SoC03 Kuibuka kwa Taasisi/vikundi vingi vya kukopesha pesa mtandaoni: Je, wananchi wana uelewa? Usalama wa Taarifa Binafsi unazingatiwa?

Stories of Change - 2023 Competition

DON YRN

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
475
999
Na DON YRN.
Habari za wakati huu wadau wa JamiiForums?, matumaini yangu tupo salama katika ujenzi wa Taifa letu. Lengo langu kutoa mada hii siyo kuleta uchonganishi au kuchafuliana biashara, hapana, lengo ni kufichua kile kinachoonekana kipo kinyume kwenye jamii.

Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la taasisi/vikundi mbalimbali vinavyokopesha fedha kupitia mitandao mbalimbali ya simu hapa nchini Tanzania kama Airtel, Vodacom, Tigo, Halotel, Zantel, n.k. Vikundi/taasisi hivi vimekuwa vikijitangaza kutoa mikopo hii kupitia majukwaa mbalimbali ya kijamii kama facebook, twitter, Instagram, n.k. na muda mwingine vimekuwa vikitumia kujitangaza kupitia baadhi ya vyombo vikubwa vya habari vinavyoaminika kwa umma.

Swali la kujiuliza hapa ni Je, hivi vikundi/taasisi zinatambulika na serikali au hazitambuliki?.

Lengo la kutolewa kwa mikopo huwa ni jema kwa maana ya kumsaidia mhusika/mkopeshwaji palipo na uhitaji wa pesa na mkopeshaji apate faida. Pamoja na yote hayo, hakuna elimu ya kueleweka inayotolewa na hizi taasisi/vikundi kwa wakopaji vilivyoibuka ghafla kabla ya kuchukua mkopo bali elimu hutolewa baada ya mkopaji kuchukua mkopo.

Kwa mfano; katika uchunguzi wangu kwenye hili jambo, niliwahi kuomba mkopo kwenye mojawapo ya taasisi inayokopesha pesa mtandaoni. Niliwapigia kuuliza namna ya kupata mkopo nikajibiwa kuwa tuvuti yao ina maelezo zaidi yanayojitosheleza. Nilifungua wavuti yao nikaambiwa kujaza taarifa zangu muhimu binafsi km Majina yangu matatu(3), Namba ya simu, barua pepe, namba ya kitambulisho cha Taifa(NIDA), mahali ninapoishi pamoja na kupakia picha inayoonesha sura yangu(Passport size). Baada ya hapo nikaandikiwa "OMBA MKOPO", hapo kwenye OMBA MKOPO nilitegemea nitaletewa chaguo la kuomba kiasi ninachohitaji lakini haikuwa hivyo, nilitumiwa ujumbe kwamba nimekopeshwa TSH 4,850 na ninapaswa kulipa TSH 7,750 ndani ya siku saba(7).

Niliwapigia kuwauliza inakuwaje napewa mkopo ambao sijaomba?, nikajibiwa kuwa mpangilio wao wa uombaji mkopo ndo ulivyo na RIBA yao ni 35% (kiasi cha RIBA kilicho kikubwa sana)na zikizidi siku 7 deni litakuwa linaongezeka kwa RIBA ya 5% kila siku. Hii ina maana Elimu au taratibu zilizokamilika za mkopo nilipewa baada ya kupewa mkopo hali ambayo inazua utata na kuhusisha UTAPELI.
Screenshot_20230522_163312_PesaX.jpg
Picha mbalimbali zikionesha namna ya kujisajili kwenye mojawapo ya taasisi ya kukopesha pesa mtandaoni.
Screenshot_20230522_163651_PesaX.jpg

Hali nyingine ni kwamba; Hizi taasisi/vikundi vya kukopesha hela mtandaoni, vinatambulika na taasisi za kiserikali zinazosimamia masuala ya fedha kama wizara ya Fedha, Benki kuu, wizara ya viwanda na biashara, n.k?. Na sheria zinatafsiri vipi kuanzishwa kwa taasisi za kukopesha pesa sana sana kwenye RIBA na muda wa kurejesha?. Kama havitambuliki, ni hatua gani zimechukuliwa maana udhibiti wa mitandao inayotumika kutangazia hizi taasisi iko chini ya usimamizi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)?.
Screenshot_20230522_163521_Permission controller.jpg

Kama vikundi/taasisi hizi za kifedha havitambuliki, taarifa za wananchi/mwananchi mmoja mmoja zinaweza kuwa hatarini kwa maana mwananchi anaweza asielewe taarifa zinazochukuliwa tena mtandaoni zinaenda kutumika kwenye malengo yapi. Hii inarejea mfano wa taarifa nilizozitoa wakati nafanya uchunguzi wangu binafsi kuhusu mikopo ya mtandaoni. Taarifa hizo ni kama Majina yangu Matatu(3), barua pepe, namba ya simu, namba ya kitambulisho cha Taifa(NIDA), Mahali ninapoishi na kupakia picha ya passport size. Hizi taarifa ni muhimu mno maana zinaweza kutumika hata kufanyia UTAPELI/UHALIFU wa kimtandao au kutumika na majasusi wa nje kudukua taarifa muhimu za NCHI maana wananchi wanakuwa hawana uelewa kama wakopeshaji ni watu wema au siyo wema kwa maana mikopo inatolewa bila kuonana bali njia ya mtandao. Mfano, hizi taasisi/vikundi zinatumia programu tumishi(Apps) ambazo ili mkopaji apate mkopo, inamlazimu apakue programu tumishi husika na ajisajili. Hii ni hatari sana sababu watu wengi siku hizi wanatumia simu hata kuhifadhi nyaraka za kiofisi.

Kwa upande wangu na mawazo yangu huenda hivi vikundi/taasisi vimebadili mfumo kutoka kushawishi wananchi kwamba wakiwekeza kiasi fulani cha fedha wanaweza kupata FAIDA baada ya muda fulani na sasa vimekuja na mtindo huu wa kukopesha. Muda mwingine vinatumia hata majina ya watu maarufu kama viongozi, wasanii, n.k.

Kwa ujumla, ni jukumu na wajibu serikali kutoa elimu kwa wananchi wake ili kuendana na mabadiliko ya ukuaji wa teknolojia hasa biashara za mtandaoni ili kuepusha mianya yote ya UTAPELI inayoweza jitokeza. Pia hatua kali za kisheria zinapaswa kuchukuliwa kwa wale wanaopatikana na hatia ya UTAPELI ili kufikia hatua halali ya ujenzi wa nchi yetu pendwa Tanzania.
Screenshot_20230519_175351_Facebook.jpg
Screenshot_20230521_072750_Facebook.jpg
Screenshot_20230521_072907_Facebook.jpg
Screenshot_20230521_084114_Facebook.jpg
Screenshot_20230522_043620_Facebook.jpg
Screenshot_20230522_043954_Facebook.jpg
Screenshot_20230522_044221_Facebook.jpg

Hizi ni baadhi ya picha zinazowakilisha baadhi ya taasisi zinazokopesha fedha kwenye mitandao hasa.
Chanzo: Facebook.
 
mi nalipa aisee maana naomba kwa hiari na wananipa kistaarab.
cha kujadiri ni riba zao. wengi au wote ni 60% riba!!!!!!!
kwa wale waungwana tujuzane wenye riba rafiki.
tuache kujisifia WIZI! mana unakopa kwa hiari! miafrica aisee!
 
Back
Top Bottom