani cheupe cha kampuni yake kilichokuwa na shingo ndefu na kumuacha shingo yake kama ya Kinyarwanda wazi na kumfanya apendezeshwe Zaidi na mkufu wa madini ya Almasi uliokuwa ukimeremeta shingoni kuonekana vyema , kigauni hiki kilikuwa sio kirefu sana na kumfanya miguu yake ya bia ilionona na kuwa na michirizi flani kuonekana vyema , kilichomfanya Edna kuzidi kuwa mzuri ni rangi ya sura yake iliokuwa sio nyeupe wala sio nyeusi , alikuwa na karangi flani hivi kiasi kwamba ukimwangalia baba yake na mama yake Edna kwenye picha ungejiuliza ilikuwaje wakawa na mtoto wa aina hio maana mzee Adebayo alikuwa ni mbaya wa sura

“This is God Masterpiece of creation which he ever did”Aliwaza Roma huku akitabasamu na kumeza mate kwa wakati mmoja akiwa anamwangalia mke wake.

“Mke wangu umzuri sana mpaka nayaonea wivu macho yangu”Aliongea Roma na kumfanya Bi Wema agune na kutabasamu na kwa Edna alionyesha hali ya aibu kwani macho ya Roma yalikuwa yakimtazama sana kwa matamanio.

“Twende tunachelewa”Aliongea Edna na kisha Roma alitangulia mbele kuelekea kwenye magari na kutoa V8 nyeusi ya bei ghari na kuisogeza mpaka katikati ya jumba hili na kisha akatoka na kumfungulia Edna mlango.

“Kuitwa mume wa Edna ni heshima Tosha hata kama haonekani kuwa na mpango wa kunipa kitumbua” Aliwaza Roma na kisha alitoa gari hio taratibu kuelekea ikulu.

SEHEMU YA 16.

Wakati Roma anatoa gari kwenye Geti kuna hisia flani zilimfanya aangalie nyuma kwenye kioo , kwani alihisi kuna gari ambayo ilikuwa ikiwafatilia, hakujua ni watu gani ila hakutaka kujali sana kwani alijiamini mno .

“Nimeona ile habari kwenye gazeti Roma na nikutahadharishe tu achana na yule mwanamke atakuingiza kwenye matatizo”Aliongea Edna wakati wakiwa wanakaribia ndani ya Lango la ikulu wakisubiria kufunguliwa.

“Hilo lisikupe shida mke wangu”.Edna hakuongeza Zaidi mpaka wanaegesha gari na kushuka chini , huku wakwanza kutoka ni Roma na akakimbilia upande wa kushoto na kumfungulia Edna mlango huku Edna akiweka tabasamu bandia mbele ya watu waliokuwa ndani ya eneo hilo wakiwa wapo kwa ajili ya kuwapokea.

“Fatma kutana na mume wangu anaitwa Roma , Roma huyu ni katibu muhtasi wa ikulu anafahamika kwa Fatuma Adinani”Aliongea Edna kwa tabasamu akimtambulisha Roma mbele ya fatuma ambae alikuwa yupo eneo hilo kwa ajili ya kuwapokea .

Fatuma alikuwa ni mwanamke ambaye kwa haraka haraka umri wake haukua mkubwa sana ni kati ya miaka therathini kupanda , lakini alionekana kuwa na cheo kikubwa ikulu.

“Nafurahi kufahamiana na wewe Fatma”Aliongea Roma na kisha walitangulizana na Fatma kuelekea sehemu maalumu ndani ya eneo hili la ikulu.

Upande wa Roma hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuingia ndani ya eneo hili la Ikulu , lakini alionekana kama mtu ambae alikuwa mzoefu kwani hakuonesha uoga wa aina yoyote ile na hata walivyokuwa njiani pale alipoambiwa kuwa safari hio ni ya kwenda ikulu ni swala ambalo halikumshangaza sana kwani aliamini mke wake ni mtu mkubwa hivyo ni swala la kawaida kwa yeye kualikwa na mheshimiwa kumtembelea Ikulu.

Wafanya kazi wa hii ikulu walionekana kuwa katika kazi zao , huku ulinzi ukiwa umeimarishwa kila kona , jambo ambalo kwa Roma lilimfurahisha.

“Angalau wanajitahidi , licha ya mapungufu mengi”Aliongea Roma baada ya kuongekana kukagua eneo hilo pamoja na ulinzi wake wote.

Chakula cha usiku kiliandaliwa baina ya familia ya mheshimiwa Raisi na mualiko huo hakukuwa wa kikazi ulikuwa ni kama wa kifamilia , kwani hata waandishi hawakuwepo , swala ambalo pia lilimshangaza Roma kuona mke wake kuwa na ukaribu sana na familia ya mheshimiwa Rais.

“Edna karibu mwanangu”Alionekana mwanamke mmoja mrembo wa makamo akiwasogelea wakina Roma , huyu hakuwa mwingine bali mke wa mheshimiwa Raisi Senga afahamikae kwa jina la Damasi Senga.

“Asante Mama”.

“Huyu ni mume wako Doris , jamani unatabia mbaya , umefunga ndoa hata kuniambia mama yako”Doris aliona aibu kidogo.

“Nisamehe sana Mama ila ukweli swala hili lilitokea ghafla sana na ni makubaliano yangu na mme wangu , tumefunga ndoa lakini hata sherehe hatujafanya”.

“Nimekuelewa Doris wala hata usijisikie vibaya , Karibu sana Mr Roma Doris ni kama mwanangu maana mama yake alikuwa rafiki yangu sana tulisoma wote”Aliongea Mama huyu kwa ukarimu wa hali ya juu na kumfanya Roma atabasamu.

“Nashukuru sana kwa kunikaribisha kwa ukarimu”

“Dorisi twendenii tulikuwa tunawasubiri ninyi tu mfike”Aliongea mama huyu na kisha aliongoza njia na kuingia kwenye chumba kilichokuwa kushoto kilichokuwa kimetanganishwa na mlango mkubwa.

Baada ya kuingia hapa ndani ndipo Roma aliposhangazwa na ufahari wa hili eneo , kulikuwa na mpangilio mzuri sana wa samani zilizokuwepo hapa ndani , huku katikati kukia na meza kubwa ambayo ilikuwa imezungukwa na watu watatu wawili mwanaume na mmoja mwanamke.

“Oh!Doris karibuni sana ,tulikuwa tukiwasubiri nyie tu”Aliongea mzee huyu ambaye anafahamika kama raisi kwa waanzania ,lakini ndani ya eneo hili alionekana kama baba wa familia.

“Asante sana Mheshimiwa” huku wakisalimiana .

“Karibu sana Roma jisikie huru kabisa”Aliongea mheshimiwa huyu na kumfanya Roma atabasamu huku akiangaliana na mheshimiwa kiume.

“Ashley kumbe umerudi , sina taarifa zako”.

“Ndio Doris nina siku nne tu tokea niingie nchini”Aliongea huyu mwanamke mrembo huku macho yake yote yakimwangalia Roma , na alionekana ni mtu ambaye hakufurahishwa na uwepo wa Roma hapo ndani na Roma mwanzoni hakumuona Ashley baada ya kukutanisha macho yao ni kama waliwasiliana kwa macho na Roma aliketi karibu na mke wake.

“Ushamaliza masomo yako ya PhD?”

“Ndio nishamaliza”

“Hongera sana ni hatua kubwa umefikia”Aliongea Doris na kumgeukia kijana ambaye muda wote alikuwa kimya akiwa pembeni.

“Denis mbona huwachangamkii wageni kama hujawaona”Denisi alikuwa ni kijana ambaye umri wake hakuonekana kuwa mkubwa sana , alikuwa na rika la miaka 22 hivi na alikuwa chuo mwaka wa mwisho huko nchini Norway.

Denis alimwangalia Edna na kisha aliweka tabasamu feki usoni na kisha akamsalimia Edna na Roma , ila kwa upande wa Roma kuna ambo ambalo aliligundua katika macho ya Denis ila hakutaka kufikiria sana , aliweka kapuni swala hilo.

Basi Roma alitambulishwa kwa mheshimiwa Senga kama mume halali wa Edna na chakula kilifana sana kwani kilienda na stori nyingi za hapa na pale huku pongezi zikielekezwa kwa Edna kwa kupata mume kwani lilikuwa ni jambo la kipekee sana katika maisha ya mwanamke na hakuka aliekuwa anajua kuwa wawili hao walikuwa na ndoa ya mkataba na yote waliokuwa wakifanya ni maigizo..

Mheshimiwa Raisi muda wote alikuwa akimwangalia Roma kama mtu ambaye alikuwa na maswali mengi juu yake , ukweli ni kwamba mheshimiwa Raisi licha ya kutumia ushawishi wake na mamlaka yake kupata taarifa zilizokuwa zikimuhusu Roma lakini hakuambulia chochote .

“Mheshimiwa Taarifa zinazomuhusu Roma zinaonekana kuwa nyeti sana ndani ya shirkika la CIA na wamegoma kutuatia taarifa yake”.Aliongea Kabwe baada ya kuwasilisha utafiti wake aliokuwa ameufanya juu ya Roma.

“ kwa hio unamaanisha kuna taarifa inayomuhusu Roma ambazo CIA hawataki kuzitoa?”.

“Ndio mheshimiwa ni Top Confidential na hata baadhi ya viongozi wa CIA hawana uwezo kuangalia taarifa yake ni baadhi ya viongozi wakubwa tu ndio wenye uwezo huo”Aliongea Kabwe na kumfanya mheshimiwa ashangae Zaidi na kuzidi kujiuliza maswali ya Roma ni nani kiasi cha taarifa zake kufichwa na CIA.

Baada ya kuona swala lake limegonga mwamba aliona njia pekee ni kumkaribisha Edna ikulu kwenye chakula cha jioni ili aweze kuoanana na Roma aweze kumfahamu hata kwakumuangalia.

Ukweli licha ya Senga kumkaribisha Roma ikulu lakini alikuwa akikumbuka vyema kwa kitendo cha Roma kumuita babu, hivyo hakuwa akimpenda kwa dhati.

Baada ya chakula mheshimiwa alimwita Edna kwenye ofisi yake kwa maongozi Zaidi akimuacha Roma akiongea na wanafamilia.

Edna mara baada ya kufika kwenye ofisi ya mheshimiwa , Senga aliingiza mkono kwenye mfuko wa suruali yake na kisha alitoa Flash disk na kumkabidhi Edna.

“Hii inahusu nini mheshimiwa?”

“Ukifika nyumbani chukua muda wako kuangalia kilichomo humo ndani kila kitu kinajieleza ni wakati wako kujua swala hili”Aliongea Mhesimiwa na kumfanya Edna ashangae lakini hakujiuliza maswali mengi aliichukua na kuiweka kwenye mkoba wake.

“Umekutana kutana vipi na Roma mpaka kufikia hatua ya kufunga ndoa?”.

“Ni stori ndefu mheshimiwa, ila naweza kusema ni mwanaume wangu wa kwanza katika maisha yangu na atakuwa wa mwisho vilevile”Snga alishangazwa na jibu hilo la Edna na kisha akatabasamu.

“Unamwamini?”Edna alishangazwa na swali hilo , ila hapo hapo akakumbuka kuwa Roma alionekana kuwa na mwanamke mwingine kwenye mitandao hivyo alijua hueana mheshimiwa atakuwa na taarifa hizo ,ila asichokijua Edna ni kwamba Senga anajua pia uhusiano wa Roma na Edna.

“Kusema ukweli kuhusu kumuamini bado , ila moyo wangu unamuhitai Zaidi kuwa karibu yake”Alijibu Edna.

Mheshimiwa alishangazwa na maneno hayo na kujiuliza Roma ni mwanaume wa aina gani kiasi cha kuliliwa na kila mwanamke.

Huku upande wa Roma muda wote alikuwa akimangalia Ashley kwakumuibia ibia na kwa Ashley alikuwa akimwangalia Roma kwa kuibiaibia.

Roma aliomba kuoneshwa sehemu ya maliwato na alielekezwa na mfanya kazi na hio ni kama ikawa nafasi kwa Ashley kwani na yeye alinyanyuka na kuelekea upande huo huo, huku Denis aliekuwa akionga na mama yake wasielewe kitu baina ya hao wawili.

“Naona ushakuwa mume wa mtu tayari?”Ilikuwa ni sauti iliosikika nyuma ya Roma aliekuwa akikojoa na kumfanya atabasamu kifedhuli.

“Wewe unamuonaje mke wangu chombo kile”.

“Mwanaume unaroho mbaya sana wewe , hivi unajua ni kiasi gani mimi na Profesa Clark tulivyoteseka na tunavyoendelea kuteseka juu yako?”.

“Juu ya Clark , mimi na wewe ni swala ambalo lilikoma nilivyoamua kurudi Tanzania na nadhani itakuwa jambo jema mkiendelea kuheshimu uamuzi niliochukua , sasa hivi nishaoa na nitaishi kumlinda mke wangu na kuishi maisha ya kawaida”.

“Unajidanganya Ramoni Edna sio Seventeen licha ya wao kufanana kila kitu ,Seventeen ashakufa Ramoni”

“Ashley nadhani unakosea sehemu moja , hakuna sehemu ambayo nimesema Edna ni Seventeen , kwangu yule mwanamke ashakufa alivyojirusha baharini kipindi kile na nishaacha kumfikiria katika maisha yangu , Edna ni Edna na nimeamua kuishi naye maisha ya kawaida”Aliongea Roma na kisha kumpita Ashley kurudi alikowaacha wenzake.

“Clark kashapata dawa ya kukutibu Ramoni”Aliongea Ashley na Roma hakusimama alimsikia vyema , lakini aliongeza mwendo na kurudi alikotoka.

Baada ya madakika kadhaa mheshimiwa Senga aliomba kuongea na Roma na Edna bila shida alikubali na Roma aliitwa ofisini.

“Karibu sana Mr Roma”

“Asante sana mheshimiwa , nimeitikia wito”

“Nimekuita hapa tuongee kidogo maana Edna kwangu ni kama mtoto wangu wa kumzaa , na mama yake nafahamiana nae vizuri tu”Roma alitingisha kichwa kukubaliana nae.

“Japo sikufahamu vyema ulikotoka na wapi umezaliwa , ila nataka unihakikishe kwamba Edna atakuwa salama na hataumizwa na matendo yako”.

“Mheshimiwa unaonekana umetafuta taarifa zinazonihusu mimi tayari”aliongeaRoma.

“Ni kweli nimejaribu na inaonekana wewe sio wa kawaida na ndio maana nataka kukupa onyo . lolote likimtokea Edna basi jua mimi na wewe tutakuwa maadui”.

“Mheshimiwa Edna ni mke wangu na swala la kumlinda pia litakuwa juu yangu kama mume hivyo naomba swala hili lisikuumize kichwa , lakini pia unachojaribu kutafuta kuhusu mimi naomba uache na uendelee kuwaongoza watanzania wazidi kupata mema ya nchi”Aliongea Roma na kumfanya Senga aone kweli anaongea na mtu ambae hakuwa wa kawaida , kwani Roma hakuonesha hofu yoyote ile ya woga mbele yake na alikuwa mtu wa kunyoosha maneno tofauti na viongozi wengi walio chini yake.

“Okey ni hayo tu bwana Roma”

“Hakuna shida mheshimiwa naamini na wewe pia utaacha kufukunyua taarifa zinazonihusu” Mheshimiwa Senga aliitikia kwa kichwa na Roma alitoka.

“Fii***ck huyu Roma ni nani kwanini anajiamini hivi?” Mheshimiwa alionekana kuwa mwenye hasira kwa kutokumjua Roma ni nani.

Mheshimiwa alikuwa akitweta kwa hasira kwani katika maisha yake aliamini kama atakuwa raisi basi atakuwa na uwezo wa kuogopwa na kila mtu ndani ya taifa hili , lakini jambo hilo likawa rofauti kwani mpaka sasa amekuwa na watu wawili ambao hawakuwa wakimuogopa , wa kwanza alikuwa ni The Doni na wa pili ni Roma aliejitokeza.

Uliongea nini na mheshimiwa?” Aliuliza Edna baada ya kutoka nje ya geti hili la ikulu baada ya hafla yao kuisha .

“Hehe mke wangu nadhani ushajua alichoniambia”

“Sijui ndio maana nimekuuliza”

“Aliniambia ohh yeye na wewe ni kama mwana na baba hivyo nisije kukuumiza”

“Kama ni hivyo walausijali maana mkataba wetu wa ndoa uko pale pale , baada ya miezi sita kuisha kila mtu atafanya mambo yake”

“Hata usijali”Aliongea Roma huku akiendelea kuendesha gari kwa umakini na ndani ya madakika kadhaa alikuwa mbele ya geti la nyumba , lakini kabla hajaingiza gari ,wakai huo geti likiwa limefunguliwa , mara simu yake ilianza kuita mfululizo na kumfanya Roma aangalie na kuona mpigaji ni Juma , alishangazwa na upigaji huo , kwani tokea siku alivyoagana na Najma hakuwasiliana na Juma

“Juma kuna nini?”.

“Roma Wamemteka Najma ?Ilikuwa ni sauti ya wasiwasi ambayo aliisikia Roma na alijua kuna tatizo.

“Edna naomba ushuke kwenye gari?”

“Nini?”

“Nimekuambia shuka kwenye gari kuna sehemu naenda”

“Yaani uende kwa hawara wako na gari yangu”Roma hakutaka kumsikiliza , alirudisha gari nyuma kwa spidi akitaka kugeuza kitendo ambacho kiliwafanya hata walinzi kushangaa.

“Sawa ngoa nishuke”Aliongea Edna na kuhcukua mkoba wake na ile anashuka tu gari ya Roma ilitokomea kama mshale kiasi cha kumfanya atumbue macho kwa spidi aliotoka nayo Roma.

*****

“Erick umepata taarifa gani inayomuhusu?”Aliuliza mheshimiwa Kigombola mara baada ya Erick kuingia ndani ya ofisi ndogo ya mstaafu ndani ya Village G.

“Mheshimiwa kwa taarifa niliopata inamuonesha Roma ni mbeba mizigo kutoka soko la Kariakoo mpaka siku chache zilizopita”

“Unamaanisha nini mpaka siku chache zilizopita?”

“Roma sikuchache zilizopita alifunga ndao na CEO Edna”

“Niniii!” Mheshimiwa alijikura akishangazwa na swala hilo.

“Ndio mheshimiwa Edna na Roma ni wanandoa”

“Nadhani kuna taarifa nyingine Zaidi ya hio Erick inawezekanaje mbeba mizigo amuoe mtu mkubwa kama Edna bila ya sababu”.

“Mkuu kuhusu hilo sijui , ila taarifa nyingine ambayo imenishangaza inaonesha Roma ni mhitimu kutoka chuo cha Harvard amemaliza masoko katika uongozi wa biashara , lakini pia katika CV yake aliowasilisha ndani ya kampuni yetu , inaonekana anauwezo wa kuzungumza lugha ishirini na mbili”

“Lugha ishirini na mbili , hilo sio jambo la kawaida kwa mtu wa kawaida Erick , watu wa nmna hio huenda wakawa majasusi wanaofanya kazi kwa siri au ni Assasinators”.

“Ndio muheshimiwa nimejaribu kufatilia taarifa Zaidi kuhusu mahali anapotokea na alipozaliwa inaonekana hakuna taarifa hizo”Mheshimiwa huyu alimwangalia Erick kwa muda na kisha akafikiria jambo.

“kazi nzuri Erick unapaswa kwenda sasa , mpaka hapo nitaendelea mwenyewe”

“Sawa mheshimiwa”

Baada ya Erick kutoka Kigombola alitafuta namba ya simu yenye kodi ya nje ya nchi na kisha kupiga simu.

“Mr kigombola it`s pleasure to hear from you after long while”

“It s true mr Keneddy and am so sorry thar I did not contact you for this long but you are one of people that have special place in my life”

“It`s good you realise that , but I presume this call has request you want to ask me”.

“Its true kenneddy , I need all informations regarding someone who graduated at harvad”

“Just give me the name and I will look for it in minutes”

“He is Roma Ramoni he is now living here in Tanzania”

“Okey wait a second I will get back to you”

Mheshimiwa alikata simu akisubiria taarifa hio na alichokuwa anawapendea wazungu nikwamba ukiwaomba jambo hawanaga maswali mengi ,ingekuwa ni wabongo angekuwa ashakuuliza maswali kibao kwa mfano unataka taarifa zake za nini na ilichukuwa dakika chache tu taarifa simu yake ilianza kuita.

“ Yes Kennedy”

“I got info.. about him , it seems odd but it is true there is information regarding him graduating at havard business School”.

“What is odd Kennedy?”

“He was adopted with one of Michigan tycoon in business Mr Robert Eglon from when he was fourteen”.

“So what is Odd”

“There is no information regarding where he lived before being adopted”

“You mean there is no info .. like he was from Tanzania or anything like that?”

“Yes!, that which looks Odds Kigombola”.

Huyu Roma ni nani” Ni swali pekee ambalo liliibuka kwenye kichwa chake maada ya kupataa maelezo hayo kutoka kwa Kennedy , aliemwambia kuwa ni kweli Roma anaonekana kumaliza chuo Harvad lakini pia anaonesha kulelewa na familia ya mfanyabiashara mkubwa huko Michigan Marekani lakini jambo ambalo linaonekana sio kawaida ni kwamba haikuelleweka Roma aliishi wapi kwa miaka kumi na tatu nyuma kwani alianza kulelewa akiwa na miaka kumi na nne.

“Nadhani swala pekee ni kuagiza vijana wangu wamteke ili tumuhoji nadhani ndio njia rahisi”Aliwaza mheshimiwa
 
Tuendelee kula mtori nyama zipo chini
DAUDI 1 Shunie Peramiho yetu y-n Doctor G
IMG_20220812_210956_515.jpg
 
WAKUBWA NIMEWEKA VIPANDE VYA KUTOSHA TUTAONANA BAADA YA WIKI KUISHI , ILA UNAWEZA KUNIPATA WATSAPP:0687151346

GRUPU IPO SEHEMU YA 25 LEO LIPA 2000 UNISAPOTI NIKUUNGE GRUPU USOME KWA SPIDI YA 4G, UKILIPA NAKUTUMIA WALIKOPITA WENZAKO , NAMBA ZA MALIPO NI 0687151346AIRTEL/0657195492TIGO/0623367345 HALOTEL UKILIPA NICHEKI WATSAPP NAMBA 0687151346 JINA ISSAI SINGANO GRUPU N UNAUNGANISHWA KWA MWEZI.
KAMA HUPENDI KUUNGWA KWENYE GRUPU NAKUTUMIA INBOX
Asante sana mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom