Sijaona sababu za msingi kwanini Serikali haitaki kutoa takwimu za idadi ya wafuasi wa dini

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
11,278
19,115
Hadi leo sijaona kwa nini serikali haitaki kabisa kutoa takwimu za idadi ya watu katika dini mbali mbali, yaani tujue Tanzania kuna Waislamu wangapi, kuna Wakristo wangapi, kuna wapagani wangapi. Na katika Waislamu kuna Suni wangapi, Shia wangapi. Na katika Wakristo, kuna Wakatoliki wangapi, Walutheri nk.

Na pia ningependa kujua kuna Wasukuma wangapi, Waha wangapi nk. Ubaya wake nini kujua hii idadi? Kusema itaeta udini au ukabila ni sababu yebo yebo.

Wanawake wanajua wako wengi kuliko wanaume, mbona hatuoni wakidai mawaziri na wakuu wa mikoa na wilaya wengi wawe wanawake kuliko wanaume?
 
Khaaaaa? Basi ongezea na hizi
Walioolewa...
haaaaa? Basi ongezea na hizi
Walioolewa - idadi ipo
Walioachika - ipo kaa wana file divorce
Mabikra - mjinga tu ndio atapendekeza hili
Mafisadi - idadi ipo kwa waliohukumiwa
Marehemu - idadi ipo mjajiri wa vifo
Wanaojiuza - mjinga tu ndio atapendekeza hili

Kwa ujumla, nimeona post yako ina ujinga wa kiwango cha juu. Na hasa ukizingatia kuna nchi nyingi tu, kama sio zote isipokuwa Tanzania, zinatoa takwimu za mambo niliyotaja
 
Hadi leo sijaona kwa nini serikali haitaki kabisa kutoa takwimu za idadi ya watu katika dini mbali mbali, yaani tujue Tanzania kuna Waislamu wangapi, kuna Wakristo wangapi...
Hata wanawake na wanaume wangeainisha na umri. Maana ninaamini wanawake wanaosemwa wengi ni wale ambao siyo umri wa kuolewa au kuzaa(vizaa vya over 45yrs) na visichana under 18.

Hata wanaume pia wangeainisha umri in groups
 
Waongeze idadi ya wachawi Ili tujue kama wanaongezeka au la maan naona wako wengi Huku uswahilin
 
Ila nahisi Waislamu wakiambiwa ni wachache kuliko Wakristo hawatakubali hizo takwimu, wanaamini mno kwamba wao ni wengi, kwa kuwa wao ni wengi Dar.

Neno kubwa hapa ni "unahisi".

Tafuta takwimu za wakoloni zina kipengele cha idadi ya watu Kwa dini.

Unaweza tumia Kama base ya estimates za sasa
 
hata wanawake na wanaume wangeainisha na umri. Maana ninaamini wanawake wanaosemwa wengi ni wale ambao siyo umri wa kuolewa au kuzaa(vizaa vya over 45yrs) na visichana under 18.

Hata wanaume pia wangeainisha umri in groups
Point nzuri sana. Kutoa matokeo ya sensa na kusema tuko milioni 61, wanaume milioni 30, wanawake milioni 31, mie nimeona ni ujinga na kukosa busara.

Nilitegemea Samia angeenda mbali na kusema, katika milioni 61, idadi ya vijana kati ya miaka 20-30 ni hii. Na hivyo serikali itajipanga kuweka mikakati ya ajira kwa sababu hapa ndipo watu wasio na ajira wamejaa.

Na angesema wazee kuanzia miaka 60 hadi 80 ni hii. Kwa hiyo bima ya taifa ya afya itakuwa hvi na vile na hivi. Yaani anakuja kusema tuko milioni 61, wanaume 30 wanawake 31 halafu anaondoka? Angemtuma hata housegirl wangu angefanya hiyo kazi vizuri tu
 
Ila nahisi Waislamu wakiambiwa ni wachache kuliko Wakristo hawatakubali hizo takwimu, wanaamini mno kwamba wao ni wengi, kwa kuwa wao ni wengi Dar.
Dar Haina waislamu wengi umedanganywa ,Dar kwa vile Haina wenyeji wengi wa Pwani labda baadhi ya maeneo ...Dini iliyodominate kanda ya ziwa ndo yenye watu wengi sawa na makabila..

Upande wa dini na ukabili dar itoe maana ni capital city kila mtu anaweza kuinjet capital hata kuishi mji unapanuka sana
 
Neno kubwa hapa ni "unahisi"..
Tafuta takwimu za wakoloni zina kipengele cha idadi ya watu Kwa dini..
Unaweza tumia Kama base ya estimates za sasa
Kuna dini zinazaa kama free fall Mkuu. Kwa hiyo hizo projections zinaweza kutokuwa sahihi ukizingatia mambo kadhaa kama birth rates katika dini tofauti ambazo zimebadilika toka enzi za mkoloni kutokana na shule nk.
 
Serikali iliogopa kitu gani? Kwamba mtakuja na unreasonable demands mkijua nyie ni wengi kuliko Wapagani au Wakristo?
Serikali iligoma kwasababu tangu nchi ipate uhuru haikuwahi kuhesabu makabila wala dini waliona ingekuwa jambo jipya, mara ya mwisho watu walihesabiwa dini na makabila ilikuwa kipindi cha ukoloni kabla ya uhuru
 
Back
Top Bottom