Wito, Kuna Mashindano ya Kombe la diwani huku Tegeta kwa ndevu mshindi anaondoka na bajaji mpya, Tunawaalika Simba sc waandike barua mwisho tar 1

Ndiyo maana kuna wakati nasema huu tunaoita utani wa jadi tuufutilie mbali maana watu wamekuwa wajinga wajinga tu na wengine inasababisha mioyo yao inabeba roho za husda, chuki, wivu na takataka zingine.

Morocco wana Kombe la Mfalme. Hakuna ubaya kuwa na mashindano ambayo yanaenzi mfumo wetu wa nchi. Watu wajinga wajinga ndiyo wanaweza kutoa kauli kama hizi za kulibeza.

NB. Kombe la Muungano lipangiwe ratiba maalumu na utaratibu unaoeleweka badala ya kuwa la kushtukiza kama ilivyotokea mwaka huu. Pia zawadi kwa mshindi iwe kubwa zaidi ingawa nimesikia kuanzia mwakani mshindi anaondoka na milioni 100.

Mods Cookie Active futeni huu uzi, hauna tofauti na kuikashfu nchi.
Sidhani kama ni Kashfa Kwa nchi kama unavyosema. Ila haiwezekani Chama cha soka kikaanzisha mashindano mwishoni mwa kalenda ya mwaka ya Soka halafu Wenye busara wakakaa kimya. Muungano unajulikana ni 26 April na maadhimisho ya miaka 60 yalijulikana kitambo, iweje mashindano yaanzishwe ghafla kàma tumbo la kuhara?
 
Nyie mbona kama mmevurugwa.....hahaha tupe barua tuje tushiriki...
 
Mangungu na try again wapewe 5 Tena kwa maana wamevunja rekodi ya mafanikio kwa kubeba kikombe Cha muungano na milioni 50 juu!
Iyo itaongezeka kwenye mafanikio ya klabu ya msimu mzima baada ya wasap channel kuongoza kwenye mafanikio ayo! Milioni 50 wataweza kushusha vyuma vya maana kwenye usajili wa wachezaji ikiwemo kuwaongezea mikataba kina jobe na fred timu iwe tishio!
Mangungu na try again Amna baya pigeni kazi na mjumuike na wenzenu kupokea kikombe icho kikubwa kabisa kitapowasili pale bandarini kikitokea Zanzibar!
 
Sidhani kama ni Kashfa Kwa nchi kama unavyosema. Ila haiwezekani Chama cha soka kikaanzisha mashindano mwishoni mwa kalenda ya mwaka ya Soka halafu Wenye busara wakakaa kimya. Muungano unajulikana ni 26 April na maadhimisho ya miaka 60 yalijulikana kitambo, iweje mashindano yaanzishwe ghafla kàma tumbo la kuhara?
Msimu huu kulikuwa na matumaini makubwa kuwa mojawapo au timu zote mbili za TZ kufika mbali katika mashindano ya CAF. Nadhani sababu kuu ya ratiba kutopangwa mapema ni ratiba ya CAF. Nia ya kuyarudisha mashindano ya Muungano ilishawahi kutangazwa miezi mingi iliyopita kwa hiyo chini kwa chini naamini mazungumzo na maandalizi yalikuwa yanafanyika.

Kama Simba+/Yanga ingevuka hadi hatua ya nusu fainali kwenye CAFCL ina maana mashindano haya ya Muungano yangegongana na mechi za nusu fainali CAF.

Labda useme baada ya hizi timu kutolewa tu ratiba ingetangazwa ila hapo bado tunaongelea kama wiki 3 tu zimepita kwa hiyo tunarudi pale pale tu.
 
Back
Top Bottom