- Source #1
- View Source #1
Wakuu,
Nimesikia sikia sehemu kuwa wakati wa tendo pale mwanaume akiwa anabana pumzi stamina inakua inaongezeka na anaweza kudumu kwa muda mrefu zaidi.
Kuna mwenye amewahi kushuhudia hili au kuna maelezo ya kisayansi yanayothibitisha hili? Mimi naona nilipigwa kamba tu hapa!
Kwenu wataalam wa JamiiCheck, ni ukweli au uzushi tu?

- Tunachokijua
- Kupumua ni kitendo cha kusukuma au kuvuta hewa ndani na nje ya mapafu kupitia pua au mdomo ili kuweza kubadilishana gesi na mazingira ya ndani, hasa kwa kuleta oksijeni na kutoa kaboni dioksidi.
Ngono (Tendo la ndoa) ni kitendo cha kujamiiana kati ya mwanamke na mwanamume ambapo tendo hilo humalizika vizuri kwa wenza hao kufika kileleni
Kufika kileleni ni msisimko wa kipekee unaoleta hisia nzuri baina ya wenza wanaojamiiana na huwa ni moja ya ishara ya kumalizika kwa haja za tendo hilo.
Je, ni kweli kubana pumzi wakati wa tendo kunaweza kusababisha Mwanaume kuchelewa kufika kwenye mshindo?
JamiiCheck ilimtafuta na kuzungumza na mtaalam wa Afya, Dkt. Godfrey Chale Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake ambae alibainisha kuwa:
Ni kweli inawezekana kubana pumzi wakati wa tendo kunaongeza nguvu kwa Mwanaume na kuweza kuendelea na hilo tendo kwa muda.
Unapofika kuelekea katika hali ya mshindo, mwili unakuwa unajiachia, hivyo kwa kubana pumzi unakuwa umeuzuia mwili kuendelea kujiachia.
Kubana pumzi ni mojawapo ya njia ya kujizuia, kwa Kiingereza inaitwa “stop-start technique”. Ukiona ukaribia kufika mshindo unabana pumzi huku ukiwa unabana makalio, hili huzuia manii zisitoke, hivyo unaweza ukaendelea na tendo.
Kutokana na majibu ya mtaalam wa afya JamiCheck inathibitisha kuwa ni kweli kubana pumzi mwanaume akiwa anakaribia kufika mshindo humsaidia kuchelewa kuchelewa kufika mshindo.