Rais Samia amtaka Kamishna Wakulyamba kutatua Matatizo ya Jeshi Usu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,883
12,133
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha viongozi wateule Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo 16 Juni, 2023.

Viongozi watakaoapishwa ni:
  1. Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi kuwa Balozi
  2. Mhe. Rogatus Hussein Mativila, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuwa naibu katibu Mkuu Tamisemi.
  3. Ndg. Iddi Seif Bakari, Konseli Mkuu Dubai, Kuwa Balozi Nchini Uturuki.
  4. Dkt. Salim Othman Hamad, Msaidizi wa Rais - Siasa, Kuwa Balozi.
  5. Dkt. Kassim Mohamed Khamis, Msaidizi wa Rais - Hotuba, Kuwa Balozi.

Rais Samia amesema amewateu watendaji wapya wa Kabidhi Wasii Mkuu na Naibu wake kutokana na uwepo wa ugomvi na kutokutekelezeka kwa kazi. Amewataka waende kushirikiana na kutoa huduma kwa wananchi badala ya kuendeleza migogoro.

Rais Samia amesema kuna kesi zinakuja juu lakini wakiwarudisha wahusika ngazi ya chini husema kuwa huko hakuendeki, wateule hawa wapya wanapaswa kutatua changamoto hii, kutoa huduma kwa wananchi na kufanya kazi kama walivyokula kiapo.

Aidha, Rais Samia amebainisha kuwa amempeleka Kamishna Wakulyamba kwenye Sekta ya Utalii na Maliasili kutokana na Changamoto ya Jeshi Usu ambalo limekuwa na kesi za kila siku ikiwemo kuuliwa na kuuana wao kwa wao na mambo mengine mengi yasiyofaa. Amemtaka Kamishna Wakulyamba kwenda kusimamia nidhamu ya jeshi hili.

Wengine wamepewa hadhi ya Ubalozi na baadhi wameteuliwa kwenye vitengo mbalimbali ili kuongezewa nguvu kwenye kazi zao kwa kuwa nchi yetu inakua kwa mambo baada ya kufunguliwa hivyo wasaidizi wanapaswa kuwa wengi. Idadi ya watu imeongezeka pia na watu wanahitaji huduma. Wanaoteuliwa wanapaswa kufanya kazi.
 
Kila mtanzania akichangia elfu 2 tu tutapata pesa ya kutosha kuendeshea na kununulia mashine za kisasa kuweza kuendesha bandari yetu badala ya kuwauzia warabu milele.

Watanzania walioaminishwa na Hayati Magufuli kwamba wanaweza na nchi yao ni tajiri na wakaanza kujenga miradi ya matrillioni ya fedha kama ndege, SGR, bwawa la umeme, kuhamia Dodoma, elimu bure, madaraja marefu Afrika mashariki na ya kati etc, ghafla sasa upepo umebadilika viongozi wote wanahubiri watanzania hawawezi na hawajiwezi kwa lolote kabisa! Bunge linasema kila kitu kipitishwe kwa sababu watanzania hawana uwezo wa kifedha wala akili ya kuendeleza miradi mikubwa kama ya bandari. Wapo pia wanasema hata taasisi za bunge na urais nazo zibinafisishwe ili ziweze kutoa matokeo chanya na ya haraka kwa wananchi.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha viongozi wateule Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo 16 Juni, 2023.

Viongozi watakaoapishwa ni:
  1. Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi kuwa Balozi
  2. Mhe. Rogatus Hussein Mativila, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuwa naibu katibu Mkuu Tamisemi.
  3. Ndg. Iddi Seif Bakari, Konseli Mkuu Dubai, Kuwa Balozi Nchini Uturuki.
  4. Dkt. Salim Othman Hamad, Msaidizi wa Rais - Siasa, Kuwa Balozi.
  5. Dkt. Kassim Mohamed Khamis, Msaidizi wa Rais - Hotuba, Kuwa Balozi.

Rais Samia amesema amewateu watendaji wapya wa Kabidhi Wasii Mkuu na Naibu wake kutokana na uwepo wa ugomvi na kutokutekelezeka kwa kazi. Amewataka waende kushirikiana na kutoa huduma kwa wananchi badala ya kuendeleza migogoro.

Rais Samia amesema kuna kesi zinakuja juu lakini wakiwarudisha wahusika ngazi ya chini husema kuwa huko hakuendeki, wateule hawa wapya wanapaswa kutatua changamoto hii, kutoa huduma kwa wananchi na kufanya kazi kama walivyokula kiapo.

Aidha, Rais Samia amebainisha kuwa amempeleka Kamishna Wakulyamba kwenye Sekta ya Utalii na Maliasili kutokana na Changamoto ya Jeshi Usu ambalo limekuwa na kesi za kila siku ikiwemo kuuliwa na kuuana wao kwa wao na mambo mengine mengi yasiyofaa. Amemtaka Kamishna Wakulyamba kwenda kusimamia nidhamu ya jeshi hili.

Wengine wamepewa hadhi ya Ubalozi na baadhi wameteuliwa kwenye vitengo mbalimbali ili kuongezewa nguvu kwenye kazi zao kwa kuwa nchi yetu inakua kwa mambo baada ya kufunguliwa hivyo wasaidizi wanapaswa kuwa wengi. Idadi ya watu imeongezeka pia na watu wanahitaji huduma. Wanaoteuliwa wanapaswa kufanya kazi.

Hakuna mtanganyika anayehitaji kusikia habari za hawa madalali
 
Back
Top Bottom