Mbowe kijana wa CCM kwa kivuli cha upinzani

CCM kama chama dola nchini Tanzania kimefanikiwa sana kujitengenezea upinzani wake na wapinzani wake ambao kwa uhalisia nao ni Ccm nje ya Ccm. Mmoja wao ni Mbowe na chama chake cha Chadema.

Historia inatuambia, waanzilishi wote wa Chadema walikuwa Benki kuu. Yaani Mtei, Bob Makani na Mbowe na walitolewa kwa sababu maalum kutengeneza chama cha upinzani ili Tanzania itambulike na dunia kama imeruhusu mfumo wa vyama vingi na demokrasia.

Tangu Chadema iasisiwe, hatujashuhudia kiongozi tofauti ya hao watatu waliotoka BOT kwa shughuli maalim kuulaghai umma wa kimataifa juu ya uwepo wa vyama vingi na demokrasia Tanzania.

Baada ya Chadema kuasisiwa, wakaja wanachama wengi ambao hawakuwa sehemu ya mpango huo (Kuilaghai dunia) hawa wakaja kwa nia ya dhati kabisa ya kuiondo Ccm na hapo ndio Mbowe akawa mkali kama pilipili.

Tunaanza na Kaburu, huyu bwana alikuwa mwiba kweli kwa serikali ya Ccm. Mbowe ili kulinda maslahi yake mwaka 2005 alishilikiana na Ccm Bega kwa Bega kuhakikisha Kaburu anashindwa na Serukamba. Kwanza Mbowe hakumpigia kampeni Kaburu, Kaburu hakupewa sapoti na Chama kabisa mpaka alipoangushwa. Na kama zawadi Mbowe akapewa jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto kabwe.

Baada ya Kaburu kikaja kizazi cha pili, kizazi cha vijana waliokuwa na uchu wa mabadiliko kweli kweli. Hapa nawazungumzia kina Zitto, kafulila na Machali. Hawa wote walisambalatishwa kama upepo. Ccm ikapumua tena.

2010 mpaka 2015 hakuna mwanamageuzi aliyeonyesha njia kama Dr Slaa, Ccm ilikuwa inaondoka. Mbowe akakumbushwa wajibu wake wa kuilinda Ccm. Akaletewa criminal Lowasa na kumpoteza Dr Slaa ambae angeweza kutunishana misuli na Magufuli. Tukapoteza tena kizembe.

Kumpongeza Mbowe kwa kuiongoza Chadema miaka 20 pasipo kuitoa Ccm ni ujinga, kuimba nyimbo za Mbowe kuwaita wanaompinga wanafiki ni ujinga. Tunatakiwa kumuhoji Mbowe kwanini ndani ya miaka 20 ya uongozi wako hatujaona matokeo zaidi ya kubadilisha bendera na kauli mbiu?

Wanasiasa aina ya Mbowe wapo wengi duniani, upinzani ni sehemu yao ya agizo la kuvilinda vyama tawala na kuhakikisha upinzani wa kweli haupatikani.

Baada ya kuonekana Mama Samia hana Ushawishi Mbowe kaamua kumfanyia kampeni kwa dirisha la upinzani. Kuandamana bila bugudha mama aonekane ni mwana demokrasia, kumsifia majukwaani na kukiri kusaidiwa nae.

Mbowe anatengenezea sana sympathy na Ccm ili aendelee kuaminiwa kama kinara wa upinzani ila kiuhalisia hizo ni niia tuu za ku block upinzani wa kweli kuaminiwa. Wanaoelewa siasa watanielewa.

View attachment 2946424

Kwa leo naweka kalamu chini.
Anzisha chama cha kwako
 
Kwa miaka mingi kumekuwa na tuhuma nyingi za kubumba zikimlenga mh Mbowe zikilenga kuuaminisha umma kwamba eti mamluki .Ajabu tuhuma hizo mara nyingi hutolewa na vijana wa fisiemu.Kama ndio hivyo kwa nini wasifurahie hiyo hali ili chama chao kiendelee kutawala kelele za nini?
 
Kwa ufinyu wa fikra zako kila anayemkataa Mamluki Mbowe ni Ccm. Fahamu tuu mimi ni Chadema niliyefahamu michèzo ya Mbowe. Hatukubali mtu mmoja kutuharibia harakati za ukombozi hata kama chama ni Mali ya familia yake. Kwanza tunaikomboa Chadema then tunaikomboa Tanzania toka mikononi mwa Ccm na vibaraka wao kina Always Chairman
 
Hicho chama kimejengwa na watu wote kupitia Kodi zao, hiyo taasisi ya umma Ila yeye Mbowe ndo anaitumia kama Mali yake binafsi ambapo ni makosa

Sent from my Nokia C10 using JamiiForums mobile app
 
CCM kama chama dola nchini Tanzania kimefanikiwa sana kujitengenezea upinzani wake na wapinzani wake ambao kwa uhalisia nao ni Ccm nje ya Ccm. Mmoja wao ni Mbowe na chama chake cha Chadema.

Historia inatuambia, waanzilishi wote wa Chadema walikuwa Benki kuu. Yaani Mtei, Bob Makani na Mbowe na walitolewa kwa sababu maalum kutengeneza chama cha upinzani ili Tanzania itambulike na dunia kama imeruhusu mfumo wa vyama vingi na demokrasia.

Tangu Chadema iasisiwe, hatujashuhudia kiongozi tofauti ya hao watatu waliotoka BOT kwa shughuli maalim kuulaghai umma wa kimataifa juu ya uwepo wa vyama vingi na demokrasia Tanzania.

Baada ya Chadema kuasisiwa, wakaja wanachama wengi ambao hawakuwa sehemu ya mpango huo (Kuilaghai dunia) hawa wakaja kwa nia ya dhati kabisa ya kuiondo Ccm na hapo ndio Mbowe akawa mkali kama pilipili.

Tunaanza na Kaburu, huyu bwana alikuwa mwiba kweli kwa serikali ya Ccm. Mbowe ili kulinda maslahi yake mwaka 2005 alishilikiana na Ccm Bega kwa Bega kuhakikisha Kaburu anashindwa na Serukamba. Kwanza Mbowe hakumpigia kampeni Kaburu, Kaburu hakupewa sapoti na Chama kabisa mpaka alipoangushwa. Na kama zawadi Mbowe akapewa jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto kabwe.

Baada ya Kaburu kikaja kizazi cha pili, kizazi cha vijana waliokuwa na uchu wa mabadiliko kweli kweli. Hapa nawazungumzia kina Zitto, kafulila na Machali. Hawa wote walisambalatishwa kama upepo. Ccm ikapumua tena.

2010 mpaka 2015 hakuna mwanamageuzi aliyeonyesha njia kama Dr Slaa, Ccm ilikuwa inaondoka. Mbowe akakumbushwa wajibu wake wa kuilinda Ccm. Akaletewa criminal Lowasa na kumpoteza Dr Slaa ambae angeweza kutunishana misuli na Magufuli. Tukapoteza tena kizembe.

Kumpongeza Mbowe kwa kuiongoza Chadema miaka 20 pasipo kuitoa Ccm ni ujinga, kuimba nyimbo za Mbowe kuwaita wanaompinga wanafiki ni ujinga. Tunatakiwa kumuhoji Mbowe kwanini ndani ya miaka 20 ya uongozi wako hatujaona matokeo zaidi ya kubadilisha bendera na kauli mbiu?

Wanasiasa aina ya Mbowe wapo wengi duniani, upinzani ni sehemu yao ya agizo la kuvilinda vyama tawala na kuhakikisha upinzani wa kweli haupatikani.

Baada ya kuonekana Mama Samia hana Ushawishi Mbowe kaamua kumfanyia kampeni kwa dirisha la upinzani. Kuandamana bila bugudha mama aonekane ni mwana demokrasia, kumsifia majukwaani na kukiri kusaidiwa nae.

Mbowe anatengenezea sana sympathy na Ccm ili aendelee kuaminiwa kama kinara wa upinzani ila kiuhalisia hizo ni niia tuu za ku block upinzani wa kweli kuaminiwa. Wanaoelewa siasa watanielewa.

View attachment 2946424

Kwa leo naweka kalamu chini.
Zito huyu huyu malaya wa kisiasa? Kafulila huyu huyu malaya wa chawa?
 
Wewe endelea kutawaza watoto wa Mbowe, Achana na mambo anayotakiwa kujadili baba yako
Umeshindwa ku defend andiko lako la kuunga unga unaleta mada nyingine ambazo zinazidi kukuvua nguo kuwa wewe ni zero brain.
 
Hivi unataka kujisahaulisha kuhusu nini ambacho kilitokea kwa makada na viongozi mbalimbali wa CDM ikiwamo hata Mbowe mwenyewe katika utawala wa JPM miaka michache iliyopita!? Watu kuteswa, kutekwa, kujeruhiwa, kuuwawa, kubambikiwa kesi za uongo, mali zao kuhujumiwa, n.k.
Halafu anakuja mngese mmoja amekaa na kuvimbiwa futari anaandika gazeti la kuwapaka matope watu walioteseka kwa kusema ukweli, kukaa magerezani wakati yeye yuko na mumewe analiwa, watu wanashambuliwa kwa risasi na mabomu, kesi za kubambikwa na ushenzi wa kila aina.
Hizi propaganda za kishetani kabisa

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom