Vidonda Vya Kisukari: Fahamu Chanzo, Athari, Tiba na Kinga

Dr Adinan

Member
Jul 11, 2021
14
22

Madhara Ya Ugonjwa wa Kisukari na Namna Ya Kuepuka​

Vidonda kwa wagonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa sana inayosababisha ulemavu unaotokana eidha kuwa kukatwa miguu au mikono.

Haya yote yanaweza kudhibitika kama tahadhari itachukuliwa katika muda muafaka.

Kabla ya kufahamu ufanye nini na upi ni wakati muafaka inabidi ufahamu kisukari husababishaje matatizo haya.
Sukari inatakiwa ihifadhiwe kwenye tishu, isikae ndani ya damu. Inapokaa kwenye damu kwa kiwango kikubwa husababisha sumu inayofanya uharibifu kwa namna tatu.

1. Kwanza huaribu mishipa ya fahamu na hivyo hutoweza kuhisi. Ukosefu wa hisia husababisha mwenye kisukari kutokufahamu kama mguu unaumia-mkandamizo kwamfano kubanwa na kiatu nk.

2. Kisukari pia huaribu mishipa ya damu na -kama tulivyoona- kusababisha hali inayoitwa artherosclerosis. Hatimaye mishipa ya damu huziba haswa ile ya pembeni ya mwili kama vile miguu. Kukosekana kwa damu maana yake sehemu husika hukosa chakula, hewa safi na kinga. Hivyo sehemu hiyo hufa na kama utapata maambukizi hutapona kwa urahisi. Mara nyingi hii imekuwa sababu kubwa ya wagonjwa wa kisukari kukatwa miguu.

3. Njia ya tatu, sukari huathiri kinga ya mwili kwa kuharibu na kupunguza muda wa kuishi wa seli zinazopambana na magonjwa.

Vidonda Vya Miguu na Namna Ya Kuviepuka​

Vidonda miguuni vinawapata wengi wenye kisukari, na ni sababu inayoongoza kwa wagonjwa hawa kukatwa miguu.

Tumeona namna kisukari kinavyoathiri mwili, mishipa ya fahamu na kinga.
Kwasababu ya kuharibiwa kwa mishipa ya fahamu, mgonjwa wa kisukari hukosa hisia miguuni.

Ukijumlisha na athari za kisukari kwenye kupunguza kinga na kupunguza kiwango cha damu kwenye miguu, kama mgonjwa akipata kidonda sehemu hizi kidonda hupona kwa shida na mara nyingi hupata maambukizi.

Viashiria vya kidonda:
  • ugonjwa wa mishipa ya pembeni
  • ugonjwa wa mishipa ya fahamu
  • udhibiti duni wa sukari
  • uvutaji sigara
  • ugonjwa wa figo uliosababishwa na sukari
  • kuwa na vidonda kabla / au kukatwa mguu kwasababu ya kisukaria
Dalili za kuwa na kidonda cha kisukari
Wagonjwa wanaweza kuonesha dalili za ugonjwa wa mishipa ya fahamu au kuziba kwa mishipa ya damu, kama vile:
  1. maumivu ya miguu au kubana katika mapaja wakati wa mazoezi ya mwili
  2. kuhisi maumivu ya kuchoma choma, kuchoma, au maumivu ya miguu
  3. kupoteza hisia ya mguso au uwezo wa kuhisi joto au baridi vizuri sana
  4. mabadiliko ya muonekano wa miguu kwa muda – kama vile kuwa myeusi
  5. ngozi kavu, iliyopasuka kwenye miguu
  6. mabadiliko ya rangi na joto la miguu
  7. kucha zilizo na unene,
  8. manjano
  9. maambukizi ya fangasi kati ya vidole
  10. malengelenge,
  11. kidonda,
  12. kidonda,
  13. sugu yaliyoambukizwa,
  14. Kuchaa zinazooea ndani.
Lakini, kukosekana kwa dalili hakujumuishi shida za miguu ya kisukari.

Vidonda-Miguuni_Sehemu-ambazo-hupata-vidonda-mara-kwa-mara.webp
Vidonda hivi hutokea haswa katika zile sehemu ambazo hukandamizwa wakati unatembea au umesimama au umelala.

Sehemu hizi ni chini ya vidole gumba, na sehemu ya mbele ya nyayo kama inavyoonekana kwenye picha hii

Fanya Mambo Haya Kuepuka Vidonda Vya Miguu​

Ili kuepuka shida kubwa za mguu ambazo zinaweza kusababisha kupoteza kidole, kiganja au mguu:

1. Kagua miguu yako kila siku. Angalia mikwaruzo, malengelenge, uwekundu, uvimbe, au kucha
matatizo. Tumia kioo cha kukuza ili kuangalia nyayo zako.

2. Osha miguu katika maji ya uvuguvugu, kamwe isiwe moto. Weka miguu yako safi kwa kuosha kila siku. Tumia maji tu ya uvuguvugu – joto ambalo ungetumia kwa mtoto mchanga.

3. Osha taratibu miguu yako. Osha kwa kutumia kitambaa cha kufulia au sponji. Kausha kwa uangalifu katikati ya vidole.

4. Kata kucha kwa uangalifu. Usikate kucha fupi sana, kwani hii inaweza
kusababisha kucha kuotea ndani.

5. Kamwe usijitibu sugu mwenyewe. Muone mtumishi wa afya akushauri.

6. Tizama viatu vyako ndani kabla ya kuvaa. Kumbuka, miguu yako
inaweza kutokuhisi kokoto au kitu kingine.

7. Vaa soksi na viatu sahihi. Kiatu kisikubane sana au kupwaya sana.

8. Kamwe usitembee bila viatu, hata nyumbani. Kila mara
vaa viatu au malapa. Unaweza kujikwaa na kuumia.

9. Dhibiti sukari yako: Hakikisha sukari yako inakuwa katika kiwango kinachokubalika kiafya:
  • Kama umejipima asubuhi wakati hujala basi iwe kati ya 3.5mmol/L-7.0 mmol/L.
  • Kama umejipima baada ya kula basi iwe kati ya 7.0mmol/L-13.0 mmol/L.
10. Usivute sigara. Uvutaji sigara unazuia mtiririko wa damu miguuni mwako.

11. Mhudumu wa afya akague miguu yako mara kwa mara unapokwenda kliniki. Jitengenezee utaratibu wa kumkumbusha daktari anayekuhudumia ili atizame mguu wako. Njia nzuri ni kumuuliza daktari, unauonaje mguu wangu?

Vipimo Muhimu Kuwa Navyo Kujikinga na Vidonda​

Vidonda vya kisukari vinaepukika. Hata wale waliokatwa miguu wangelifahamu haya wangeweza kuwa wanatembea hivi tunavyoongea kwani wasingekuwa wamepata kidonda na hivyo kuepuka haya yote yalioysababishwa na vidonda.
Kumbuka sukari inapozidi na kupungua kwa hisia miguuni ukijumlisha na kushuka kwa kinga mwilini ni huongeza hatari zaidi. Hivyo utahitaji kufahamu kiwango chako cha sukari ili upange mkakati wa kuidhibiti na pia kuweza kufahamu kama unahisi kwenye miguu.
 
Mkuu hongera kwa post yako vidonda vya ugonjwa wa kisukari vinatibika kama kuna mtu mwenye vidonda vya ugonjwa wa kisukari anitafute kwa wakati wake ili nipate kumtibia na atapona kabisa.
 
Back
Top Bottom