Dkt. Biteko: Bwawa la Mwalimu Nyerere lipo Salama. Limepunguza athari za mafuriko

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
319
524
DKT. BITEKO ASEMA BWAWA LA UMEME JULIUS NYERERE LIKO SALAMA

đź“Ś Asema limepunguza athari za mafuriko

đź“Ś Atoa pole kwa waathirika wa mafuriko Rufiji

đź“Ś Aeleza jitihada za Serikali kwa waathirika

đź“Ś Azungumzia umuhimu wa Nishati Safi ya Kupikia, Bei ya Gesi

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa licha ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini, Bwala la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) lipo salama kutokana na kujengwa kisayansi na hivyo kuendelea kuzalisha umeme kupitia mtambo namba tisa huku mitambo mingine miwili ikiwa ukingoni kukamilika.
IMG-20240418-WA0013.jpg

Dkt. Biteko amesema hayo tarehe 18 Aprili 2024 jijini Dodoma katika mahojiano Mbashara kupitia kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC kuhusu Maonesho ya Wiki ya Nishati 2024 yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

“ Bwawa letu lipo salama kwani limejengwa kisayansi, ujazo wake wa maji ni mita za ujazo 183 na kwa takwimu za leo ni mita za ujazo 183.4, huko nyuma maji yalikuwa yakiingia mengi sana kwa kiasi cha mita za ujazo 8400 kwa sekunde hivyo yalipaswa kupunguzwa ili kuendana na ujazo wa bwawa.” Amesema Dkt. Biteko
IMG-20240418-WA0012.jpg

Amesema kuwa, bila ya kuwepo kwa Bwawa hilo athari za mvua zingeanza kuonekana tangu mwezi Oktoba mwaka jana lakini hali hiyo haikutokea mapema kwa sababu maji yalikuwa yakiijazwa katika bwawa kwa ajili ya kuzalisha umeme.

Ameongeza kuwa, Wizara ya Nishati na TANESCO ilishabaini uongezekaji wa maji katika mto Rufiji kuanzia mwezi Februari, mwaka huu na tahadhari ilianza kutolewa kuhusu kasi hiyo ya maji ili kuanza kuchukua hatua stahiki.
IMG-20240418-WA0011.jpg

Dkt. Biteko ameeleza kusikitishwa kwake na athari zilizotokea kutokana na mafuriko ambayo yamesababisha athari katika maisha ya watu na mali zao na kueleza kuwa Serikali inafanya kila jitihada kurejesha hali ya kawaida kwa wananchi waliokumbwa na maafa hayo.

Kuhusu utekelezaji wa ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia nchini, Dkt. Biteko amesema kuwa, watu wengi bado wanatumia nishati isiyo safi ya kupikia kama vile mkaa na kuni na wananchi wachache wanatumia gesi na nishati nyingine kama vile umeme.
IMG-20240418-WA0010.jpg

Ameeleza kuwa, lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa ndani ya miaka 10 asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia na kwamba Serikali imepitisha Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia ikiwa ni moja ya njia za utekelezaji wa ajenda hiyo ambayo inanadiwa na Kinara wake, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ameongeza kuwa, katika kutekeleza mpango huo wa Nishati Safi ya Kupikia, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, imeshatoa waraka wa kutotumia kuni na mkaa kwa taasisi zinazolisha watu kuanzia 100 na zaidi kama vile Shule na Magereza.
IMG-20240418-WA0009.jpg

Kuhusu upatikanaji wa umeme wa uhakika Dkt. Biteko amesema kuwa kwa sasa uzalishaji umezidi mahitaji hivyo kinachofanyika sasa ni kuboresha miundombinu ya umeme ikiwemo ya kusafirisha umeme kwani baadhi ya sehemu laini za umeme ni ndefu sana hivyo vitajengwa vituo vya kupoza umeme takriban 83 nchini ili kuondoa athari za watu wengi kutopata umeme pale laini inapopata hitilafu.

Kuhusu Bei ya Gesi amekiri kuwa bei ni kubwa na kueleza kuwa, Serikali inaangalia kwa karibu sana suala hilo ili kuweza kupunguza gharama na hii haiishii kwenye gesi pekee bali kwenye majiko banifu na katika mwaka huu wa fedha Serikali itaanza kutengeneza majiko ya bayogesi kwenye nyumba za wananchi wanaofuga mifugo ili watumie nishati hiyo kwa ajili ya kupikia.
 
Bwawa letu lipo salama kwani limejengwa kisayansi,
,
No research no right to speak.

Nawashauri tumieni muda kidogo kufanya tafiti nyepesi ya kimtandao "simple internet research" kabla ya kuja kudanganyana. Nimeitaama hiyo video sijaona "concern" yoyote ya masingi iiliyooneshwa na engoineer anaetowa maelezo wala waziri biteko. Au tunasikiliza vitu tofauti?

Kuna wanaonesha wamelishika neno "nyufa" na hawajali hizo nyufa ziko wapi. Nyufa zinazoongelewa hazipigiki picha kama ule uharo uliosambazwa.

Yaani Watanzania mmeshindwa kuelewa maana ya nyufa za kwenye mwamba zinazofanyiwa "grouting" ambazo engineer anazielezea hapo. Hizo kwa macho hazionekani, huwa kwa siku hizi zinaonekana kwa vifaa maalum au vipomo maalum, mradi hakuna nyufa kwenye "diaphragm walls" silioni tatizo.

Huo unaoongelewa kwenye hiyo video ni uboreshaji wa kawaida sana kwenye ujenzi, kama vifaa vilivyowekwa vimeonesha "abnormality".

Mara nyingi kutokana na vipimo vya awali vya mwamba unaweza kuweka grouting kwenye "design" au ikaamuliwa kuwa "grouting" itafanyika au isifanyike baada ya kuwepo na "load" kwenye bwawa. Kwa ujenzi na vifaa vya siku hizi Uwepo au usiwepo, mara nyingi au mara zote hufanyika ujenzi ukifikia stage fulani.

Hilo mbona ni jambo la kawaida kwenye miradi yoyote ya ujenzi mkubwa. Soma:

THE CONSTRUCTION CHALLENGES ASWAN HIGH DAM, EGYPT

View: https://m.youtube.com/watch?v=0VaCxQnrAFY
The designing of the Aswan High Dam faced many difficulties, for it has to be constructed on a pervious foundation in the lake of the existing Aswan Dam.

The whole extent of the main dam foundation will be covered with a layer of compacted dune sand about 82 feet deep.

The rockfill above this layer will have a clay core made of Nile silt. The dam will be protected against seepage by two lines of defence, a horizontal impervious blanket in the upstream part and a vertical grout curtain descending in the pervious bed of the river to a depth of 690 feet until it strikes natural bed rock.

This grout curtain will plug the voids in the layers of sedimentary materials underneath the dam.
 
Yetu ni design hii na hatukufikia viwango!?
 
Yetu ni design hii na hatukufikia viwango!?

TAREHE 18 September 2023
Maelezo ya mhandisi katika mradi wa bwawa la umeme la JNHPP Rufiji kwa mh. Naibu Waziri Mkuu, jinsi ya kuimarisha mwamba ambao ndiyo msingi wa ukuta na tuta la bwawa la JNHPP Rufiji kitaalamu zoezi linaitwa grout curtain.

Hivyo kwa sasa maji yanafunguliwa kwa wingi yasijaze bwawa maana linaweza kubomoka kutokana na michoro ya ramani ilivyotaka haikufuatwa.

ZIARA YA NAIBU WAZIRI MKUU BWAWA LA JNHPP TAREHE 18 September 2023

Mhandisi wa mradi anafafanua kwa naibu waziri mkuu aliye pia waziri wa nishati Mh. Dotto Biteko juu umuhimu wa kufanya grout curtain kuimarisha msingi wa bwawa kuzuia maji kupenya ktk msingi / foundation kuzuia hatari kubwa ya dhahiri :

View: https://m.youtube.com/watch?v=Y8CkZ4Za7Gw
 
Ndiyo shida ya kupenda cheap
 
Silt inayotuwama bwawa la Nyerere lazima itakuwa na dhahabu ya kutosha.
 
..wapige kazi kimyakimya.

..aache kutusumbua na habari za mgao wa umeme kuisha.

..aache wananchi na wateja tuwe mashuhuda kama mgao umekwisha, au la.
 
Zamani athari ktk

1)mazao yaliyokuwa yakiharibika

2) nyumba zilizokuwa zikiharibika

3) Watu walikuwa wanakufa
4) n.k

Kumlinganisha na msimu huu wa mafuriko. Tofauti ikoje?
 
Back
Top Bottom