USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 9,896
- 22,667
Baada ya maji kuwasomba watoto na kuwauwa kule Arusha nilijua serikali ingeona nini kitatokea, na sasa wanasema itachukua wiki mbili kunyesha kwa kiwango kikubwa namna hii na watoto wa kitanzania wanasota huku wale wa nchi za jirani wamesitisha ukatili huu kwa muda
Ukiwa njiani unawaona watoto wadogo 5yrs na ziada wakiwa njiani wamenyeshewa wanakwenda shule au wanatoka wapo chepechepe kwa mvua, viatu vimejaa tope na kulowa maji yanayotililika kwenye barabara zilizojaa maji na vidibwi .
Vitabu na madaftari yamelowa wengine hawana hata masweta wanapigwa na baridi
Kuna ulazima gani haswa wa watoto hawa wateseke kipindi kigumu cha namna hii wakati uwezo wa kutatua hili upo wazi.