LATRA yawataka Wamiliki mabasi ya Sauli na New Force kujieleza kabla ya kuchukuliwa hatua

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,317
5,479
WAMILIKI MABASI YA SAULI NA NEW FORCE WATAKIWA KUJIELEZA KABLA YA KUCHUKULIWA HATUA ZA KIUDHIBITI

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imefanya kikao kilichohusisha Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na wamiliki wa mabasi ya Sauli na New Force yaliyosababisha ajali ya tarehe 28 Machi, 2024 majira ya saa tisa na dakika arobaini na mbili (09:42) alfajiri, ambapo magari matatu yaligongana eneo la Mashamba ya Mpunga Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani katika barabara ya Morogoro. Kufuatia kikao hicho, Mamlaka imewataka wasafirishaji hao kutoa maelezo kwa maandishi kabla ya kuchukua hatua za kiudhibiti dhidi yao.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, ajali hiyo imetokana na uzembe wa dereva wa basi namba T668DTF Scania mali ya Mwalabhila Sauli kutaka kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari ya watumiaji wengine wa barabara.

Aidha, madhara ya ajali hiyo yalichangiwa na uzembe wa dereva wa basi namba T175DZU linalomilikiwa na kampuni ya New Force kushindwa kuacha umbali wa gari lililokuwa mbele yake kama inavyopaswa na kusababisha vifo vya watu wawili (2), majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali.

Kwa mujibu wa taarifa za Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS), tarehe ya tukio magari namba T175DZU na T6668DTF yalianza safari kutoka Dar es salam kwa pamoja saa nane na dakika arobaini na nne (8:44) usiku, ambapo kwa mujibu wa leseni walizopewa, mabasi hayo yalipaswa kuanza safari saa tisa kamili (9:00) na saa kumi na dakika thelathini (10:30) alfajiri, mtawalia.

Aidha, uchunguzi zaidi kwenye mifumo ya Mamlaka unaonesha kuwa madereva wa mabasi hayo wamesajiliwa kwenye mifumo ya Mamlaka lakini hawakutumia vitufe vya utambulisho (i-Button).

Kwa jumla, makosa yaliyobainika yamechangiwa na madereva pamoja na wamiliki wa mabasi hayo. Mamlaka inawakumbusha wamiliki na madereva kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria katika kutoa huduma za usafiri.

Hata hivyo, takwimu zinaonesha kuwa, safari za mabasi ya usiku nchini, zina matukio machache ya ajali na vifo ukilinganisha na safari za mchana. Kati ya mwezi Oktoba 2023 na Februari, 2024 kulitokea jumla ya ajali 68 ambazo kati yake ajali 10 tu zilitokea usiku.

Vilevile katika kipindi hicho, vifo vilivyotokana na ajali za mabasi vilikuwa 9 ambapo vifo 4 vilitokana na safari za usiku. Mamlaka inawashukuru watoa huduma za usafiri wa mabasi ya masafa marefu kwa ushirikiano wao katika kutekeleza ratiba za safari za usiku.

Imetolewa na;
Salum Pazzy
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano


photo_2024-04-02_21-27-49.jpg

photo_2024-04-02_21-27-51.jpg
 
Sawa

Ajali 10 usiku

Ajali 58 sio usiku.


Inatakiwa aeleze usiku kuna tutor ngapi

Mchana kuna ruti ngapi.

Na taarifa nyingnezo

Angalau Tuone kiasilimia.

Hiyo takwimu ina taarifa chache sana kuweza kufikia hitimisho ya mlinganisho wa usiku na mchana
 
WAMILIKI MABASI YA SAULI NA NEW FORCE WATAKIWA KUJIELEZA KABLA YA KUCHUKULIWA HATUA ZA KIUDHIBITI

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imefanya kikao kilichohusisha Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na wamiliki wa mabasi ya Sauli na New Force yaliyosababisha ajali ya tarehe 28 Machi, 2024 majira ya saa tisa na dakika arobaini na mbili (09:42) alfajiri...

1. Kwani hayo magari yaliyopata ajali Ruvu hayakuwa namba E au D?

2. Wamiliki wake wakajieleze nini, si wa kujieleza walikuwa madereva tena polisi na mahakamani?

3. CHADEMA wekeni wazi kwenye agenda, hawa ni Moja ya zile taasisi zisizokuwa na Tija za kuondosha mara TU nchi hii ikikombolewa.
 
Hizo barua zikatazo rudi za kujieleza,zitarudi na bshasha
Zilizojaa hela
Hayo mabasi aka majeneza zitaendelea kuua kama kawaida

Ova
Kila siku watu wamekuwa wakilalamika humu na sehemu mbalimbali kuhusu hayo mabasi lakini sio LATRA wala Polisi waliowachukulia sheria.

Kimsingi magari hayo kuua ilikuwa ni jamno la Muda tu, pia wanaopanda hayo mabasi ni watu wenye mtindio wa ubongo. Mi siwezi panda hayo magari hata nikiwa naumwa.
 
Hata hivyo, takwimu zinaonesha kuwa, safari za mabasi ya usiku nchini, zina matukio machache ya ajali na vifo ukilinganisha na safari za mchana. Kati ya mwezi Oktoba 2023 na Februari, 2024 kulitokea jumla ya ajali 68 ambazo kati yake ajali 10 tu zilitokea usiku.

😁

Kuna bosi kashaandika ripoti na kajiona kaweka facts...
 
Sio LATRA ndio wawafuate hao vigogo wa ajali huko waliko?
Kuna mhindi Fulani alitakiwa akatoe maelezo central police, jamaa kwa kujiamini kabisa alimwambia yule afisa wa police kwamba Yuko busy kwa muda ule.
 
Back
Top Bottom