Bashe hana jipya zaidi ya Siasa kwenye Wizara muhimu

Ndata

JF-Expert Member
Mar 2, 2017
226
321
Kwanza I have to declare interest mimi ni mkulima wa mazao ya biashara. Na kama mkulima wizara ya kilimo ndio mlezi wangu ila kwa uongozi wa Bashe nachelea kusema tutachelewa sana.

Tanzania ilikuja na wazo la kufanya mchikichi kuwa zao la biashara, ilikuwa hatua nzuri kweli na Kigoma ikachaguliwa kama mzalishaji mkuu. Kinachoniuma hii project iliishia juu kwa juu pasipo muendelezo. Bashe alishakimbia huko leo Uganda anatuuzia mafuta na sabuni.

Mwaka huu tumeingia kwenye shida ya sukari, siasa zimepigwa kweli kweli ila Bashe tatizo analijua ni vyama vya ushirika ndio vinakwamisha viwanda. Miwa inafia shambani mpaka ushirika uamue kuvuna, mkulima analima, analipa ada kwenye vyama na kuvuniwa mpaka atoe rushwa. Kwanini tusiwe kama Uganda na Kenya mkulima aruhusiwe kuuza muwa wake direct kiwandani.

Llikuja Ombwe la kilimo cha parachichi, mawaziri wa Kenya na Uganda walijitahidi kuwashawishi wakulima kulima. Serikali zao zimenunulia wakulima miche, zimetoa elimu na kutafuta masoko. Tanzania yenye eneo kubwa na lenye uwezo mkubwa wa kulima parachichi Bashe anahubiri majukwaani ila hajaonyesha nia yoyote ya kuisaidia Tanzania kuongia kwenye ushindani wa kuzalisha parachichi.

Vijana wanakufa mipakani haswa Uganda wakijaribu kuvusha kahawa. Wakati Tanzania kahawa ikiwa tsh 2000 na unalipwa baada ya miezi na kudhulumiwa kukiwemo upande wa pili Uganda kahawa inauzwa tsh 3000 kwa kilo na malipo ni papo hapo. Matokeo yake Uganda inaingia top 10 ya wazalishaji wa kahawa duniani huku Tanzania tukiwa mbali hatuonekani.

Bei ya mbegu haswa mahindi, nilimsikia siku moja akisema mbegu ya mahindi bei elekezi ni tsh 12000 wakati madukani tunanunua tsh 20000 hajawahi chukua hatua yoyote. Wenzetu Uganda na Kenya bei ya mbegu za mahindi hybrid zinauza mpaka tsh 7000 kwa kilo. Bashe anakwama wapi?

Bashe na wizara anayoiongoza wameshindwa kabisa kufanya jitihada za kumsaidia mkulima wa Tanzania, mkulima wa Tanzania anabaki kulima kwa ajili ya chakula ukiachilia mbali wawekezaji wachache wenye kipato na elimu.

Ushauri wangu kwa Bashe, wizara anayoiongoza ndio wizara mama kwa nchi yetu, ajitahidi kujifunza kwa wenzake wa Afrika mashariki, ajitahidi kutafuta majibu ya kilio cha wakulima ajitahidi kutafuta wawekezaji watakaosaidia wakulima. Ashirikiane na waziri wa viwanda kuangalia namna ya kuwa na viwanda husika sehemu ya zao husika. Mfano viwanda vya mafuta na sabuni Kigoma.

Mwisho wa siku, watubadilishie sheria inayozuia kufungua kiwanda mfano karibu na kiwanda kilichopo ili zao la mkulima Liwe linashindaniwa kununuliwa.

Asanteni
 
Mbona anajitahidi na ako na maono makubwa yatakayonufaisha watanzania?!

Hiyo wizara inamfaa na tunamwombea kisha arejee tena.

Muhimu kwa Sasa tunamtaka wafungue mipaka nchi jirani waje mashambani wanunue nafaka maana kuhifadhi ni gharama kubwa.
 
Mbona anajitahidi na ako na maono makubwa yatakayonufaisha watanzania?!

Hiyo wizara inamfaa na tunamwombea kisha arejee tena.

Muhimu kwa Sasa tunamtaka wafungue mipaka nchi jirani waje mashambani wanunue nafaka maana kuhifadhi ni gharama
Ni sahihi pia kuona anajitahidi ndugu. Lakini wakulima haswa wa mazao yasio nafaka bado tunaumizwa sana na hatuoni akichukua hatua.
1. Kahawa
2. Muwa
3. Parachichi

Tunaomba kwanza waondoe sheria ya mkulima kuwa controlled na vyama vya ushirika ambavyo lwa asilimia kubwa vimejaa upigaji na kumuumiza mkulima.

Tunaomba kama waziri ajitahidi sana kuhimiza mazao husika katika maeneo husika. Nimetolea mfano zao la michikichi. Tangu single ofisini hakuna lolote alilofanya kumsaidia mkulima wa michikichi zao muhimu kabisa ila mkulima anabaki kuwq ombqomba
 
Kwa hiyo hakuna mazuri yoyote aliyoyafanya huyo sijui basha sijui nani?
Ni jukwaa huru bro, unaweza underline mazuri yake kama waziri wa kilimo. Article yangu haikuwa kwa ajili ya kumpongeza ila kumsema kwa mianya mikubwa inayotuumiza wakulima yeye akiwa kakaa ofisini pasipo kuchukua hatua
 
Back
Top Bottom