Ugeni wa TBC Safari Channel Maktaba

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,071
30,419
UGENI WA TBC SAFARI CHANNEL MAKTABA
Leo asubuhi Maktaba ilibahatika kupokea ugeni kutoka TBC Safari Channel watayarishaji na Warushaji wa vipindi vya historia.

Walinifahamisha kuwa wapo katika kutafiti historia ya Abushiri bin Salim Al Harith ambae wao wamepita ulipokanyaga mguu wake Pangani na Bagamoyo wakati yeye na jeshi lake walipokuwa wanapigana na jeshi la Hermann von Wissmann.

Walinifahamisha kuwa wamenisikia mara nyingi na kunisoma pia nikieleza historia za majemadari hawa wawili na wamenitembelea tubadilishane fikra kwani kuna mengi katika historia ya Abushiri ambayo hayako wazi na kuwa rahisi kueleweka.

Walitaka kujua kuhusu wapi Pangani lilipo kaburi la Abushiri.
Walitaka kujua asili ya Abushiri.

Abushiri ni Muarabu au Mwafrika?
Bushiri ni mzalendo aliyekuwa akipigania uhuru wa nchi yake?

Walitaka kujua kwa nini Abushiri aliwashambulia na kuua Wamishionari Pugu.

Walitaka kujua uhusiano wa Mtwa Abdallah Mkwawa chifu wa Wahehe na Abushiri.

Mtwa Mkwawa alisilimishwa na Abushiri na kuwa Muislam na Uislam uliotamalaki kwa Wahehe chanzo chake ni Bushiri.

Tumebadilishana notes katika mengi yaliyotokea nyakati hizi kufikia Wissman alivyoingia vitani na Mangi Meli.

Tulijadili jeshi la Wajerumani lililokuwa na askari mamluki wa Kizulu kiasi cha 400 kutoka kijiji cha Kwa Likunyi Imhambane, Mozambique na Wanubi kutoka Sudan ambamo ndani ya jeshi hili alikuwamo Chief Mohosh Shangaan na Sykes Mbuwane.

Walishangaa nilipowafahamisha kuwa Chief Shangaan Mohosh alikuwapo Nzole, Bagamoyo pamoja na Wissmann katika mapigano yaliyosambaratisha jeshi la Bushiri.

Chief Shangaan alikuwapo Nzole chini ya Wissmann akiongoza lile jeshi la Wazulu na Wanubi dhidi ya Abushiri.

Bushiri alinusurika katika mapigano hayo na kukimbia.
Haukuchukua muda mrefu kuanzia pale Bushiri akakamatwa baada ya kusalitiwa.

Bushiri alishirakiwa katika mahakama ya kijeshi na kuhukumiwa kifo.
Baada ya kumshinda Abushiri Wissmann akaelekea Kalenga kupambana na Mkwawa.

Majeshi haya yakapambana Lugalo.
Historia hii ni maarufu.

Inakumbukwa miaka mingi baada ya ngome ya Mtwa Abdallah Mkwawa kufa.

Huyu Chief Mohosh baada ya German Ostafrika kutulia Wajerumani wakamfanya ndiye Mkuu wa German Constabulary jeshi lao la ulinzi.
Chief Mohosh Shangaan kuanzia hapo akajulikana kwa jina la Affande Plantan.

Tumekubaliana kuendelea na utafiti na mazungumzo zaidi kujaribu kuiweka vyema historia ya Abushiri.

Kishindo kikubwa nimewaachia nilipowaeleza kuwa ukoo wa Abushiri upo hadi leo Zanzibar na mimi nimebahatika kufahamiana kwa karibu na kitukuu cha Abushiri.

Wajukuu na vilembwe wa Abushiri bado wana ardhi Zanzibar iliyokuwa ya babu yao ingawa mali zote za babu yao zilitaifishwa na Wajerumani Bushiri alipokimbia Zanzibar na kuhamia Pangani.

Nimetengeneza video za mazungumzo yetu mnaweza mkaziangalia na nimeweka picha ya Bushiri na picha ya Hermann von Wissman.

https://youtube.com/@samitungo?si=C5e5U5NLdiuxFXJe
https://youtu.be/OLkRG1iNA7E?si=nsorqzEQF8pvONX3


View: https://youtu.be/hXt1-whsetY

View: https://youtu.be/dG9dGMidw4c

View: https://youtu.be/OLkRG1iNA7E

1715183979844.png

1715184046366.png

1715184088412.png
 
Hongera sana mzee wetu, wewe ni kisima kisichokaukiwa, Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu ili tuzidi kujifunza kutoka kwako mzee wetu.
 
Back
Top Bottom