Fatma Karume amjibu Jaji Warioba; asema Bunge lina Wabunge 50 wa Zanzibar na zaidi ya 250 wa Tanganyika ambao Maamuzi yao huiathiri Zanzibar pia!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
85,071
143,882
Mjukuu wa baba wa Taifa la Zanzibar Fatma Karume amesema Bunge la Dodoma lina Wabunge 50 wa Zanzibar ( Minority) na Wabunge 250 wa Tanganyika ( Majority) hivyo wakati mwingine hufanya Maamuzi yanayoiathiri Zanzibar kutokana na Wingi wao bungeni

Karume alikuwa akijibu baadhi ya Hoja alizotoa Jaji Warioba Kwenye Kipindi cha Dakika 45 Runingani ITV

Fatma amejibu Ukurasani X

Wanasheria Nguli Hawa 😂😂
 
Mjukuu wa baba wa Taifa la Zanzibar Fatma Karume amesema Bunge la Dodoma lina Wabunge 50 wa Zanzibar ( Minority) na Wabunge 250 wa Tanganyika ( Majority) hivyo wakati mwingine hufanya Maamuzi yanayoiathiri Zanzibar kutokana na Wingi wao bungeni

Karume alikuwa akijibu baadhi ya Hoja alizotoa Jaji Wariioba Kwenye Kipindi cha Dakika 45 Runingani ITV

Fatma amejibu Ukurasani X

Wanasheria Nguli Hawa 😂😂
Maamuzi mfano yapi
 
Hao 50 wa Zanzibar hapo Dodoma wanafanya nn? Km wanaona wanaonewa na kuathiriwa si watoke hapo haraka sana warudi huko Unguja?

Sisi hatuwataki hata hao 50, waondoke warudi kwao Jambiani, na sisi wa bara tubaki na Dodoma yetu.
Tatizo ni Tanganyika kujivisha koti la muungano,cc wazanzibari muda mrefu muungano huu hatuutaki lakini nyinyi wabara mliushikilia kwa sababu ya wingi wenu mpaka mkamtoa roho karume na mkamfukuza kazi rais halali aliyechaguliwa na wazanzibari yaani mzee aboud jumbe lakini sasa mnapiga kelele kwa sababu rais kutoka Zanzibar.
 
..Zanzibar wana baraza la wawakilishi, ambalo linaamua mambo yasiyohusu muungano.

..Tanganyika hatuna Baraza letu la wawakilishi, masuala yetu yanaingiliwa na wabunge 50 toka Zanzibar walioko ktk bunge la muungano.
 
Wabunge 50 hawawezi kabadili Chochote kwani maamuzi ya Tanganyika hupitishwa kwa 2/3

Wabunge wote wanafikia 395+
 
Hao 50 wa Zanzibar hapo Dodoma wanafanya nn? Km wanaona wanaonewa na kuathiriwa si watoke hapo haraka sana warudi huko Unguja?

Sisi hatuwataki hata hao 50, waondoke warudi kwao Jambiani, na sisi wa bara tubaki na Dodoma yetu.

Wabunge 50 wa Zanzibar, Huwa wanafuata nini Dodoma kwenye bunge la Tanganyika? Sisi mbona hatupeleki wabunge hata mmoja kwenye bunge la Zanzibar?​

Mjukuu wa baba wa Taifa la Zanzibar Fatma Karume amesema Bunge la Dodoma lina Wabunge 50 wa Zanzibar ( Minority) na Wabunge 250 wa Tanganyika ( Majority) hivyo wakati mwingine hufanya Maamuzi yanayoiathiri Zanzibar kutokana na Wingi wao bungeni

Karume alikuwa akijibu baadhi ya Hoja alizotoa Jaji Wariioba Kwenye Kipindi cha Dakika 45 Runingani ITV

Fatma amejibu Ukurasani X

Wanasheria Nguli Hawa 😂😂
Fatma anakosea, kwa sababu amejikita kwenye uwiano wa namba, na kusahau kwamba ni mara chache sana Bunge litaamua mambo ambayo yanaathiri Zanzibar moja kwa moja, japo linasemekana kuwa ni Bunge la muungano.

Kwa mfano, mara ngapi Bunge limefanya maamuzi makubwa katika sekta ambazo hazina usimamizi wowote kule Zanzibar, kama vile JWTZ, Polisi nk? Siku hizi kimsingi ni kwamba Bunge la Muungano limekuwa kwa ajili ya maamuzi ya mambo yanayoihusu bara. Mfano upo karibu, Bunge la Muungano lilipitisha azimio juu ya Mkataba wa Bandari, ambao japo hauihusu Zanzibar lakini wabunge wa Zanzibar walikuwa sehemu ya uamuzi huo.

Labda Fatma aanze kwa kutuambia ni maamuzi gani ya Bunge la muungano yamefanywa katika miaka mitatu iliyopita, ambayo yalikuwa na athari upande wa Zanzibar. Kubadili jina la Tume ya Uchaguzi kuwa Tume Huru ya Uchaguzi, Zanzibar imeathiriika na huo uamuzi?
 
Unadhani kwanini Zanzibar ina Wabunge wachache Dodoma?
 
Zanzibar wana bunge lao na spika wao (baraza la wawakilishi) wanajadili mambo yao na masuala yasiyo ya muungano

Hivyo kama ni mialiko ya sherehe Zanzibar wabahudhuria sherehe mbili huku watanganyika wanahudhuria sherehe moja.

Wanapanga na bajeti zao zitokazo na makusanyo ya kodi za watanganyika.

Kiambatanisho hiki hapa chini

Hapa upo wasifu wa spika wa bunge la Zanzibar (baraza la wawakilishi)

Sasa nadhani wanatumia hili neno baraza la wawakilishi ili kupunguza nguvu ya neno " bunge" nani hapa anatudanganya?

Tutakubali vipi kuaminishwa hili ni baraza la wawakilishi tu ilhali kuna wabunge humo wa Zanzibar na wanawasilisha miswada na utungaji wa sheria kabisa?
 
Hao 50 wa Zanzibar hapo Dodoma wanafanya nn? Km wanaona wanaonewa na kuathiriwa si watoke hapo haraka sana warudi huko Unguja?

Sisi hatuwataki hata hao 50, waondoke warudi kwao Jambiani, na sisi wa bara tubaki na Dodoma yetu.
Umeamua kwenda live hewani!
 
Tatizo ni Tanganyika kujivisha koti la muungano,cc wazanzibari muda mrefu muungano huu hatuutaki lakini nyinyi wabara mliushikilia kwa sababu ya wingi wenu mpaka mkamtoa roho karume na mkamfukuza kazi rais halali aliyechaguliwa na wazanzibari yaani mzee aboud jumbe lakini sasa mnapiga kelele kwa sababu rais kutoka Zanzibar.
Usisahau rais wenu hupitishwa dodoma kwanza ili kujua uzalendo wake
 
Tatizo ni Tanganyika kujivisha koti la muungano,cc wazanzibari muda mrefu muungano huu hatuutaki lakini nyinyi wabara mliushikilia kwa sababu ya wingi wenu mpaka mkamtoa roho karume na mkamfukuza kazi rais halali aliyechaguliwa na wazanzibari yaani mzee aboud jumbe lakini sasa mnapiga kelele kwa sababu rais kutoka Zanzibar.
Hadi lini tutaendelea kuwaambia huu Muungano wenye maslahi nayo ni CCM? Waondoeni CCM muone huu Muungano kama utamaliza mwaka.
 
Tatizo linaloonekana wazi ni uwiano.
Bars wabunge 250 wanawakilisha watu mil 60 wakati Zanzibar wabunge 50 wanawakilisha watu mil 1 na nusu.
Wabunge 50 hawawezi kabadili Chochote kwani maamuzi ya Tanganyika hupitishwa kwa 2/3

Wabunge wote wanafikia 395+
Kama hawawezi kubadili chochote wanafanya Nini huko bungeni?!

Kujikusayia tu posho za vikao??!!
 
Back
Top Bottom