Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA SITA

Najma alimwangalia Roma aliekuwa na Begi lake mgongoni na kumfanya taswira ya miezi sita nyuma ijijenge katika kichwa chake , alikumbuka siku ambayo alimpokea Roma alikuwa amebeba begi hilo hilo utofauti wa leo ni kwamba Roma alikuwa kwenye mavazi mazuri kuliko kipindi kilichopita.

“Kaka anaroho mbaya ni kweli kamfukuza Roma kama alivyosema”

Najma alimwangalia Roma kwa uso uliojaa maswali mengi , huku akiwaza moja kwa moja kuwa Juma atakuwa amemfukuza Roma na sasa Roma alikuwa akiondoka kwenda kupanga kwingine.

“Najma naomba tuongee kabla sijaondoka”

“Juma naomba niongee na Najma , sitaki kuacha deni nyuma”Aliongea Roma na Juma alitikia kwa kutingisha kichwa huku akiwaacha.

“Jana ulikuwa wapi Roma , Nisamehe kaka yangu kachukua maamuzi ya kukufukuza”

“Nifate Najma nje tukaongee”aliongea Roma huku akitangulia na Najma alitangulia , ila Najma alishangaa pale alipomuona Roma akifungua mlango wa gari ya kifahari ambayo hakuwahi kuwaza mtu kama Roma anaweza kuinunua , ghafla yale mawazo aliokuwa nayo juu ya Roma kuwa mtu mkubwa aliekuwa akijifanyisha masikini yalianza kurudi upya , ila kwake hakuwa na shida , aliingia ndani ya gari kwa kusitasita.

“Hii gari umeitoa wapi Roma , ni nzuri mno nitakuja kununua yangu kama hii”Aliongea Najma na kumfanya Roma Atoe tabasamu lililojaa uchungu moyoni mwake kwani aliamini taarifa anayokwenda kumwambia mwanadada huyu itamwachia machungu mengi moyoni.

“Najma naomba unisikilize jambo ninalokuambia, na pia nitaomba unisamehe kama nitakukwaza na kukuumiza , ila sitaki kukuficha ukweli wote Najma”Aliongea Roma na kumfanya Mrembo huyu amwangalie.

“Usijali wewe niambie tu Roma nipo tayari kusikilia lolote ili mradi liwe jambo la ukweli”Roma alivuta pumzi na kukusanya ujasiri aliokuwa nao ndani yake .

“Jana nimefanikiwa kukutana na mwanamke niliepotezana nae kwa miaka mingi ambaye nilidhania amefariki na baada ya kuonana tumefunga ndoa rasmi na unavyoniona hapa mimi ni mume wa mtu , najua ni kiasi gani unanipenda Najma na ndio maana siku zote nilikuwa nikijizuia kutokuzikubali hisia zako….”Roma kabla hata hajamaliza mlango wa gari ulifunguliwa na Najma alitoka na kukimbilia ndani kwao hakutaka tena kusikiliza maneno ya Roma,

Roma alibaki akiwa hajui ni kipi afanye , lakini hakuwa na jinsi , ili mradi ashauweka wazi ukweli wote mbele ya Najma, basi aliona ni vyema kwa mwanadada huyo kumsahau kaika maisha yake.

****

Ni muda wa Asubuhi ndani ya jengo la Club B, katika chumba ambacho kilikuwa ni ofisi ya mwanadada mrembo maarufu ndani ya eneo hili la Chalambe Maji matitu , alionekana Rose akiwa amekaa kwenye kiti chake cha kuzunguka huku mbele yake kukiwa na tarakishi kubwa iliokuwa imewashwa , huku mwanadada huyu akionekana kusoma taarifa iliokuwa kwenye mfumo wa Softcopy.

Ofisi yake ilikuwa ni kubwa , iliokua imependezeshwa na samani za bei ya juu kuonesha kuwa mwanadada huyu hakuwa vibaya kwenye swala la kifedha na kwa namna alivyokuwa amevaa na namna ambavyo alikuwa kaitumia Tarakishi hio alionekana kuwa Profesheno.

Baada ya dakika kadhaa za kukaa hapo ndani , mlango wake uligongwa na akaingia kijana mmoja alievalia suti na miwani ya jua akiwa na kipara kilichokuwa kinang`aa , bwana huyu alionekana kuwa ni wale vijana waliokuwa wakifanya mazoezi.

“Niambie Zonga unataarifa gani?”

“Madam taarifa niliokuwa nayo ni kwamba Roma kapata mke”

“Unamaanisha nini?”

“Kwa taarifa nilizokuwa nazo sasa Roma kafunga ndoa jana na leo amekuja sehemu anayoishi na kuchukua mizigo yake na kuhamia kwa mke wake”Maneno ya Zonga yalikuwa kama kisu cha moto kilichokuwa kikipita katika moyo wa mwanadada huyu.

“Bosi..!”Aliita zonga mara baada ya kumuona bosi wake akitoa machozi, na Rose aliyafuta haraka haraka na kisha aliachia tabasamu la ujasiri.

“Endelea kufatilia ni mwanamke gani Roma kamuoa” Aliongea Rose na Zonga alitoka

“Huyu fala ana nyota bwana , yaani mrembo kama bosi anatoa machozi kwa ajili ya fala mbeba mizigo , huyu jamaa ana nini mimi sina” Alijiongelesha Zonga ndani ya moyo wake huku akitoka ne ya ofisi.

Rose alisimama na kusogelea dirisha na kuangalia baadhi ya watu waliokuwa kwenye pilikapilika za kutafuta maisha huku akionekana ni mwenye mawazo sana huku akijizuia kulia.

“Stori yetu haiwezi kuisha hivi Roma ,Siku ulionikoa kwenye mikono ya baba yangu ndio ulikuwa mwanzo wa stori yetu na haikuwa bahati mbaya hata kidogo , nimetumia pesa nyingi sana kukutafuta na mpaka kukupata , siwezi kukuachia kirahisi” Alijiongelesha Rose.

****

Roma hakujali sana , aliendesha gari lake mpaka Kigamboni na kupokelewa na Bi Wema kwani mke wake hakuwa amerudi kutoka kazini, baada ya kuweka lile begi , alitoka nje na kuzunguka upande wa Yard ya magari huku mkononi akiwa ameshikilia kile kiboksi alicho toka nacho Mbagala , aliangalia sehemu ya kificha kiboksi hiko , lakini hakupata na mara akapata wazo na kuondoka ndani ya eneo hilo na kuingia chumba cha mazezi , aliangalia sehemu rahisi ya kuhifadhi kiboksi hicho , na alifanikiwa kupaona na kisha alikiweka vizuri na kuziba na kisha alitoka nje.

Baada ya kurudi ndani kwenye chumba chake aliwasha tarakishi na kisha akaingia kwenye mtandao na kuangalia namna ya kupata kazi , bahati nzuri , aliona baadhi ya makampuni mbalimbali yaliokuwa yakitangaza ajira , alichagua kazi aliona inafaa na kisha aliandika CV yake na kuituma pamoja na vivuli vya vyeti ambavyo alivitoa kwenye akaunti ya Barua Pepe yake , aliomba kwenye kampuni tatu harakaharaka na kisha alijilaza kitandani , lakini hakukaa muda mrefu , aliitwa na Bi wema na kuambiwa chakula tayari ashuke wakale.

Roma baada ya kula chakula kitamu kilichokuwa kimeandaliwa na Bi Wema , alirudi chumbani kwake huku kwenye kichwa cheke akiwa na mpango wa kwenda kupiga misele mjini maana alikuwa na kiasi cha pesa kilichokuwa kikimruhusu kufanya hivyo.

Alijiandaa haraka haraka, kwa kuvalia tisheti yake iliomtoa vyema na Jeans pamoja na Raba kisha alichukua ufunguo wa gari na kumuaga Bi Wema na kisha alitoa gari nduki.

Masaa machache tu alikuja kuonekana akiwa maeneo ya Posta kwenye moja ya saluni ya kisasa maarufu ,aliegesha gari yake kwa ustadi mkubwa huku waliokuwa karibu na eneo hilo wakiliangalia gari lake kwa matamanio.

Roma hakujali sana , alitoka kwenye gari na kisha aliingia ndani ya saluni hii ya kiume kwa ajili ya kutengenezwa nywele zake kitendo ambacho kilifanyika kwa muda mfupi sana , baada ya kupendeza kwa staili aliokuwa anataka yeye , aliendesha gari yake kuelekea upande wa Ocean road.

Muda wa saa kumi na mbili ndio muda ambao Roma alikuwa anarudi na sasa alikuwa anaingiza gari yake ndani ya jumba lao la kifahari , lakini ile anaingia aliona gari ambayo kwa haraka haraka alijua sio gari ya Edna , aliamini kulikuwa na ugeni ila hakujua ni ugeni wa mtu gani , ila aliamini kwakuwa ashafika , basi majibu ya maswali yake yatajibiwa akiingia ndani.

Baada ya kuingia ndani ni kweli aliona mwanaume mmoja ambae baada ya kumwangalia sura yake ilikuwa inakuja hivi na kupotea , mwanaume huyu hakuwa peke yake bali na mke wake alikuwepo.

“My Wife Am back!”Aliongea Roma na kumfanya kijana aliekuwa amekaa kwenye sofa amwangalie huku akionyesha chuki ya waziwazi na Roma aliliona hilo na kwakua alikuwa sio mtu wa kujali sana alisogea upande wa kushoto alipokuwa mke wake na kumbusu shavuni , kitendo ambacho Edna hakuzuia na Roma aligundua jambo pia kwa mara ya pili.

“Babe huyu ni nani?”

“Anaitwa Abubakari ni mwanaume ambaye nilikuwa nikikuambia”.

“Oooh ! unamaanisha yule mwanaume ambaye humpendi ndio huyu bwana”.

Maneno hayo yalimkera mno Abuu ila alijitahidi kujizuia mbele ya Edna.

“Braza vipi mimi ni Roma , ni mume wa Edna nimesikia habari nyingi juu ya kumsumbua mke wangu hivyo braza kaa mbali na mke wangu ama nitakufanya jambo baya”Aliongea Roma na kumfanya Abuu atabasamu kifedhuli.

“Wewe mbeba mizigo utanifanya nini labda.. usifikiri nimekaa kimya ukajua nakuogopa Edna ni wangu wewe ni wakuja tu na muda wowote utaondoka na kuurudia umasikini wak..”Ilikuwa ni kitendo cha haraka sana ambacho Roma alikifanya kwani kabla ya Abuu hajamaliza kuongea alikuwa hewani akining`inia kwenye mkono wa Roma,bwana huyu alikuwa akivuta pumzi kwa shida huku akijaribu kuongea neno lakini ni kama Roma hakujali na nia ya kumuua bwana huyu ilionekana waziwazi kwenye macho ya Roma.

“Roma Stoop..!!”Ilikuwa ni sauti ya kitetemeshi ya Edna iliomfanya Roma amtupe Abubakari chini kama furushi.

“Nikihesabu mpaka nne bado upo hapa ndani nakuaa .. moja,, mbili .. tatu..” Lakini kabla hajamaliza Abuu alisimama na kumwangalia Roma kwa macho makali na kisha alitoka huku akishika shingo yake, na hii ni baada ya kuona kuwa Roma hakuwa akitania kwani macho yake yalikuwa yamejaa hasira kali kiasi kwamba alionekana kuwa tayari kwa kuua muda wowote.

Upande wa Edna alishangazwa na uwezo wa nguvu aliokuwa nao Roma, namna ambavyo Roma alimning`iza hewani Abuu kilimuogopesha na kumuacha kwenye maswali.

“Mbona haupo makini Roma , unajitafutia matatizo , unajua nguvu iliokuwepo nyuma ya Abuu wewe?”

“Kwa hio kukiwa na nguvu kubwa nyuma yake nimuogope na akikanyaga mguu wake hapa tena namuua..”Aliongea Roma huku kiini cha macho yake kilichokuwa kimebadilika rangi kuwa kijani kilirudi na kuwa kama kawaida na kutokana na hasira alizokuwa nazo Roma hakutaka kubaki hapo sebuleni na kupandisha ngazi kwenda chumbani kwake na kufunga mlango kwa nguvu , huku akimuacha Edna aliekuwa akimwangalia kwa wasiwasi mkubwa.

Baada ya Roma kuingia kwenye chumba chake moja kwa moja alienda kuoga huku akituliza hasira zake, baada ya kujiona yupo sawa alisogelea Laptop yake na ile anaiwasha aliona ‘Notification’ kwenye barua pepe ikionesha kuna ujumbe , alifungua na kukuta kuna jumbe tatu.

“Mr Roma Ramoni we are happy to inform you that tomorrow we would like to do an interview with you regarding the job request you submitted to us , it will be our honor to see you tomorrow at xxx time”

“Ndugu Roma tunafuraha kukuambia kwamba tunapenda kufanya usaili na wewe kesho kulingana na ombi la kazi uliloliwasilisha kwetu , itakuwa heshima kwetu kama tutakuona kesho”.

Alifungua meseji ya pili na kisha akasoma.

“Hellow Mr Roma Ramoni we reviewed your job Request and your Credential’s that you submitted to us and confirmed they are Valid,We are replaying back to inform you to attend interview tomorrow morning at xxx time”

Karibia kampuni zote tatu zilikuwa zimerudhisha majibu ya kumtaka Roma kwenda kwenye interview siku ya kesho , alitabasamu na kuona kumbe kutafuta kazi ni rahisi hivyo, lakini licha ya majibu hayo alipanga kwenda kwenye kampuni moja tu na hivyo alitakiwa kuchagua kamouni moja ya kwenda kwa siku ya kesho.

“Vexto Group of Companies ndio moja ya kampuni ambayo Roma alidhamiria kwenda kufanya usaili kesho , kilichomvutia kuhusu hii kampuni kwanza ilikuwa ni kampuni kubwa sana ndani ya Afrika Mashariki na Kati yote ambayo ilikuwa inaendeshwa kwa thamani ya pesa kiasi cha Dola bilioni ishirini, Pili makao makuu ya kampuni hii yalikuwa makao makuu ya kampuni ya mavazi na mitindo ifahamikayo kwa jina la E- Styllus Wear , kampuni ambayo ilikuwa ikiaminika kwa kuwa na warembo wakali.

“Hii ndio kampuni nzuri , nitakutana na warembo wengi”

SEHEMU YA SABA

Muda wa saa mbili kamili za usiku Roma alishuka kwa ajili ya chakula , chakula ambacho alikula kama alikuwa na njaa ya wiki nzima , kwani alimaliza kalibia chakula chote kilichokuwa kwenye mabakuli.

Edna aliishia kujisemea kuwa Roma hakuwa ni mwenye aibu hata kidogo kwa upande wa Bi Wema alifurahishwa sana na uwezo wa kula wa Roma.

“Bebi Edna kesho naenda kwenye usaili”

“Sawa mafanikio mema”Aliongea Edna huku akinyanyuka na kutoa vyombo na baada ya kumaliza alipandisha ngazi na kwenda chumbani kwake , upande wa Roma hakuwa na mudi ya kubaki ndani hapo kwani alitoka na funguo zake na kuondoka.

Nusu saa mbele alikuwa alikuwa akiingia Chalambe Mbagala katika Rango kubwa la Club B, aliegesha gari lake na kuingia ndani huku akikutana na watu waliokuwa wamechangamka.

Zonga ndio mtu wa kwanza kumuona Roma, na alimsogelea kisha akamkaribisha kwa bashasha.

“Rose yuko wapi?”

“Madam Boss yupo ofisini kwake , itakuwa vyema kama utaenda kumuona”Aliongea Zonga na Roma alichukua upande ambao ofisi ya Rose ilikuwepo , alifungua mlango bila kugonga na kuingia ndani na kumkuta Rose aliekuwa amejiegamiza kwenye masofa huku pembeni kukiwa na chupa kibao za bia.

“Romaaa!”Aliongea Rose huku akinyanyuka na kivivu na kumsogelea kisha akamkumbatia huku machozi yakiwa yanamtoka , alianza kulia kwa kwikwi kiasi ambacho kilimshangaza Roma.

“Roma kwanini hukuniambia unamwanamke mpaka unaniumiza kiasi hiki”Aliongea Rose na kumfanya Roma atambue Rose anataarifa za yeye kuoa , Roma hakutaka kuongea chochote Zaidi ya kumtoa kifuani na kumwangalia usoni na kuona uso wa mrembo huyu ulivyokuwa kwenye majonzi , alisogeza mdomo wake na kugusisha na mdomo wa Rose na mwanamke hakuleta shida kwani aliupokea kwa pupa na walianza kukiss huku hisia zikiwa zinaongezeka kila baada ya sekunde

Ni ndani ya robo saa mbele Rose na Roma walionekana ndani ya kitanda kilichokuwa ndani ya ofisi hii ya Rose , huku mwanadada huyu akitoa miguno ambayo ilimfanya Roma kuongeza spidi ya kupiga kiuno.

Mchezo ulichukua Zaidi ya dakika tisini mpaka pale ambapo Roma aliweza kutua mzigo wake huku akiwa ni mwenye kuhema kwa nguvu , lakini kwa upande wa Rose akionekana akiwa hoi,Roma alimwangalia mwanadada huyu na kuona alikuwa kwenye maumivu na yote hio ni mara baada ya kugundua kuwa Rose alikuwa Bikra , jambo hili lilimshangaza.

“Twende nyumbani kwako , nitalala huko”Aliongea Roma na Rose alitingisha kichwa na walikokotana kwamlango tofauti na ule wa Bar na kisha Roma alimpandisha Rose kwenye Gari na kuondoka.

Sehemu aliokuwa akiishi Rose ni hapo hapo kwani walichukua dakika mbili kufika ndani ya Jumba la Kifahari la mwanadada huyu.

Roma alimsaidia Rose kwa kumkanda sehemu zake za siri ili kupoza maumivu na kisha waliingia kwenye shuka na kukumbatiana.

“Masikini nimeshakuwa mchepuko”

“Ndio huo ndio uhalisia unaopaswa ukubali , lakini sitokulazimisha kuendelea na mimi”

“Siwezi Roma nipo tayari kuwa mchepuko wako ila sio kukukosa kabisa”

Roma hakuongea kitu Zaidi ya kumkumbatia Rose huku akitabasamu.

“Mke hatanuna ukilala kwangu?”

“Hilo lisikusumbue mrembo eh , au unataka niondoke”

“Hapana nimeongea tu baba usiondoke”

“Saa moja kamili Roma aliamka na kuanza kumpapasa Rose ambaye alimpa ushirikiano wa kutosha na ndani ya dakika kadhaa mbele walipiga cha asubuhi na Roma akaingia bafuni na kumuaga Rose kwa kumuambia kuwa alikuwa na Usalili na kampuni

“Karibu nyumbani Mr Roma”Aliongea Bi wema baada ya kumuona Roma akiingia sebuleni , na wakati huu Bi wema alikuwa na Edna mezani wakinywa chai ya Asubuhi.

Roma alisalimia , huku akiliwa buyu na Mke wake wala hakujali na kukaa mezani na kujisevia msosi na kuanza kula kama hana akili nzuri , hakujali macho mabaya ya Edna.

“Bi Wema Asante kwa chai nzito , mimi ngoja nikajiandae kwa ajili ya kwenda kwenye usaili”.

“Bebi Edna niweke mume wako kwenye maombi nipate kazi”Aliongea Roma na bila hata ya kusubiri jibu alipandisha ngazi kuelekea kwenye chumba chake.

Ni muda waa saa tatu na nusu Roma aliegesha gari yake sehemu maalumu ndani ya jengo hili refu lililokkuwa likipatikana ndani ya Posta mtaa wa Samora , baada ya kutoka kwenye gari moja kwa moja alienda mapokezi na kujieleza kwa mwanadada mmoja mrembo huku akiwa ni mwenye kushangazwa na uzuri wa kila mfanyakazi wa kampuni hii.

“Hii sehemu ni sahihi kabisa kwangu”Alijiongelesha Roma huku akimkonyeza mrembo Mmoja aliekuwa eneo la mapokezi na mrembo huyo alitabasamu na kisha kumpita Roma .

Roma alishangazwa na watu waliokuwa wamekuja kwa ajili ya usahili kwani wote walikuwa ni wanawake tena warembo huku mwanaume aliemuona hapo ndani ni mmoja tu , tena ni jamaa mmoja hivi kibonge.

“Hey Boy na wewe umekuja kwenye usaili?”

“Ndio kaka , vipi wewe?”

“Hata mimi pia ,niite Jacob”

“Namini niite Roma”

“Sasa Roma wewe nini kimekuvutia kuja kuomba kazi hapa?”

“Sababu kubwa mimi ya kuja kuomba kazi hapa ni Warembo , nasikia hii kampuni ina mapini sio mchezo”

“Kaka nadhani umejionea mwenyewe ni kweli hii kampuni imejaa warembo”

“Vipi wewe?”

“Mimi sababu kubwa sio warembo ila kuna mrembo mmoja ndio amenifanya kuja kufanya kazi hapa”

“Yupi huyo”

“CEO”

“Unamaanisha CEO wa hii kampuni ni mwanamke na ni mrembo pia?”

“kaka ndani ya hii kampuni hakuna anaemfikia kwa uzuri CEO , kama huamini uliza uambiwe”Aliongea Kibonge

Wakati Roma na kibonge wanaongea , kibonge zamu yake ilifikia na kuingia kwenye chumba cha usaili na baada kama ya nusu saa alitoka huku akionekana kama mtu aliekosa tumaini.

“Vipi kaka mbona hivyo”

“Nimeulizwa maswali yote nimeshindwa kujibu sina ninalojua , ndoto yangu ya kuwa karibu na CEO imekufa kila la kheri kaka”Aliongea Kibongea na wakati huo huo Roma alisikia jina lake na kusogelea mlango na kuingia .

Ile anaingia tu alijikuta akipokewa na sura mbili anazozifahamu na sura moja asioifahamu , jumla ya wasaili walikuwa watatu , mtu wa kwanza Roma alimkumbuka vyema kwa urembo wake , lakini sio hivyo tu pia alimkumbuka kwa kumsaidia Shilingi Elfu tano siku ambayo aliachwa njiani na mke wake Edna, Mrembo yule msaili pia alimkumbuka vyema Roma na kujikuta akitabasamu mara baada ya kukutanisha nae macho,Siura ya pili Roma kuifahamu ni mdada alipishana nae Mapokezi , huyu ni mrembo aliemkonyeza.

“MisterRoma Ramoni nini kimekuvutia mpaka ukaomba kufanya kazi na sisi??”Aliuliza mrembo wa Buku tano.

“Kilichonivutia kwakweli si kingine Zaidi ya warembo, napenda kufanya kazi kwenye mazingira ambayo nazungukwa na warembo”Alijibu Roma kwa kujiamini na kuwafanya wasaili waangaliane na kutabasamu.

“Okey Mr Ramoni kwenye CV yako ulioanisha kwamba unajua kuzungumza Lugha za mataifa mbalimbali Zaidi ya kumi jambo ambalo tunamashaka nalo licha ya kwamba vyeti vyako vinaonesha una Masters ya uongozi wa biashara kutoka chuo cha Harvard , hivyo basi tumekuandalia maneno kumi ya lugha tofauti tofauti unazojua ili utuambie maana ya hayo maneno”

“Hakuna shida hilo ni rahisi sana kwangu”Aliongea Roma na kisha yule dada wa Mapokezi alionyesha maneno hayo kwa kutumia tarakishi na projekta na Roma alianza kusoma maneno hayo.

Yalianza kuonekana maneno ya kijerumani na Roma aliyasoma na kuyatolea tafsiri na wale walithibitisha ni sahihi , ikaja lugha ya kiarabu nayo hivyo hivyo , ikaja lugha ya kireno ikawa hivyo hivyo , ikaja kifaransa , kikorea , kichina Kinyarwanda …

Wasaili hawa walishangazwa mno na uwezo wa Roma , hawakuwahi kukutana na mtu ambae anajua Lugha nyingi kama Roma ..

Roma aliulizwa maswali mengi mengi na kuyajibu kiufasaha na wasaili wakakubaliana kumpa kazi Roma katika kitengo cha Public Relation.

“Karibu Vexto Roma, kwa kupata kwako kazi naamini Mke hatakuacha njiani tena mpaka kukosa nauli”Aliongea mwanadada yule msaili huku akitabasamu.

“Asante sana”

“Naitwa Doris Alex afisa mwajiri mkuu wa kampuni”.

“Nafurahi kufahamina na mrembo kama wewe Doris”Aliongea Roma na kumfanya mwanadada huyu kutabasamu na kufanya mashavu yake kuacha vishimo(Dimples)

“Naomba nichukue fursa hii kukuonesha baadhi ya maeneo ya kampuni kabla hatujaanza kazi rasmi”Aliongea Doris na Roma alitingisha kichwa na wote wakaingia kwenye Lift , Roma muda wote tabasamu halikuwa likimwishia usoni , alijiona kama vile yupo kwenye mbingu ya warembo, mrembo Dorisi alikuwa amempagawisha mno.

“Hii ndio Floor ambayo viongozi wa juu ya kampuni ofisi zao zipo , hii ni ofisi ya mhasibu mkuu wa makampuni ya Vexto , hii ni ofisi yangu”Huku wakiingia na Roma aliisifia ofisi ya Doris.

Wakati Dorisi akiendelea kumpa shule Roma mara simu ya ofisi yake ilitoa mlio kuashiria inaita , alipokea na kuweka sikioni na kisha akashusha mkonga.

“Unaonekana kuwa na bahati sana Roma,CEO anataka kuonana na wewe jambo ambalo sio la kawaida”Aliongea Doris na alimpeleka mpaka kwenye mlango wa ofisi uliojitenga na kisha alifungua na kukutana na sekretari alimchangamkia na kumkaribisha , Sekretari alikuwa wakawaida sana , hakuwa mrembo sana.

“Boss! Mr Ramoni has arrived”Aliongea Sekretari

“Let him in”

“You may go in na tafadhari hakikisha unakuwa na heshima mbele ya bosi , sio mtu ambaye kila mtu anaweza kuingia kwenye ofisi yake”Aliongea mwanadada huyu na Roma aliingia ndani ya ofisi hio kubwa huku akiwa na tabasamu la kukutana na CEO mrembo maana kwenye kichwa cheka alikuwa akikumbuka maneno ya Kibonge aliekuja nae kufanya usaili muda mfupi uliopita.

“Akinivutia namtongoza ,CEO kitu gani bwana”aliwaza

Roma alijikuta akipagawa baada ya kumuona mtu ambae hakumtegemea kuwa ndio CEO”

ITAENDELEA JUMATATU WADAU
 
CEO ni mkewe.
 
SURA YA NANE

Abubakari Hamadi ni mtoto alielewa ndani ya familia ya tajiri maalufu ndani ya Tanzania afahamike kwa jina la Alex Kaoneka tokea akiwa mdogo ,Mzee Alex kaonekana alimchukua Abuu ndani ya kituo cha kulelea watoto yatima ndani ya wilaya ya lushoto miaka ya nyuma wakati akiwa moja ya wafadhili wakuu wa kituo hicho.

Moja ya sababu kubwa ya Mzee Alex kuvutiwa na Abuu ni kutokana na uwezo wake wa akili, kwani katika watoto wote waliokuwa ndani ya kituo hiki Abuu peke yake ndie aliekuwa akionesha uwezo wa kipekee sana wa akili kuwashinda wenzake wote.Sababu ya pili ya mzee Alex kumchukua Abuu ni kutokana na Mzee huyu kubahatka kupata watoto wa kike tu katika familia yake.

Miaka ya nyuma Mzee Alex wakati anamuona Abuu alikumbuka ugonjwa aliokuwa nao ambao aliupata na kumpelekea kupoteza uwezo wake wa kumpa mimba mwanamke, na kupitia ugonjwa huo alikuwa akiishi sana kwa mawazo , kwani aliona licha ya kuwa na mali nyingi , lakini alikosa mtu ambaye anakuja kumrithi na tumaini lake lilikuja kufufuka tena mara baada ya kumpata Abuu.

Mke wake Bi Anna alipinga vikali swala hilo , ila kwa mzee huyu alikuwa na tabia moja tu , akishafanya maamuzi hakuna mtu wa kumzuia , hivyo mke wake hakuwa na nguvu tena ya kumshawishi na hivyo kukubaliana nae na wakamchukua Abuu katika familia yake.

Sifa kuu ya Mzee Alex katika maisha yake ni ubaguzi wa kijinsia , bwana huyu alisifika sana kwa kudharau wanawake na katika maisha yake aliamini kwamba wanawake hawawezi kufanya vitu ambavyo vilikuwa vikifanywa na wanaume na kwa kasumba hio iliokuwa imejaa ndani ya akili yake hakuwahi kufikiria kuwarithisha kabisa watoto wake makampuni yake na chaguo sahihi kwake ilikuwa ni Abuu.

Abuu alikulia kama mtoto kabisa wa Mzee Alex kwa kupokea matunzo na upendo wote ambao kama mtoto ni moja ya mahitai yake makuu , alilelewa kitajiri , alisoma katika mashule makubwa ya hela nyingi, maisha ya Alex yalibadilika kabisa na hakuwa yatima tena bali alikuwa mtoto mwenye familia ambayo ilikuwa ikimjali , lakini licha ya hivyo Abuu hakuwahi kuwaza kubadili dini yake kutoka uislamu kwenda kwenye ukristo na mzee Alex pia hakuwa na shida juu ya hilo kwani kwanza hakuwa mpenzi wala mfatiliaji sana wa Imani za kidini , kwake Imani yake kubwa ilikuwa ni Pesa , alikuwa akiabudu pesa kama Mungu wake, na alikuwa yupo tayari kufanya lolote juu ya pesa na aliamini matatizo yote yanaweza kutatuliwa na pesa.

“Kama matatizo yote ninaweza kuyatatua kwa kutumia pesa kuna haja gani ya mimi kuwa na dini inayomhusisha mtu asieonekana , mimi naamini vitu vinavyonekana kama pesa”Ni siku moja mzee huyu alipokuwa akihojiwa na kituo kimoa cha Redio.

Kama alivyopanga mzee huyu baada ya Abuu kumaliza masomo yake ya chuo kikuu kutoka Princeton Marekani alirudi Rasmi nchini kwa ajili ya kufanya kazi katika makampuni ya baba yake , mwanzo wa kufanya kazi katika makampuni haya ndio mwanzo uliomfanya kijana huyu kumfahamu mwanamke mrembo CEO ,afahamikae kwa jina la Edna Adebayo.

Mara yao ya kwanza kukutana na mwanadada huyu ni kipindi ambacho alikutana na mwanadada huyo kwa ajili ya mazungumzo ya kibiashara juu ya bidhaa mpya ambayo ilikuwa ikifanywa kimkataba baina ya kampuni mbili yaani Vexto na JR , kipindi hiki Abuu alikuwa ni Assistant CEO na kwa mrembo Edna alikuwa pia Ni Assistant CEO.

“Abuu Nadhani umemuona Edna?”

“Ndio baba”

“Mzuri Eh?”Aliuliza mzee huyu wakati wakiwa ndani ya kampuni hii ndani ya ofisi ya Mzee Alex.

“Nimzuri sijawahi ona baba, nimemkubali”

“Haahaha.. ndio maana nimekupatia dili hili la kibiashara ulifanyie kazi”Abuu alishangaa huku Mzee Alex akitabasamu huku akinywa wine iliokuwa kwenye glass kidogo na kurudisha kwenye meza.

“Unajua katika familia ya Adebayoo , wanawake ndio wanaongoza familia na ndio maana mpaka sasa unaona kampuni karibia yote imejaa wanawake , Mzee Adebayoo mwenyewe hana nguvu kwa mke wake na yeye ni mmiliki wa kampuni pekee alizoanzisha yeye , lakini za kifamilia hana nguvu yoyote”Abuu alishangaa lakini mzee huyu aliendelea

“Mzee Adebayoo mtoto pekee aliekuwa naye ni Edna na kwa maana hio ni Dhahiri miaka ijayo mrithi mkuu wa makampuni yote ya Vexto yatakuwa chini yake baada ya mama yake kuachia uongozi na ndio maana unamuona Edna sasa hivi yupo kwenye nafasi kama yako”

Abuu alionekana kumuelewa baba yake huyo mlezi anakoelekea.

“Labda nikuambie tu kampuni ya Vexto ni kampuni yenye nguvu kubwa kwa ukanda wetu huu wa Afika mashariki na Kati , nguvu yake ni kubwa mno na hakuna kampuni yoyote inayoweza kuipita likija swala la nguvu , kampuni inayofuatia ni ya kwangu , lakini bado sijaridhika na nafasi ya pili , nataka kampuni yangu miaka ijayo ichukue nafasi ya Vexto na hii ndio misheni yangu kubwa mabayo nataka kuitimiza kabla ya kuingia kaburini , hivyo njia pekee ya mimi kukumiliskisha makampuni yangu na kuyaongoza ni kuhakikisha unampata Edna anakuwa mkeo , akishakuwa mkeo automatically kampuni itakuwa yako na hapo utaifanya kampuni ya Vexto kuwa sehemu ya JR na kampuni yetu itakuwa na nguvu kubwa mno kiasi cha kampuni yoyote ile kuifikia”

Abuu alielewa sasa maelezo ya baba yake na ndoto aliokuwa nayo , maana katika maisha yake alikuwa akiwaza ni namna gani anaweza kumfurahisha baba yake huyo wa kambo ili amuaachie nafasi katika makampuni yake , lakini siku hio ndio alipopata kujua ni nini ndoto ya baba yake.

Kwanzia siku hio Abuu alianza kuweka ukaribu na Edna , alijaribu kumtongoza mara kwa mara apatapo nafasi , kumjali na kujipendeza kwake , lakini kwa Edna hakuambulia chochote , kwani mwanamke huyo alikuwa mgumu kama chuma , lakini licha ya hivyo Abuu hakuwahi kukata tamaa , aliamini Edna ni mwanamke na wanawake wameumbiwa kuwa wadhaifu kuliko wanaume hivyo aliamini ipo njia ya kumpata.

Miaka miwili mbele ya Abuu kuhangaika , mama yake Edna alifariki kwa ugonjwa wa kisukari na hapo ndipo Edna aliporithishwa uongozi wa juu wa kampuni ya Vexto na kuwa CEO na mmiliki halali wa makampuni hayo , jambo ambalo baba yake Edna alilipinga vikali , lakini kwakua sheria ilikuwa ikimlinda Edna basi baba yake Edna hakufua dafu mbele ya sheria .

Mzee huyu baada yakuona amekwama kabisa juu ya mpango wa yeye kumiliki kampuni ambazo zilikuwa zikimilikiiwa na mke wake na hatimae kuangukia kwenye mikono ya mtoto wake , mipango aliokuwa nayo miaka mingi ya kumiliki mali za familia na hapo ndipo alipokuja kutafuta mbinu mbadala , katika kutafuta kwake mbinu mbadala ndipo alipomuaomba ushauri rafiki yake mkubwa Alex kaoneka , sababu za mzee huyu kumuomba ushauri ni kutokana na kwamba mzee huyu alikuwa akijua kuwa kijana wa Alex alikuwa akimpenda Edna.

“Mimi naona njia pekee ya wewe kumshinda Edna ni kumfanya aolewe na Abuu kijana wangu , Edna akishaingia kwenye mikono ya Edna kihalali jina lake litabadilika kutoka kuwa Adebayoo mpaka kuja kuwa jina la Familia yangu na hapo mwanafamulia pekee ambaye utabaki kuwa na uhalali kwa kumiliki makampuni ya familia ni wewe”Aliongea Mzee alex na kumfanya Adebayoo kutabasamu , aliona hilo lilikuwa ni wazo zuri mno.

Baada ya ushauri huo kutoka kwa rafiki yake moja kwa moja alianza harakati za kumlazimisha Edna kuolewa na Abuu , jambo ambalo Edna alilipinga vikali , kwanza alikuwa na sababu nyingi sana za kumkataa Abuu , sababu ya kwanza ni kwamba hakuwa amempenda na katika maisha yake alipanga kama atakuja kuolewa basi lazima aolewe na mwanaume ambae anampenda, sababu ya pili Edna alikuwa akikumbuka wosia wa mama yake kabla ya kufa.

“Mwanangu hakisha unalinda kampuni hii kwa namna yoyote ile,epuka wanaume ambao watakulaghai na kukupokonya sehemu yako ndani ya kampuni” huo ni moja ya wosia aliopatiwa na mama yake na kwake ulikuwa ni kama Imani na kwa wosia huo alimuona kabisa Abuu kama mmoja ya watu ambao ni maadui dhidi ya kampuni na ndio maana hakutaka ukaribu kabisa.

Kwa upande wa Abuu yeye licha ya kwamba alikuwa amepewa misheni ya kumuweka mikononi Edna ila ndani ya moyo wake alikuwa akimpenda kwa mapenzi kabisa ya dhati , kiufupi alikuwa amekufa ameoza kwa mwanamke huyo , alikuwa haambiwi chochote juu ya Edna , alikuwa yupo radhi kufanya chochote kwa ajili ya kumpata mrembo huyo.

Baada ya kuona swala lake linazidi kuwa gumu la kuutingisha moyo wa Edna kwa njia za kiushawishi aliona atumie nguvu na njia pekee ya kutumia nguvu alipanga kumuhusisha baba yake Edna katika mapambano na hapo ndipo alipoharibu Zaidi kwani Edna alizidi kukaa nae mbali.

Baada ya Abuu kuona ameshindwa kwa njia zote kumpata Edna, huku akipata presha kubwa kutoka kwa baba yake ndipo alipoanza kupanga mbinu za kumnasa mrembo huyo , lakini katika mbinu zote alizopanga hakuweza kufanikiwa hata mara moja na hii yote ni kutokana na uwezo mkubwa wa kiakili wa Edna.

Edna alikuwa na akili sana na ndio maana kwa kipindi kifupi tokea apewe uongozi wa makamouni ya kifamilia , aliweza kuleta mafanikio makubwa sana ,Edna alikuwa ni msomi kutoka chuo kikuu cha Oford uingereza alikochukua masomo yake ya kibiashara kwa ngazi ya Degree na Mastaers na katika kipindi chote cha masomo Edna aliweza kufanya vizuri sana kuliko wanafunzi wote , sifa ya Edna chuoni ilikuwa ni Mrembo Mgumu’ kwani Edna licha ya kubarikiwa kuwa na uzuri wa Ajabu , lakini hakuwahi kujihusisha na aina yoyote ile ya mahusiano , alikuwa na marafiki wachache ambayo alikuwa nao kwa sababu moja tu ya kimasomo na hii ndio sabau iliompelekea kuzidi kung`ara kwenye masomo.

Hata aliporudi nchini Edna tabia yake ya chuo haikuwa imbevadilika kwanza alikuwa mwanamke mkimya sana na mpole , hakuwa muongeaji sana na hii ilimfanya kuwa na mzunguko mdogo wa watu anaofahamiana nao nje ya kazi, ukimya wake uliongezeka baada ya mama yake kipnezi kufariki.

Edna kwake ndugu pekee aliekuwa akimpenda alikuwa ni Bi Wema , kwake mwanamke huyo licha ya kwamba hawakuwa ndugu wa damu lakini alimchukulia kama mzazi wake mwingine baada ya mama yake ,Edna na baba yake hawakuwa na mapenzi ya kuwafanya waonane kama ndugu , uhusiano wake ulikuwa kwenye damu tu na kwenye jina lakini ule ukaribu wa kibaba na mwana haukuwepo kabisa na hii yote ni kutokana na kwamba mzee Adebayoo hajawahi hata siku moja kumchukulia Edna kama mwanae na hakuwa akimpenda kabisa.

Siku moja baada ya miaka kadhaa na Abuu kuwa CEO wa makampuni ya JR , alipanga mpango wa mwisho kabambe wa kumpata Edna , katika mpango wake jambo la kwanza aliloloifanya ni kuhakikisha kuwa yeye na Edna wanaonana mara kwa mara na njia pekee ya kufanikisha wao kuonana mara kwa mara ni kwa maswala ya kibiashara , kwani Abuu alikuwa akimjua vyema Edna kuwa likija swala la biashara hana upinzani na kutokana na hivyo , aliingia dili nono na kampuni ya Edna na hii ni mara baada ya tawi la kampuni ya JR kupata zabuni ya ujenzi wa barabara ya mwendokasi iliokuwa ikianzia maeneo ya Rangi tatu mpaka Chamazi , katika zabuni hio kampuni ya JR ilikuwa ikihitaji malighafi nyingi kutoka nje kwa ajili ya kukamilisha ujenzi na hapa ndipo Abuu alipokuja na wazo la kuwapa tenda Vexto kuwa kampuni pekee itakayowasaidia katika manunuzi na usafirishaji wa ‘material’ kutoka nje ya nchi na dili hili lilipowekwa mezani kwa CEO Edna hakutaka kufikiria sana , alikubali moja kwa moja kwani aliamini kupitia dili hilo atakuwa amepiga hatua kubwa.

Mpango wa kwanza wa Abuu ukawa umefanikiwa wa kumuweka Edna karibu na alipanga dili hilo la kibiashara angelifanya yeye mwenyewe na mpango wa pili aliupanga siku ya kusaini makubaliano baina ya kampuni hizi mbili.

Siku ya kusaini mkataba ilifika na Abuu aliwasiliana na Edna kumpa eneo husika ambalo makubaliano hayo yatafanyika na eneo alilolichagua Abuu ilikuwa ni ndani ya hoteli yao ya kitalii ya nyota tano iliokuwa ipo maeneo ya Maji matitu Mbagala(JR Hotel) huku muda ukiwa ni saa mbili za jioni kwani walipanga tukio hilo lifanyike wakati wa chakula cha usiku.

Edna na yeye bila ya kufikiria mara mbili alikubali na muda wa saa moja na nusu ndio aliingia ndani ya hoteli hii , akiwa mwenyewe bila ya mlinzi wake Suzzane.

Baada ya kufika alionyeshwa sehemu sahihi ya kuketi na akaletewa juisi na mhudumu baada ya kuagiza kwani hakutaka kunywa kilevi chochote huku akiwa anamsubiria Abuu , Edna hakuwa na wasiwasi , kwanza alikuwa akimuamini Abuu na sababu kubwa iliomfanya amuamini ni kutokana na kwamba alijua fika kwamba Abuu alikuwa akimpenda kwa mapenzi ya dhati ni vile tu yeye hakuwa na hisia nae na pia hata kama angekuwa na hisia nae asingekubali kuolewa nae kwani aliogopa nguvu kubwa iliokuwa nyuma yake.

Ilimchukua dakika kadhaa tu baada ya kunywa juisi ile na kupotelea usingizini kabla hata ya Abuu kuonekana , kwa upande wa Abuu yeye alikuwa ashapanga vijana wake kwa ajili ya kazi hio, baada ya vijana wa Abuu kuona mpango umeenda kama ulivyopangwa walichukua chupa za bia na kuziweka katika meza ya Edna ili kuonyesha kwamba mrembo huyu alikuwa amelewa na pombe , lakini Jose na mwenzake walishangazwa na kitendo cha bosi wao kuchelewa na hata pale walipo mpigia simu hakuwa hewani , Zaidi ya masaa manne yalipita ndipo bosi wao alipoingia kwa pupa na kwenda moja kwenye meza waliokuwa wamekaa vijana wake.

“Mmeshadaa chumba , nataka kila nitakachofanya kiwe kinarekodiwa sitaki uzembe katika hili”Aliongea Abuu mara baada ya kuambia vijana wake kwamba alipata tatizo la kikampuni ndio maana alichelewa.

Wakati akiongea na vijana wake ndio wakati ambao mwamba Roma aliingia na kujibebea mzigo akimdhania mwanamke huyo kama kahaba , kwanza walishindwa kuchukua maamuzi hapo kwa hapo kwani hawakua wakimjua mwanamme huyo na mpaka Roma anatokomea nje ya mlango ndio Abuu alipotoa amri ya vijana wake wakamdhibiti Roma , lakini wakaishia kumkosa na mpango ukawa umefeli.

Upande wa Edna baada ya kuamka na kujikuta akiwa kwenye Godoro , kwanza alishangaa ni vipi alivyofika hapo , lakini alipojiangalia na kujiona alikuwa uchi huku akihisi maumivu sehemu zake za uzazi ndipo alipojua mwanaume aliekuwa mbele yake ashaitoa bikra yake bila ya ridhaa yake.

Alikumbuka kila kitu tokea akiwa hotelini , lakini baada ya kupotelea usingizini hakujua ni kipi kiliendelea .

Baada ya kurudi nyumbani na kujichua na maji ya moto kupunguza maumivu hapo hapo ndipo alipo mpa kazi Suzzane kufatilia kilichotokea , lakini kwa bahati mbaya Abuu alikuwa na akili kwani alifuta hatua zote, kwani kwanza hoteli ile ilikuwa ni ya kwao hivyo mpango wake ulihusisha kuzimwa kwa Camera, hivyo Suzzane alivyofika kwenye hoteli kwa ajili ya kuomba picha ya matukio ya jana yake , aliambiwaCamera hazikuwa zikifanya kazi.

Baada ya Suzzane kutoa jibu hilo kwa Edna alimwambia kuwa afanye uchunguzoi wa taarifa za mwanaume alielala nae na katika kutafuta taarifa hizo ndipo alipopata taarifa kamili ya kilichotokea kwani Suzzane alirudisha taarifa inayoonyesha Roma alikuwa ni mbeba mizigo ndani ya soko Rangi tatu , Suzzane pia aliweza kupata eneo na Muda wa eneo alilokuwepo Roma kwanzia anarudi kazini na kwenda Club B na hapo ndipo Edna alipojua Roma hakufanya kitendo kile makusudi bali alimdhania yeye kama kahaba na hii yote ni baada ya kukumbuka wakati akiondoka ndani ya chumba can Roma kwani mwanaume yule alitaka kumpatia pesa yake.

“Yaani kulala na kuamka nimekuwa kahaba”Aliwaza Edna kwa uchungu mkubwa sana moyoni mwake , lakini kwa upande mwingine alishukuru kwani aliamini huenda mambo ambayo yangemkuta yangekuwa makubwa Zaidi kuliko yaliomtokea kulala na Roma.

“Miss jitahidi utafute mwanaume , huwezi ukaishi hivi milele itakuumiza na kukuathiri katika maisha yako , unahitaji mtu wa kukufariji katika nyakati ngumu , mimi siwezi kufanya hivyo kila siku nishaanza kuzeeka na sijui hata kesho nitakuwepo kwa ajili yako”Aliongea Bi Wema baada ya kumuona Edna akiwa ni mwenye mawazo mengi baada ya kutokurudi nyumbani usiku mzima.

M aneno ya Bi Wema kwake yalikuwa na maana , lakini hakuwa tayari kuwa na mwanaume , hakuwa akiwaamini kabisa , siku ya kwanza ilipita , ikaja ya pili yake , wakati wa usiku akiwa anajisomea ndipo alipoweza kupata wazo la kufunga ndoa na mwanaume yoyote kwa mkataba ili mradi kujiweka mbali na baba yake anayemsumbua kuoelewa na Abuu mwanaume ambaye hakuwa tayari kueolewa nae.

“Lakini mwanaume huyo ni nani?” Aliiwazia kwani hakuona mwanaume sahihi kwa yeye kufunga nae ndoa kimkataba.

“Nataka mwanaume ambaye atanisikiliza kwa kila kitu , ambaye atakuwa tayari kufanya kile nitakachokua namuambia , mwanaume ambaye nitaweza kumuendesha nitakavyo”Aliwaza kwa sifa hizo , lakini bado hakuona mwanaume anaefiti ndani ya sifa hizo , kila mwanaume aliekuwa akimjua alikuwa mbabe na mwenye utawala na tamaa ya pesa hivyo wote anaowajua walikosa sifa , yeye alitaka mwanaume bwege , lakini wanaume wote aliokuwa akiwajua kazini kwake wote hawakuwa na sifa za ubwege.

“Napata wapi manaume Bwege wa kufunga nae ndoa ya mkataba?”Aliwaza na kuwaza na kujiona swala hilo alipe kiporo , lakini ile anajaribu kunyanyua mguu kupanda kitandani mara alijihisi maumivu kwenye kitumbua chake na hapo jina la Roma liliibuka katika kichwa chake.

“Ndio atanifaaa , japo simjui ila naamini atakuwa ni wale wanaume mabwege na hata kama sio bwege pesa zangu zitamfanya kuwa bwege na nitamuendesha ninavyotaka , ndio anafiti kabisa , kwanza hana pesa ni masikini na hii ndio sifa kubwa”Alijiongelesha na kutoa tabasamu la ushindi.

“Ila nitamshawishi vipi..? , ila atakubali tu kama nitamwambia nitamlipa , lakini akikataa je..?, hawezi kukataa , nani anaweza kunikataa mrembo kama mimi kama nitamwambia nampenda , wanaume wote ni wadhaifu juu ya wanawake warembo”

Alijiongelesha na akili yake ikawa na jibu sahihi ,jibu aliloata ni kumfanya Roma mume BWEGE.

SEHEMU YA TISA.

Roma alishangaa kujua mke wake ndio CEO na mmiliki wa Makampuni ya Vexto ,Unajua Roma licha ya kujua Edna ana hela lakini hakuwahi kuwaza mke wake anaweza kuwa na pesa nyingi kiasi cha kumiliki mkampuni huu mkubwa ambao ulikuwa ukichangia asilimia mbili za uchumi wa Taifa , Makampuni ambayo yalikuwa na wafanya kazi Zaidi ya elfu hamsini , yaani kwa maneno marahisi ni kwamba maisha ya familia Zaidi ya Elfu hamsini zilikuwa zikimtegemea mke wake mrembo Edna.

“Bebi yaani nahangaika vyote hivyo na makaratasi na mausaili kumbe wewe ndio bosi”

“Roma chunga kauli yako , hapa ni kazini sio nyumbani mambo ya kuitana bebi siyataki mimi ni bosi wako”.

“My beutifull Edna , usiniambie kuwa tukiwa kazini mimi sio mumeo?” Edna hakujibu Zaidi ya kumwangalia Roma na kumtafakari ni mtu wa namna gani , yaani yale mawazo aliokuwa akiyawazia juu ya Roma yalikuwa ni Zaidi ya tofauti.

“Huyu baada ya miezi sita ya mkataba wetu kuisha nampa chake , siwezi kuishi na mwanaume asie na aibu kama huyu” Aliwaza Edna

Roma hakumjali Edna , alikuwa ashamjua ni mtu wa namna gani hivyo hakutaka kufanya kama alivyokuwa akitegemea yeye kufanya , alipanga kufanya mambo kinyume chake na hivyoo kumtania utani unaomkasirisha alikuwa akifanya makossa kabisa , lakini ni ukweli kabisa Roma hakuwa mtu mwenye aibu.

“Haya niambie My wife umeniitia nini , Au unataka unipe cheo kikubwa kikubwa” Edna alikunja ngumi maana alikuwa akichukiwa na neon ‘Wife’.

“Usomi wako hauendani na wewe kabisa , uliwezaje kumaliza ndani ya chui kikubwa duniani na tabia kama ulokuwa nayo”

“Hehe .. mke wangu hilo swali hata siwezi kujibu , mimi nilienda chuo kuchukua maarifa na ujuzi wala sikwenda kubadili tabia yangu”.

“Okey!, nimekuita hapa kukupa onyo mimi na wewe kuwa mke na mume ni nyumbani , mtu yoyote asijue sawa! , pili nakupongeza kwa kuwa mfanya kazi wetu , kampuni yetu inajali wafanya kazi , hivyo kama kuna jambo lolote usisite kuwasiliana na uongozi”

“My Edna siwezi kukubali onyo lako bila ya malipo”.

“Nishamaliza kuongea unaweza kwenda”Roma alitabasamu kifedhuli na kisha kusogelea ofisi ya sekretari na kumuita ndani ya ofisi.

“Mimi na bosi wako ni…”.

“Monica unaweza kwenda kuendelea na kazi”Aliongea Edna na Monicca alijikuta akishangaa , ila hakusema neno alitoka nje.

“Yaani wewe…Haya unataka nikulipe nini?” Roma alitabasamu na kwenda kukaa kwenye sofa na kukunja nne.

“Unaonaje ukinikiss”.

“Roma nipo kazini naomba ujichunge “Aliongea Edna kwa kukasirishwa.

“Haya mke wangu kipenzi usikasirike .. malipo yangu ni kwamba usije ukanifukuza kazini”.

“Hilo sina maamuzi nalo ukifanya mambo ambayo yataenda kinyume na maadili ya kampuni basi nitakufukuza”.

“Msimamo wangu ndio huo , wewe ndio boss , ukitaka nimtangazie kila mfanya kazi kama sisi ni wanandoa basi nifukuze kazini”Aliongea Roma na kutoka huku akimwacha Edna akizidi kumtafakari.

“Nimeingia cha kiume , huyu sio mwanaume bwege niliokuwa nikimtaka”Aliwaza Edna.

Baada ya Roma kutoka ndani ya ofisi ya CEO alienda moja kwa moja mpaka sehemu ambayo alikuwa akitakiwa kufanyia kazi , baada ya kuingia ndani ya ofisi kubwa iliokuwa na Tarakishi nyingi , huku kila meza ikionekana kuwa na mwanamke aliekuwa akifanya kazi , yaani Roma alishangazwa na warembo waliokuwa katika hii ofisi.

“Habari zenu Warembo mniite Roma Ramoni ni mfanyakazi mpya , ninafurahi kufanya kazi na warembo kama nyie na naamini tutashirikiana kwa ukaribu” Warembo wote walijikuta wakishangazwa na utambulisho huo.

“Karibu sana Roma , naitwa Benadetha , mimi ndio kiongozi wa idara hii ya Public Relation na kwa niaba ya wafanya kazi wa idara hii tunakukaribisha”Aliongea mrembo mmoja mwenye mwanya na kumfanya Roma atabasamu na kisha alionyeswa meza yake na tarakishi yake ya kufanyia kazi.

“Hivi hii kazi kwanza inahusiana na nini maana sina ninachojua mimi , wangeujua sijawahi hata kukanyaga ndani ya chuo cha Harvad wasingenipa hii kazi”Aliongea Roma baada ya kuona hana cha kufanya.

“Hey! Handsome , unaweza kuanza kazi kesho sio lazima leo”

“Nimeamua kuanza leo mrembo , ili tuzoeane mapema, unaitwa nani vile?”

“Niite Recho”Aliongea Recho huku akionekana ni wale wanawake waongeaji na wajana wajanja.

“nafurahi kufanya kazi karibu na mrembo kama wewe”Aliongea Roma huku akimkonyeza na Recho aliishia kutabasamu na kisha kuendelea na kazi.

“Huyu mwanaume anaonekana kuwa muhuni”Alijiwazia Recho.

Roma alifungua Tarakishi yake na kutafuta cha kufanya na alijikuta akiishia kwenye Gemu la Zuma lililokuwepo ndani ya tarakishi hio na kuanza kucheza kupoteza muda.

Wakati akiendelea kucheza mara aliingia mwanamke aliemfanyia usaili , kwanza mwanamke huyu hakumuona mpaka pale aliposhituliwa kwani muda wote alikuwa akicheza Gemu.

“yaani wewe wenzako wanafanya kazi wewe unacheza gemu…”

“Mrembo wa mapokezi ni wewe..!?”.

“Mimi sio mremnbo wa mapokezi niite Nasra, tabia ya kucheza gemu muda wa kazi ni kinyume na sheria za kampuni leo nitakusamehe ila siku nyingine nikikukuta unacheza gemu mshahara wako utakatwa nusu”.Huku akiondoka kwa hasira lakini Roma alimwita

“Eti Nasra, hakuna kazi nyingine tofauti na kukaa chini kukodolea Komputa , kazi kamaaa.. kubeba mizigo ya kampuni au kazi yote inayotumia nguvu mimi kazi kama hii sijaizoea”Aliongea Roma na Nasra alimshangaa na hakuongea neon aliondoka

Muda wa chakula ulifika Recho alimwambia Roma waongozane kwenda kantini ya Kampuni, Recho alikuwa na tabasamu muda wote , alifurahia uwepo wa Roma kwenye idara yao, kwani hakukuwa na mwanaume hata mmoja kitendo kilichompelekea kukosa kampani.

“Sasa mrembo sijabeba hela utanilipia basi”

“Usijali , kampuni hii ina wajali wafanya kazi hivyo kuna chakula cha bure”

“Kumbe..!!”

“Ndio” Walikuwa wakiongea huku wakitembea na ile wanafika kwenye lift walimkuta Nasra na waliingia huku Roma kama kawaida yake alimkonyeza Nasra na Nasra alietua mdomo ila Roma hakujali.

“Nasra unaonaje tukienda kukaa meza moja na Roma”Nasra alimwangalia Roma na Roma aliachia tabasamu.

“Umeongea pointi ya maana Recho, ni vizuri tukila pamoja au unasemaje mrembo Nasra..”

“Sawa.. ila punguza kuongea kama uko mtaani hapa ni kazini”.

“Ndio Tabia yangu unizoee na isitoshe sina nilipokosea ni kweli wewe ni mrembo”Recho na Nasra waliangaliana.

Baada ya sekune chache walifika chini kabisa ya Kantini na walichukua sahani zao , Roma alichukua sahanni mbili na kujaziwa zote huku akiwafanya wadada wamshangae , na walizidi kumshangaa Zaidi alivyoanza kula.

“Utakimaliza chote hiko Roma..?”

“Ndio mimi napenda sana kula”Aliongea na wakati huo mara waliingia warembo wawili , waliofanya hali ya hewa ya hapo kantini ibadilike , mrembo wa kwanza alikuwa ni Dorisi na wapili alikuwa ni Edna CEO.

Edna ndio wa kwanza kumuona Roma , alimwagalia namna alivyokuwa amezungukwa na wanawake huku akila bila wasiwasi na kujiwazia huyu mtu kawezaje kutengeneza marafiki ndani ya muda mfupi.

“Romaa..”Aliira Doris na Edna alishangaa na Roma alimkonyeza Dorisi na kumfanya acheke huku Edna akizidi kushangazwa na vitendo vya Roma na kuchukia zaidi.

*****

Abuu hakuwa tayari kumuacha Edna kizembe hivyo , alijua namna ambavyo alihangaika juu yake , aliona itakuwa ujinga sana kumwachia mtu kama Roma kumchukua mwanamke wake kizembe, lakini pia Abu alikuwa akitakiwa kuhakikisha anaingia kwenye kampuni ya Vexto ili kukamilisha mipango ya baba yake na pia kukamilisha mpango wa The City Master(Doni).

Unajua licha ya Abu kulazimishwa kukamilisha mpango wa kumuweka Edna kwenye mikono yake na kulazimishwa na baba yake kuhakikisha swala hilo linafanikiwa , hakuwa akimjua mtu anaeitwa The Done au The City Master.

Mara ya kwanza kusikia jina la mtu huyu ni kutoka kwa baba yake , miezi sita baada ya yeye kukabidhiwa kiti cha Uraisi wa makampuni ya JR.

“Sikia Abu sasa umekuwa CEO wa makampuni haya na najua fika una uwezo mkubwa wa kuyaongoza haya makampuni , na siku zote nilikuwa nikikufundisha kufanya kazi kwa kufuata sharia za nchi , lakini kuna jambo pekee ambalo sikuwa nimekueleza”Aliongea Mzee Alex siku moja akiwa na kijana wake Abuu kwenye kampuni alivyomtembelea.

“Katika ulimwengu wa kibiashara kuna vitu vingi unapaswa uvijue , vile vinavyoonekana na vile visivyoonekana”

“Unamaanisha nini mzee?”

“Kuna ulimwengu wa biashara unaonekana na kuna ulimwengu wa kiabiashara usio onekana , licha ya kuonekana ama kutokuonekana hivi vitu vyote vinaenda sambamba ,yaani biashara zisizo onekana unaweza kuziita zile ambazo si halali kisheria,nafikiri ushawahi kusikia Black Market?”

“Ndio nishawahi kusikia”

“Good! , basi kwa kukurahisishia kuelewa ni kwamba Black markert ni sehemu tu ya ulimwengu wa biashara zisizoonekana” Abuu alitingisha kichwa kuonesha alikuwa anamuelewa vyema baba yake mlezi.

“Hii kampuni usione imekuwa kubwa hivi kwa miongo kadhaa tokea kuanzishwa kwake , yote haya niliweza kuyafanikisha kwa kuhakikisha ninajiweka katika uwiano kati ya ulimwengu wa biashara unaonekana na ule usio onekana, na kwakuwa wewe ni mrithi niliekuchagua basi hili unapaswa ulielewe na ndicho kitu ninachokufundisha sasa”Abuu aliitkia kwa kichwa.

“Watu pekee wenye nguvu ndani ya ulimwengu huu usionekana hapa nchini ni The Doni au The Master , unaweza kumuita wewe mwenyewe kwa namna inayokupendeza”Abuu alishangaa .

“The Doni?”

“Nfdio huyu ni mtu pekee ambae hata mimi mwenyewe sijawahi kuua jina lake halisi , ila ninachojua huyu mtu katika ulimwengu unaonekana ni moja ya wanasiasa wakubwa sana ndan ya taifa hili , lakini katika ulimwengu usionekana ni mfanyabishara mkubwa”.

“Kwwanini unaniambia haya mzee??”

“Nakuambia haya kama nilivyokwisha kukuambia awali kwamba ukitaka kuendesha biashara kubwa kama hii na ifanikiwe unatakiwa kuwa na uwiano wa mambo yote mawili yaani ni nikimaanisha unatakiwa kujiweka kwenye usawa katika ya ulimwengu wa kibishara unaonekana na ule usio onekana , bila hivyo utaishia kuwa mfanya biashara mdogo na wakati , hivyo basi hakikisha swala la kwako na Edna linafanikiwa kwa asilimia mia moja kwani ni swala ambalo pia limepewa Baraka zote kutoka ulimwengu wa kibiashara usio onekana”.

Abuu alishangazwa na maneno hayo ya baba yake , aliona swala la yeye kumpata Edna ni swala ambalo ni Zaidi ya biashara za baba yake , kitendo cha kusema mpaka The Doni anataka swala hilo lifanikiwe na macho yote yapo kwake kufanikisha swala hilo lilimshangaza.

Hayo ndio yalikuwa mazungumzo ya Mzee Alex na Abuu miaka miaka kadhaa nyuma , abuu hakuwa akimjua The Doni na alichokuwa akijua kuwa mtu huyo alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa kwenye ulimwengu usiooonekana , lakini pia ni mwanasiasa mkubwa nchini katika ulimwengu unaonekana , mtu huyo ni nani?, kwanini tageti yao ni Edna na kampuni yake , kuna nguvu gani ipo ndani ya kampuni ya Edna ? yaliokuwa ndani ya kichwa cha Abu na kadri alivyokuwa akifkiria maswala hayo ndivyo alivyozidi kutaka kujua Zaidi aliokuwa hayajui.

“Hakikisha swala hili linafanikiwa kwa namna yoyote ile , kama utashindwa kumpata Edna chukua kampuni yake , mpango wako B unaonekana kuwa mzuri , lakini pia nataka ujiandae kwa mpango mwingine kama huo hautafanikiwa”

“Sawa baba”Abuu alikumbuka maneno ya mwisho wiki siku chache zilizopita baada ya kumueleza mpango B

“The instinct of person wanting to know what he/she doesn’t know its what makes a human” kwamba ile hali ya mtu kutaka kujua kile asichojua ndio kinamfanya mtu kuwa binadamu, na kwa upande wa Abu alitaka kujua hivyo kwenye moyo wake aliamini jambo pekee ambalo litamuwezesha kujua asichokijua ni kuhakikisha Edna anakuwa chini yake , alimchukulia Edna kama ‘Portal’ ya kuingia ulimwengu usioonekana.

Abu anaonekana akiwa ndani ya ofisi yake kubwa hii iliokuwa ikiwakilisha ukubwa wa makampuni ya JR kutokana na muonekano wake wa kifahari, wakati akiwa anaendelea na majukumu ya kazi aliingia Marasta ndani ya ofisi hii na kumfanya Abu amwangalie.

“Bosi tayari nishatafuta vijana watakaomaliza mpango B usiku wa leo”.

“Good , Sitaki uzembe kwenye mpango huu kabisa , nataka ufanikiwe kwa asilimia mia moja hivyo hakikisha wewe na wenzako mnakuwa makini”

“Sawa Boss”Aliitikia Marasta na kisha alitoka huku Abuu akiinuka na kulisogelea dirisha , baada ya kuangalia kwa madakika kadhaa nje ya jiji hili la Dar alitoa simu yake na kupiga namba.

“Kila kitu kipo tayari jiandae kwa ajili ya ukamilishaji wa Plan B”.Na kisha akakata simu.
ITAENDELEA JUMATATU WADAU
 
SEHEMU YA KUMI

Roma alitoka kazini muda wa tisa kamili na kwenda moja kwa moja mpaka nyumbani , baada ya kufika na kusalimiana na Bi Wema moja kwa moja aliingia kwenye chumba chake kwa aili ya kupumzika , huku akiwaza aende kiwanja gani cha bata , baada ya lisaa limoja la kupumzika , simu yake ilitoa mwanga kuashiria kuna ujumbe ulikuwa umeingia , aliichukua na kuutazama na kisha alitabasamu.

“Hey! Malkia Doris naona ushanimiss”.

“Acha kujishaua mwanaume , nimekutafuta kwani ninahitaji msaada wako , ila sio lazima kama hautonisadia”.

“Nipo tayari kufanya lolote kwa mrembo kama wewe na isitoshe ushawahi kunisaidia nina deni kwako”

“Kama unalijua hilo tuonane jioni saa moja The palm Hotel”.

“Nitafika hapo muda huo mrembo wala usiwaze”

“Sawa ila uje umevaa vizuri sasa , na pia kuwa makini na mkeo usimuage kama unakuja kwangu”Roma alitabasamu na ujumbe huo wa meseji na kisha kuweka simu pembeni na kuuchapa usingizi alikuja kuamka muda wa saa kumi na mbili na nusu , aliona ni muda mzuri wa yeye kujiandaa na ndani ya dakika kumi na tano alikuwa tayari yuko vizuri.

Alitoka na kumkuta Bi Wema akiangalia TV sebuleni .

“Bibi, Edna asharudi?”.

“Bado hajarudi , ila kanipigia simu saa kumi kuwa atachelewa ana miadi na mtu”Aliongea huku akiendelea kuangalia runinga na Roma Kuna kajiroho ka wivu kalimuingia na kujiuliza ni mtu gani Edna anamiadi nae pasipo yeye kujua , ila hakutaka kujali Zaidi , alikumbuka vyema ndoa yao sio kama ndoa za kawaida ni ndoa ya maigizo tu na hakukuwa na mapenzi katikati hivyo kila mtu alikuwa na mishe zake.

Alimuanga bi Wema kwamba anatoka na anaweza kurudi ama asirudi kabisa na kisha aliondoka , licha ya Roma kupotezea swala la Edna ila kama mwanaume kuna kitu kilichokuwa kinamuendesha katika moyo wake , hakujua sababu ni nini ila alikuwa na hasira mno.

Ndani ya dakika kumi aliingiza gari yake ndani sehemu ya geti la hoteli hio na kusimamisha gari na kumkabidhi funguo Valet(mtu anaehusika na kuegesha magari ndani taasisi, kampuni au hoteli) , alikaribishwa na ufahari wa hali ya juu wa hoteli hii.

“Waoh! Umependeza Roma”Aliongea Doris baada ya wawili hao kuonana sehemu ya kusubiria wageni , upande wa Doris alionekana kama Malaika , mavazi aliochagua kuvaa siku hio yalikuwa yamempendezesha mno huku uzuri wake ukizidi kumfanya kuonekna wa kipekee sana ndani ya eneo hilo.

“Umependeza pia mrembo, hakika wewe ni mzuri Doris”

“Haha.. Acha unafiki Roma mimi ni mzuri Zaidi ya mkeo?”Hapa ni kama swali hili lilimkosesha raha Roma kwani akikumbuka uzuri aliokuwa nao Edna sio wa kawaida na hata kwa Doris hakuwa akimfikia hata kidogo , ila sasa swala lililomkosesga raha ni kwamba mke wake muda huo hakujua ana miadi na mtu gani.

“Hehe.. nisikufiche mke wangu mzuri bhana ndio maana nimemuoa”Aliongea Roma na kumfanya Doris ajifanyishe kununa , lakini Roma alitabasamu.

“Kuna mtu nataka leo nikutambulishe kwake , naomba uigize kuwa mpenzi wangu kwa usiku wa leo”Aliongea Doris na Roma alijikuta akishangaa , inakuwaje mwanamke huyu akamchagua kwa kazi hio ilihali anajua kabisa ana mke , lakini pia kwanini amemchagua yeye , ila hakutaka kuwaza sana , alikubali kwani bidada huyo alikuwa akimkubali kwa roho yake nzuri , kitendo cha siku ile kumsaidia nauli bila ya kujuana kilikuwa na maana kabisa ndani ya ulimwengu wenye watu wenye roho mchanganyiko.

“Hata usijali mrembo , mimi kama ningeamua kuwa mwigizaji ningekuwa maarufu sana , maana nina kipaji cha kuigiza”Aliongea Roma na kumfanya Doris atabasamu.

Baada ya kuingia kwenye Lift walikuja kutoka kwenye floo namba ishirni ,Floor ambayo ndani ya hoteli hii ilikuwa ikihudumia VVIP.

Roma alishangazwa na ulinzi wa ndani wa hili eneo , kwani kulikuwa na walinzi waliokuwa wamevalia suti wakionesha kuimalisha ulinzi , alishangaa ni mwanaume gani Doris alikuwa anaenda kumtambulisha kwake , lakini majibu yake yalijibiwa mara baada ya kuingia ndani ya chumba namba 700 na kukutana na mwanaume aliekuwa amevalia Suti huku akiwa anakunywa mvinyo.

Bwana huyu kwanza alionekana kuwa mtu mzima , kwani sura yake ilikuwa ishaanza kukunjamana , alikuwa mrefu wa wastani mweupe mwenye kipara kwa makadirio ya umri alionekana kuwa na umri kati ya 45 kuendelea.

“Mister Kijembe huyu ndio mwanaume ninaempenda na ninapanga kuolewa nae , hivyo naomba unielewe ninapokuambia swala la mimi na wewe kuwa wapenzi haliwezekani”Aliongea Doris mara baada ya kukaribishana na kukaa , huku huyu mzee muda wote macho yalikuwa kwa Roma.

“Huyu Doris ananitafutia matatizo huyu , mtu mwenywe anaonekana kuwa na mipesa mingi na walinzi kibao si nitakufa akipanga kuniua”Aliiwazia Roma lakini hakuonesha hofu yoyote jambo ambalo Lilimvutia sana Doris.

“Doris huyu ndio babu ulieniambia anakutaka na hataki kukuelewa?”

Mzee yule alitaka kutapika wine iliokuwa mdomoni kwake mara baada ya kusikia anaitwa babu, na Doris alishangazwa na ujasiri aliokuwa nao Roma kwani licha ya kutaka kumtumia katika mpango wake lakini alikuwa akihofia Roma atamwangusha lakini imekuwa kinyume na mategemeo yake kwani Roma alifanya kazi Zaidi ya alivyokuwa akitaka kazi ifanyike yaani too perfect.

“Mzee usinifikirie vibaya ila kwa umri wako na wetu sisi tunapaswa tukuite babu , sasa ni aibu kwa mtu mzima kama wewe kusumbua vijana wakati muda wako kwa hayo mambo ushaisha, mimi nakushauri achana tu na vijana na kwanzia sasa endelea kujikita Zaidi kwenye kumuomba Mungu maana kwa ninavyokuona siku zako sio nyingi hapa duniani angalau tubu dhambi uingie peponi”.

“Kijana Chunga maneno yako , mimi sio babu kuwa na heshima .. halafu Dorisi huyu kichaa umemtoa wapi asiekuwa na heshima hata kwa wakubwa”.

“Mr Kijembe nimempenda huyu na ukichaa wake hivyo lililonileta hapa lishaisha na nadhani kuanzia leo utakuwa mbali na mimi”Aliongea Doris na kuamka ili waondoke , lakini kabla hajapiga hatua mbili Roma alimvuta Doris na kutua katika kifua chake na katika hali ya kutokutegemea alimpiga kiss kitendo kilichomuacha Doris katika mshangao maana ilikuwa ghafla sana.

“Bebi una vijilipsi vizuri nashindwa kuvizoea kila siku nitaving`ata mimi”Aliongea Roma kwa kumtania na kumfanya Doris aone aibu za kike.

“Babu kwaheri nadhani utazingatia maneno yangu”Aliongea Roma na kisha wakatoka.

“Halafu Roma umevuka mpaka mimi nimekuambia uigize kuwa Boyfriend wangu sio kunikiss umenikera”

“Hehe muone sasa .. kwani maana ya maigizo ni nini Doris .. halafu mbona umekuwa mwekundu hivyo, usiniambie kwamba nimezipandisha hisia zako , aliongea huku akimsogelea Doris wakati wakiwa kwenye Lift na Doris alizidi kujibana kwenye ukuta wa Lift.

“Bebi unaonaje ikawa kweli”Baada ya kumfikia kuinamisha uso wake mbele ya Dorisi aliekuwa ameangalia chini kama mwanamke asiewahi kukisiwa.

Mlango ulifunguka haraka kiasi cha kumkera Roma , ila hakujali Zaidi , waliongozana mpaka nje.

“Unaonaje Doris tukienda sehemu kwa ajili ya chakula kabisa , mimi nishatoa maagizo kwamba nitachelewa hivyo siwezi kurudi kabla sijala”.

“Sawa hata mimi pia nimetoa maagizo hayo”.

Haikueleweka nini kilitokea baina ya wawili hawa hapo katikati ila ndani ya saa tatu za usiku walionekana kuwa ndani ya chumba cha hoteli moja iliokuwa ikipatikana ndani ya meneo ya Ubungo , hawakuwa tena wale wanaogiza ila wakati huu Doris alikuwa akitoa miguno ya kimahaba huku Roma akiwa ni mwenye kushusha viuno kama hana akili nzuri.

Baada ya lisaa limoja la Roma kumpindua mwanadada Doris huku mrembo huyu akifunga magori yasiokuwa na idadi kitu ambacho hakuwahi kufikia , Roma alihema kama mbwa aliekuwa akifukuzwa.

“Wewe na CEO mna ukaribu gani , maana nimewaona leo mkiongea kama marafiki?”

“Mh! Usiniambie na CEO na yeye unamtaka?”

“Yaani wewe , mbona unafikiria sana , mimi nimeuliza tu mrembo”

“Tumefahamiana muda tu , tokea kipindi hajawa CEO tuna urafiki wa Zaidi ya mika mitatu sasa”

“Nilijua mnafahamiana kikazi tu , kumbe mpo deep kiasi hiko?”

“Sio sana , ila naweza kusema mimi ni rafiki pekee wa Edna nje ya familia yake kwa hapa Tanzania”.

“Unamaanisha nini , unataka uniambie CEO mrembo kama yule hana marafiki , vipi kuhusu mume wake”

“Kuhusu marafiki kwakweli Edna hana , sifa yake yule ni mkimya sana na ni ngumu sana kutengneza marafiki , kuhusu mume kusema ukweli Edna amekuwa mgumu sana kunieleza mahusiano yake japo aliniambia hivi juzi kuwa ameshapata mume na anaishi nae na wala hajawahi kuniweka wazi kuhusu huyo mwanaume nimfahamu”Aliongea Edna lakini wakati wanaendelea na stori huku wakiwa uchi simu ya Roma ilianza kuita mfululizo na alishangaa maana hakuwa na watu waliokuwa wakimpigia mara kwa mara baada ya kuangalia jina alikuta ni Bi Wema , alishangaa na akaona huenda kuna tatizo.

“Roma uko uk.. wapi jamani Edna katekwa Romaa”

“Nini Bibi hebu niambie nini kimetokea”.

“Kuna watu wamenipigia wanasema Edna wamemteka na wanakutafuta wewe , nimewapa namba yako jamanii mimi nafanya nini ,… Edna Mugnu wangu ..”

“Bi Wema tuliza presha kila kitu kitakuwa sawa , ilimradi umesema wananitaka mimi basi jua Edna hatopata shida yoyote ile na swala hili usimwabie mtu yoyote nitalishughulikia mimi mwenywewe”Aliognea Roma na kukata simu , lakini ile anakata tu namba nyingine iliokuwa kweye mfumo wa Private numbe iliianza kupiga na Roma alipokea.

“Mr Roma tupo na mkeo na unachotakiwa kufanya ni kuja sehemu tutakayokuambia bila kutaarifu polisi au mtu yoyote yule , ukifanya ujinga wowote jua utaletewa Edna akiwa hayati”.

“Okey niambieni mko sehemu gani na nitafika mimi mwenywe”.

Roma aliambiwa eneo husika na kisha alimwangalia Dorisi aliekuwa akimwangalia kwa mshangao.

“Kuna nini Roma?”

“Mke wangu katekwa na natakiwa kwenda kumuokoa kwani watekaji wananitaka mimi”

“Nini .. usiende Roma mpenzi watakuua”

“Dorisi tutaonana , lazima nimuokoe mke wangu kwa namna yoyote ile hata kama kifo kitanihusu”Aliongea Roma na kuvaa nguo zake na kutoka akimuacha Dorisi katika hali ya wasiwasi.

****

Upande mwingine nje ya hoteli ya The Palm alionekan Mr Kijembe akitoka akiwa na walinzi wake na kuingia kwenye gari na kisha kuondoka ndani ya eneo hilo , muda mfupi baadae gari zile tatu mbili zikiwa na walinzi na moja ya katikati ikiwa na Mr kijembe ziliingia katika lango la Ikulu ya Dar es Salaam .

Baada ya kuingia Mr kijembe aliingiea kwenye chumba ndani ya jumba hili la ikulu , chumba ambacho kilionekana kuwa kama hospitali.

Baada ya kuingia ndani ya chumba hiki bwana mmoja aliekuwa amevalia gloves aliandaa vifaa flani hivi , huku Mr Kijembe akiwa amekaa kwenye kiti na bwana yule alimsogelea na kuanza kubabua ngozi kwenye sura na ndani ya dakika chache tu sura mpya ya mtu anaefahamika kwa watanzania wote ilionekana na huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Raisi Senga Kweka.

“Kabwe nipe taarifa zinazomhusu Roma sasa hivi unikute kwenye ofisi yangu”Sawa mheshimiwa.

Baada ya mheshimiwa Senga kuingia ndani ya ofisi yake alionekana kuwa ni mwenye hasira sana, hakutarajia kama atakuja kudharauliwa na kijana mdogo kama Roma katika maisha yake , alikuwa ni mwenye hasira sana .

“Nadhani hanijui vizuri huyu , yeye ni nani mpaka aharibu mipango yangu , Dorisi kwangu ndio kila kitu juu ya kutimiza mpango wangu”Alijiwazia mzee huyu na kushituliwa na mlango uliokuwa unagongwa na akaingia Kabwe Mlinzi mkuu wa kujitegemea wa Raisi Senga.

“Umepata nini mapema hivyo?”.

“Taarifa niliopata mheshimiwa juu ya Roma ni kwamba jina lake kamili anaitwa Roma Ramoni alifika ndani ya jiji la Dar Es salaam miezi sita iliopita , ni mhitimu kutoka chuo cha Harvad akichukua masomo ya uongozi wa biashara , siku chche zilizopita alifunga ndoa na CEO Edna”

“Unamaanisha Edna na Roma ni wanandoa , wamefunga hio ndoa lini na mbona hii taarifa sina Kabwe”.

“Mheshimiwa nilikuwa naandaa taarifa kwa ajili ya kukupatia na kilichonichelewesha ni ugumu wa taarifa zilizokuwa zikimuhusu Roma”Aliongea Kabwe

“Kabwe unatakiwa kuelewa kuwa Edna ni muhimu sana kwangu katika mipango yangu zidi ya The Doni na taarifa yoyote inayomuhusu lazima inifikie sawa ?”

“Sawa mheshimiwa”.

“Kuna taarifa nyingine kumuhusu huyu Roma maana siamini kama mtu kama yeye kumuoa Edna bila ya kuwa na sababu lakini pia wakati huo huo kuwa na mahusiano na Dorisi”

“Taarifa nyingine nimeweza kupita kutoka kwa kampuni ya Vexto inaonesha Roma anauwezo wa kuzungumza lugha ishirini na mbili”

“Nini!!?, lugha ishirini na mbili na mnamuona mtu huyo wa kawaida , kuna taarifa kubwa inayomuhusu huyu mtu nataka hio sio hii feki ya kusomea chuo cha Harvad”Aliongea Mheshimiw Senga huku akiwa ni mwenye kushangaa , alijua mtu wa kawaida hawezi kuwa na uwezo wa kuongea lugha nyingi kiasi hicho , kuna hisia mbaya zilikuwa zikimwandama.

“Anaweza kuwa mtu hatari kwa Edna huyu , huenda ni mpango wa The Doni Edna kuolewa na huyu Roma” Aliwaza mhesimiwa.

“Kabwe fuatilia taarifa za huyu mtu kwanzia wazazi wake na kila kitu kinachomuhusu , anaweza akawa hatari kwa Edna hivyo swala hili linapaswa kufanyika haraka”

“Sawa Mheshimiwa , lakini bipi kuhusu Doris?”

“Doris pia ni wa muhimu lakini kazi hio nitampa Kiga , lazima nimuweke Doris karibu kama ninataka kupata taarifa zote zinazomuhusu baba yake The Doni”Aliongea Raisi huku akikaa kwani muda wote alikuwa akizunguka zunguka.

“The Doni anajifanya mjanja sana kujificha , ila asichojua ni kwamba nina taarifa zote na uthibitisho wa Doris kuwa mtoto wake na kupitia yeye nitampata tu , hawezi akaniendesha kama gari bovu mimi huku wananchi wakiniita Raisi”

Mheshimiwa Raisi alijikuta akiwa kwenye wakati mgumu na kuogopa kwa wakati mmoja , kuchelewa kwa taarifa ya ndoa ya Edna kumfikia yeye aliona ni swala ambalo linaweza kumuweka Edna matatizoni alishangazwa sana na Edna kuoelewa na mtu anaeweza kuzungumza lugha ishirini na mbili bila yeye kujua , aliona usalama wa taifa walikuwa hawafanyi kazi yao kwani hio ilikuwa ni taarifa kubwa sana na ilitakiwa kufatiliwa.

“Hapana swala hili pia lazima nilifanyie kazi , licha ya Vexto kuwa kiini cha mipango yetu lakini Edna hatakiwi kudhurika hata kidogo , mkataba wa siri niliosaini baina yangu na mama yake utakuja kunifunga baadae”

TUTAENDELEA JUMATATU WAPENDWA
 
SIMULIZI NI NDEFU SANA
 
Attachments

  • DEMU 1.png
    DEMU 1.png
    91.5 KB · Views: 203

Similar Discussions

Back
Top Bottom