Serengeti: Tabitha Mwise asimulia jinsi Polisi walivyo Vamia nyumbani na kuvuliwa nguo mbele ya baba yake na kulazimisha afanye naye Mapenzi

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,276
6,642

Binti asimulia polisi alivyomvua nguo mbele ya baba yake Serengeti
Sunday September 25 2022
Tabitha Mwise (22), binti wa Mwise Simon (54), mmoja wa watu watatu waliouwawa kwa kupigwa risasi na polisi wilayani Serengeti kwa tuhuma za ujambazi amesimulia tukio la polisi kuvamia nyumbani kwao kumtia mbaroni baba yake ambaye sasa ni marehemu.

Binti asimulia polisi alivyomvua nguo mbele ya baba yake Serengeti
By Beldina Nyakeke

IN SUMMARY
Tabitha Mwise (22), binti wa Mwise Simon (54), mmoja wa watu watatu waliouwawa kwa kupigwa risasi na polisi wilayani Serengeti kwa tuhuma za ujambazi amesimulia tukio la polisi kuvamia nyumbani kwao kumtia mbaroni baba yake ambaye sasa ni marehemu.

Musoma. Tabitha Mwise (22), binti wa Mwise Simon (54), mmoja wa watu watatu waliouwawa kwa kupigwa risasi na polisi wilayani Serengeti kwa tuhuma za ujambazi amesimulia tukio la polisi kuvamia nyumbani kwao kumtia mbaroni baba yake ambaye sasa ni marehemu.

“Kwanza walifika kwa kishindo alfajiri ya Septemba 21, mwaka huu wakiwa na magari mawili; wakavunja milango na kuwatoa nje wote waliokuwemo ndani huku wakimtembezea kipigo kila aliyekuwa mbele yao,” amesema binti huyo

Amesema mlango wake ulipovunjwa na yeye kutolewa nje kwa vipigo, alimkuta baba yake na ndugu wengine wakiwa tayari wametolewa nje huku wakipigwa kulazimishwa kuonyesa silaha zilipofichwa.

“Baada ya kuwajibu kwamba sifahamu bunduki ilipo na wala sijawahi kumwona baba yangu akiwa na bunduki, askari wale waliendelea kunishambulia sehemu mbalimbali za mwili huku watuamuru mimi na baba kuvua nguo zote,” amesema Tabitha akionyesha huzuni usoni kabla ya kushindwa kuendelea kusimulia tukio hilo

Binti huyo ametoa simulizi hiyo mjini Musoma leo Septemba 25, 2022 wakati familia mbili kati ya tatu zilizopoteza wapendwa wao katika tukio hilo walipokutana na waandishi wa habari kusisitiza msimamo wa kutozika hadi uchunguzi huru na wa kina ufanyike kujua sababu na jinsi ndugu zao walivyopigwa risasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibishiwanu hakupatikana kuzungumzia tuhuma za askari wake kudaiwa kuwavua nguo baba na binti yake mbele ya wanafamilia wengine baada ya msaidizi wake aliyepokea simu yake ya kiganjani kueleza kuwa kiongozi huyo alikuwa kwenye ibada.

Msimamo wa familia

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Musoma, familia ya Mwise Simon na Mgare Mokiri wamesisitiza kutozika hadi uchunguzi wa kina utakapofanyika kubaini sababu na mazingira ya vifo vya ndugu zao.

"Tume huru tunayoomba iundwe ichunguze siyo tu mauaji ya Serengeti, bali pia ya watu wengine waliofia katika mikono ya polisi katika matukio mbalimbali wakiwemo wale waliodaiwa kuwa ni Panya Road," alisema Catherine Ruge, ambaye ni mpwa wa marehemu Mwise Simon

Catherine ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bavicha) amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala hilo kama alivyofanya kwa kifo cha mfanyabiashara wa madini Mussa Hamisi wa Mtwara aliyefia mikononi mwa polisi.

Watu hao waliouwawa na askari polisi kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu na Tarime/Rorya ambao walikuwa wanafanya operesheni ya kusaka watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi.

Mwingine aliyepigwa risasi katika tukio hilo lililotokea usiku wa kumakia Septemba 22, mwaka huu ni Mairo Togoro (56) ambaye familia yake haikuwepo kwenye mkutano wa waandishi wa habari mjini Musoma.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibishiwanu alisema watu hao walipigwa risasi walipojaribu kutoroka walipoenda na askari polisi kuonyesha maficha yao na eneo wanakohifadhi silaha walizodaiwa kuzitumia kwenye uhalifu.

Taarifa hiyo inadai watu hao ambao sasa ni marehemu walikuwa wanatuhumiwa kujihusisha na matukio ya ujambazi na waliwaongoza askari kwenda kuonyesha walipojificha wenzao watatu lakini walipofika kitongoji cha Gentamome, ghafla askari polisi walishambuliwa ndipo walipolazimika kujibu mapigo.

More From Mwananchi
 
Daaah! Hawa mapolice wetu wanatuoje sisi?? Kwamba ni watu wa kutufanyia chochote watakacho?

Kile tunapinga kama jamii ni marufuku mzazi alale na mwanaye..! Wao ndo wanatulazimisha siyo?

Ngoja, nitakuja nimlazimishe police mmoja alale na bintiye, tuone ikiwa itakuwa sawa!
 
Sasa kama baba anabunduki ulitaka wamuimbie nyimbo aseme iliko????

Unadhani mtuhumiwa wa ujambazi wa siraha ili akuoneshe bunduki iliko ni kazi ndogo??? Ukipewa wewe iyo kazi unaweza hata ukamuacha kumbe mali ipo na ataendelea kuitumia.

Izo ni mbinu tu za kumfanya mtuhumiwa afunguke.

Kama ndio hizo mbinu wanafundishwa huko chuo kazi ipo.
 
Sasa kama baba anabunduki ulitaka wamuimbie nyimbo aseme iliko????

Unadhani mtuhumiwa wa ujambazi wa siraha ili akuoneshe bunduki iliko ni kazi ndogo??? Ukipewa wewe iyo kazi unaweza hata ukamuacha kumbe mali ipo na ataendelea kuitumia.

Izo ni mbinu tu za kumfanya mtuhumiwa afunguke.
Ndio unamvua nguo yeye na binti yake na kulazimisha wafanye mapenzi?
 
Sasa kama baba anabunduki ulitaka wamuimbie nyimbo aseme iliko????

Unadhani mtuhumiwa wa ujambazi wa siraha ili akuoneshe bunduki iliko ni kazi ndogo??? Ukipewa wewe iyo kazi unaweza hata ukamuacha kumbe mali ipo na ataendelea kuitumia.

Izo ni mbinu tu za kumfanya mtuhumiwa afunguke.

Polisi speed bado ni ndogo sana, nashauri iongezwe ili wahalifu wapaone Tanzania kama jehanam
Sawa afande
 
Sasa kama baba anabunduki ulitaka wamuimbie nyimbo aseme iliko????

Unadhani mtuhumiwa wa ujambazi wa siraha ili akuoneshe bunduki iliko ni kazi ndogo??? Ukipewa wewe iyo kazi unaweza hata ukamuacha kumbe mali ipo na ataendelea kuitumia.

Izo ni mbinu tu za kumfanya mtuhumiwa afunguke.

Polisi speed bado ni ndogo sana, nashauri iongezwe ili wahalifu wapaone Tanzanaia kama jehanam
Kwanini siku baba yako alipomla mama yako akuva condom wakatuletea takataka kama wewe
 
Back
Top Bottom