Azam yaifuata simba fainali muungano

kinje ketile

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
4,370
8,377

USHINDI wa mabao 5-2 ilioupata Azam FC dhidi ya KMKM, umeifanya timu hiyo kufuzu fainali ya Kombe la Muungano, michuano inayofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.​

Azam imepata ushindi huo kupitia mabao ya Abdul Sopu dakika ya 7 na 42, huku wafungaji wengine wakiwa ni Nathaniel Chilambo (dk 9), Iddy Seleman (dk 49) na Iddy Kichindo (dk74).
Kwa upande wa mabao ya KMKM yote mawili yalifungwa na Abrahman Ali likiwemo moja kwa mkwaju wa penalti dakika ya 38.

Azam inaungana na Simba kucheza fainali ya michuano hiyo itakayopigwa Jumamosi Aprili 27, 2024 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Simba ilikuwa ya kwanza kutinga fainali baada ya jana kuichapa KVZ mabao 2-0.
Azam ambayo hii ni mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo, inalisaka taji lao la kwanza, wakati Simba ikiutaka ubingwa wa sita kufikia rekodi ya Yanga inayoongoza kuwa timu iliyobeba mara nyingi zaidi.
Michuano hiyo iliyosimama kwa takribani miaka 20, imerejea tena kwa kuanza kuzishirikisha timu nne pekee ikianzia hatua ya nusu fainali, Simba na Azam kutoka Tanzania Bara, huku KVZ na KMKM zikiiwakilisha Zanzibar. Hapo awali ilikuwa ikizishirikisha timu nane, nne za Tanzania Bara na zingine Zanzibar.
Bingwa wa michuano hiyo itakayofikia tamati Jumamosi atakabidhiwa Sh50 milioni na mshindi wa pili kuondoka na Sh30 milioni.
Michuano hiyo ni maalum kwa ajili ya kuadhimisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo mwaka huu inatimia miaka 60 tangu. Muungano huo ndio ilizaliwa Tanzania Aprili 26, 1964.

Source - Mwanaspoti
 
Walicheza jana, Wanaisubiri Fainali Kesho.

Wameonyesha kuwa na hamu ya kunyakua Kombe hilo lenye Historia Kubwa hapa Tanzania. Mmoja wa Viongozi waandamizi wa Azam amesikika akisema namnukuu "Wewe Ukisusa wenzio twala"
Okay nilidhani wamecheza leo

Kombe halina maana yoyote hilo
 
Walicheza jana, Wanaisubiri Fainali Kesho.

Wameonyesha kuwa na hamu ya kunyakua Kombe hilo lenye Historia Kubwa hapa Tanzania. Mmoja wa Viongozi waandamizi wa Azam amesikika akisema namnukuu "Wewe Ukisusa wenzio twala"
Bingwa wa hili kombe atawakilisha nchi kwenye mashindano yapi?
 
Bingwa wa hili kombe atawakilisha nchi kwenye mashindano yapi?
Atajulikana ni Bingwa wa Kombe La Muungano 2024 na zawadi atapata, na Historia itakuwa imeandikwa... ni kama vile Simba na Yanga walivyoandika historia 2024 wote wawili waliingia ROBO CL Afrika Wakatolewa..! Iwapo ile Barua ya Utopolo kulalamikia goli itagonga mwamba..
 
Kuna kila dalili Azam wanaenda kulichukia hilo kombe la mchongo! Washindwe wenyewe.
 
Atajulikana ni Bingwa wa Kombe La Muungano 2024 na zawadi atapata, na Historia itakuwa imeandikwa... ni kama vile Simba na Yanga walivyoandika historia 2024 wote wawili waliingia ROBO CL Afrika Wakatolewa..! Iwapo ile Barua ya Utopolo kulalamikia goli itagonga mwamba..
Bado mnasubiri majibu
 
Azam bingwa, kule CCM kirumba my wetu aliporochoka safari hii hatoki!
 
Wanaume Masandawana na Esperance de Tunis Wapo Uwanjani muda huu nusu Fainali CL (22')Wakati Young African Wanaendelea Kushangaashangaa Kombe La Muungano..!
 
Huko miaka ya nyuma hili kombe lilikuwepo...! Kusema eti La Mchongo ni lugha yenye ukakasi..! Na Mwakani huenda Timu zitakazoshiriki zitaongezeka.
Hii michuano ilianzishwa kwavile timu za Zanzibar zilikuwa hazishiriki michuano ya CAF kwavile hakuwa mwanachama wa CAF. ila kwasasa Zanzibar wanapeleka mwakilishi CAFCL na CAFCC hivyo hayo mashindano ya kombe la muungano inakuwa ni bonanza kama ilivyo mapinduzi cup
 
Back
Top Bottom