Tundu Lissu: Rais Samia anatumia picha zetu kujinufaisha kisiasa, tunamtaka ashushe mabango yote la sivyo tutamshtaki Mahakamani

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
150
565
Akizungumza na wananchi wa Iringa, leo Mei 2, 2024, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema Rais Samia anatumia picha za viongozi waandamizi wa Chama chake akiwemo yeye kuweka mabango nchi nzima ili aoneshe kuwa wao na yeye wapo sawa, kitu ambacho mwanasiasa huyu amekikataa hadharani.

"Hatujamruhusu yeye kufanya matangazo ya picha zetu namna hiyo na kufaidika kiasiasa kwa kuwaaminisha watanzania kwamba yeye hana shida na sisi, ana shida kubwa na sisi ndiyo maana tunaandamana" amesema Lissu.

Amesema mojawapo ya ajenda za kikao cha kamati kuu kitakachoketi hivi karibuni ni kumtaka ayatoe mabango hayo, la sivyo watamshtaki kwa kesi ya Madai na si Jinai kwani upande huo Rais Samia ni saizi yao.

"Rais huwa hashtakiwi kwenye Jinai, kwenye madai, aaaah saizi yetu" Lissu.

Aliuhadaa umma kuwa ana Nia njema kuomba maridhiano,

Tukaja stukia, Bei za bidhaa zinapanda, mikataba ovu inaingiwa, hujuma tanesco, wizi wa kura unaendelea na maridhiano yanaendelea.

Haya mambo haya, basi tu!!
 
Akizungumza na wananchi wa Iringa, leo Mei 2, 2024, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema Rais Samia anatumia picha za viongozi waandamizi wa Chama chake akiwemo yeye kuweka mabango nchi nzima ili aoneshe kuwa wao na yeye wapo sawa, kitu ambacho mwanasiasa huyu amekikataa hadharani.

"Hatujamruhusu yeye kufanya matangazo ya picha zetu namna hiyo na kufaidika kiasiasa kwa kuwaaminisha watanzania kwamba yeye hana shida na sisi, ana shida kubwa na sisi ndiyo maana tunaandamana" amesema Lissu.

Amesema mojawapo ya ajenda za kikao cha kamati kuu kitakachoketi hivi karibuni ni kumtaka ayatoe mabango hayo, la sivyo watamshtaki kwa kesi ya Madai na si Jinai kwani upande huo Rais Samia ni saizi yao.

"Rais huwa hashtakiwi kwenye Jinai, kwenye madai, aaaah saizi yetu" Lissu.

chadema + ccm nyinyi nyote kenge maji tu, cdm hata mkipewa nchi mtakuwa kama ccm tu wabinafsi na kuangalia familia zenu.
 
Back
Top Bottom