Maktaba Imetembelewa na Mwalimu wa Historia ya Tanzania

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,149
30,495
MAKTABA IMETEMBELEWA NA MWALIMU WA HISTORIA YA TANZANIA
Maktaba imepata bahati kubwa sana na heshima ya pekee kwa kutembelewa na mwalimu anaesomesha somo la historia kiwango cha shule za sekondari.
Kwa mara ya kwanza nimebahatika kusikia na nimejifunza mengi kwanza changamoto zilizomo katika kusoma historia ya Tanzania Chuo Kikuu na pili changamoto wanazopata wahitimu wanapokwenda kusomesha somo lenyewe darasani.

Nimetengeneza video nne za mada tulizojadili na nimeziweka Maktaba kwa atakae kujifunza elimu mpya katika historia ya Tanzania:
  1. Tatizo la Uandishi wa Historia ya Tanzania​
  2. Waislam na Historia ya Uhuru wa Tanzania​
  3. Tatizo la Kufundisha Historia ya Tanzania​

  2. Waislam na Historia ya Uhuru wa Tanzania
  3. Tatizo la Kufundisha Historia ya Tanzania​

Na 2. Itakusumbua sana hadi ukamilifu wa dahali!
 
Na 2. Itakusumbua sana hadi ukamilifu wa dahal
Isele....
Hapana hainisumbui.
Inawasumbua watu wengine.

Napokea wanafunzi wengi wanaotaka kujifunza historia ya uhuru wa Tanganyika.
Hapa JF Jukwaa la Histiria mijadala inaongezeka kila siku.
 
MAKTABA IMETEMBELEWA NA MWALIMU WA HISTORIA YA TANZANIA
Maktaba imepata bahati kubwa sana na heshima ya pekee kwa kutembelewa na mwalimu anaesomesha somo la historia kiwango cha shule za sekondari.
Kwa mara ya kwanza nimebahatika kusikia na nimejifunza mengi kwanza changamoto zilizomo katika kusoma historia ya Tanzania Chuo Kikuu na pili changamoto wanazopata wahitimu wanapokwenda kusomesha somo lenyewe darasani.

Nimetengeneza video nne za mada tulizojadili na nimeziweka Maktaba kwa atakae kujifunza elimu mpya katika historia ya Tanzania:
But we cannot go back!
You cannot do anything for past mistakes (historia iliyofichwa ya Uhuru wa Tanganyika)
So why do you hold onto this pain? What will it give you? If the food in our refrigerator was rotten, would we keep it as a reminder to not be wasteful in the future?
  1. Tatizo la Uandishi wa Historia ya Tanzania​
  2. Waislam na Historia ya Uhuru wa Tanzania​
  3. Tatizo la Kufundisha Historia ya Tanzania​

But we cannot go back!
You cannot do anything for past mistakes (historia iliyofichwa ya Uhuru wa Tanganyika)
So why do you hold onto this pain? What will it give you? If the food in our refrigerator was rotten, would we keep it as a reminder to not be wasteful in the future?
Isele...
Sijasema turejee nyuma.

Hayo makosa ya kusomesha historia isoyokuwa ya kweli ndiyo tayari nimesayasahihisha kupitia kalamu yangu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Haya si machungu kwangu.
 
TUFANYE NINI NA HIZI CLIP ZINAZOPOTOSHA HISTORIA YA TANZANIA?

Kuna clip inazunguka mitandaoni ikieleza mengi kuhusu Tanganyika.

Kubwa linaloshtua watu wengi ni kusema imani kuu nchini ni Ukristo.

Nimeandika makala hiyo hapo chini kutanabaisha kuhusu historia ya Tanganyika nikijaribu kueleza imekuwaje tumefikia hali hii:

DR. KWEGIYR AGGREY NA KLEIST SYKES DAR ES SALAAM 1924

Alikuwa Dr James Kwegyir Aggrey, Mwafrika kutoka Ghana ndiye mtu aliyemtia Kleist hamu ya kuingia katika siasa. Dr Aggrey alikuja Tanganyika mwaka 1924.

Dr Aggrey alikuwa katika Phelps-Stokes Commissions iliyokuwa imeundwa kuchunguza elimu ya Waafrika.

Ilikuwa katika kipindi hiki akiwa ndani ya kamisheni hii ndipo alipokuja Tanganyika. Dr Aggrey alikataliwa kupanga New Africa Hotel kwa kuwa alikuwa mtu mweusi.

Ikabidi Gavana Donald Cameron amtafutie chumba Government House ajisitiri kwa malazi.

Wakati huu alipokuwa Dar es Salaam ndipo Dr Agrrey alipokutana na Kleist.

Dr Aggrey alimtunukia Kleist moja ya vitabu vyake na akakitia sahihi yake.

Hakuna hata mtoto mmoja wa Kleist ambae anakumbuka jina la kitabu hiki.

Kleist alikithamini kitabu hiki na kilipamba shubaka lake la vitabu kwa miaka mingi.

Mwaka wa 1929 Kleist na baadhi ya rafiki zake wa karibu kama Mzee bin Sudi, ambaye wazazi wake walikuwa Wamanyema kutoka Belgian Congo, Ibrahim Hamis - Mnubi ambaye baba yake alitoka Daffur nchini Sudan, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima - Mzaramo, Suleiman Majisu, Raikes Kusi, Rawson Watts na Cecil Matola - Myao kutoka Masasi walianzisha African Association, Matola akiwa President na Kleist Secretary.

Historia ya uhuru wa Tanganyika iligeuzwa ikawa historia ya Julius Kambarage Nyerere.

Historia ya TANU ikawa historia ya mtu mmoja.

Hili lilifanikiwa kwa kuwa tulikaa kimya lau kama walikuwapo wazalendo wenyewe walioupigania uhuru kwa hali na mali zao.

Sasa tueleze harakati za uhuru wapi zilianzia.

Tunaweka picha ya Dictionary of African Biography (DAB).

Kinawekwa kipande kifupi kinachomweleza Dr. Kwegyir Aggrey (1875 - 1927) kisha ndani ya Kamusi hilo hilo tunatoa na kumwekea mtazamaji wa clip yetu kipande kifupi cha Kleist Abdallah Sykes (1894 - 1949).

Wazalendo hawa waliotajwa ndani ya Kamusi hilo tunaeleza hawamo katika historia rasmi ya Tanganyika.

Mazungumzo kati ya Waafrika hawa wawili Dar-es-Salaam mwaka wa 1924 ndiyo yalisababisha Kleist kuunda African Association mwaka wa 1929 kisha kuunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka wa 1933.

Vyama vyote hivi viwili vilitawaliwa na Waislam.

Watafute wazalendo hawa katika historia ya Tanganyika hutowakuta popote.

Jambo la kusikitisha ni kuwa watu waliamini kuwa ile historia iliyokuwa ikisomeshwa ndiyo historia ya kweli.
 
Somo la historia lifutwe tu mashuleni na vyuoni wanafunzwe wafunzwe zaidi mambo ya teknolojia na vitu vinavyoweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi kuwapa fani za kuwezesha mtu kujiajiri.Badala ya kujaza porojo za vijiweni hata ziwe za kweli au uongo zinajaza hard disk kichwani Bure tu.Somo la historia lifutwe kuanzia chekechea Hadi vyuo vikiu vyetu
 
Somo la historia lifutwr tu mashuleni na vyuoni wanafunzwe wafunzwe zaidinmbo ya teknolojia na vitu mainavyoweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi kuwapa fani za kuwezesha mtu kujiajiri.Badala ya kunjaza porojo za vijiweni hata ziwe za kweli au uongo zinajaza hard disk kichwani Bure tu.Somo la historia lifutwe kuanzia chekechea Hadi vyuo vikiu vyetu
Shoto...
Inaelekea huuelewi mjadala huu.

Itakubidi usome maudhui yake kwanza ndiyo utakuwa katika hali ya kuchangia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom