Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,471
- 11,454
Waziri mkuu wa falme za kiarabu,Abdullah bin Zayed amemshushua waziri mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu kwa kauli yake aliyoitoa hivi karibu kwamba nchi ya UAE, Saudi Arabia na mataifa mengine ya kiarabu yatasaidia kuiendesha Gaza baada ya vita.
Waziri huyo kwanza amemtaka Netanyahu kutambua kwamba hivi sasa Israel imeivamia Gaza na kwamba hakuna haki ya kufanya hivyo. Akaongeza kuwa Israel iache kuihusisha UAE na mpango wowote wa kuhalalisha nchi hiyo kuendelea kuwepo Gaza.
Zaidi ya hivyo bwana Abdullah akasema nchi yake inalaani kitendo cha jeshi la Israel kukikalia kituo cha mpakani cha Rafah na kuzuia kuingizwa misaada ya mahitaji kwa wapalestina.
UAE ndio nchi ya mwanzo katika miaka ya karibuni, mnamo mwaka 2020 kurudisha mahusiano ya kidiplomasia na taifa hilo la kiyahudi hatua ambayo imeendelea kupingwa na wananchi wa nchi hiyo.