Fatma Karume amjibu Jaji Warioba; asema Bunge lina Wabunge 50 wa Zanzibar na zaidi ya 250 wa Tanganyika ambao Maamuzi yao huiathiri Zanzibar pia!

Unajua maana ya chuki? Hivi unaona watu wanavyoporwa ardhi zao na kupewa waarabu? Magufuli alipora ardhi na kuwapa waarabu? Kwa nini Samia hakugawa bandari ya Zanzibar lakini akagawa wa Tanganyika? Kwa nini kila rais akitoka Zanzibar anaona waarabu kama ndiyo Mungu wao? Tumechoka kutawaliwa na wapiga mnada wa Tanganyika. Mfumo wa muungano ubadilike kila mtu awe na sauti na mali yake.
Maandishi yako ni ushahidi wa chuki tena za kukaririshwa na baadhi ya watu wenye nia za urais.

Bandari ya Dar haijagawiwa bure, imekodishwa kwa kampuni mbili za kigeni moja ya kiarabu ambayo ni DP World nyingine ni ya muhindi wote wawili wanaanza kazi mwaka huu, kwanini zimekodishwa?. Lengo haswa ni kukuza ufanisi wa sekta nzima ya bandari kwa maana ya wepesi wa upakuaji na upakiaji wa mizigo mingi kwa wakati mmoja.

Huwezi kuwa na reli ya matrilioni inayokwenda bara na inatumia umeme halafu uwe na bandari inayoendeshwa kizamani, ni akili ya kawaida tu sio ya kutengenezea roketi.

Jitahidi ukuze upeo wako ili uondokene na maisha ya kukaririshwa vitu kama kasuku.
 
Mjukuu wa baba wa Taifa la Zanzibar Fatma Karume amesema Bunge la Dodoma lina Wabunge 50 wa Zanzibar ( Minority) na Wabunge 250 wa Tanganyika ( Majority) hivyo wakati mwingine hufanya Maamuzi yanayoiathiri Zanzibar kutokana na Wingi wao bungeni

Karume alikuwa akijibu baadhi ya Hoja alizotoa Jaji Warioba Kwenye Kipindi cha Dakika 45 Runingani ITV

Fatma amejibu Ukurasani X

Wanasheria Nguli Hawa 😂😂
Yupo sahihi !
 
Ikiwa kama na taaluma yake ya sheria ameshindwa kutaja namna walivyoathiriwa atakuwa mropokaji kama waropokaji wengine
Logic ni moja tu na iko wazi
Kama kukihitajika kupigwa kura katika jambo lolote ili lipitishwe basi Majority ndio watakao shinda na minority wataathirika kwa uchache wao ! Huu ni mfano tu ! 🙏😇
 
Muungano ni urithi wa kudumu, tuudumishe.
Suala linaloongelewa sio kuuvunja Muungano bali ni muundo wa muungano ndio unaojadiliwa. !

Tatizo wengine wanakuwa ni wapiga ramli !
Wanasema oh muundo ukiwa hivi eti mambo yatakuwa vile !
Hizo ni ramli chonganishi. !
 
Hadi lini tutaendelea kuwaambia huu Muungano wenye maslahi nayo ni CCM? Waondoeni CCM muone huu Muungano kama utamaliza mwaka.
Sasa mkuu watanganyika kwa kuwa tupo wengi si ndo rahisi kumuondoa CCM.

Unataka ZANZIBAR watuondolee CCM tena?
 
Mjukuu wa baba wa Taifa la Zanzibar Fatma Karume amesema Bunge la Dodoma lina Wabunge 50 wa Zanzibar ( Minority) na Wabunge 250 wa Tanganyika ( Majority) hivyo wakati mwingine hufanya Maamuzi yanayoiathiri Zanzibar kutokana na Wingi wao bungeni

Karume alikuwa akijibu baadhi ya Hoja alizotoa Jaji Warioba Kwenye Kipindi cha Dakika 45 Runingani ITV

Fatma amejibu Ukurasani X

Wanasheria Nguli Hawa 😂😂
Muungano ufe tu ili tujipange Hoya
 
Fatma anakosea, kwa sababu amejikita kwenye uwiano wa namba, na kusahau kwamba ni mara chache sana Bunge litaamua mambo ambayo yanaathiri Zanzibar moja kwa moja, japo linasemekana kuwa ni Bunge la muungano.

Kwa mfano, mara ngapi Bunge limefanya maamuzi makubwa katika sekta ambazo hazina usimamizi wowote kule Zanzibar, kama vile JWTZ, Polisi nk? Siku hizi kimsingi ni kwamba Bunge la Muungano limekuwa kwa ajili ya maamuzi ya mambo yanayoihusu bara. Mfano upo karibu, Bunge la Muungano lilipitisha azimio juu ya Mkataba wa Bandari, ambao japo hauihusu Zanzibar lakini wabunge wa Zanzibar walikuwa sehemu ya uamuzi huo.

Labda Fatma aanze kwa kutuambia ni maamuzi gani ya Bunge la muungano yamefanywa katika miaka mitatu iliyopita, ambayo yalikuwa na athari upande wa Zanzibar. Kubadili jina la Tume ya Uchaguzi kuwa Tume Huru ya Uchaguzi, Zanzibar imeathiriika na huo uamuzi?
Mkuu ulivyoa andika hivi ni kwamba hujui au unapinga tu kwasababu zako?
 
Tatizo ni Tanganyika kujivisha koti la muungano,cc wazanzibari muda mrefu muungano huu hatuutaki lakini nyinyi wabara mliushikilia kwa sababu ya wingi wenu mpaka mkamtoa roho karume na mkamfukuza kazi rais halali aliyechaguliwa na wazanzibari yaani mzee aboud jumbe lakini sasa mnapiga kelele kwa sababu rais kutoka Zanzibar.
Safari hii wazanzibar mkishindwa kuwavua watanganyika koti la muungano mnalodai wamejivika tutajua kuwa kumbe ninyi mko kwenye muungano kimaslahi na ndio wanyoji wa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom