SoC03 Kitambulisho cha Taifa kiboreshwe ili kuendana na ulimwengu wa kidigitali

Stories of Change - 2023 Competition

Rs MI

Senior Member
Jul 26, 2022
182
577
Nakala.png

Kitambulisho cha taifa hutumika kuthibitisha uraia wa mwananchi kwenye taifa husika. Lakini namna ulimwengu unavyoshuhudia ukuaji wa kasi kwenye sekta ya teknolojia ni vizuri kuboresha kitambulisho cha taifa kwa kukiwezesha kubeba taarifa nyinginezo muhimu pamoja na nyaraka za mhusika. Itasaidia katika kuepuka changamoto zitokanazo na njia za utunzaji wa taarifa za mhusika.

Tanzania kitambulisho cha taifa hubeba taarifa kama, majina ya wazazi wake, eneo alipozaliwa, eneo alipokua wakati anaomba kitambulisho, kazi yake, tarehe ya kuzaliwa na jinsia. Ila kupitia ulimwengu huu wa teknolojia kitambulisho cha taifa kiongezewe taarifa na nyaraka za raia ili kuendana na ulimwengu wa kidigitali.

Kuwezesha jambo hili itabidi kutengeneza mfumo maalumu utakaobeba taarifa na nyaraka za kila raia mwenye kitambulisho cha taifa. Mfumo huo utabeba taarifa za mhusika kutoka taasisi mbalimbali, kwa maana hiyo hautaathiri/kuzuia kazi za taasisi hizo. Taarifa hizi zitahifadhiwa kwa mfumo wa akaunti za watu kama ilivyo kwa mitandao ya kijamii. Mfano mtandao wa Jamii forum unavyobeba akaunti za watumiaji wake, ila utofauti ni kwamba kwenye mfumo huu haitakua rahisi kwa mtu/watu kuona taarifa zao au za wengine isipokua kwa kibali maalumu.

Nyaraka zipi zijumuishwe kwenye kitambulisho cha taifa?
Kitambulisho cha taifa kitaweza kubeba nyaraka zifuatavyo za mhusika; pasipoti, leseni ya udereva, Cheti cha kuzaliwa, bima ya afya, vyeti vya vifo vya wazazi na watoto, vyeti vya taaluma, leseni za fani mbalimbali, tiketi za safari za mhusika, hati miliki za mali mbalimbali kama nyumba au shamba na cheti cha ndoa. Nyaraka hizi zitajumuishwa kwenye kitambulisho cha taifa kama nakala laini (soft copy) zitakazohifaziwa kwenye akaunti ya mhusika kwenye mfumo maalumu utakaoundwa kwaajili ya jambo hili kwenye kila idara/taasisi husika.

Taarifa zipi nyingine zijumuishwe kwenye kitambulisho cha taifa?
Kitambulisho cha taifa kiwezeshwe kubeba taarifa nyinginezo muhimu za mhusika kama; taarifa za mpiga kura, taarifa za kibenki, historia ya uhalifu, kazi yake, namba ya mlipa kodi, historia za maeneo aliyowahi kufika, hali yake kiafya na pia historia ya matibabu aliyopokea kwenye vituo vya afya.

Ni kwa namna gani taarifa na nyaraka hizo zitaweza kubebwa kwenye kitambulisho cha taifa?
Nyaraka na taarifa za mhusika hazitoonekana kwenye kitambulisho halisi bali zitaonekana kupitia vifaa vya kidigitali kama simu janja na kumpyuta ila kwa msaada wa kitambulisho halisi. Inaweza kua kupitia namba za kitambulisho au kuingiza/kusugua kitambulisho husika kwenye kifaa maalumu kitakachoweza kusoma taarifa za mhusika kutoka idara/tasisi mbalimbali zilizounganishwa na kitambulisho hicho au kuskani kupitia msimbo (QR code) utakaochapishwa kwenye kitambulisho hicho.
Kitambulisho cha taifa.png
Kwa maana hiyo kitambulisho hiki itabidi kuboreshwa na kukifanya cha kidigitali zaidi (kitambulisho cha kielektroniki) kwa minajili ya kuendana na mfumo huu. Picha ya chini ni mfano wa kitambulisho cha kidigitali.
Mbele.png

Nyuma.png

Je, ni faida zipi zitapatikana kupitia maboresho haya?
  • Kupunguza mzigo wa kubeba nyaraka nyingi na kupunguza upotevu wa muda,
Kitambulisho hiki kitakapobeba nyaraka nyinginezo za mhusika, ikiwemo leseni, vyeti, bima na nyinginezo, itasaidia kutobeba nyaraka nyingi zitakapohitajika sehemu/eneo fulani.

Halikadhalika itamwezesha mhusika kutoa pesa benki pamoja na kufanya malipo ya kiserikali na kibinafsi kupitia kitambulisho chake cha taifa.
  • Kurahisisha upelelezi matukio ya uhalifu,
Kitambulisho kitabeba historia za uhalifu za mhusika kutoka mahakamani na vyombo vya usalama (kama askari wa barabarani), hii itasaidia kugundua iwapo mtuhumiwa/mhusika ni mhalifu wa mara nyingi au mara chache. Pia kupitia historia za safari za mhusika iwapo alitumia vyombo vya usafiri vinavyotoa tiketi itajulisha kama mhusika alifika eneo la uhalifu.

Zaidi itatokea ulazima wa kutumia kitambulisho hiki kwenye huduma mbalimbali jambo ambalo itakua rahisi kutambua eneo ambalo mtu yupo pindi atakapotumia kitambulisho chake ikiwa anatafutwa kutokana na kutoroka baada ya kufanya uhalifu.
  • Kupunguza ughushi wa nyaraka,
Itawawia vigumu kughushi nyaraka kama vyeti vya taaluma au vyeti vya kuzaliwa, hati na leseni mbalimbali, kutokana na nyaraka zitakapowekwa kwenye mfumo huo hazitoweza kubadilishwa isipokua kupitia mamlaka rasmi.
  • Kupatiwa msaada wa kimatibabu kwa urahisi na ufanisi,
Kitakapobeba historia za matibabu na hali ya afya ya mhusika itasaidia mhusika kupata msaada wa haraka wa matibabu hata atakapokua hajitambui (amepoteza fahamu) lakini ana kitambulisho chake cha Taifa. Pia itasaidia kujua matibabu aliyopatiwa kwenye vituo vingine vya afya hapo kabla ili kuepuka mkanganyiko katika utoaji wa matibabu.
  • Kuongeza ufanisi kwenye ukusanyaji wa mapato.
Kutokana na kubeba namba ya mlipa kodi na pia kuwezeshwa kufanyia malipo itakua rahisi kwa upande wa serikali kukusanya mapato.

Je, Changamoto zipi zinaweza kuukumba mfumo huu?
  • Udukuzi wa taarifa,
Kukikosekana ulinzi imara wa mfumo huu, itakua rahisi kwa wadukuzi kupata taarifa nyingi za mlengwa kwa urahisi na muda mfupi kutokana taarifa nyingi kubebwa ndani yake.
  • Uvujishaji wa taarifa kupitia watumishi wasio waadilifu,
Watumishi wasio waadilifu waliopo kwenye sekta rasmi huweza kuvujisha taarifa za mhusika kutokana na uwezo wa kuona taarifa hizo.

Nini kifanyike kukabiliana na changamoto hizi?
  • Kutengeneza ulinzi imara wa kidigitali,
Kupitia kushirikiana wataalamu mashuhuri wa ndani na nje ya nchi watakaosimamia mfumo huu kuukinga kutokana na wadukuzi watakaojaribu kuingilia mfumo huu.
  • Kutengeneza sheria itakayowashughulikia vikali watakaobainika kudukua au kuvujisha taarifa zozote za raia,
Itasaidia watumishi kutokuvujisha taarifa na pia wadukuzi kutokujaribu kuingilia mfumo huu pindi watakaposhuhudia wengine waliojaribu/waliofanya hivyo wakiadhibiwa.
  • Kila sekta kupewa idhini ya kuona taarifa wanazoshabihiana nazo tu,
Itaongeza usiri katika taarifa na kupunguza uvujaji wa taarifa za raia.
  • Taasisi kutokua na uwezo wa kuingia kwenye baadhi ya taarifa za mhusika bila idhini yake,
Taasisi itakapohitaji kuona baadhi ya taarifa za mhusika itambidi mhusika athibitishe kukubali kupitia kuweka nywila yake au alama zake za vidole.
  • Kuwapatia raia elimu,
Itaepusha sintofahamu zitakazoweza kutokea kutokana na kutokua ufahamu kuhusu mfumo huu. Itasaidia raia kuendana na mfumo huu kwa wepesi na muda mfupi.

Hivyo basi, ulimwengu wa kidigitali utumike vyema kuboresha kitambulisho cha taifa ili kufaidika nao. Zipo faida nyinginezo zitakazotokana na mfumo huu kama utunzaji wa mazingira, kutokana na matumizi ya karatasi zitokanazo na miti yatapungua kutokana na nyaraka nyingi kuhifadhiwa kwenye mfumo huu. Ni jambo rahisi kufanikisha jambo hili iwapo tu serikali itatambua faida zake na kuamua kuwekeza jitihada zake kwenye kuwezesha jambo hili ili kuendana na ulimwengu wa kidigitali.

Angalizo: Kila taasisi itabaki kama kawaida na kazi yake ila taarifa zake zitaonekana au kufanya kazi kupitia kitambulisho cha taifa.

Wazo zuri sana ila utekelezaji wake kwa nchi yetu bado sana ..hivi vya kawaida tu vinachukua miaka hivyo vya kidigitali sijui itakuwaje
 
Shida ni usimamizi tu, ila tukiwa 'serious' inawezekana kabisa.
 
View attachment 2621440
Tumezoea kitambulisho cha taifa hutumika katika kuthibitisha uraia wa mwananchi kwenye taifa husika. Lakini kwa namna ulimwengu unavyoshuhudia ukuaji wa kasi kwenye sekta ya teknolojia ni vizuri kuboresha kitambulisho cha taifa na kukiwezesha kubeba taarifa nyinginezo muhimu pamoja na nyaraka za muhusika. Itasaidia katika kuepuka changamoto zitokanazo na njia za utunzaji wa taarifa za mhusika.

Tanzania kitambulisho cha taifa hubeba taarifa kama, majina ya wazazi wake (wa kike na kiume), eneo alipozaliwa, eneo alipokua wakati wa kuomba kitambulisho, kazi yake, tarehe ya kuzaliwa na jinsia. Ila kupitia ulimwengu huu wa teknolojia kitambulisho cha taifa kiongezewe taarifa na nyaraka za raia ili kuendana na ulimwengu wa kidigitali.

Ili kuwezesha jambo hili itabidi kutengenezwa mfumo maalumu utakaobeba taarifa na nyaraka za kila raia mwenye kitambulisho cha taifa. Taarifa hizi zitahifadhiwa kwa mfumo wa akaunti za watu kama ilivyo kwa mitandao ya kijamii. Mfano mtandao wa Jamii forum unavyobeba akaunti za watumiaji wake, ila utofauti ni kwamba kwenye mfumo huu haitakua rahisi kwa mtu/watu kuona taarifa zao au za wengine isipokua kwa kibali maalumu.

Nyaraka zipi zijumuhishwe kwenye kitambulisho cha taifa?
Kitambulisho cha taifa kitaweza kubeba nyaraka zifuatavyo za mhusika; pasipoti, leseni ya udereva, Cheti cha kuzaliwa, bima ya afya, vyeti vya vifo vya wazazi na watoto, vyeti vya taaluma, leseni za fani mbalimbali, tiketi za safari za muhusika, hati miliki za mali mbalimbali kama nyumba au shamba na cheti cha ndoa. Vitu hivi huweza kujumuishwa kwenye kitambulisho cha taifa kama nakala laini (soft copy) zitakazohifaziwa kwenye akaunti ya mhusika kwenye mfumo maalumu utakaoundwa kwaajili ya jambo hili.

Taarifa zipi nyingine zijumuishwe kwenye kitambulisho cha taifa?
Pia kitambulisho cha taifa kiwezeshwe kubeba taarifa nyinginezo muhimu za muhusika kama, taarifa za mpiga kura, taarifa zake za kibenki, historia yake ya uhalifu, kazi yake, namba ya mlipa kodi, historia za maeneo aliyowahi kufika, hali yake kiafya na pia historia ya matibabu aliyopokea kwenye vituo vya afya.

Ni kwa namna gani taarifa na nyaraka hizo zitaweza kubebwa kwenye kitambulisho cha taifa?
Nyaraka na taarifa za mhusika hazitaonekana kwenye kitambulisho halisi bali zitaonekana kupitia vifaa vya kidigitali kama simu janja na kumpyuta ila kwa msaada wa kitambulisho halisi. Inaweza kua kupitia namba za kitambulisho au kuingiza/kusugua kitambulisho husika kwenye kifaa maalumu kitakachoweza kusoma taarifa zilizopo ndani ya kitambulisho hicho au kuskani kupitia ‘QR code’ zitakazochapishwa kwenye kitambulisho hicho.
Kwa maana hiyo kitambulisho hiki itabidi kuboreshwa ili kukifanya cha kidigitali zaidi (kitambulisho cha kielectronic) kwa minajili ya kukiimarisha kuendana na mfumo huu. Picha ya chini ni mfano wa kitambulisho cha kidigitali.
View attachment 2621444
View attachment 2621446
Je, ni faida zipi zitapatikana kupitia maboresho haya?
  • Kupunguza mzigo wa kubeba nyaraka nyingi na kupunguza upotevu wa muda,
Kwakua kitambulisho hiki kitabeba nyaraka nyinginezo za mhusika, ikiwemo leseni, vyeti, bima na nyinginezo. Hivyo itasaidia kutokubeba nyaraka nyingi kwakua zote zitapatikana kwenye kitambulisho cha taifa. Pia itamwezesha mhusika kutoa pesa benki kupitia kitambulisho chake cha taifa.

Pia kitambulisho hiki kiwezeshwe kufanya malipo ya kiserikali na malipo binafsi jambo litakalorahisisha ulipaji wake.
  • Kurahisisha upelelezi matukio ya uhalifu,
Kutokana na kitambulisho kubeba historia za uhalifu za mhusika itasaidia kufahamu kama mtuhumiwa ni mhalifu wa mara nyingi au mara chache. Pia kupitia historia za safari za mhusika iwapo alitumia vyombo vya usafiri vinavyotoa tiketi itajulisha kama muhusika alifika eneo la uhalifu.
  • Kupunguza ughushi wa nyaraka,
Itawawia vigumu watu kughushi nyaraka zao kama vyeti vya taaluma au vyeti vya kuzaliwa, hati na leseni mbalimbali. Hii ni kutokana nyaraka hizi zitakapowekwa kwenye mfumo huo hazitoweza kubadilishwa isipokua kupitia mamlaka rasmi.
  • Kupatiwa msaada wa kimatibabu kwa urahisi na ufanisi,
Kutokana na kubeba historia za matibabu na hali ya afya ya mhusika basi itasaidia muhusika kupata msaada wa haraka wa matibabu hata pale atakapokua hajitambui (amepoteza fahamu) lakini ana kitambulisho chake cha Taifa. Pia itasaidia kujua matibabu aliyopatiwa kwenye vituo vingine vya afya hapo kabla ili kuepuka mkanganyiko katika utoaji wa matibabu.
  • Kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.
Kutokana na kubeba namba ya mlipa kodi na pia kuwezeshwa kufanyia malipo itakua rahisi kwa upande wa serikali kukusanya mapato.

Je,
Changamoto gani zinaweza kuukumba mfumo huu?
  • Udukuzi wa taarifa,
Iwapo kukikosekana ulinzi imara wa mfumo huu itakua rahisi kwa wadukuzi kupata taarifa nyingi za mlengwa kwa urahisi na muda mfupi kutokana na mfumo huu kubeba taarifa nyingi za mhusika.
  • Uvujishaji wa taarifa kupitia watumishi wasio waadilifu,
Pia kupitia watumishi wasio waadilifu waliopo kwenye sekta rasmi huweza kuvujisha taarifa za mhusika kutokana na uwezo wa kuona taarifa hizo.

Nini kifanyike kukabiliana na changamoto hizi?
  • Kutengeneza ulinzi imara wa kidigitali,
Kupitia kushirikiana wataalamu mashuhuri wa ndani na nje ya nchi watakaokua wanasimamia mfumo huu ili kuukinga kutokana na wadukuzi watakaojaribu kuingilia mfumo huu.
  • Kutengeneza sheria itakayowashughulikia vikali watakaobainika kudukua au kuvujisha taarifa zozote za raia,
Itasaidia watumishi wasio waadilifu watakaobainika kuvujisha taarifa na wadukuzi watakaobainika kujaribu kuingilia mfumo huu kushughulikiwa kupitia sheria zitakazowekwa na kuadhibiwa vikali.
  • Kila sekta kupewa idhini ya kuona taarifa wanazoshabihiana nazo tu,
Itaongeza usiri katika taarifa na kupunguza uvujaji wa taarifa za raia.
  • Taasisi kutokua na uwezo wa kuingia kwenye baadhi ya taarifa za mhusika bila idhini yake,
Taasisi itakapohitaji kuona taarifa za mhusika, basi ni mpaka pale mhusika atakapothibitisha kukubali kupitia kuweka nywila yake au alama ya vidole vyake.
  • Kuwapatia raia elimu,
Itaepusha sintofahamu zitakazoweza kutokea kutokana na kutokua ufahamu kuhusu mfumo huu. Pia itasaidia raia kuendana na mfumo huu kwa wepesi na muda mfupi.

Hivyo basi, ulimwengu wa kidigitali utumike vyema kuboresha kitambulisho cha taifa ili kufaidika nao. Pia zipo faida nyinginezo zitakazotokana na mfumo huu kama utunzaji wa mazingira. Hii ni kutokana kwamba matumizi ya karatasi zitokanazo na miti yatapungua kutokana na nyaraka nyingi kuhifadhiwa kwenye mfumo huu. Ni jambo rahisi kufanikisha jambo hili iwapo tu serikali itatambua faida zake na kuamua kuwekeza jitihada zake kwenye kuwezesha jambo hili ili kuendana na ulimwengu wa kidigitali.

Good
 
Wazo zuri sana mkuu,kuliko mtu kutembea na vitambulisho vingi kama.reseni,bima,bank card,kitambulisho cha kazi cha mpiga kura
 
Kwa hali yetu itakua vigumu kuwezekana japo ni wazo zuri
 
Katika purukushani za kuwahi hospitalini, unafika kwenye dirisha la malipo ukijua unatoa bima ya afya kumbe katika kuharakisha ulibeba kitambulisho cha mpiga kura. Lakini jambo hili likifanyiwa kazi utatumia kitambulisho cha taifa hutapata changamoto ya kuchanganya vitambulisho tena.
 
Back
Top Bottom