Mabasi 38 ya kampuni ya New Force yapigwa stop na LATRA kusafiri usiku, kuanza huduma saa 12 asubuhi

Munch wa annabelletz47

JF-Expert Member
Aug 13, 2019
965
1,347
Kampuni ya usafirishaji abiria ya NEW FORCE yapigwa stop leo kuendelea na safari zake baada ya kupata ajali mfululizo na kuthibitika kuwa wengi wa madereva wao hawajathibitishwa na mamlaka hiyo.

=======

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imefuta ratiba za saa 9.00 alfajiri na saa 11.00 alfajiri kwa mabasi 38 ya New Force Enteprises, ambapo mabasi 10 ni yale yanayoanza safari saa 9.00 alfajiri na mabasi 28 yanayoanza safari saa 11.00 alfajiri, kufuatia mfululizo wa ajali za mabasi hayo ambapo ndani ya Wiki nne (Kati ya June 06 - July 02,2023) mabasi matano yamepata ajali.

“Kuanzia tarehe 5 Julai, 2023, mabasi haya 38 yatafanya safari zake kuanzia saa 12.00 asubuhi na kuendelea hii ni kwakuwa uchunguzi wa awali wa LATRA ulibaini kuwepo kwa uvunjaji wa makusudi wa kanuni hususani kutumia ratiba za saa 9.00 alfajiri na saa 11.00 alfajiri bila dereva kuwa amethibitishwa na LATRA na pengine dereva kuwa amethibitishwa lakini hatumii mfumo wa utambuzi wa dereva (i-button) anapoendesha basi”

“Kanuni zinamtaka dereva anayeendesha basi la abiria kutumia kifaa cha utambuzi ili tuweze kuwafuatilia kwa mfumo wetu wa Kufuatilia Mwenendo wa Mabasi (VTS) yanapokuwa safarini lakini uchunguzi tulioufanya kwenye magari haya yaliyopata ajali tumebaini ukiukwaji wa sharti hilo kwa mabasi ya Kampuni ya New Force Enterprises”

“Kutokana na ukiukwaji huu, Mamlaka imeshindwa kuwatambua madereva waliokuwa wanaendesha mabasi haya ili kuweza kuwachukulia hatua au kupeleka taarifa zao Jeshi la Polisi - Kikosi cha Usalama Barabarani ili wawajibishwe kwa mujibu wa Sheria za Usalama Barabarani, pia tumebaini ukiukwaji wa ratiba za mabasi ambayo hayakuwa kwenye ratiba ya saa 9.00 alfajiri na saa 11.00 alfajiri kwa kufanya safari muda huo bila kibali cha LATRA”

Chanzo: Millard Ayo
 
Latra hawana uwezo wakuyafungia hayo mabasi kinachofanyika ni kiini macho tu mpo mtaniambia hazipiti siku tatu wataluwa load, maadhi ya maafisa wa latra wanajua kuwa new force ni mbia mwenzao wana kula nae.
 
Kampuni ya usafirishaji abiria ya NEW FORCE yapigwa stop leo kuendelea na safari zake baada ya kupata ajali mfufulizo na kuthibitika kuwa wengi wa madereva wao hawajathibitishwa na mamlaka hiyo

Source: Trust me bro
Trust Me:
Next week zitaitwa NEW FACE na zitakua barabarani na sura mpyaaaa.... Ruti zake kama kawa.
Usajili kampuni mpya umekamilika
 
Source: Trust Me Bro

Kumbe Tanzania tuna vyanzo vingi vya habari namna hii ?🙌

Ila ni hatua muhimu kuweza kupunguza ajali, maana ndani ya mwezi mmoja zimetokea ajali zaidi ya 7 kwa kampuni moja ya usafirishaji
 
Latra hawana uwezo wakuyafungia hayo mabasi kinachofanyika ni kiini macho tu mpo mtaniambia hazipiti siku tatu wataluwa load, maadhi ya maafisa wa latra wanajua kuwa new force ni mbia mwenzao wana kula nae.
Sema hawa jamaa ni wanakimbia hatar gari za mchina tena namba D kumuacha nyuma kila siku scania tena namba D tena Sauli sio kaz rahisi
 
Back
Top Bottom