Wananchi wa Arusha mlichofanya kwa RC ni dharau kubwa kwa mamlaka za uteuzi; acheni mgomo fungueni mioyo

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
943
4,458
Wananchi wa Arusha wameingia mitini kumpokea RC mpya. Hii siyo Ishara nzuri kwa kiongozi anayependa kuabudiwa. Vyombo vya habari vilijiandaa kurusha live msafara wake lakini wamekwama kwa kukosekana umati.

Jambo la pili lililowaudhi wananchi wa Arusha ni kitendo cha kuwa na kiongozi anayewaza kugombana na watu kila wakati. Kila anapozungumza anaonyesha kutengeneza maadui kuliko marafiki. Huu siyo uongozi

Jambo jingine nikuchukua magari ya utalii na kuyapeleka KIA ambacho ni tafsiri ya rushwa. Haya magari kwanini wanapoteuliwa wakuu wengine wa mkoa hayalazimishwi kujitokeza kumlaki?

Mkuu wa mkoa wa Mwanza amekwenda kuripoti hakuna misafara, mkuu wa mkoa wa Mara hakuna msafara; Mongela hakuwa na misafara. Kwanini tunaamini kupanga watu kwenye msafara ndio utandaji?

Mkuu wa mkoa ni nafasi ya utumishi siyo siasa; kuchukua magari ya watu binafsi na kufanya nayo siasa ni rushwa. Kwanini tusikemee haya? Kama tunaamini ndio utaratibu basi wakuu wote wa mikoa wawe wanalazimisha misafara kila wanapokwenda tuone kama umaskini unaisha.

Viongozi wa juu jifunzeni kukemea la sivyo itanonekana kuna baraka kutoka juu
 
Wananchi wa Arusha wameingia mitini kumpokea RC mpya. Hii siyo Ishara nzuri kwa kiongozi anayependa kuabudiwa. Vyombo vya habari vilijiandaa kurusha live msafara wake lakini wamekwama kwa kukosekana umati...
Umesema nafasi ya mkuu wa mkoa sio siasa halafu unasema magari yamechukuliwa na kupelekwa kwenye siasa hapo sijaelewa
 
Wananchi wa Arusha wameingia mitini kumpokea RC mpya. Hii siyo Ishara nzuri kwa kiongozi anayependa kuabudiwa. Vyombo vya habari vilijiandaa kurusha live msafara wake lakini wamekwama kwa kukosekana umati...
gubu ni mzigo mzito sana kuubeba moyoni.....
 
Back
Top Bottom