Paul Makonda kumjengea nyumba bibi anayenyanyaswa na Familia yake kisa hana Mtoto

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
16,028
10,509
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Paul Christian Makonda Anaendelea kufanya kazi ya kitume, kazi ya kugusa maisha ya watu, kazi ya kuwafuta wabubujikwao machozi,kazi ya kurejesha matumaini na tabasamu kwa waliokata tamaa na kupoteza matumaini,kazi ya kuleta nuru katika mioyo ya watu wenye giza ndani yao,kazi ya kuleta faraja kwa wenye mioyo ya huzuni na maumivu,kazi ya kuwapa watu mwanzo mpya wenye matumaini katika maisha yao.

Katika muendelezo wa kliniki yake yakusikiliza matatizo na kero za watu mbalimbali amejikuta katika wakati mgumu sana kibinadamu,amejikuta moyo wake ukijawa na huzuni,uchungu,machozi na huruma pale alipokutana na kukumbana na kilio cha juu sana kutoka kwa Bibi Penina mwenye umri wa miaka 70 ambaye hana makazi ya kuishi baada ya nyumba yake ya awali kubomoka, na ndugu zake kukataa kumjengea nyumba nyingine kwa madai kuwa hana mtoto yeyote yule ambaye atarithi nyumba hiyo na isitoshe yeye ni mzee sana na anaweza kufa wakati wowote ule.

Maneno hayo yalitua kama mkuki wa moto katika moyo wa Mheshimiwa Makonda ambaye alishikwa na huzuni na huruma kubwa sana, na kuamua kumpa faraja na kumtaka bibi huyo anyamaze nakuacha kulia kwa kuwa tumaini jipya limepatikana na kwamba mkuu huyo wa mkoa anakwenda kumjengea nyumba bora na ya kisasa kabisa ya vyumba viwili ambayo inakwenda kukamilika ndani ya mwezi huu wa mei pamoja na kumpatia ulinzi.

Bibi huyo ameripuka kwa furaha na shangwe kubwa sana iliyogusa hisia za watu wengi sana, ambao waliguswa na ahadi hiyo ya Mheshimiwa Makonda na kumpongeza sana kwa moyo wake wa Upendo na huruma kwa watu. Mheshimiwa Makonda ni mpango wa Mungu Mwenyewe kumuinua ili aguse maisha ya watu wanyonge na maskini wanaoteseka na shida mitaani.

Ndio sababu Anaendelea kubarikiwa na kulindwa na mkono wa Mungu Mwenyewe,ndio maana Anaendelea kupata kibali mbele za watanzania,ndio maana Anaendelea kuishi katika mioyo ya watanzania wanyonge wanaomuona kama mkombozi wao.ndio maana watu hawataki kwenda mahakamani wakiwa na kesi na badala yake wanamkimbilia kwanza Mheshimiwa Makonda ili awasaidie.

Ni kupitia Mh Makonda watu wengi waliokuwa wamedhulumiwa haki zao kama vile kunyang'anywa ardhi, kuporwa mali zao wamepata na kulipwa haki zao. Leo bibi huyu ambaye ameona nuru katikati ya giza ataendelea kumuombea Mh Makonda mbele za Mungu wakati wote wa uhai wake ili ambariki sana na kumlinda.hata siku atakapokuwa mbele za Mungu ataendelea kumuomba Mungu amkumbuke kijana wake Mheshimiwa Makonda aliyempatia tabasamu.

Tuwatunze wazee wetu na kuwapenda.kupata watoto na kuwa na watoto ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu. tutambue ya kuwa anayetoa watoto ni Mungu mwenyewe. Usimnyanyase mtu kwa kuwa hana watoto. Hana alikuwa Tasa na hakuwa na mtoto lakini baadaye Mungu alimpatia watoto miongoni mwao ni Samweli aliyekuja kuwa mfalme.kwa hiyo kupata mtoto au kutokupata ni mapenzi ya Mungu mwenyewe.

Pia suala la kusema huyu ni mzee anaweza akafa wakati wowote ule nalo ni wazo baya sana mbele za Mungu, kwa sababu ajuaye hesabu yake ya kuishi binadamu yeyote yule hapa Duniani ni Mungu pekee.leo hii kuna watu wanaishi hadi miaka mia moja yaani karne moja. Leo kule Marekani kuna watu wana miaka kama ya Bibi huyo na bado wanautaka Urais wa Marekani na wanaungwa mkono na watu wengi. Kwetu sisi tuna msemo kuwa embe bichi huanguka na kuliacha lililoiva mtini yaani inyembe indinda yikugwanga na kuileha intonu. Unaweza kujiona wewe ni kijana na ukajikuta unakufa na kutangulia mbele za haki na kumuacha huyo bibi akiendelea kuishi maisha marefu tu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Mimi nampenda sana Paul Makonda
Makonda anapendwa na mamilioni ya watanzania na ndio maana watu hufurika na kumiminika kwa wingi kama mchanga wa baharini au nyota za angani mahali popote pale awapo na mkutano. Mungu kampa kibali na Karama ya uongozi. Lakini kubwa zaidi ni kuwa Mheshimiwa Makonda ni kiongozi mchapa kazi,mbunifu na mwenye moyo wa kujitoa na kujitolea sana kwa watu.
 
Makonda yupo vizuri anaiweka CCM kwenye ramani
Ni kiongozi mchapakazi na mwenye moyo wa kujituma sana. Siyo viongozi wengine unakuta amejifungia ofisini kila siku mwaka hadi mwaka utafikiri kuku anayeatamia mayai.kiongozi ni lazima uwe karibu na watu unaowaongoza ili kujuwa na kufahamu shida na kero zao na kuwasaidia kwa kadri iwezekanavyo.
 
Kuna mambo mengi kwenye maisha huyazungumzii kazi tu.kupapatikia wanaume wenzako bashite atakuja kukufanyia jambo utashangazwa! Wewe endelea kushoboka
 
Back
Top Bottom