Nashauri mikopo ya elimu ya juu ifutwe, mbona wenzao wa diploma wanasoma bila mkopo iweje wao?

Nilipomaliza degree yangu nkakuta nadaiwaa mil 23 aiseee... degree ningeipatiaa wapi sasaa..!!
 
Utakuwa mpuuzi fulani hivi! Mkopo itolewe kwa wanafunzi wote bila kufuata vigezo. Watoto wasiokuwa na mikopo wanateseka mno chuoni!
 
Nashauri hii mikopo ya elimu ya juu ifutwe,mbona wanachuo wenzao wa diploma wanasoma bila mkopo na hatusikii kelele zozote?

Tofauti yao na wenzao wa diploma ipo wapi?

Nimeona serikali inataka kuwapa mikopo na hawa diploma,, hili nalo litakuwa kosa kubwa sana, yani kujibebesha mzigo juu ya mzigo ,,, cha muhimu hapo serikali wapige kimya tu na huko kwa ngazi ya degree wawafutie kabisa kama ikibidi labda wawape ada tu ,pesa ya kula wajitegemee.
Ungekuwa unajua gharama za masomo ya juu ungeshauri serikali iongeze mikopo.
Lakini ndiyo hivyo tena, umeishia diploma ambako laki 6 tu inatosha...
 
Hivi ni nini kazi ya Serikali na Kodi tunazotoa zinatakiwa kufanya nini ?

Yaani katika karne ambayo information / elimu ipo wazi naona watu tunazidi kukosa uelewa...

Na hapo mtu anaongelea mkopo na sio grant..., na heri angejua hao waliopo sasa hivi huko juu walisomeshwa bure wala bila mkopo....

Tofautisha Hisani na Wajibu....
 
Aisee jamaa we acha tu nimepitia msoto wa degree bila mkopo na home mambo yalikuwa sio shwari.
Chamoto nilikiona nimelala sana misikitini nimekula Sana mihogo,some time halfcake au kulala njaa kabisaaaaa.
Chupuchupu nibwage chuo mwaka wa 3 classmate na mkuu wa idara wakasema hapana kama nimepambana na shida za miaka miwili bila supplementary Wala carry licha ya changamoto zote wakaniunga mkono kwa kunilipia ada na wakaniwekea bili ya msosi.
Nawashukuru sana adi Leo kiukweli mungu awabariki Sana,🙏.
Naishauri serikali hii nchi pesa nyingi sana zinaliwa na wachache ni vema serikali ikaanza kutoa mikopo ya elimu kuanzia darasa la awali Tena Kwa wote wanaoomba.
Kiukweli hapo ndio watakuwa wameupiga mwingi sasa
 
Moja kati ya hoja za kishenzi na kipuuzi ya mwaka 2024 hapa jf ni hii unafaa kupuuzwa tu, inaoenakana wew umeishia form 4(div0) so roho inakuuma kweli shenz typ
Ushajiuliza hizo degree zina msaada Gani Kwani Kwa taifa kama sio wewe ndio mpumbavu
 
Nashauri hii mikopo ya elimu ya juu ifutwe,mbona wanachuo wenzao wa diploma wanasoma bila mkopo na hatusikii kelele zozote?

Tofauti yao na wenzao wa diploma ipo wapi?

Nimeona serikali inataka kuwapa mikopo na hawa diploma,, hili nalo litakuwa kosa kubwa sana, yani kujibebesha mzigo juu ya mzigo ,,, cha muhimu hapo serikali wapige kimya tu na huko kwa ngazi ya degree wawafutie kabisa kama ikibidi labda wawape ada tu ,pesa ya kula wajitegemee.
Mwenye akili timamu hawezi toa hoja ka kurupuka hivyo mkuu kunywa chai then soma tena uzi wako utagundua umeongea hakuna.
 
Mtoa uzi anaamini ada ya degree inaweza kua laki moja kwa mwaka then matumizi ya chakula na makazi yanacost 100000
 
Kuna vyuo vya private ada zake ni kubwa mno hasa kwa course za afya, hajafikiria kuhusu jamii zenye mazingira magumu ya kiuchumi, Sjapata majibu alifikiria nini kuandika huu uzi.
 
Back
Top Bottom