SoC03 Sote Tuwajibike Kutokomeza Ushoga na Usagaji Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

Tukuza hospitality

JF-Expert Member
Jul 30, 2022
242
615
Utangulizi
Waalimu Forum (Agosti 25, 2021), inaeleza maana ya Ushoga na Usagaji:
Ushoga ni nini? Kwa muktadha huu, ina maana tofauti na ile ya Urafiki (hasa kwa wanawake), ni ile hali ya mwanaume/mvulana kujihusisha kingono na mwanaume/mvulana mwenzie kinyume na maumbile yaani uume kuingizwa ndani ya puru (sehemu ya haja kubwa) au utumbo mpana kisayansi.

Usagaji ni nini? Ni ile hali ya mwanamke/msichana kujihusisha kingono na mwanamke/msichana mwenzie yaani kusuguana uke kwa uke, kunyonyana uke,na kutumia uume bandia wa kuvaa (dildos) na kuingizana katika uke zao.

Katika Makala haya, nitajikita zaidi katika dhana ya Ushoga, maana ndio wenye madhara makubwa zaidi ya kiafya na kijamii, ukilinganisha na Usagaji!

Regina Mpogolo – Habarileo (Machi 12, 2019), anaandika, “Ushoga siyo kitu kigeni kwa baadhi ya jamii ya watu hapa duniani. Kilicho kigeni ni ushoga uliorasimishwa, yaani ule unaotungiwa sheria za kuwatambua na kuwalinda mashoga, yaani, ushoga unaodai kuzuia kunyanyapaliwa, na kudai haki ya mashoga kuishi pamoja kama wanandoa.”

Kimsingi, vitendo vya ushoga ni kosa la jinai nchini Tanzania kama yalivyo makosa mengine. Sheria za Tanzania haziruhusu ushoga, na hii imeainishwa katika Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16.

Kielelezo Na. 1: Waumini wa Dini y Kiislamu Wakiandamana Kupinga Ushoga Jijiji Dae-ES-Salaam
Waumini wa Kiislam Dhidi ya Ushoga.png

Chanzo: Habarileo (2019)

Chanzo cha Ushoga Duniani
Kwa mujibu wa Waalimu Forum (Agosti, 2021), inaaminika kwamba tabia hii ya kulawiti au kulawitiwa (wanaume kuingiliana kinyume na maumbile) ilianza tangu kale, kidini ilianza na kushamiri katika miji ya Sodoma na Gomora. Lakini tofauti na habari za kidini, Ngono hii ilikuwa inafanywa na tamaduni zisizokuwa na hali ya utambuzi; ikaenea katika mataifa mengi ya Ulaya na Amerika na kisha Afrika.

Sababu ya Kusambaa na Kushamiri kwa Ushoga Duniani
Kwa sasa, nchi nyingi za Magharibi zimehalalisha ndoa za jinsia moja. Katika bara la Afrika, nchi ya Afrika Kusini, tayari imehalalisha ndoa za jinsia moja.
Baadhi ya madhehebu ya kidini husasani huko Ulaya Magharibi na Marekani, yameruhusu ndoa za jinsia moja.

Kwa muktadha huu, nchi za Magharibi zimekuwa zikishinikiza nchi mbalimbali duniani (hasa za Afrika) kuhalalisha ndoa za jinsia moja, na hata kufikia hatua ya kutishia kuzinyima misaada au mikopo ikiwa zitapinga.
Hali hii imewafanya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja (hasa mashoga) katika nchi mbalimbali (hasa Afrika) kushinikiza serikali zao kuhalalisha vitendo hivi, kwa kuwa wanaona dunia ipo upande wao.

Chanzo cha Ushoga Tanzania
Waalimu Forum (Agosti, 2021), inaendelea kusema, kuingia kwa tamaduni mpya za wakoloni waliokuja Afrika, na kuongezeka kwa biashara za Waarabu Pwani ya Afrika Mashariki kulichangia kwa kiasi kikubwa jamii ya Kitanzania kuiga tabia hii, ambapo kwa sasa karibu mikoa yote vitendo hivi vinafanyika.

Kuna maeneo makuu matatu ambako vitendo vya ushoga na usagaji vinafanyika na baadaye kusambaa kwenye jamii.

Mashuleni
(hasa zile za kulala): Vitendo vya Ushoga, vinajitokeza sana katika shule za sekondari, hasa zile za wavulana pekee; vile vya Usagaji katika shule za Wasichana.

Magereza: Wanaume hulala sehemu moja, ambapo kuna uwezekano wa vitendo vya ushoga kufanyika na wanawake sehemu nyingine, ambapo pia usagaji huweza kufanyika. Kuna baadhi hulazimishwa kufanya vitendo hivyo kwa mara ya kwanza na wale wenye nguvu, na baadaye wanajikuta wamezoea na kupenda tabia hiyo.

Majumbani: Kumeripotiwa matukio mengi ya watoto kulawitiwa na ndugu zao wa karibu majumbani, (Kaka, Mjomba, na hata Baba). Matendo haya yanafanyika kwa siri sana, na huwafanya waathiriwa (hasa watoto) kuwa waraibu wa matendo hayo, na hata kuyaendeleza mitaani.

Pia, kwa mujibu wa Waalimu Forum (Agosti, 2021), inasemekana, Watalii wanaotembelea maeneo ya Zanzibar,Tanga, Dar, Moshi na Arusha hasa Wagiriki na Waitaliano huwatumia vijana kingono kinyume na maumbile na kuwalipa pesa, aidha waingiliwe wao au wao wawaingilie vijana wa Kitanzania katika mahotel ya kitalii.

Vitendo vya Ushoga na Usagaji Vinapingwa Vikali na Viongozi wa Kidini Tanzania
Wakati serikali ikiweka bayana msimamo wake dhidi ya vitendo vya ushoga na usagaji, viongozi mbalimbali wa kidini nchini wameungana na serikali kwa kupinga hadharani vitendo hivyo.

Veronica Mheta, (Januari 5, 2023) wa Habari Leo, anasema, Viongozi wa dini mkoa wa Arusha, wameonya jamii kuhusu suala la kuiga tamaduni za baadhi ya nchi za kimagharibi na kukemea vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Blog ya Amuasasa (Oktoba, 2011) inasema, Ushoga wa aina yoyote ule ni Haramu kwa mujibu wa Qur'an na Biblia kwa kupitia mifano ya Kaumu Lut. Aya zifuatazo zinatufahamisha wazi kuwa Ushoga kwa jinsi yake umekatazwa kwa binadamu wote.

Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Walawi 18:22

Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume? Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!" Q 26:165-166

Madhara ya Ushoga
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, kuna madhara mengi yatokanayo na matendo ya ushoga, mojawapo ni kulegea kwa puru (sehemu ya haja kubwa) – kiasi cha kushindwa kuzuia kinyesi kutoka, saratani ya haja kubwa, kuathirika kisaikologia hadi kufikia hatua ya kufikiria kujiua (kutokana na unyanyapaa ndani ya jamii), na mengine.

Kilelezo Na. 2: Wakazi wa Kilimanjaro katika Maandamano Dhidi ya Vitendo vya Ushoga
Maabdamano dhidi ya Ushoga Tz.png

Chanzo: U-Tube: Maandamano ya Kupinga Ushoga Kilimanjaro

Nini cha Kufanya Kutokomeza Ushoga Tanzania?
  • Kuweka mfumo maalum wa kusimamia shule zote hasa zile za bweni na kuhakikisha vitendo vyote vya ushoga na usagaji vinakoma.
  • Kuweka mazingira mazuri, pamoja na usimamizi wa kutosha magerezani kudhibiti matendo haya.
  • Kuanzisha kampeni maalum na endelevu ya hamasa dhidi ya matendo ya ushoga na usagaji mashuleni, nyumba za ibada na maeneo mengine ya umma.
  • Kuanzisha vituo au kambi maalum watakapopelekwa watu wanaothibitika kufanya matendo hayo (ushoga na usagaji) kwa lengo la kuwatibu na kuwapatia ushauri nasaha, na hivyo kuwawezesha kuacha vitendo hivi.
  • Kuanzishwa kwa madawati maalum mashuleni na ofisi za serikali za mitaa/vijiji yakayoshughulikia malalamiko juu ya vitendo vya ushoga/usagaji.
Marejeo
Kushamiri Kwa Ushoga Na Ukahaba

Michuzi TV (Aprili 10, 2023), Serikali: Ushoga, Usagaji, Mapenzi Ya Jinsia Moja Hayana Nafasi Tanzania

Regina Mpogolo – Habarileo (Machi 12, 2019), Haya Ndiyo Madhara ya Ushoga.

Veronica Mheta, Habari Leo (Januari 5, 2023), VIONGOZI wa dini Mkoa wa Arusha, wameonya jamii kuhusu suala la kuiga tamaduni za baadhi ya nchi za kimagharibi na kukemea vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Waalimu Forum (Augusti 25, 2021), Fahamu Ushoga Na Usagaji Ulivyo na Unavyozidi Kuenea Nchini, Sababu na Athari Zake katika Jamii*
 
Elimu zaidi juu ya madhara ya vitendo vya kishoga na usagaji itolewe kwa watoto, vijana, na makundi mengine na wajengewe ujasiri wa kutoa taarifa za matukio haya, katika madawati maalumu mashuleni, ofisi za serikali na polisi.
 
Watoto wanatakiwa kujengewa ujasiri wa kusema kuhusu matukio haya ya ushoga, maana mambo haya wanafanyiwa watoto na watu wao wa karibu sana (hata Baba mzazi).
 
Baadhi ya madhehebu ya kidini katika nchi za Magharibu yanatetea Ushoga! Hii ni changamoto kubwa kwa waumini wao katika nchi za Afrika ambako vitendo hivi vinapingwa vikali.
 
Back
Top Bottom