Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Riwaya ya ujasusi unajaza mavisa ya kufikirika mara Majini,mara mashtani
Hili hata mimi nililiona,
Hii riwaya haikupaswa kabisa kuitwa ya Ujasusi hata kidogo. Yaani sio riwaya mbaya ila haina ujasusi wowote ule.

Ingeitwa SIMULIZI YA KIJINI, NIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
 
Hili hata mimi nililiona,
Hii riwaya haikupaswa kabisa kuitwa ya Ujasusi hata kidogo. Yaani sio riwaya mbaya ila haina ujasusi wowote ule.

Ingeitwa SIMULIZI YA KIJINI, NIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
Hii ni contemporary fantansy novel ambapo ndani yake kuna Subgenre za espionage , labda nielekeze tu ujasusi sio lazima uhusishe mambo ya kisiasa hapo sasa kwenye Majini na miungu weka Fantansy maana sio proven facts.
 
Unaweza kusema hii ni story tu lakini ina asilimia kubwa za uhalisia wa Maisha ya binadam na Viumbe wengine (Creatures of universe).

Kwa asilimia kubwa matukio yanayotokea kwenye simulizi hii yanatokea pia kwenye dunia yetu hii ya Leo. Hapa unasikia habari za kupanda Level kwa Majini, hii Scenarial ina apply pia kwa binadama kwa asilimia nyingi. Mwili wa binadamu ukiwa msafi kimwili na kiroho huwa kuna ufunuo unakujia wa uelewa na uwezo fulani wa kufanya mambo katika Maisha.

Mfano:
1) Mtoto mdogo anapo balehe huwa anapata ufunuo(anapanda level) wa kujitambua (Biologicaly) na napata uwezo mkubwa wa kiakili.

2) Kijana aliyebalehe akitoa bikra(kufanya tendo kwa Mara ya kwanza) huwa anapata ufunuo(Anapandanda Level)

3) Kijana huyo akifikia umri fulani anapata ufunuo mwingine (Anapanda levo) na kupata uwezo wa kubeba majukumu fulani na hata kuanzisha familia.

4) Pia unapofikia hatua ya mtu mzima/ mzee huwa napata ufunuo (kupanda level ) unajawa na busara na Maono.

Sasa kinachotokea ni kwamba tuna vitu vingi mno vinatutoa kwenye reli (Distractions) na kushindwa kupata ufunuo mkubwa zaidi na kuwa na uwezo wa kufanya mambo makubwa hapa duniani Mfano: Ngono zembe(Uchafu wa kiroho) ,Pombe, Vyakula vibovu, matumizi yaliyopitiliza ya Teknologia, kukosa Mwongozo wa Misingi ya Maisha ya Mwanadamu na Mengine Mengi.

Binadamu Tuna uwezo wa kimaajabu ila wajanja wanaojua hizi siri wamezificha na wanatuwekea vizuizi tusijitambue kwa Wingi.

"The greatest Potential, Strength and Powers of Human being are hiden within us, Within our Mind"
Ni kweli. Ninachooomba na Kutaka kupata ufahamu kuhusu mbinu ya:

Andiko la Urejesho Lisilo na Kikomo

Jinsi ya Kuvuna Nishati ya Anga na Ardhi

Jinsi ya Kutumia Kanuni za Anga

Kupanda Levo
 
Hili hata mimi nililiona,
Hii riwaya haikupaswa kabisa kuitwa ya Ujasusi hata kidogo. Yaani sio riwaya mbaya ila haina ujasusi wowote ule.

Ingeitwa SIMULIZI YA KIJINI, NIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
Tayari umeshapata TITLE, sasa endelea na hiyo yako tuone utafika EPISODE ya ngapi.

Tujifunze ku appreciate pale wenzetu wanapofanya jambo zuri katika jamii. Singano Jr ameweza kutuburudisha kwa miaka miwili sasa hapa JAMII FORUMS bila kuchoka ama kunung'unika. Hata kama ameitafsiri riwaya hii kutoka chanzo kingine, (na sidhani kama ilishakuwpo kwa lugha ya kiswahili hapo kabla) mimi namkubali kwa ubunifu, uvumilivu, kipaji na moyo mkuu kama wa GAIA 🤣 😬
 
The greatest Potential, Strength and Powers of Human being are hiden within us, Within our Mind"
Mkuu Singano, mara kwa mara Marehemu Sheikh Yahya Hussein katika vipindi vyake vya unajimu katika TV, radio na Magazeti alikuwa akisisitiza hiki unachosema. Hata hivyo, falsafa ya mafunzo yake ilikuwa kinyume na imani nyingi za kidini na hata kanunui za kawaida za maadili. Niliweza kumkubali baada ya kuona hali ya uongozi wa Taifa letu na kuisema itakavyokuwa baada ya kipindi fulani licha ya kutotamka bayana jina la Mwanamke aliyekuwa akimsema.

Ninaomba utuambie namna binaadamu anavyoweza kuamsha hizi potentials, strength and powers ili zimfae katika kupambana na mazingira yake.
 
Mwamba Roma aka Hades ongea na miungu wenzako mambo yanatuzidia maji huku, mvua barabara zinakatika, aridhi zinatembea basi watuachie hata kidogo mambo yaendele
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 735
Callum waziri mkuu wa Uingereza alikuwa akimjua Roma na uhusiano wake na Edna pamoja na Raisi Jeremy , idara ya usalama ya Uingereza haikuwa kwa ajili ya maonyesho tu walikuwa wakijua mambo mengi.
Lakini hata hivyo hakuwa akijua nia halisi ya Raisi Jeremy kuja mpaka hapo lakini kwasababu ni swala ambalo lilikuwa linahusiana na Roma hakutaka kuvuka mipaka yake hiyo alijitahidi kuwa makini.
“Hakika una ushawishi mkubwa Raisi Jeremy , kuja London tu umeweza kutupata mara moja?”Aliongea Catherine akionekana kumtania raisi Jeremy, licha ya kwamba hawajawahi kukutana lakini bado alionyesha hali ya kumdharau pengine ni kutokana na kutokea taifa dogo.
“Nimesikia habari za kutosha kuhusu malkia wa Wales lakini sikutegemea kukuona hapa ,nipo hapa kwa ajili ya kikao cha umoja wa mataifa kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa dunia nzima na mara baada ya kusikia habari za binti yangu na mume wake wapo hapa nikaona sio mbaya kuwatembelea”Aliongea huku akiwa na uso uliopambwa na tabasamu.
Maelezo yake yalikuwa kamilifu na ilimfanya kuonekana kama vile alikuwa na ukaribu sana na Roma pamoja na Edna.
Baada ya salamu wengine wote walitoka nje na kumuacha Roma na familia yake ndani ya chumba hicho cha VIP.
“Kama upo hapa kwa ajili ya kunifanya nikutane na mkuu wako wa miliki basi sahau maana sina mpango wa kuonana nae kabisa , kama anataka sana kuonana na mimi basi mwambie aje huku yeye mwenyewe”Aliongea Roma na kufanya tabasamu la raisi Jeremy kupotea mara moja.
“Roma kuna haja ya kuwa hivyo mbele yangu , ninaweza nikawa nilifanya makosa lakini yaliopita si ndwele na isitoshe hatuna vinyongo kati yetu , nilifanya mambo yale kwasababu ya kutaka wewe na Edna kuishi kwa furaha”
Wakati wa kuongea alikuwa akimwangalia Edna kwa sura ya kumwambia amsadie kumuomba mume wake lakini Edna alionekana kumpotezea.
“Usingekuwa hai mpaka sasa kama sio kwa uhusiano uliopo kati yako na Edna , hiyyo acha kuzunguka zunguka na sema kilichokuleta”
“Sawa nitaenda moja kwa moja , mkuu wa miliki ya Panas anataka kuongea na wewe , kama utakataa kwenda katika miliki au kwenda Rwanda yupo tayari kuongea na wewe kwa njjia ya vidio Call , ukikataa kusikiliza utakuja kujutia baadae”
Ijapokuwa ulimwengu wa kijini ulikuwa ukijitegemea lakini majini waliokuwa wakiishi huko walikuwa na uwezo wa kufanya mawasiliano na ulimwengu wa nje bila shida yoyote kutokana na teknolojia ya ajabu ambayo iliasisiwa na mababu wa miliki hizo.
Kuhusu Roma hakushangazwa na maneno yake kwani alikuwa ashajua kiasi kuhusu miliki hizo za kijini hiyo aliamini ilikuwa ikiwezekana.
“Kama ni hiyo niunganishe nitaongea nae"
Raisi Jeremy alijisikia furaha na kujivunia huku akijiambia pengine Roma alikuwa akiogopa miliki ya Panas.
“Nifuate nje tutafute sehemu nzuri kama ni hiyo , kuna watu wengi hapa”
“Hakuna haja , hawa wote ni marafiki zangu na familia yangu hiyyo sio lazima kuficha kitu kwao, labda kama mheshimiwa Jeremy anaogopa kugundulika ana uhusiano na majini?”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu la uchokozi.
Baada ya kusikia maneno hayo hakutaka kusita tena na alitoa kishikwambi cha aina yake na alianza kukipangusa na ilionekana Panas walikuwa washajiandaa muda mrefu kupokea simu hio.
Sura ya jini Gefu iliweza kuonekana katika kioo cha kishikwambi hicho na alikuwa ndani ya ofisi yake.
“Sir, Mr Roma Ramoni yupo hapa tayari kwa kuongea na wewe”Aliongea Jeremy kwa sauti ya unyenyekevu huku akiwa amepamba uso wake na tabasamu.
“Sikutegemea kukutana kwetu kwa mara ya kwanza kutakuwa kwa namna hii , Roma hakika ni ngumu sana kukupata”Aliongea Gefu akiwa na tabasamu.
“Oh! Kumbe mkuu wa miliki ya Panas ndio upo hiyyo ..”Aliongea Roma lakini upande wa pili Gefu hakuelewa Roma anachomaanisha.
“Nilikuwa na haja ya kuonana na wewe kwa haraka kwasababu nina jambo muhimu napaswa kukuambia linahusiana na usalama wako na wanaokuzunguka”
“Unajaribu kumaanisha kuna kundi la majini ambao wanataka kuniua muda si mrefu?”
“Ndio , kwasasa ni kama unatembea juu ya barafu nyembamba, lakini sio tu kwmaba najua maadui zako wote lakini pia nipo tayari kukusaidia”
“Haina haja , sijakubaliana kuongea na wewe ili kusikia unaongea upumbavu”
“Nini!!. Roma unamaanisha nini kuongea hivyo au huamini maneno yangu?”
“Sio maswala ya kuaminiana, mimi nilitaka tu kujua mkuu wa miliki ya Panas anaonekana ipi ili nikiivamia miliki yenu nisipate shida ya kukutafuta na kukuua”
Ishara ya hasira iliweza kuonekana katika uso wa Gefu mkuu wa miliki ya Panas lakini fasta sana alirudi katika hali yake.
“Kijana mdogo chunga kauli zako naamini haipaswi kuwa na ugomvi kati yetu”
“Nyie ndio mliovujisha taarifa ya Rufi kuishi Tanzania kwenda kwa miliki ya Xia , hio ni sababu tosha ya mimi kutaka kuivamia miliki yenu na kulipa kisasi kwa umbea wenu”Aliongea Roma bila ya ishara ya utani.
Maneno yake ya kibabe yalimshitua Master Namba nne huku akijiuliza Roma alijuaje yeye ndio alivujisha taarifa.
“Kwa muonekano wenu inaonyesha nilikuwa sahihi , kama ifahamikavyo ukuu wa miliki ya Panas katika kujua kinachoendelea kwenye ulimwengu wa kawaida”
Upande wa Gefu alijua Roma hakuwa na ushihidi hivyo hakutaka kukamatika kizembe na alijua pengine Roma anamjaribu.
“Unathubutu ipi kunijaribu wewe bindamu?”
“Kwahio unatakaje?”
“Unafikiri tunakuogopa , tunakupatia nafasi ya mwisho ya kuungana na Panas, kwasasa umekuwa adui wa miliki ya Xia ,Kekexil na Braki , unadhani kujificha huko nje ya nchi kunaweza kukufanya ukawa salama na miungu wenzako dhaifu kukusaidia?”Aliongea kwa kufoka.
“Braki!!!”
Roma sura ilijikunja mara baada ya kusikia anahusishwa na Braki na kujiuliza Braki ndio kitu gani lakini Gefu alionekana kujua kinachoendelea kupitia sura ya Roma.
“Unajisikiaje kutokujua baadhi ya maadui zako?”
Roma hakujibu swali na badala yake palepale alipiga chini kile kishikwambi na kupasuka pasuka vipande vipande.
“Siogopi kiumbe chochote mimi , kama kuna adui anajiona mbabe anitafute tumalizane”Aliongea Roma na palepale macho yake yalisinyaa wakati wa kmwangalia Jeremy.
“I am not in a good mood , so get lost now when I still give a damn about your relationship with my wife”Aliongea akimaanisha aondoke wakati anajali uhusiano uliopo kati yake na mke wake.
“You .. you are Vexing … kwa ajili ya Edna!?, Roma nataka nikupatie ushauri … sisi binadamu tunao wajibu wa kufuata sheria za hii dunia , kila mtu yupo chini ya sheria na kila mtu atakushambulia kama utazivunja kutokana na ukiburi wako na wakati hayo yanatokea hakuna ambaye atakusaidia”
Baada ya kuongea kauli hio palepale licha ya kuwa na hasira zake aliondoka ndani ya eneo hilo , kwani alijihisi kutamani kumuua Roma ni hivyo tu uwezo huo hakuwa nao.
Mara baada ya kuondoka Roma alisimama na kusogelea dirisha na kuangalia upande wa uwanjani ambako mechi ilikuwa mapumziko , huku hali ya hewa ikiwa sio ya kawaida ndani ya eneo hilo kwani watu wake wa karibu wote walionekana kuwa na wasiwasi.
Bila kujua Roma alikuwa amejiongezea adui mwingine ambaye hamfahamu anaefahamika kwa jina la Braki.
Ukweli ni kwamba alikuwa na maadui wengi ambao hakuwa akiwajua na baadhi yao walitokana na wanawake wake na wengine walikuwa wakimchukulia kama adui kutokana na kuwa na uwezo mkubwa.
“Rufi unajua chochote kuhusu miliki ya Braki?”Aliuliza Roma mara baada ya kujituliza.
“Sijawahi kuisikia , Nanny ushawahi kuisikia?” Rufi alionekana kutokukujua na alimtupia swali Sui lakini hata yeye alionyesha kutokujua chochote.
Ijapokuwa ilikuwa ikihusiana na ulimwengu wa majini lakini kutokana na ukawaida wao hawakuwa wakiijua.
“Mimi nadhani Braki inahusiana na familia ya Mzee Sharif , si ulisema walishawahi kuleta majini wengi kupambana na wewe , nadhani tufikirie hivyo kwa sasa?”Aliongea Rose na Roma alitingisha kichwa baada ya kuona alikuwa na pointi .
“Hubby unataka kweli kwenda kuivamia miliki ya Panas?”Aliuliza Edna ambaye alikuwa amekunja sura.
“Hautaki niende?”
“Nili…”
“Edna siwezi kukusikiliza awamu hii , kila kitu kingekuwa sawa lakini katika vitu ambavyo vinahusisha uhai wa wengine sitokuruhusu ubadilishe mawazo yangu”
Edna mara baada ya kuona usiriasi uliopo katika macho yake alishia kuvuta pumzi na kuzishusha.
“Sijasema nataka kukuzuia , nikwamba naona itakuwa hatari sana”
“Tatizo hata kama niseme nisiende kuwavamia na kuwasambaratisha najua hawawezi kutulia na watatafuta tu namna ya kutaka kuniua … Hili ni daraja ambalo napaswa kuvuka na nikishapita kila kitu kitakuwa kimekwisha”Aliongea.
“Roma sidhani kama itakuwa ni rahisi, tayari tuna uadui na miliki tatu za kijini kubwa na tuna maadui maelfu na maelfu , unadhani ni sawa kuua na kuendelea kutengeneza maadui? , mimi naona labda hakuna haja ya kuua na tunaweza kutatua haya matatizo kwa njia nyingine , wao wanasheria zao pia na pale wanapojihakikishia kwamba huwezi zivunja hawawezi kukufanyia chochote”Aliongea Sophia.
“Sophia unaongea ujinga , hivi unajua tafsiri ya sheria mbele ya watu wenye nguvu ni tofauti na inavyotafsirika mbele ya watu dhaifu?”
Aliongea Roma na kisha alinyoosha kidole kuelekea uwanjani wakati wachezaji wakitoka katika vyumba ya mapumziko kwa ajili ya kuanza kwa kipindi cha pili.
“Hivi unajua ni kwasababu gani mpira wa miguu ni maarufu sana duniani na kwanini watu wengi kama hivi wanaupenda?”
Wanawake hao wote waliishia kushangaa tu wasiweze kuelewa swali lake,walijiambia wanaongea topiki ya hatari hiyo kuna haja gani ya kuhusisha mpira wa miguu lakini Roma alionekana kutojali mawazo yao.
“Ni kwasababu katika mechi ya mpira haijalishi timu ni bora kiasi gani au ni dhaifu kiasi gani lakini siku zote matokeo yanaanza sifuri kwa sifuri na mpira unachezwa kwa sheria, hii inamaanisha kwamba haijalishi timu ni dhiafu lakini kama watakuwa tayari kupambana katika kukaba kukimbia na kufunga hata wao pia wanaweza kuwa mabingwa , kwa maneno mengine hapo ndio wakati watu ambao sio wachezaji ndio wanajipatia riziki , sehemu ambayo uvumiliu wao huonekana , katika uwanja mshindi ndio bingwa hata kama ni dhaifu au alipendelewa kwa namna yoyote ile ili mradi tu ameifunga timu bora na yenye nguvu hata kama ni mara moja katika historia yake , hii inamaanisha kwamba wao pia wanayo nafasi ya kuwa nyota na hii ndio maana mpira wa miguu ni wa kuvutia sana”Aliongea na kisha akavuta pumzi na kuendelea.
“Lakini unadhani hio ni sawa kati ya wachezaji na wamiliki wa timu au wasimamizi wa mashindano? , ingawa mechi inaanzia sifuri kwa sifuri lakini kwa matajiri na wasimamizi wa UEFA mambo ni tofauti , kwao haijalishi nani anashinda bado watapiga pesa na kupata faida na ipo hivyo siku zote , kwa mfano mchezaji katika timu kama akishindwa kutoa ushirikiano wa maelekezo viongozi wanaweza kuto kumjumuisha katika mechi na kutoa sababu kama vile ni majeruhi au haendani na mfumo na mengineyo .. ,kwa lugha nyepesi ni kwamba wanaoendesha michezo na timu ndio wenye maamuzi ni taarifa gani iwafikie mashabiki na kuamua mchezo uwe vipi , unaweza kuona mechi kabisa hii mshindi ni wa kupangwa lakini wewe kama shabiki utafanya nini tofauti na kuongea ongea na kugoma, hakuna cha ziada ambacho unaweza kufanya kwasababu kwa nje wewe unaburudika na wachezaji wakicheza mpira lakini kwa ndani kuna mfumo ambao umetengenezwa kwa ajili ya kurahisisha maswala mengi aidha yawe ni ya kifedha au Ajenda zao za kijamii labda tu kama watu waache kuangalia mpira .. na huu ni mfumo endelevu na utaendelea hivi labda siku tu watu dunia nzima waseme hawaangalii mpira tena , sasa hili halipo kwenye mpira tu kila michezo maarufu yote wewe kama shabiki utaona ni burudani lakini nyuma ya pazia kuna mfumo..”
“Ndio inaweza kuonekana yanayofanyika ni uchafu lakini maisha ya kibinadamu tokea mwanzo yalianzia katika uchafu , sasa tuseme mimi ni kama mchezaji , Kocha au tuseme timu nyenye nguvu ambayo imepata umaarufu hivi karibuni, viongozi waandamizi na matajiri wote macho yao yatakuwa kwangu kwasababu mbili tu; mosi nifanye kazi kwao na niwasaidie kupata pesa au kutimiza ajenda zao , pili hawataki niwasaidie wengine kupata pesa, kwa maneno mengine ili nipate faida lazima na wao wapate faida na sasa hapa hizi ndio sheria ambazo wameweka ambazo hawataki mchezaji kuzivunja kwasababu zinaathiri utajiri wao pamoja na ushawishi wao”
“Kama nitafanya kazi nzuri kama mchezaji wataniacha niendelee kuishi kama mchezaji na kunifanya niendelee kuwa maarufu na watanipatia Ballon d‘or au Kiatu cha Dhahabu au watafanya hata timu yangu ya taifa kuwa bingwa wa dunia au club yangu kuwa bingwa wa UEFA na kama sitofanya vizuri au nikikataa matakwa yao watahakikisha wananizimisha aidha kwa kuniundia mchezaji uwanjanni ambaye atanijeruhi au kuanza kunitengenezea Zengwe nyingi tu ili kunitoa mchezoni hizi ndio sheria ambazo wameweka .. wakati nikiwa chini hawakuwa na habari na mimi na hawakuwahi kunichukulia siriasi lakini sasa nimekuwa tishio kwao hawataki kuzembea, hii haipo kwenye mpira tu kwa kila nyanja kuna huu mfumo na ambao wanasuka mipango hii ya kimfumo hawatojionyesha kamwe mpaka sekunde ya mwisho , isitoshe lazima wahakikishe mchezo ulikuwa ni wa haki”
Kila mmoja alijikuta akiwa kimya na kuangalia uwanjwani ambako mechi ilikuwa ikiendelea.
Maneno ya Roma yanaweza kuonekana kama yamebase upande mmoja lakini yalikuwa yamejaa ukweli mgumu(Harsh truth).
“Ijapokuwa hatuwezi kushiriki katika vita yako lakini kama mtu ambaye unapambania maisha ninaelewa hisia zako”Aliongea mmoja wapo na kumfanya Roma kuonyesha shukrani na palepale alimbeba Lanlan na kumpakata.
“Sina chaguo nyingine , kwasababu mpaka sasa hawaniangalii kama mtu Dhaifu , kama ninataka kuendelea kuishi ni aidha nishirikiane nao au kama sitaki kushirikiana nao niwaweke chini yangu kwa kuwapiga na kisha kuweka sheria zangu mimi”Aliongea na kisha aligeuza macho yake na kuangalia warembo wake waliokuwa wakimwangalia kwa macho ya matamanio na kisha akageuzia macho kwa Lanlan.
“Sio mimi tu lakini ni kwenu pia na kwa mtoto wangu”Aliongea Roma kwa sauti hafifu akionekana kama vile ni mtu ambaye anakumbukia maisha yake yaliopita na kitendo kile kilimfanya Blandina kukosa ujasiri wa kuendeea kusikiliza na machozi yalimtoka na kwenda kumkumbatia Roma na Lanlan na kuanza kulia.
Kila mmoja alijua hisia za Blandina zinatokea wapi , ilionekana alikuwa na hatia kama mzazi na kumfanya mwanae kupitia magumu mengi lakini kwa wakati huo machozi yake hayakuwakilisha huzuni tu lakini bali kujivunia kwa mafanikio ya mtoto wake.
Ukumbuke hapa ni ndani ya Chumba cha VIP ndani ya uwanja wa Wembley hivyo ni kama wamejitenga na mashabiki wengine.
Unadhani Roma yupo sahihi , ni kweli kuna mifumo ambayo imewekwa kwa ajili ya kushikiria mafanikio ya watu??






SEHEMU YA 736.
Ni upande wa Tanzania jijini Iringa muda wa mchana katika makazi ya Afande Kweka kulikuwa na kikao cha siri kilichokuwa kikiendelea.
Kikao hichi kilikuwa kikijumuisha watu kama saba hivi ambao ni Paster Cohen, Mellisa , Phill Knight , Nadia Alphonso , Suzzane , Linda na mwanamama mrembo kutoka Hungury afahamikae kwa jina la Zoe Kovacic.
Nadia ndio ambaye alikuwa akionekana kusoma ripoti licha ya kwamba kila mmoja ambaye alikuwa hapo ndani alikuwa ameshikilia kishikwambi, ilionekana ni kama vile walikuwa wakirudia kile ambacho Nadia alikuwa akisoma.
“Mzee kama mwanachama mkongwe wa jamii yetu, viongozi wameniagiza nikuelezee kuhusu ubini wa kiongozi wetu”Aliongea Mellisa kwa lugha ya kingereza.
“Kiongozi amekwisha kupatikana?”
“Ndio Komredi katika kikao cha mwisho kilichofanyika Saudi Arabia tumeweza kupata mawasiliano na Kiongozi kwa mara ya pili”Aliongea Pastor Cohen na kumfanya Nadia kuangaliana na Suzzane.
“Kulingana na Kalenda ya jamii yetu kiongozi alipaswa kufanya mawasiliano na viongozi wa juu ndani ya tarehe husika , ijapokuwa ilikuwa ni hatua ya pili ya kumthibitisha kama kiongozi, umoja umefurahi kwamba mpango A wa kalenda ulitimia na kwanzia tarehe hio Edna Adebayo anatambulika kama kiongozi wa Umoja wa Ant-Illuminat”Aliongea Mellisa na kumfanya Linda kuonyesha mshangao huku Afande Kweka yeye macho yake ya kizee yakichanua.
“Komredi ni kama tulivyotarajia”Aliongea Pastor Cohen.
“Kuna maswali mengi juu ya hili Komredi nilijua kiongozi ni Seenteen kulingana na maelezo yako Komred”
“Wote tulidhania kiongozi anakwenda kuwa Seenteen, kuna maswali mengi juu ya hili lakini kulingana na maelekezo ya mwasisi wa umoja wetu anasema Kalenda inakwenda kujibu maswali yote lakini ni Aidha kama Binadamu tutafanikiwa kuishinda vita na Miungu”.
“Viongozi wengi pia hawakuamini kama siku ya kikalenda Edna angefanya mawasiliano na sisi lakini ajabu alifanya hiyo na kila mmoja alishangaa lakini imeondolea umoja harakati za kuona mchoro wa Unabii?”
“Huu mchoro wa Unabii unaonyesha kitu gani , kwanini imekuwa kitu muhimu kwa pande zote mbili Mellisa?”
“Hatuwezi kujua kwa uhakika mchoro huu unamaanisha nini na nani anaonekana katika picha lakini makisio yetu ni kwamba mchoro huu unahusiana na kiongozi wa umoja wetu”
“Kwa taarifa za Shekh Assad ni kwamba mchoro huu pia una umuhimu kwa Illuminat na ndio kiongozi ambaye wanamsubiria, kama usemayo ni sahihi Edna ana uhusiano na huu mchoro wa unabii lakini si inamaanisha kwamba pia ndio kiongozi wao ambaye wanamtarajia kulingana na unabii?”
“Upo sahihi Zoe lakini kwasasa hata Illuminat wenyewe bado hawajaweza kuona mchoro huu wa Unabii kwani upo chini ya Vatican”Alijibu Mellisa.
“Madam kuna uwezekano wa Edna kuwa Seventeen?”Aliuliza Nadia.
“Kulingana na mpango ulivyokuwa , Seventeen ni zao la mpango LADO kama alivyo Roma Ramoni lakini majukumu yao tokea mwanzo yalikuwa ni tofauti , ijapokuwa mpaka sasa hivi hatujui Seventeen yupo hai chini ya Zeros lakini tokea mwanzo Seventeen ndio alikuwa ni msingi wa kufanikiwa kwa Ant-Illuminat”
“Kama ni hivyo kwanini Edna ndio awe kiongozi , sijawahi kuona ishara yoyote ya Edna kujua chochote kuhusu Ant- Illuminat?”Aliongea Suzzane.
“Ukweli ni kwamba tunaamini Seventeen amekwisha kufariki mpaka sasa chini ya maagizo ya Athena na kwa maelezo ya Chriss ili mchoro wa unabii kukidhi vigezo vya ki’unabii hakupaswi kuwa na uwepo wa watu wawili wenye sura zinazofanana”Aliongea Mellisa.
“Melllisa hili linajibu kilichopo kwenye mchoro huo wa Unabii , kama kweli maneno ya Chriss ni sahihi basi kuna uwezekano Mchoro wa Unabii unaonyesha sura ya Edna au Seventeen lakini kwasababu ni unabii wa mtu mmoja basi moja kwa moja mmoja wapo lazima atoweke”
“Naunga hoja ya Komredi lakini kwangu bado swali linaibuka Athena ni nani na kwanini mchoro wa Unabii kuwa na sura ya Edna , wote kati yetu tunajua mpango wa Athena ni nini zidi ya binadamu na hatari ya mipango yake kufanikiwa?”
“Afande mpaka sasa hatuwezi kujibu maswali lakini pia hatuwezi kufanya makisio kwani ipo kalenda ambayo inatuongoza ambayo haijawahi kufeli na hata pale ilipofeli kulikuwa na mpango B, nadhani wote tuamini katika Kalenda”
“Naunga hoja ya Mellisa akini je wakuu wanasemaje kuhusu hali inayoendelea kwa sasa?”Aliuliza Phill.
“Unazungumzia kushuka kwa joto la dunia?”Aliuliza Zoe na kufanya kila mmoja kumwangalia mwenzake kwa shauku kubwa ya kusikia jibu.
“Kulingana na Kalenda tukio muhimu ambalo ndio ishara kubwa ya hatua muhimu ya Athena kuchukua lakini vilevile hatua ambayo Umoja wetu unapaswa kuchukua ni kuona majira ya theluji katika bara la Afrika, nadhani hali hii ya hewa tunaelekea kuona ishara hii hivi karibuni hivyo tunaweza kusema mpaka sasa tunaingia katika hatua muhimu sana katika umoja wetu na kwa dunia kwa ujumla , hiki ndio ambacho viongozi waeniusia nikiseme katika kikao hichi na sio hapa tu dunia nzima vikao vya ajenda hii kwa wenzetu vinaendelea”Aliongea Mellisa.
“Mellisa yupo sahihi kushuka kwa joto la Dunia sio nchi moja bali ni dunia nzima lakini ni Afrika pekee ambayo inaonyesha joto kupungua taratibu sana , hii inamaanisha mpaka nyakati za theluji zikitufikia kuna uwezekano baadhi ya maeneo ya Dunia joto kushuka sana kiasi cha kuathiri maisha ya binadamu”
“Nadhani ndio maana Wanachama wengi wa Freemason na Illuminat wamenunua maneo mengi ndani ya Afrika kwa kipindi cha hivi karibuni huku wakifosi sheria nyingi za kimataifa kupitishwa , hii inaonyesha walikuwa wakiandaa mazingira rafiki kwa ajili ya kuishi wakiwa huru”Aliongea Zoe.
“Hii ni kweli na ni swala ambalo tulikuwa tukipambana nalo kama umoja,kuna baadhi ya mataifa ambayo tumeyachagua kama nguzo muhimu ya Umoja kwa ajili ya kulinda tamaduni zake ikiwemo Tanzania lakini kuna maeneo ambayo pia ndani ya Afrika yapo chini ya Illuminat na ushawishi wao ni wa juu na hili hatuwezi kulifanyia kazi kwani litaibua migororo”
“Nadhani naona unachojaribu kumaanisha Miss Mellisa , ni miezi kadhaa iliopita mataifa zaidi ya kumi ya Kiafrika yamepitisha sheria ya Ushoga kuwa huru hili ni swala ambalo linahusiana na ulichosema”
“Upo sahihi Linda , Tanzania ilikuwa ni nchi ambayo ingekuwa ya kumi na moja kutangaza hii sheria kama sio sisi kuingilia , shukrani kwa Suzzane na Nadia wameweza kutiisha misheni yao vizuri na sasa Tanzania imekuwa Neutral kwa sisi pamoja na wao”
“Urusi wanazungumziaje hili?”Aliuliza Afande Kweka.
“Wapo ndani ya mfumo , wanaweza kupinga wazi lakini ni taifa ambalo limegawanyika katika pande mbili”.
*******
Pumbavu zako Roma Ramoni , nitakuua tu siku moja”Aliongea Gefu kwa sauti kubwa na kwa hasira zake alipelekea kuharibu kila kitu kilichokuwa ndani ya ofisi yake lakini bado haikuwa ikitosha kutuliza hasira zake.
Mbele yake alikuwa ni Master Namba nne na mwingine mmoja ambao wote walikuwa katika hali ya wasiwasi kutokana na hasira za kiongozi wao mara baada ya kumaliza maongezi yake na Roma Ramoni.
Ilikuwa ni mara chache sana kwa Gefu kuwa katika hasira kama hizo , kitendo cha Roma kumdharau waziwazi mara nyingi mfululizo kilimfanya chuki yake kuongezeka maradufu.
“Kaka punguza jazba, ni sawa tu kama amekataa kuungana na sisi na kwasababu maadui zake ni pamoja na Braki lazima atakufa na sisi ndio tutachukua fursa hio ya kummalizia akiwa chini kabisa”
“Hawa majini kutoka Braki hawajawahi kuwepo katika uso wa dunia kwa zaidi ya milenia moja , nimesikia kutoka kwa wazee wanasema hawajui kabisa uwepo wa binadamu mwenye uwezo mkubwa kama Roma , Roma huyu mjinga amejitengenezea uadui na hawa mashetani ambao walikuwa wameshasahaulika”
“Namba nne fanya mawasiliano na Jeremy kusitisha mipango yetu yote ya kimsaada na Tanzania hususani familia ya Raisi Senga na kisha atasubiria maelekezo yangu ya mpango wa pili unaofuatia , pia tuma barua kwenda katika miliki zote zenye uadui na Roma hususani katika miliki ya Xia na Kekexil na waambie kupitia mashushusu wetu waliopo katika kila pande ya dunia ya kawaida watasaidia kujua nchi ambayo Roma anaishi na familia yake na kama wanahitaji msaada watuambie”
“Sawa kaka”Aliongea Master namba nne.
“Gegu chukua baadhi ya wazee kuelekea mlima Yoshe na mrudishe yule mtu kurudi Panas”
“Kaka namba moja sio kwamba ni mapema sana kumrudisha?”
“Fanya kama nilivyosema , vipi kama Roma akitushambulia unadhani nitaweza kuilinda miliki mwenyewe?”
“Umeeleweka bro”
Lakini sasa muda huo huo sura zao zilibadiika mara baada ya kuhisi kitu ambacho sio cha kawaida na Gefu ndio aliekuwa wa kwanza kupotea ndani ya ofisi hio na kuja kuibukia nje na kufuatiwa na wengine.
Wingu jeusi lilikuwa limejikusanya katika upande wa Kusini mwa eneo la miliki ya Panas , ngurumo na mwanga wa Radi vilikuwa vikisikika na kuonekana.
Sauti za ngurumo za radi zilikuwa kubwa kama vile anga linataka kuondoka chini.
Majini wengi wa miliki hio walikuwa nje wakiangalia hali hio ya kustaajabisha ambayo ni adimu sana kuonekana katika miliki za majini.
“Hii nii…”Jini mmoja ambaye alikuwa katike levo ya maji ya barafu aliongea.
“Hahaha…. tayari amekwisha kuipita levo ya maji ya kiroho , hii ni radi ya mapigo tisa ya adhabu ya anga”Aliongea mkuu wa miliki ya Panas kwa furaha.
“Hakika inashangaza ni juzi tu hapa Anjiu wa Xia ameweza kupita levo hii na leo ni zamu ya Rozu”
“Huu ni wakati wa kuwa na majini wa levo za juu katika ulimwengu wetu,ni heshima kwetu kuangalia kitu kama hichi kikubwa”Aliongea na kufanya wazee pamoja na majini wa miliki hio kuonyesha furaha zao.
“Kimya!!, huu ni mwanzo tu lakini hatuna uhakika kama ataweza kuvumilia mapigo hata matatu ya radi ya rangi ya Zambarau”
Baada ya kusikia kauli hio kila mmoja alipiga kimya kwani ni kweli radi hio haikuwa imeshuka bado na walikuwa na wasiwasi kwamba wanaweza kumpoteza mtu wao.
Majini wanaweza kupitia radi lakini sio wote ambao wanaweza kuihimili kwani ilikuwa na nguvu kubwa kwani dhumuni la kushuka kwake sio kwa ajili ya kunufaisha jini bali ni kwa ajili ya kutoa Adhabu kwa kukiuka sheria za anga.
Dakika chache mbele radi hio ilianza kuonyesha ghadhabu yake na boriti ya radi iliokuwa katika rangi ya Zambarau na bluu ilionekana ikishuka kama vile ni nyoka na kwenda kupiga katika sehemu ambayo yupo jini aliefahamika kwa jina la Rozu.
Ilikuwa ni sauti ya kuumiza masikio ya mwangwi ndio iliweza kusikika na kuwafanya majini kuogopa na kuwafanya wengine kukimbia
“Hii inatisha , sidhani kama Rozu ana Dhana ambayo inaweza kumkinga,atakuwa na uwezo wa kupita hii Adhabu bila kifo kweli?”
“Ni ngumu kusema na hatuwezi hata kusogelea eneo alipo kwasasa bila ya kupoteza nafsi zetu , hata mimi sijui kama ataweza kweli kuhimili?”.
Kila mmoja alikuwa akijiuliza swali linalofanana na kuna ambao walikuwa wakijutia kwa Rozu kukasirisha anga mpaka kupatwa na radi hio.
Dakika chache mbele radi ya pili ilipiga na ilikuwa kubwa kuliko ya mwanzo kiasi cha kutengeneza shimo na ndani ya dakika chache mara baada ya kufifia kitu kinachofanana na Dhahabu kilionekana katka lile eneo.
Kuna ambao waliweza kuona kitu hicho lakini hawakuweza kujua ni kitu gani lakini wakuu wa miliki hio walikuwa na uwezo wa kuhisia Rozu alikuwa hai bado kutokana na msisimko aliokuwa akidhalisha.
Hali hio iliwafanya wazee kujiuliza amewezaje kutoathirika katika mapigo hayo ya radi.
Radi ya tatu iliweza kupiga kwa awau nyingine na ilikuwa na nguvu kubwa zaidi lakini hata hivyo kile kitu ambacho kilikuwa katika muonekano wa Dhahabu bado kilikuwa kikionekana katika eneo lile.
Radi ile ilionekana haikuwa na mpango wa kuendeleza mapigo kwani mara baada ya mapigo matatu wingu lilianza kutawanyika na palepale shimo kubwa lilionekana kwa macho.
“Rozuu..!!!”
Mkuu wa miliki ndio aliekuwa wa kwanza kuita jina hilo lakini kufumba na kufumbua palepale alionekana mwanamke jini ambaye ameshikilia upinde wa Dhahabu akisogelea mbele ya kila mmoja akitokea eneo lile
Nywele zake ndefu zilikuwa hazijafungwa na zilisambaa kulingana na upepo ulivyokuwa ukivuma lakini licha ya hivyo hazikuweza kuficha uzuri wake wa ajabu na macho yake angavu , alikuwa mrembo haswa kwanzia ngozi , umbo la uso na kila kitu.
Alikuwa na muonekano wa ajabu kidogo mzungu sio mzungu , alikuwa ni kama vile ni mfilipino.
Ijapokuwa hakuwa na mavazi ya kirembo kama wanawake wa kidunia lakini upole wake pamoja na uwezo wake ulimfanya kuzidi kupendeza na kuwa ni mwenye kutamanika.
Huyu mwanamke alikuwa akifanana kwa kila kitu na mrembo ambae Hermes mjumbe wa miungu alikuwa akiongea nae katika kilele cha mlima kilimanjaro muda kadhaa mara baada ya Roma kumuokoa Edna katika mikono ya Vampire waliokuwa wakitafuta mshipi feki.
Ki ufupi ni kwamba ni huyu mwanamke bila shaka na haikueleweka ilikuwaje akawa katika jamii ya majini wa miliki ya Panas lakini ndio hivyo alionekana kupitia levo ya mapigo matatu ya radi ya mbingu na jina lake alikuwa akifahamika kwa jina la Rozu.
Ijapokwa Rozu hakuwa ameonyesha uwezo wake wote lakini kwa majini hao walijua alikuwa ni wa levo za juu sana , pengine alikuwa akilingaina ki uwezo na Jini Anjiu wa miliki ya Panas au kumpita.
“Hongera sana , kwasasa upo na uwezo mkubwa wa nguvu za kijini na hakuna ambaye anaweza kukushinda katika ulimwengu wa majini watu”Aliongea Master namba nne huku ile hofu yake ya kumhofia Roma na Anjiu ikiwa imetoweka kabisa , alijua kwa uwezo aliokuwa nao Rozu anapaswa kuwa na amani.
“Hongera sana , nilikuwa na wasiwasi muda si mrefu lakini kwa bahati nzuri umeweza kufanikiwa kupitia mapigo ya radi”Aliongea Mkuu wa miliki hio huku akijiuliza kimoyo moyo.
“Imekuwaje akapitia mapigo hayo ya dhiki ya radi kirahisi hivyo , anaonekana hajapatwa na majeraha ya aina yoyote yale”Aliwaza.
Ukweli ni kwamba kuna namna majini hao walikuwa wakimjua Rozu kama Rozu jini mwenzao lakini hawakumjua Rozu kama sehemu ya miungu , kitendo cha Rozu kuongea na Hermes juu ya mlima kilimanjaro ilimaanisha kwamba ni sehemu ya miungu lakini jina lake halifahamiki ni lipi katika miungu yote iliobaki ambayo hatujawaona wahusika wake.
“Kama hizi ni pongezi za dhati basi sina budi ya kuzipokea”Aliongea mwanadada mrembo Rozu huku akimwangalia Gefu kwa macho makali kidogo kiasi cha kumfanya Mkuu wa miliki hio kuwa na wasiwasi lakini alijitahidi kuonyesha tabasamu.
“Unapenda sana utani , sina haja ya kumuonea wivu mdogo wangu wa kike mafanikio yake , leo ni siku ya kusherehekea, uwepo wako unatufanya tusimhofie tena jini Anjiu”Aliongea.
Ukweli ni kwamba Rozu na Anjiu kidogo walikuwa na tofauti , wakati wa Anjiu anapokea mapigo ya radi chungu cha Roma ndio ambacho kilimkinga lakini kwa jini Rozu yeye ilikuwa tofauti kwa maana kwamba mapigo yote ya radi yalimfikia.
Majini wote walikuwa kwenye shangwe wakimzunguka Rozu na kumpa pongezi za dhati kabisa kwa kupigi hatua hio Adhimu.
Kuipita Dhiki ya radi ni hatua kubwa sana katika ulimwengu wa majini ndio maana.
Rozu mara baada ya kuweka upinde wake wa Dhahabu katika hifadhi ya pete alivuta pumzi nyingi na kisha kutoa tabasamu.
“Anjiu huna uwezo tena wa kunizidi, Hades namsapoti Athena na mipango yake na nataka nione ikifanikiwa”Aliwaza.
Haya sasa kuna kiumbe kingine katika miliki ya Panas , unadhani huyu jina lake halisi ni lipi kati ya miungu kumi na mbili ya mlima Olympus kutoka sayari ya Mars.
Hades A.k. a Roma Ramoni atamuweza kweli?.




SEHEMU YA 737.
Upande wa Roma mara baada ya mechi kumalizika hakuna ambaye alitamani kuangalia ugawaji wa makombe na medali hivyo walirudi moja kwa moja kwenye boti yao ya kifahari.
Upande wa Raisi Jeremy hakuwasumbua tena kwani alikuwa ndani ya Uingereza kwa ajili ya kikao cha Umoja wa mataifa kinachohusu mabadiliko ya hali ya hewa na hata Raisi Senga alikuwa ni moja ya viongozi ambao walihudhuria kikao hicho muhimu.
Kilikuwa ni kikao muhimu kutokana na mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa ya joto la dunia kuporomoka na kusababisha baridi kali licha ya kwamba katika maeneo mbalimbali ya dunia ilipaswa kuwa majira ya joto.
Ukiachana na wakuu wa mataifa lakini pia wanasayansi wengi na watu wa maswala ya kimazingira walikuwa wakihudhuria kikao hicho ili kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo mara baada ya kujua chanzo.
Clark ni moja ya wanasayansi muhimu kabisa ambao walialikwa katika kikao hicho muhimu lakini licha ya hivyo hakukuwa na maelezo ya moja kwa moja ambayo angeongea kwani ni swala ambalo bado hakuwa amelifanyia utafiti.
Roma mara baada ya kuingia katika boti ndio maandalizi ya kurudi katika visiwa vya wafu yalianza rasmi lakini ndio muda ambao aliweza kupokea simu kutoka kwa Afande Kweka.
“Wewe mtukutu hivi utaacha lini kuwa na huo ukiburi?”Aliongea Afande Kweka na kumfanya Roma kuishia kushangaa.
“Ongea vizuri mzee basi”
“Kwanini umekataa kuongea na wajumbe wa Hongmeng ?, angalau hebu ongea nao maana kwasababu yako kila saa wapo ndani ya makazi yetu, unafikiri nadili nao vipi viumbe wa ajabu kama hawa?”
“Unamaanisha huyo Xuan Jizi yupo ndani ya makazi yako?”Aliuliza Roma huku hasira zikianza kumvaa maana aliona ni kama usumbufu.
“Anaonekana kuwa na hasira sana na amesema kama hutorudi mapema anaenda kutoa taarifa Hongmeng , hebu rudi udili na hii hali nishazeeka sitaki kuingizwa kwenye matatizo ya namna hii mimi”Aliongea na palepale alikata simu ikionyesha dhahiri alikuwa amekasirika.
Roma aliweka simu yake mfukoni na kisha aliwasogelea wanawake wake na kuwaambia juu ya hali inayoendelea nchini Tanzania hivyo anapanga kuondoka.
Kwasababu walikuwa ni waelewa hawakumzuia Roma na dakika hio hio alianza safari kurejea nchini Tanzania.
Ulaya na Tanzania masaa yalipishana kidogo sana hivyo Roma alifika wakati wa usiku pia ndani ya jiji la Iringa na wakati wa kutua tu aliweza kuona kuna wageni wamekaa katika sebule ya wageni ndani ya nyumba hio , walikuwa wawili na wote ni Wachina.
Moja kati yao alikuwa akimjua na mwingine hakuwa akimjua lakini alionekana kuwa handsome mno , ilikuwa ni kama vile sio mchina na alikuwa katike levo ya maji ya kawaida.
“Naona Mjumbe umeimarika kuliko mara ya mwisho tulivyoonana”Aliongea Roma akimlenga mjumbe wa Hongmeng mpenda rushwa.
“Haha… sipo hapa kwa ajili ya kukumbushia namna tulivyoonana mara ya mwisho nimemleta balozi”Aliongea na kisha alimpa ishara balozi Xuan Jizi.
“Wewe ndio Roma Ramoni ulietibua hali ya hewa katika miliki ya Kekexil na Xia?”Aliuliza yule bwana bila hata ya salamu , alionekana kuwa na hali ya ujeuri hivi.
“Ndio umekuja kote huku kwa ajili ya kuuliza ujinga?”
“Acha maneno yako makali , hivi unajua upo kwenye matatizo?”
“Nielimishe”
“Nikuelimishe nini? , unadhani kuna hata haja ya kufanya hivyo , unajua mwenyewe namna ambavyo umekasirisha majini kutoka miliki ya Xia na Kekexil , ukaenda mbali na kuchokoza miliki ya Braki , nguvu iliokuwa nyuma ya familia ya Sharif , unaonekana kabisa unaogopa ndio maana ukaikimbiza familia yako nje ya nchi”
“Umongea sana lakini sijui kilichokuleta ni nini?”
“Nipo hapa kwa ajili ya kupitisha maagizo niliopewa na wakuu wa miliki ya Hongmeng, wasimamizi wakuu wa sheria ya the gods treaty , ili kuongezea nguvu utulivu wa dunia na kukuzuia kupigana na miliki za kijini na kusumbua raia , Hongmeng kwasasa itakuwa ndio kimbilio lako licha ya kwamba kutakuwa na mashariti, ukikukubali hakuna miliki yoyote ambayo itakugusa”
“Roma usishangilie bado kuna masharti”Aliongea yule mjumbe na Xuan jizi aliendeea.
“Umekiuka sheria nyingi sana na kutumia uwezo wako vibaya na kuua wajumbe ambao waliagizwa kuja duniani kutimiza majukumu yao , lakini licha ya hivyo Hongmeng hawataki kulipiza kisasi na wameaua kukusamehe ili mradi tu kwa hiari yako utoe mbinu yako ya mafunzo , vidonge na Dhana ya Chaos cauldron na baada ya hapo sisi tutakupatia ulinzi”Aliongea akiwa siriasi na kumfanya Roma kuangua kicheko.
“Unacheka nini?”
“Wewe Mzee Jizi, lazima kwenye kwenye kichwa chako kuna nati zimechomoka au hao Hongmeng hawajui nini kinaendeea , nadhani napaswa kuwafafanulia kwa sentensi rahisi”
“Acha kunitukana … tunazo taarifa umeiba hazina yote ya Kekexil na Xia na unazo Dhana na vidonge kedekede , hivi unadhani vitu vya thamani kama hivyo utaweza kuvilinda peke yako, hivyo acha ukiburi na sikiliza tunachokuambia”
“Vipi kama nikikataa mtanifanya nin?”
“Roma acha kujifanyisha kijogoo , sekunde ambayo nitakuripoti katika miliki ya Hongmeng basi ndio utakuwa mwisho wako kwani utakuwa ni adui namba moja wa Hongmeng”
Roma aliwaza na kujiambia tokea siku anajua uwepo wa Hongmeng ndio uadui wao ulipoanzia hivyo hana mpango wa kuwasikiliza kwa chochote , kwanza kabisa alikuwa na deni kwa Zenzhei kumsaidia kulipa kisasi na tokea siku waagane ni kama Zenzhei katika ulimwengu huo wa kijini alikuwa akimsubiria.
Roma bila ya kujiuliza mara mbili mbili aliita nguvu ya Cauldon bila ya kukitoa nje na kuingiza katika mwili wa Xuan Jizi na kuanza kunyonya nguvu zake za kijini na nguvu ya Cauldron ilikuwa kubwa mno na ndani ya dakika chache tu alikuwa ashapoteza uwezo wake wote na kubakia binadamu wa kawaida.
Xuan Jizi hakuwa jini kama jini wa Hongmeng , alikuwa ni binadamu tu ambaye alikuwa na mafunzo ya kijini hivyo ilikuwa rahisi kwa Roma kudili nae kwani alikuwa ndio kwanza yupo katika levo ya maji ya kawaida.
Hakuna ambaye alitegemea Roma kuchukua maamuzi kama yale , lakini kwa Roma alitaka kuonekana kuwa siriasi na kutangaza vita vyake rasmi na Hongmeng kabisa na ili kuonekana yupo siriasi alitaka kwanza kumuadabisha balozi wao.
Mjumbe wa Hongmeng aliebakia ndio alipewa jukumu la kurudi Hongmeng na kutoa taarifa ya kile kilichotokea,
“Rudi ujinini na toa taarifa hizi , kama hao majini wanataka Dhana zangu , vidonge vyangu na mbinu yangu ya mafunzo basi waje huku nilipo wavichukue kwa nguvu kama nilivyofanya katika miliki ya Kekexil,likija swala la watu wenye nguvu kama haina haja ya kutii sheria za ulimwengu bali sheria ya msituni ndio itumike , atakae weza kuishi mpaka mwisho huyo ndio mtawala”
Baada ya kusema hivyo Roma alimbeba mzobemzobe yule Xuan Jizi na kisha kumtupia mbele ya walinzi akiwaagiza kwenda kumtupia mtaani huko kwani ashakua ni wa kawaida.
Alijua asingeweza tena kurudi Hongmeng kwani miliki hio haichukui majini wadhaifu kama yeye.
“Vipi kila kitu kimemalizika?”Aliuliza Afande Kweka mara baada ya Roma kuingia katika sebule ya kawaida na Roma aliishia kutingisha kichwa tu akiitikia amemaliza.
“Unajisababisha matatizo zaidi na zaidi juka uchao kulikuwa na haja gani ya kumuondolea nguvu zake za kijini?”Aliongea Afande Kweka bila ya kubadilisha muonekano wake , yaani hakuwa na furaha wala hakuwa na huzuni na hata usingizi hakuwa nao licha ya kwamba muda ulikuwa umeenda.
“Babu hicho ndio kitu pekee ambacho unaweza kuongea”
“Unadhani ni kipi ambacho naweza kuongea , mwenyewe nipo najiuliza mambo ambayo yanaendelea katika hii dunia, nina hasira nyanya zangu zote zimekauka kutokana na baridi kali , hii baridi sijawahi kuiona na uzee wangu huu”Aliongea na kumfanya Roma amuone huyu mzee anaonekana kuficha mambo mengi na kila anachoongea ni kama anamwigizia lakini hakutaka kumhoji sana.
Huo ndio ulikuwa ukweli ugomvi wa Roma na majini ulikuwa ni wa kutisha lakini ulikuwa haukwepeki lakini kubwa zaidi ni kwamba Mzee huyo alitamani sana Roma kwenda kuwashambulia Hongmeng ili kulipa fadhila za Zenzhei kwa kumlinda kwa miaka mingi, ukiachana na hilo lakini pia Afande Kweka ni mwanachama wa umoja wa Ant- illuminat na ni juzi tu hapo alikuwa na kikao cha siri na baadhi ya wanachama na alikuwa akijua Edna ndio mkuu wake.
Yani kwa lugha nyepesi ni kwamba Edna ni mkuu mbele ya Afande Kweka lakinin mzee huyo licha ya kujua hayo yote hakuwa tayari kumwambia Roma kwani alijua itafikia siku yeye mwenyewe atakuja kujua ukweli na hata hivyo sheria za umoja huo hazikumpa ruhusa ya kuongea chochote kwani ingeharibu kabisa mipango inayoendelea.
“Babu nadhanni baada ya Hongmeng kupokea ujumbe wangu sitoweza kuendelea kuishi hapa Tanzania kwa muda , unaonaje na wewe ukielekea visiwani kwa muda , unaweza kuondoka na baadhi ya watu wako wa karibu pia”
“Unataka nitoke hapa Tanzania kwenda wapi na kwanini?”
“Si kila kitu kipo wazi mzee , sitaki waje wakukamate na kutaka kunitishia uhai wako kama chambo cha kunikamata”
“Mimi nipo nje ya maswala yote ambayo yanahusiana na maadui zako na sio kwangu tu hata kwa baba yako , kinachoendelea ni vita kati yako na majini na hayahusiani na ukoo wetu hivyo pambana kivyako”
“Unaongea tu lakini wanaweza wakapania sana na kutumia njia yoyote ile”
“Hata iweje nasema hapa siondoki “Aliongea kibishi.
“Kwannini sasa , huu sio muda wa kuonekana shujaa mzee”
“Mimi ni mzee wa taifa hili lakini pia mkuu wa familia ya Kweka , siwezi kuondoka na kwenda mahali pengine nje ya Tanzania, unaweza kutafuta chumba ulale , muda umeenda naenda kupumzika”Aliongea na kisha aligeuza na kuingia chumbani kwake.
Roma alikuwa na usingizi na wakati akiwaza kwenda katika chumba cha wageni kwa ajili ya kulala simu yake ilianza kuita mlio wa kuingia meseji na alipoangalia ilikuwa imetokea kwa Tannya.
“Master kuna kundi la majini wamefika na wanakuulizia hapa Bagamoyo”Ujumbe wa meseji ulisomeka hivyo.
“Naona hatimae wamejitokeza licha ya kwamba ni kwa kuchelewa kama nilivyotegemea lakini ni bora wamekuja kabla sijarejea katika ulimwengu wa majini watu”Aliwaza Roma
Sasa mara baada ya Roma kuona kwamba nguvu ambayo ipo nyuma ya familia ya mzee Sharif imejitokeza hakutaka kupoteza muda kabisa na shauku ya kutaka kujua Braki ni majini wa namna gani ilimvaa.
Roma mara baada ya kuondoka ndani ya eneo la Iringa dakika chache tu aliweza kufika mkoa wa Pwani katika makazi ya Sharif na aliweza kumuona Tannya akiwa amesima katikati ya ukumbi wa mikutano , ilikuwa ni eneo ambao hutumika kupokelea wageni mara nyingi.
Mbele yake kulikuwa na wanachama wa familia ya Sharif na mara baada ya kuwachunguza kwa umakini Roma aligundua hawakuwa wa kawaida wote walionekana kama waarabu hivi na hajawahi kuwaoana na walikuwa na nguvu za kijini.
Tannya tokea muda tu alikuwa amebadilisha wafanyakazi wote wa Sharif na kuweka wa kwake , ijapokuwa alikuwa mjapani lakini alikuwa mjuzi sana katika kuigiza na tokea siku ambayo amefika na kujifanyisha ni Maimuna hakuwahi kuonyesha dosari yoyote na hata ibada alikuwa akiongoza.
Roma kwa kutumia jani lake la upofu aliishia kujificha juu ya jengo hilo huku akihakikisha anasikia kinachoendelea kwa kutumia uwezo wake na majini hao hakuna hata mmoja ambaye aliweza kugundua uwepo wake.
Kulikuwa na majini jumla saba, wote walikuwa wamevalia kanzu kwa upande wa wanaume na wanawake wenyewe walikuwa wamevalia Abaya nyeusi , karibia wote walikuwa na muonekano wa ki utu uzima.
Kati yao mmoja tu ndio ambaye alikuwa na uwezo wa juu wa mafunzo ya kijini kwani alikuwa mwanzoni mwa maji ya kiroho. Na wengine wote walikuwa katika levo za maji ya barafu kushuka mpaka moto wa njano.
“Wewe ndio kiongozi wa familia ya Sharif katika ulimwengu huu unaefahamika kwa jina la Maimuna si ndio?”Mwanaume ambaye alikuwa na muonekano wa kizee alimuuliza Tannya , alikuwa na nywele nyeupe na ndevu nyeupe kama vile ni Nandra Modi waziri mkuu wa India na ndio ambaye alikuwa na uwezo wa juu wa kijini.
“Ndio , kwasasa mimi ndio nililazimika kuwa kiongozi , hivyo sina uhakika namna ya kuwaita kwani siwafahamu”Aliongea Tannya aliekuwa katika sura ya Maimuna.
“Hakuna shida kwani hata babu yako Sharif hana uwezo wa kututambua,kwa majina nafahamika kama Zando , nikiwa mwanachama kutoka makao makuu ya miliki , hapa kuna mzee Nuli na Yejini pamoja na majini wanne unao waona , tumekuja hapa kujua ni kipi kinachoendelea kwasababu hatukuweza kusikia habari zozote kuhusu mwizi alieiba hazina yetu , taarifa za kubadilika kwa kiongozi wa familia na imani ni zaidi ya matarajio yetu”












SEHEMU YA 739.
Katika moyo wake Tannya ukweli hakuwa akijua namna ya kujibu, ijapokuwa alikuwa akijua muda kama huo ungewadia lakini ndio mara yake ya kwanza kukutana na majini wa namna hio na angalau ni kwamba alikuwa tayari ashamtumia Roma ujumbe wa meseji.
Tannya simu yake ilitoa mnguruo mara baada ya kutaka kujibu na mara baada ya kuangalia aliona Roma alikuwa ametuma ujumbe kwa lugha ya kijapani.
“Tafuta njia yoyote upate taarifa zinazohusiana na wanakotokea na historia yao kwa ujumla”Aliongea Roma katika ujumbe huo.
Roma alitumia kijapani kwa kuamini ingekuwa ngumu kwao kuelewa kile alichokuwa ameandika.
Tannya mara baada ya kujua Roma ashafika hali ya kujiamini iliongezeka kidogo na palepale aliomba radhi
“Naombeni mniwie radhi wakubwa zangu, nilitamani pia kutoa taarifa kuja makao makuu lakini kwa bahati mbaya babu , walinzi na wengine walikufa vifo vya haraka sana na sikujua namna ya kuwasiliana na nyie hivyo…”
“Haina haja ya kujilaumu , hata sisi pia tunaelewa namna ilivyo ngumu kuwasiliana na sisi , umefanikisha kuongoza familia ndani ya muda mfupi na kuendeleza ibada taarifa hizi zikimfikia mkuu wetu atafurahi”Aliongea.
“Tafadhari naomba mniwie radhi kama nitavuka mpaka , lakini je mnaweza kunielezea historia yote ya familia pamoja na imani yake , ili mimi Maimuna niweze kuwa na uelewa mzuri na kufanya vizuri kwa ajili ya manufaa ya miliki kwa ujumla”
“Kwasababu umekuwa kiongozi pekee uliebakia basi ki asili umekidhi vigezo vya kujua historia yote ya Kibraki , Babu yako Sharif ana uelewa mdogo sana kuhusu jamii ya majini wa Braki pengine amewahi kusikia hili jina mara moja au mara mbili tu , lakini kutokana na mabadiliko ya hali na matukio ya kutotarajia hapa duniani makao makuu wameona ni sahihi familia za binadamu zinazotuwakilisha hapa duniani kujua uhalisia wa historia yetu na imani yote kwa ujumla, hivyo nitakuelezea kila kitu”
Roma ambaye alikuwa akipiga chabo alijikuta akifurahi mara baada ya kusikia kauli hio kwani hakutegemea jini aliefahamika kwa jina la Zando angeweka wazi kuhusu nguvu iliokuwa nyuma ya familia ya Sharif.
*****
Miaka elfu hamsini iliopita dunia iliingia katika hatua nyingine kubwa katika ustaarabu.
Wakati huu pia upande wa majini walikuwepo pia na wengi wao walikuwa katika levo za juu sana pengine levo ambayo haijawahi kufikiwa katika nyakati za sasa.
Kipindi hiki ni kabla ya miungu kufika katika sayari ya Dunia na ndio kipindi ambacho majini wengi walianza kupotea katika uso wa dunia na kuwaacha binadamu na baadhi ya majini watu.
Majini ni vumbe ambavyo vipo vya aina nyingi sana na tabia tofauti , ni kama ilivyo kwa makabila ya kibinadamu basi ndio ilivyo kwa majini hivyo hivyo.
Sasa kati ya majini wa enzi hizo ambao walikuwa na nguvu kubwa katika uso wa dunia ni majini pepo na hawa majini pepo wenyewe walikuwa wamegawanyika katika aina nyingi sana.
Inasemekana katika kipindi hichi majini walikuwa wengi kuliko hata idadi ya binadamu kutokana na spidi yao ya kuzaliana.
Kati ya majini pepo ambao waliweza kufahamika enzi hizo ni kama vile Mbweha na Majoka ambao ndio walikuwa na uwezo mkubwa sana .
Majinii jamii ya Mbweha walikuwa ndio wenye busara kubwa na mbinu nyingi za kimaajabu tofauti hata na majini Joka ambao walikuwa wamezaliwa na nguvu za kimwili sana sana.
Ukiachana na majini hao lakini pia majini watu hawakuwa nyuma pia kwani wengi wao walikuwa katika levo za juu kwa kuweza hata kudhibiti radi na ilikuwa ni kawaida kwa majini watu kuweza kumiliki Dhana za hali ya juu kabisa na shida ilikuwa tu kwamba licha ya uwezo wao hawakuweza kupata mbinu ambayo inaweza kuwainua zaidi na zaidi.
Hawa majini watu ndio ambao walipenda kuwa wa wazi kabisa na waliweza kuishi katikati ya binadamu wa kawaida tofauti na majini pepo ambao walikuwa ni hatari kabisa kwa binadamu.
Majini pepo waliishi katika maumbo yao ya kawaida pasipo ya kubadilika na ukweli ni kwamba walikuwa wakitisha sana na hali hio ki ufupi ni kwamba hawakuipenda na hii iliongeza chuki yao zidi ya binadamu na majini watu.
Lakini mwishowe walijitahidi kutafuta namna ya kuboresha muonekano wao ndipo walipokuja kugundua mbinu mbadala ambayo ilikuwa ni kuamsha pepo wao wa ndani tofauti na kuwazimisha au kuwakata kama ilivyokuwa kwa majiini watu ,hapo sasa ndio ikazaliwa majini halisi ambao walikuwa na nguvu za kijini, majini ambao walikuwa na uwezo wa kupaa.
Sasa kutokana na kuwa na maumbo yenye nguvu kubwa pamoja na kumiliki nguvu za kijini pamoja na kuwa wengi walikuja kuwa tishio kubwa kwa jamii nyingine za kijini na binadamu wa kawaida kiasi cha kupelekea kuibuka kwa vita ambayo majini watu waliungana na binadau kuwashambulia Majoka.
Sasa kati ya majini pepo wakaja kuibuka jamii nyingine kati ambao walijiita mashetani pepo wa anga , hawa ndio walikuwa wabaya zaidi kwani walikuwa na uwezo wa kumuingia binadamu na kumfanya afanye kila anachotaka huku wale majini pepo wengine wakichinja binadamu na kunywa damu yao.
Binadamu alionekana kuingia katika hatari na kuanza vita na viumbe hawa majini ,vita ambayo ilidumu kwa muda mrefu sana takribani miaka mia moja na siku moja tu ilitokea majini pepo wengi katika ulimwengu wa kawaida kuanza kupotea ikiwemo Mbweha na Majoka.
Kupotea kwao baadae ilikuja kujulikana walikuwa wakivutwa katika ulimwengu mwingine kwa kutumia aina ya mitego ambayo ilikuwa imewekwa mfano wa mnara ambao Roma aliingia.
Ni asilimia chache tu ya majini pepo ambao walibakia na kati yao hawakuwa hata na uwezo mkubwa na hapo ndipo majini watu wa enzi hizo walipoona hakuna haja ya kuwaua bali kwenda kuwafungia katika ulimwengu Tenganifu wa jangwa.
Kitendo cha mashetani pepo wa anga, Majoka na Mbweha kufungiwa katika ulimwengu wa Jangwa Tenganifu kwa muda mrefu iliwafanya kuchukulia hapo kama makazi yao rasmi.
Mara baada ya kuwasili kwa miungu katika uso wa dunia ndipo ilipoibuka vita kati ya majini watu yaani Hongmeng na jamii nyingine za kijini , vita ambayo ilidumu muda mrefu sana mpaka Zeus na Athena kushindwa vita na kuzaliwa kwa the Gods treaty.
Mpaka vita hio inakuja kufikia mwisho majini pepo ambao walikuwa katika ulimwengu wa jangwa tenganifu walikuja kugundua miliki za majini watu walikuwa wamepungukiwa nguvu sana kutokana na kupigana vita na miungu na wengi wao kuuliwa na hapo ndipo walipoona ni fursa adhimu ya kujiendeleza wao wenyewe kutokana na kipindi hicho majini watu kutokuwa nao makinu.
Mbinu pekee ambayo iliwafanikisha kujiendeleza ni kufanya ushirikiano wa kiimani na binadamu wa ulimwengu wa kawaida taratibu taratibu kwa namna ambayo waliweza wao na mwisho wa siku wakajikuta wanakuwa na nguvu kubwa kwani walijipatia mali asili nyingi kutoka Duniani na kuziingiza katika ulimwengu wao huku wakibadilishana na binadamu madini mengi ya thamani.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba majini pepo wengi ikiwemo majoka na Mbweha ambao walikuwa na uwezo mkubwa walimezwa katika ulimwengu wa majini pepo kwa njia ambazo mpaka siku hio hawakuelewa imetokeaje , huku upande wa majini watu , yaani majini wa kawaida ambao mbinu zao sio kuamsha mapepo wao walijitenga na binadamu wa kawaida mara baada ya kugundua Dimension nyingine na kuanzia hapo kila majini wakajitegemea na kukawa na ulimwengu wa majini watu , ulimwengu wa majini pepo na ulimwengu wa Jangwa Tenganifu sehemu ambayo hupatikana miliki moja tu ya kijini ambayo hufahamika kwa jina la Braki.
Kwa historia hio ilimaanisha kwamba hapo zama za kale majini na binadamu waliishi katika ulimwengu mmoja kabla ya vita kutokea, vita ambayo mpaka wakati huo majini wote wanajiuliza ilimalizwa na nani kwani sio wao ambao waliwafanya majini pepo wenye nguvu kuvutwa kwenye ulimwengu mwingine.
Sasa kati ya majini pepo hao ambao walivutwa ni kama vile Aoiline Mbweha wa mikia tisa , Majoka na mashetani pepo wa anga.
Roma mara baada ya kusikia habari hio aliishia kushangaa , katika ulimwengu wa majini pepo Zimo alisema ulimwengu wao ulikuwa ni wa miaka mingi kuliko hata Hongmeng na hio ilimaanisha kwamba kabla ya kumezwa ulimwengu huo ulikuwepo.
Sasa Roma mara baada ya historia hio anajua nguvu ambayo ipo nyuma ya familia ya Sharif ni majini pepo na ni sawa na kusema ni ndugu wa Aoiline.
Kulinganana msaada ambao Aoiline alimfanyia na wengine Roma aliona ni dhambi kama ataingamiza miliki hio ya Braki ambayo inapatikana katika Ulimwengu wa Jangwa na anachopaswa ni kujaribu kufanya urafiki nao lakini kabla ya yote lazima ajue hazina yao ilikuwa ikimaanisha nini.
“Asante sana kwa kunielezea haya”
“Hivyo licha ya familia ya Sharf kuumiza watu wengi katika ulimwengu huu wa kawaida lakini kwa upande wetu sio jambo kubwa sana na sio maagizo yetu , Sisi sio kama majini kutoka Hongmeng na miliki nyingine ambao wanachotaka ni umaarufu tu , sisi leo tumetoka kuja katika ulimwengu wa kawaida kwasababu ya muovu Roma Ramoni ambae ameiba hazina yetu”
“Je naweza kuuliza, Hazina hio ina matumizi gani , je kutakuwa na athari zozote kama isipokuwa kwenye mikono yetu?”Aliuliza Maiuna feki na hapo ndipo Roma alipokuwa akitaka kujua ile kokoto ina maana gani.
ITAENDELEA ,WATSAPP 0687151346
Hatari
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.

MTUNZI:SINGANO JR

Mono no aware.

SEHEMU YA 745.
Kama kawaida yake Poseidon alijitokeza akiwa amevalia mavazi ya ki’upishi ,ijapokuwa nywele zake hazikuwa zimejichana vizuri pamoja na kuwa na masharubu mengi lakini alionekana kama mtawala.
“Hmmp! , nilikuwa bize mwenyewe kutengeneza radha mpya ya supu ya samaki ,kama msingetumia bahari yangu ningewaacha muondoke hapa mkiwa hai”Aliongea Poseidon mungu wa bahari .
“Tafadhari , tafadhari bwana Poseidon hatujatumia nguvu zetu zote hapa”Aliongea Apollo kwa dharau.
“Ni nusu ya nguvu zetu ambazo zimeturudia mpaka sasa , hivyo najua mwisho wako vizuri acha majigambo”Aliongea
Kwa namna ambavo walikuwa wakiongeleshana ilionekana kama vile hawakuwa wakijali majini hao , yaani ilikuwa ni kama vile tayari ni wafu kwenye macho yao.
Lakini upande wa Chaopi na wengine waliweza kugundua mtu aliesababisha mlima huo wa maji ni Poseidon mungu wa bahari., mbaya zaidi sasa ilionekana miungu hao walikuwa na nusu tu ya nguvu zao.
“Inawezekana vipi hii na wanamaanisha nini kusema kurudiwa na nguvu kidogo tu, kama Apollo na Artemis ndio wana uwezo wao nusu na wanatupelekesha hivi inamaana wakirudiwa na uwezo wao wote watakua juu zaidi kuliko yeye?”Aliwaza Chaopi.
Sasa walishajua Poseidon alikuwa na nguvu kubwa kuliko ya Apollo na Artemis na kama hawatokimbia basi watageuzwa maiti muda huo.
“Kimbieni , kimbieni wotee”Aliongea Chaopi kwa nguvu na alikuwa ndio wa kwanza kukimbia huku nguvu ya siraha yake ikiwa imemfunika alielekea upande wa Kaskazini mashariki.
Baadhi ya majini walifuatia na kufanya kila namna kupita katika ukuta wa maji unaochemka angani lakini unadhani Poseidon angewaacha wakimbie kabla ya kuua wakati kaacha shughuli yake ya upishi na kuja mpaka hapo.
“Kwa jina la mungu wa bahari nakuitwa ewe Abisi Majoka wa bahari”Aliongea Poseidon.
Kitendo cha kuinua tu mkono , makumi ya majoka yaliokuwa katika maumbo ya kisamaki yaliibuka kutoka baharini , majoka hayo yalikuwa yakisafirishwa na Poseidon kwa kutumia kanuni za anga na kufanya yaonekane kama vile ni makombora.
Majini hao mara baada ya kuona tukio lile walijitahidi kujilinda kwa kujaribu kushambulia kwa kutumia Dhana zao na nguvu zao za kijini lakini walichoweza kufanya ni kujikusanya sehemu moja ili kushambulia lakini wakati huo mlima wa maji uliotengenezwa kwa kutmia kanuni za anga na Poseidon ulikuwa ukizidi kupanda hewani na kukaribia kuwafunika na kuwafanya washindwe kukimbia.
Chaopi mara baada ya kukutana na ule mlima wa maji ambao ulikuwa ukimzuia kama ukuta aliweza kupokea mishale mfululizo kutoka kwa Artemis na Apollo.
“Ndio mnajaribu kukimbia sio ngoja tuwaonyeshe”
Ilikuwa ni mfuatano wa mashambulizi wa nishati za ajabu zilizoanza kuwashambulia wale majini kwa mfululizo , mlindimo wa mishale ilikuwa mingi na kufanya washindwe kupambana na kitu kimoja kwa wakati kwani Majoka walikuwa wakiwashambulia lakini wakati huo huo na Artemis na Apollo walikuwa wakifanya mashambulizi.
Ndani ya sekunde tu walijikuta wote wakiwa ndani ya mtego wa viumbe hao kutoka sayari nyingine.
“Imetuchukua zaidi ya karne kuweza kufikisha uwezo wetu katika levo hizi , haiwwezekani tupotee kirahisi hivi”Wote waliwaza na palepale waliamua kutumia kila mbinu kwa ajili ya kuchepuka katika mtego hata kama ilimaanisha kupata majeraha.
Kwa muda huo ilikuwa sasa ni vita ya miungu mitatu pamoja na majini wote , ijapokuwa walikuwa ndani ya mtego wa miungu hao lakini hawakuwa wameshindwa pambano.
Wakati Chaopi , Anjiu na Gefu wakipambana na Apollo na Artemis majini wengine walikuwa wakipambana na Poseidon.
Bila shaka walikuwa wakijua miungu wengine lazima watakuwa washagundua kinachoendelea na hawakujitokeza kwa kuamini kwamba hao watatu peke wanatosha , lakini ilikuwa ni swala la muda tu kwa wao kujitokeza pia hivyo walichotaka ni kuondoka hapo haraka iwezekanayo , hawakuwa na ile haja tena ya kutaka kumuangamiza Roma au kuua wanawake wake , walichokuwa wakitaka ni kukimbia na kurudi katika ulimwengu wao.
Kubwa zaidi ambalo walihofia Roma anaweza kujitokeza na ingekuwa ni hatari zaidi na zaidi.
Upande mwingine wakati vita hio ikiendelea , warembo wa Roma walikuwa wamejikusanya katika makazi ya Bi Wema na Sui.
Waliwaza kwenda kujificha sehemu nyingine lakini waliona itakuwa ni hatari na kuamini pengine majini hao wanaweza kuwazuia kutokana na uwezo wao kuwa wa chini na jini yoyote ambaye alikuwa levo ya kuipita Dhiki angeweza kuwahimili wote.
Lakini sio hivyo tu waliamini kama watajificha wanaweza kuwa mzigo kwa wakazi wa kisiwa hicho ndio maana walikosa chaguo lingine zaidi ya kukaa ndani ya kisiwa hicho wakitegemea miungu watu kushinda.
Sasa mara baada ya kuona majini wanakaribia kushindwa pambano hatimae walijihisi kuwa na ahueni.
Wale ambao walikuwa tayari katika levo ya Nafsi kama vile Rose , Magdalena m Amina na wengine hawakuweza kukaa ndani hivyo walibakia nje wakiangalia pambano.
Upande wa Clark yeye alikuwa amekwisha kurudi katika maabara yake kutafuta namna ya kuwasiliana na Roma.
Sasa katika wakati kama huo wa hatari warembo hao wote walikaa katika mkao wa tahadhari.
“Sister Rose unaamnini Hubby anaweza kurudi ndani ya muda , maadui zetu wana nguvu mno sidhani kama miungu wanaweza kuwashinda”aliongea Amina.
“Ni ngumu kujua , kama Clark atashindwa kuwasiliana nae sidhani kama atarudi mapema”
“Hatuna faida kabisa , ndio maana mpenzi wetu haturuhusu kwenda ulimwengu wa majini”Aliongea Yezi.
Kila mtu alikuwa na hali ya wasiwasi na walijua ni kwa namna gani hawana mchango wakati wa vita kama hio na ni wakati ambao waliweza sasa kujua ni kwa namna gani Roma alikuwa na nguvu mpaka kufanikisha kumuokoa Rufi na Sui kutoka katika ulimwengu wa majini yeye peke yake.
Wakati huo huo wakiwaza mlango ulifunguliwa na msichana mdogo alitoka ndani akiwa ameshikilia paja la kuku katika mikono yake huku midomo yake ikiwa imechafuka kwa mafuta , alikuwa ni Lanlan.
Kibonge huyo aliwapita mashangazi zake na kwenda kusimama mbele kabisa na kuangalia angani akiwa na furaha.
“Wow! So pretty”Aliongea huku akiruka ruka kwa furaha na kung’ata kipande cha nyama kutoka kwenye paja la kuku.
“Lanlan rudi ndani haraka”Bi Wema alichomoka kutokea ndani akiwa na wasiwasi akimpigia kelele Lanlan.
“Hapana shangazi zangu wote wapo nje wakiangalia , hata mimi pia nataka kuangalia”Aliongea huku akitingisha mabega.
Bi Wema alimsogelea na kisha akamfuta midomo kwanza na kisha alimshika mkono akitaka kumrudisha ndani kwa nguvu.
“Utasababisha matatizo tu, rudi ndani la sivyo mama yako atakasirika”
Lanlan aliishia kubidua midomo huku akiangalia juu angani kwa namna ambayo alipenda kuendelea kuangalia kwa muda mrefu.
Mwanzoni wanawake hao walishangazwa na muonekano wake kwani pengine ilikuwa ni kawaida kwa mtoto wa kawaida kuogopa kile kinachoendelea lakini kwa Lanlan hakuwa na woga wa aina yoyote ile, alikuwa amerithi kila kitu kutoka kwa baba yake kwa kutokuwa na woga kabisa lakini sasa ndani ya sekunde tu tabasamu zao zote zilizima.
Ilikuwa ni kufumba na kufumbua vivuli vya watu viliibukia mbele yao kutokea upande wa msitu na mwanaume ambaye alikuwa ni wa makamo alimsogelea Lanlan na kumshika kiuno na kumbeba kwa nguvu juu juu.
“Lanlanii…”Bi Wema aliishia kupita kelele lakini dakika ileile kwa spidi ya hali ya juu alishikiliwa shingo na mwanaume mwingine ambaye alikuwa ni jini.
Kila kitu kilitokea kwa spidi sana , yaani ni ndani ya seukunde tatu Lanlan na Bi Wema walikuwa tayari washakamatwa na majini na Rose na wenzake waliweza kujua majini wale walikuwa na nguvu kubwa kuliko wao.
“Nyie ni wakina nani?”Rose aliongea lakini ndani ya dakika hio hilo waliongezeka majini watatu wengine na kufikia watano .
Majini hao walikuwa ni Mohi mkuu namba tatu wa miliki a Kekexil , Mohena baba yake Rufi na majini watatu kutokea miliki ya Xia.
Kitendo cha Roma kutojitokeza kwa muda mrefu walijua lazima hayupo kisiwani hapo na ndio maana walichukuana na kuja mpaka kisiwani wakati wengine wakiendeleza mapambano juu angani na kwa kutumia uwezo wao waliweza kupata eneo ambalo warembo hao wamejificha.
Mpango ulikuwa ni kuiteka familia ya Roma na kuwashurutisha miungu kuzuia mashambulizi.
Walipata wazo hilo kutokana na kwamba kwanza hao ndio walikuwa na uwezo wa chini kidogo, hivyo hata kuondoka kwao kusingeshitukiwa na miungu.
Sasa mara baada ya kujitokeza mbele yao na kumuona Lanlan moja kwa moja waliamini lazima atakuwa ni mtoto wa Roma kutokana na kuwa na nguvu za kijini na rangi yake ya kiafrika.
“Haha.. haina haja ya kutufahamu , haja yetu ni kwamba tunahitaji kuwakamata watu wote ambao wana uhusiano na Roma”Aliongea Mohi na kufanya wanawake hao kuingiwa na ubaridi wa woga.
Lanlan hakujua hata alivyokamatwa na alikuja kugundua tayari nyama yake ilikuwa ishadondoka chini na machozi yalianza kumtoka , hakulia kwasababu alikuwa amekamatwa bali uchungu wa nyama yake kudondoka.
“Mtu mbaya niachie… paja langu , paja langu ,. Nyie watu ni wabaya na baba atawapiga”Alitoa kilio.
“Kimya!!!” Mohi ambaye alikuwa na hasira alimsogelea Lanlan na alimpiga kibao cha shavuni.
Ijapokuwa hakutumia nguvu za kijini lakini kibao hiko kilimfanya Lanlan kuvimba shavu.
“Tayari unatoa msisimko wa nishati ya mbingu na ardhi katika umri mdogo hivyo , lazima utakuwa mtoto wa Shetani Roma Ramoni, tumekamata mtu sahihi”Aliongea Mohena mara baada ya kumkagua Lanlan.
“Pumbavu zako wewe , unathubutu vipi kumpiga Lanlan kwa mfano”
Mage mara baada ya kuona Lanlan akilambwa kibao tayari alishindwa kujizuia na palepale aligeuza nguvu zake na kutengeneza moto wake mweupe.
“Mage hapana , sio saizi yako”Magdalena alitaka kumzuia pacha wake lakini Mage hakutaka kuogopa tena na alimrushia shambulizi jini Mohi lakini kwa Mohi ni kama vile anacheza na mtoto kwani hakutumia nguvu nyingi kusambaratisha shambulizi lile lakini wakati huo huo alimpiga Mage na wimbi la nguvu za kijini na kumrusha juu na alipokuja kutua chini alikuwa akitema damu na bahati nzuri Magdalena alifanikiwa kumdaka.
“Nimeshangazwa na uwezo wako wa kudhalisha ‘Heartflame’ lakini nishati yako ni dhaifu sana kuifanya iwe na makali, kama ningejua mpo dhaifu namna hii nisingejisumbua kukamata mmoja mmoja bali ningewasweka wote kwa wakati mmoja kujiepushia usumbufu”
Wakati huo Bi Wema alikuwa amemkodolea macho mwanaume mmoja bila ya kukwepesha na kumbukumbu zake zilionekana kurudi nyuma , ijapokuwa mwanaume huyo alikuwa na misharubu lakini alionekana sura yake kuifahamu.
“Wewe ni Mohena!!!”Aliongea Bi Wema , ijapokuwa alikuwa akimjua Mohena kwa jina lingine lakini Rufi alimtajia jina lake halisi.
Muonekano wa Mohena ulibadilika na kuwa wa mshangao kidogo na mara baada ya kumwangalia mwanamke alietaja jina lake alionekana kukumbuka kitu na kutoa kicheko cha kebehi.
“Oh my… Za siku nyingi kipenzi changu Wema?”








SEHEMU YA 746.
Maneno yake yalishangaza lakini ni palapale waliweza kujua nini kinaendelea kwani walikuwa wakiijua historia ya maisha ya Rufi.
Wote walishangazwa mara baada ya kujua huyo ndio ambaye alimdhalisha Bi Wema pasipo ya kujua ni jini na mara baada ya kujifungua akamchukua Rufi na kupotea nae , sasa palepale ndio wanajua majini hao wametokea Kekexil.
“Haha mdogo wangu naona Ex wako nae yupo hapa , nadhani ndio atakuwa amemzaa yule binti yako malaya malaya … mh ila anaonekana hajatumika muda mrefu na bado mrembo , amejua kujitunza”aliongea Mohi kinafiki akimwangalia Bi Wema kwa shauku ya kutaka kujua ni kipi kilichomfanya mdogo wake kutembea na binadamu.
“Mohena , Mohena unathubutu vipi kujitokeza mbele yangu, wewe wanaume ni mkatili sana”Alibweka Bi Wema huku machozi ya hasira yakimtoka.
“Ninaweza kukuacha ukiwa hai kulingana na historia yetu ya kimapenzi”
“Wewe mwanaharamu , nilikuwa kipofu kutokukujua lakini niseme hukustahili mapenzi yangu na kuwa baba kwa binti yangu , niue sasa kama unao huo ujeuri, unanitia kichefu chefu”
“Wema umenikatisha tamaa sana, sijawahi kuwaza kama huna akili namna hii kama binadamu wengine”
“Mnafiki mkubwa wewe..puu!”Aliongea Bi Wema na alimtemea Mohena mate lakini aliyakwepa na muda uleule alimsogelea na alimfinya shingoni na akapoteza fahamu palepale.
Muda ule wale ambao walikuwa ndani ndio waliweza kugundua purukushani ambayo ilikuwa ikiendelea nje na walitoka haraka haraka na Rufi ndio wa kwanza kumuona mama yake ameshikiliwa na Mohena.
“Muachie mama yangu”
Mohi na Mohena mara baada ya kumuona Rufi muonekano wao ulibadilika mara moja.
“Kumbe na huyu ma*ya yupo hapa pia , kwasababu Roma yupo tayari kuingia katika miliki yetu kwa ajili ya kukuokoa nadhani tukikutumia kama mateka tutaweza kutoka hapa salama”aliongea Mohi.
Rufi alijikuta akirudi nyuma mara baada ya kusikia kauli ile na warembo hao walimkingia Rufi kwa mbele huku wakidhamiria kuvuta muda hata kama ilimaanisha wangekufa.
“Magdalena spidi yako ya kukimbia ni kubwa , mtaarifu Apollo kinachoendelea”Aliongea Rose kwa kutumia nguvu za kijini ili wale majini wasisikie.
Magdalena alionekana kumwelewa Rose na kujiandaa kukimbia kwenda angani ili kumpasha habari Apollo na wengine kinachoendelea lakini sasa kabla hajachukua hatua Mohi ni kama amekwisha kugundua mpango wao.
“Ukithubutu kuondoka hapa kwenda kutoa taarifa nitamuua huyo mtoto na mwanamke”
Kauli hio ilimfanya Magdalena kushindwa kuondoka na kuishia kumwangalia Rose kwa huzuni.
“Huna aibu wewe”Aliongea Amina.
“Niwe na aibu nisiwe na aibu ili mradi hii mbinu itafanya kazi sisi hatujali , Roma alivyoingia katika miliki yetu na kutuibia ndio aliekosa aibu”
“Acheni kuongea ujinga , kama mnajua niachieni niwaondolee nguvu zenu na kisha tutawaacha mkiwa hai”Aliongea Mohena na kauli ile iliwafanya warembo hao kuingiwa na woga kiasi cha kuwafanya wapauke sura, mbaya zaidi walijua lazima wangetumika kumfanya Roma aingie kwenye mtego.
Katika hali hio kinzani ndio wakati ambao Edna alitoka ndani akiwa katika hali ya utulivu kabisa na kusogea mbele kabisa na kuwaangalia hao majini kwa macho makali.
“Muachieni binti yangu”
Akiwa amewakodolea macho bila ishara ya utani aliongea kauli ya kibabe,ilikuwa ni kama vile anawaamrisha.
Lanlan alikuwa akijitahidi kujitoa kwenye mikono ya majini hao lakini ilishindikana kwani uwezo wake ulikuwa mdogo.
“Huyu ni binti yako , kama jibu ni ndio basi utakuwa ndio mke wake yule mshenzi , hakikaanajua kuchagua , hawa wanawake wote ni warembo tupu, lakini kwa bahati mbaya kwanzia leo mtakuwa watumwa wetu”Aliongea Mohi huku akionyesha hali ya tamaa kutokana na uzuri wa Edna na alijiambia lazima amtumikishe kingono hawezi kuacha mwanamke mrembo kama huyo hata kama ni binadamu.
Edna mara baada ya kuona majini hao hawana mpango wa kumwachia Lanlan kama alivyoamrisha uso wake ulizidi kuongezeka ukauzu na hali ya hasira iliojaa nia ya kimauaji ilijionyesha katika macho yake.
“Yezi !?”
“Naam Sister…!!”Yezi alishituka marra baada ya Edna kuita jina lake lakini mara baada ya kuitika Edna alimgeukia.
“Niazimishe ule upanga wako”
Kitendo cha Edna kuongea kauli hio iliwafanya wote kumwangalia kwa mshangao lakini mara baada ya kukutanisha macho walijiktua wakihisi ubaridi wa uoga.
Muonekano wa Edna ulikuwa ni wa tofauti kabisa , iliwakumbusha namna ambavyo Roma akiwa na hasira ya kuua.
Yezi akiwa katika hali ya kutetemeka kutokana na muonekano wa Edna aliishia kutoa ule upanga wa Manjushage na kisha akampatia Edna.
Mara baada ya kuushikilia ni kama vile anaukagua makali yake na kisha alitembea kwa kupiga hatua mbele kama vile anazihesabu na kumsogelea Mohi na wenzake.
Hali ya hewa ilikuwa sio ya kawaida kutokana na muonekano wa Edna, Rose na wenzake mara baada ya kugundua Edna anachotaka kufanya wote walikumbwa na hamaki.
“Edna hajafikia hata levo ya nafsi anachokifanya ni kujitafutia kifo”Waliwaza wote kwa wakati mmoja.
“Edna najua una wasiwasi na usalama wa Lanlan lakini huwezi kufa kirahisi namna hio”Nasra alishindwa kuvumilia kile ambacho Edna anataka kufanya na alimkimbilia kwenda kumzuia.
Lakini sasa sekunde tu ile anataka kumshika alimkosa , ilionekana Edna alipiga hatua nyingine ya haraka sana.
Magdalena na yeye kutokana na spidi yake alimkimbilia kwenda kumzuia lakini na yeye alimkosa na kuishia kushika hewa.
Edna alikuwa kama upepo , ijapokuwa alijongea mdogo mdogo lakini kwa hali isiokuwa ya kawaida ilikuwa ngumu kumshika.
Edna hakugeuka na palepale alikuwa tayari alishawafikia Mohi na wenzake.
Mohi macho yake yalisinyaa , ukweli ni kwamba hakuona kitu cha kipekee kutoka kwa Edna lakini aliamua kujihami.
“Bora usisogee la sivyo nitamgeuza binti yako kuwa kiwete”Alionya lakini kwa Edna ni kama vile hajamsikia na alimsogelea jini aliemshikia Lanlan na kilichotokea kiliwafanya wengine wote kuwa katika hali ya mshituko.
Yaani ilikuwa ni kama vile yule jini alikuwa amegandishwa na kuwa sanamu na Edna akamchukua Lanlan bila ya ukinzani wowote ule.
Kitendo cha kumshikilia Lanlan na kumgeuza, Edna alizungusha mkono wake wa kushoto kwa namna ya kimapozi kabisa bila hata ya kutumia nguvu na sekunde hio hio kichwa cha yule jini kilidondoka chini huku damu ikifyatuka kama bomba la Dawasco lililotobolewa.
“Imewezekana vipi hii..?”
Majini wote walijikuta wakipagawa na kilichotokea ikiwa hawaamini macho yao.
Hakuna ambaye aliweza kujua imewezekana vipi kwa mwanamke binadamu ambaye hakuwa hata na nguvu za kijini kubwa kuweza kumfyeka kichwa jini ambaye alikuwa na uwezo wa juu bila hata ya kufanya shambulizi wala kuonyesha ukinzani.
Yaani iliwashangaza kwani hakukuwa na mabadiliko ya presha katika hewa wala mkandamizo wowote ambao ulikuwa ukimtoka Edna.
Rose na wenzake walikuwa katika hali ya mshangao pia, mwanamke mrembo zaidi yao ambae walikuwa wakimwangalia akili zao ziliwaambia kabisa sio Edna wanaemjua pengine ni mtu mwingine.
Ukweli ni kwamba hata Roma ambaye alikuwa na uwezo wa juu hakuwa na uwezo wa kumuua jini ambaye yupo levo ya kuipita dhiki katika kudhibiti barafu kirahisi namna hio.
Edna hakubadilika muonekano wake , ilikuwa ni kama vile hajafanya chochote , aliishia kumkumbatia binti yake na kuangalia mashavu yake kuona kama kuna kidonda cha aina yoyote.
“Nilikuambia usikimbie kimbie lakini husikii , kuwa mtiifu wakati mwingine la sivyo watu wabaya watakupiga , unanisikia?”
Lanlan alitingisha kichwa kukubali lakini muda uleule ni kama sasa hali yake ya kujiamini imerudi na aliinua kidole chake na kumnyooshea jini Mohi.
“Mama yule ndio alinipiga kibao”Lanlan alimsemea Mohi kwa mama yake.
“Najua alikupiga ndio”
Edna hakumuweka chini Lanlan na alimsogelea Mohi kwa kasi , jini Mohi palepale kengele ya tahadhari iligonga, kutokana na mjongeo wa Edna licha ya kwamba alikuwa mwanzoni mwa maji ya kiroho lakini alimuogopa.
Akili yake ilimwambia akimbie lakini alishangaa mara baada ya kuona ni kama vile ameshikiliwa na anga kwani hakuweza hata kutingisha kidole zaidi ya kutetemeka tu.
Dhana alioshikilia Edna ilikuwa ni ya daraja la kati na haikuwa na madhara makubwa kwake kama jini wa levo ya maji ya kiroho lakini alikosa utulivu.
Mkuu namba tatu wa miliki ya Kekexil jasho lilimtoka na alianza kuhema kwa nguvu akijitahidi kuita nguvu za kijini na kujaribu kuongea lakini alishindwa kabisa.
Ni dakika hio hio aliweza kujua ni kwanini jini mwenzake aliweza kufyekwa bila kuonyesha ukinzani , ilionekana kilichomtokea na yeye ndio kinachomtokea na kinakwenda kukamilika kwa kufyekwa kichwa.
Nguvu ambayo ilikuwa imemshikilia alishindwa kuijua kabisa wala kuielezea ilikuwa kwani ya kimaajabbu mno na kwake ni kama vile yupo kwene ndoto.
Aliishia kumwangalia Edna kwa taharuki huku akisubiria kile kinachokwenda kumtokea, ukweli ni kwamba hakujua hata namna alivyokatwa kwani alijihisi tu akihisi kukosa muunganiko wa mwili wake na kichwa na ndio wakati ambao kichwa kilitua chini.
Ndani ya dakika moja Edna alikuwa ashakata vichwa vya majini wawili wenye nguvu bila ya kujichafua wala ule upanga kuchafuka, ikioneysha kwamba mkato wake ulikuwa ni wa kasi mno na nguvu isiokuwa ya kawaida.
Wakati Lanlan akishangilia ushindi wa mama yake kufyeka maadui upande wa michepuko ya Roma vigoti vya miguu yao vilikuwa vikilainika na kutamani kupiga magoti.
“Huyu ni Da’ Edna kweli?”Yezi aliuliza.
“Ni yeye ndio lakini kuna uwezekano akawa sio yeye”Aliongea Magdalena kauli yake ikiwachanganya wenzake.
Edna hakujali maneno yao na aliwagandisha wale majini wote na kisha aliwapitia mmoja mmoja na kuwapitishia upanga shingoni na kilichosikika ni ‘swii.. swii..swiii’ tayari vichwa vyao vilidondokwa kwa wakati mmoja ikidhihirisha spidi yake ilikuwa sio ya kibinadamu.
Aina hio ya vifo ni hakika wakifika mbele ya haki lazima wataishi kwa aibu kubwa mno kwa kufa vifo vya kiabu namna hio, kufa bila ya kuonyesha ukinzani wa namna yoyote ile.
Edna mara baada ya kumaliza kazi alirusha ule upanga mbele ya Yezi na kisha akamuweka chini Lanlan na kujaribu kumuamsha Bi Wema ambaye alikuwa amepoteza fahamu.
Lakini muda huo wenzake ilikuwa ni kama vile wamegandishwak wani walikuwa wamemkodolea macho kama kama vile wanaangalia kiumbe cha ajabu.
“Mbona mnaniangalia hivyo , sidhani kama kuwaua kunaweza kutuletea shida”aliongea Edna akiwa katika hali ya tabasamu.
“Edna uwezo wako…nini kimetokea?”Rose ndio aliekuwa wa kwanza kutoka katika mshituko na Edna alimpa ishara Rufi kumchukua Bi Wema.
“Sijui nini kimetokea ,,, ninachojua mimi ni kwamba sikutaka kumuona Lanlan akiumia ndio maana nikamuokoa , ni kama ilivyotokea mara baada ya Lanlan kutekwa”Aliongea Edna lakini hakuna ambaye alikuwa akiamini maneno yake kwani walichoshuhudia kilikuwa kikiogofya mno na waliamua kukaa kimya bila kuhoji zaidi.
Upande wa Edna alionekana kabisa kama vile hadanganyi kwa namna ambavyo amewaua kwa namna nyepesi namna ile.
Edna alikuwa ndio kwanza yupo levo ya mzunguko kamili na kama utamfananisha na wanawake hao yeye na Neema Luwazo ndio walikuwa wa mwisho mwisho.
Neema Luwazo alikuwa nchini Angola kikazi na pengine angekaa chini na kumuliza Edna kilichotokea kwani kidogo ndio ambae alikuwa na ujasiri wa kumhoji.
“Rufi nadhani hutonilaumu kwa kumuua baba yako”Aliongea Edna.
“Ameyataka mwenyewe”Alijibu Rufi mara baada ya kuangalia kichwa cha baba yake ambacho kilikuwa kimemkodolea macho na Edna palepale alimbeba binti yake na kisha alianza safari ya kurudi ndani.
Lanlan alikuwa na furaha anakwenda kumalizia msosi kwani kwake hakuna kitu cha thamani kubwa kama chakula , lakini kwa wengine wote hakuna hata mmoja ambaye alikuwa na hamu ya kuendea kula.
“Huu upanga sijawahi kudhani una nguvu kubwa namna hii”Aliongea Yezi akikagua upanga wake uliokata vichwa vya majini , alijitahidi kutafuta hata tone la damu kwenye upanga huo lakini hakukuwa hata na ishara kama umetumika yaani ulikuwa mkavu.
“Hio ni siraha nzuri lakini inategemea na mtu anaeitumia”Aliongea Magdalena huku akijitahidi kujituliza.
Majini ambao walikuwa wakipambana juu ya bahari hawakuwa wakijua nini kimetokea huko kisiwani , vita hio ilikuwa imefika katika kiwango cha juu kabisa na anga lilikuwa ni kama vile linayumba.
Poseidon alikuwa na kazi ya kuwazuia majini wasikimbie kwa kutumia mbinu yake ya ukuta wa maji huku akiwapandisha viumbe wakali wa majini kushambuliana na wale majini.
Ijapokuwa Chaopi na Anjiu walikuwa wakipambana na Poseidon ili kuwaruhusu kukimbia lakini Apollo na Artemtis walikuwa wamekwisha kuua majini wengi tu ikiwemo waliokuwa katika levo ya maji ya kiroho.
Ni majini ishirini tu ambao walikuwa katika levo ya maji ya kiroho waliokuwa wamebakia na kumfanya Anjiu na wenzake kuwa katika hali ya wasiwasi.
Ki ufupi ni kwamba majini hao waliokuwa wamebakia ndio walikuwa msingi wa miliki zao kutokana na uwezo wao na kama watakufa wangekumbwa na aibu hata ya kurudi ujinini na kuelezea habari ya kilichotokea na miliki ya Hongmeng pengine ingeweza kuchukulia kama fursa na kuweka miliki hizo chini yao.
Mpango wao ulikuwa umekwama na sasa kila mmoja alikuwa akihofia maisha yake.
“Baba kama hali hii ikiendelea ni swala la muda tu kufa wote hapa , mbinu zao za anga zina uwezo kuliko uwezo wetu wa kijini hivyo mashabulizi yetu hayana madhara kwao na tunazidi kupoteza nguvu..”Aliongea Anjiu akijitahidi kujikinga na mashambulizi.
Chaopi alikuwa akijitahidi kujikinga na mashabulizi ya Apollo bila ya kuweza kushambulia kutokana na kwamba hakupewa nafasi ya kupumua wala kufikiria.
“Hatukufanya maandalizi na mazingatio ya kutosha , Anjiu nitavunja huu ukuta wa maji na nyie wengine mfuatie”Aliongea
“Baba unapanga…”Anjiu sura ilijikunja maana alijua anachotaka kufanya baba yake ni hatari sana maana ilimaanisha angeacha kujilinda na kupitia mabadiliko.
“Usiwe na wasiwasi hata kama nikipata majeraha itanichukua angalau mwezi kupona na miliki yetu haitokosa kiongozi , kama sitofanya hivi uwezekano wetu wa kutoka ni mdogo kwani miungu wengine watafika”
Mara baada ya kuongea kauli ile nguvu za kijini zilianza kujikusanya kwa kasi katika mwili wake na misuli ilianza kupanuna kwa kasi na sekunde tu alibadilika na kuwa jitu la kutisha kiasi kwamba hata joho lake alilokuwa amevalia lilichanika kutokana na kutomtosha na sasa kumfanya kuonyesha mishipa ya rangi nyeusi katika mwili wake huku akionekana kuwa wa rangi ya hudhurungi.
Apollo na wenzake mara baada ya kushuhida mabadiliko yale ya kimwili kutoka kwa Chaopi walirudi nyuma huku wakiendelea kumshambulia kwa kila mmoja kwa namna yake.
Lakini sasa nguuu za kijini za Chaopi zilibadilika na kuwa kama visu ambavyo vilifyatuka na kwasogelea kwa kasi kubwa mno na baadhi ya visu vile waliweza kuvizuia kwa kutumia kanuni za anga lakini vingine vilipita na waliishia kuvikwepa.,
“Ni uchawi gani huu?”Aliongea Poseidon kwa mshangao.
“Nadhani ni mbinu ya siri ya majini ambayo hutumia kubusti uwezo wao , uwezo wake unaongezeka haraka”Aliongea Artemis.
“Kama wana mbinu za namna hii basi tumewachukulia poa , uwezo wake umeongezeka kwa asilimia therathini kuliko mwanzo”Aliongea Apollo.
Sio kwao tu ambao walishangaa lakini hata kwa majini wote hawakujua nini kinamtokea Chaopi.
Ndani ya sekunde tu Chaopi alikuwa ni mrefu kwa mita mbili hivi huku akitoa harufu ya damu na kuzingiwa na ukungu na kumfanya aonekane kama vile ni kidonda.
“Chaopiii..!!”
Senji alihamaki mara baada ya kumuona mtoto wake akitumia mbinu ambayo alikuwa amemzuia asiitumie.
“Hio ndio mbinu ya siri ya Chaopi ambayo inafahaika kwa jina la Brahma?”Aliuliza Gefu.
Kama mkuu wa miliki ya Panas alikuwa na maarifa mengi na hio mbinu ilikuwa ikivumishwa sana , ilikuwa ni mbinu ambayo ilifahamika kama jini akiitumia basi lazima imletee madhara na haikuwahi kutumika kwa zaidi ya miaka elfu mbili katika ulimwengu wa majini.
Mbinu hio ilikuwa ikifanya nguvu za kijini kushambulia seli za mwili na misuli na kuifanya kupitia hali kama vile ni saratani, kwani seli zinapanuka na kuwa kubwa na kuongezeka kwa kasi mno na kitendo hicho hufanya nguvu ya mtumiaji kupanda kwa kasi.
Hasara kubwa ni kwamba mara baada ya kuitumia zile seli zote zinakufa na kwasababu seli ndio zinashikilia nishati ya mbingu na ardhi basi kunauwezekano wa jini kupoteza uwezo wake wote na hata kama wakipona kwa jini ambaye amekwisha kuipita radi basi akija kurudi katika hali ya kawaida uwezo wake utaishia katika levo ya maji ya kawaida tu.
Kitu cha kusikitisha ni kwamba mbinu hio hudumu kwa dakika tano tu na zaidi ya hapo jini linapoteza mwili wake na kurudi katika hatua ya awali ya kuzaliwa , yaani hugeuka kutoka jini aina ya mtu na kwenda jini roho.
Ndio maana mpango wa Chaopi alikuwa akitaka kutumia mbinu hio sio kwa ajili ya kuwaua wale miungu bali ni kwa ajili ya kuwafanya wenzake kukimbia na kurudi ujinin.
Mara baada ya kufikia katika kiwango cha juu kwa kuita nguvu ya Brahma, palepale alipiga makelele kama vile ananguruma kama simba na ilikuwa ni kama upepo unageuka na kuwa vinyoka nyoka na kusababisha wimbi kubwa mno la upepo.
Kitendo kile kilimfanya Poseidon kumsha wanyama wa baharini ili kudhibiti mashambulizi ya Chaopi.
Wimbi lile lilikuwa la kasi mno na lilifyatua ukuta wa anga na kufanya ule mwinuko wa maji aliotengeneza Poseidon kuporoka kushuka chini kwa kasi.
Artemis na Apollo walimshambulia Chaopi kwa kutumia mishale lakini ilionekana kutomletea madhara.
“Kimbieni , kimbieni sasa”Aliongea kwa nguvu na majini wale wakiongozwa na Anjiu waliweza kukimbia na ndani ya sekunde tu waliweza kupotea na muda uleule na Chaopi na yeye alipotea na kuwafanya miungu hio kubakia wenyewe katika hali ya bumbuwazi.
Hatimae vita ile ilifikia ukomo mara baada ya majini kukimbia na mshindi alikuwa ni viumbe hao kutoka sayari nyingine, walikuwa wameshinda kwasababu idadi ya majini walioua ni kama vile wamepunguza nusu ya nguvu ya majini kutoka katika ulimwengu wao, isitoshe hata Chaopi aweze kupona hawezi kurudiwa na uwezo wake wote hivyo kufanya kati ya majini wenye nguvu za juu katika ulimwengu huo waliobakia kuwa Anjjiu wa miliki ya Xia na mrembo Rozu wa miliki ya Panas.
Hawakukaa hapo kwa muda mara baada ya kupeana ishara kwa kuangaliana, iliikuwa ni kama vile wanatumbukia kwenye hewa kwani wote walipotea.







SEHEMU YA 747.
Mara baada ya vita ya miungu na majini kufika mwisho warembo wa Roma walifurahi , ukweli ni kwamba hawakutegemea kama mwishoni miungu ndio itashinda.
Siku nzima kisiwani hapo hali yake ilikuwa ya furaha sana na hakuna madhara makubwa yalioweza kutokea.
Ilikuwa ni jioni ndio wakati ambao Roma aliweza kurejea akiwa ameambatana na majini pepo watatu yaani Latina , Weni na Yunu.
Roma mara baada ya kungia tu katika anga la kisiwani aliweza kuhisi kilichotokea na kwa haraka sana alienda mpaka nyumbani kujua kilichotokea na alishukuru kukuta hakuna aliepata majeraha lakini alishangazwa na kile alichosikia.
Ilikuwa ni kwa bahati nzuri kwamba miungu ilikuwa imerudiwa na nusu ya uwezo wao la sivyo matokeo yake yasingekuwa yakuvumilika kwake kabisa.
Wanawake hao walikuwa na haraka pia ya kumwelezea Roma kile kilichotokea lakini mara baada ya macho yao kutua kwa wanawake warembo walimgeukia na kumwangalia kwa maswali na kuona pengine Roma kaleta wanawake wengine kwenye himaya yake.
“Tukaongeeni kule Ngomeni sio kama mnavyofikiria”Aliongea Roma.
Upande wa Latina na majini wenzake walikuwa katika mshangao mkubwa mara baada ya kugundua Roma alikuwa na wapenzi wengi namna hio.
Mwanzoni walichodhania ni kwamba kwa binadamu kama Roma ili kuweza kufikia katika uwezo huo lazima atakuwa ametumia muda mwingi katika kuvuna nishati lakini ajabu ilionekana kama vile Roma muda wake mwingi alitumia kula bata.
Walichowaza ni sahihi Roma hakuwahi kuwa siriasi sana kama majini likija swala la kuvuna nishati , ukweli ni kwamba uwezo wake ulikuwa ukiongezeka kwa kasi kutokana na changamoto alizokuwa akipitia.
Mara baada ya kufika katika ngome ya makazi yake ya kifalme Roma aliwatambulisha majini hao kwamba wanahusina na familia ya mzee Sharif na ni majini pepo.
Mara baada ya wote kujua warembo hao walikuwa ni majini katika asili ya wanyama walipigwa na bumbuazi lakini pia walishangazwa majini wa aina hio kuwa na uhusiano na familia ya Sharif.
Wakati wa maongezi majini hao muda wote macho yao yalikuwa ni kwa Amina tu ikiwa ni kama vile wanamshangaa.
Roma pia aliweza kuona jambo hilo kwani licha ya kwamba hakuwa amemtambulisha Roma kwao lakini ilionyesha wamekwisha kumtambua .
“Amina naweza kufahamu kama unae mdogo wako?”Aliuliza jini Latina na kufanya wengine wote kushangaa na kujiuliza amejuaje jina lake.
Amina hata yeye mwenyewe alishangaa kwa sekunde na aliishia kutingisha kichwa.
“Nimezaliwa peke yangu”
“Oh …je wazazi wako wote wapo hai?”
“Mama alikwisha kufa ila baba yupo hai”
“Kama ni hivyo je baba yako ana wadogo zake , je ndugu upande wa mama yako wapo wapi?”Aliuliza Latina bila ya kupumua na kumfanya Amina kuzidi kuchanganyikiwa.
“Hubby kwanini anauliza maswali mengi hivi?”Aliuliza huku akimwangalia Roma.
Ijapokuwa Amina alikuwa mchangafu na ambae sio mwepesi wa kukasirika lakini haikumaanisha hakuwa na hasira pale mipaka inapovukwa.
“Punguza hasira mpenzi , Mkuu wa Dhehebu amekuja mpaka huku kwa ajili yako”
“Kwa ajili yangu!?”Aliuliza Amina huku akimwangalia Latina.
Roma ilibidi aelezee na wanawake hao walijikuta wakiona aibu mara baada ya kusikia maneno ya kike na kiume na ndio wakati ambao waliweza kujua Amina aliweza kupanda levo sio kwasababu ya kuvuna nishati kwa wingi bali alifaidika na tendo.
Upande wa Amina alijikuta akiwa mgumu kuamini kama yeye alikuwa ni nusu jini tena sio jini mtu bali ni jini pepo , majini ambao wanazaliwa kama wanyama aina ya Mbweha kabla ya kupata miili.
“Miss Amina unaweza usiamini lakini wewe na sisi ni ndugu na tunamiliki damu safi , tunaweza kabisa kuhisi mfanano wa damu yako na yetu na kuna uwezekano ukawa ni sehemu ya mbweha wa daraja la juu , damu yako imekwisha kuanza kufanya kazi na kuzima damu ya kibinadamu na mapema tu uwezo wako utaongezeka kwa kasi , hongera sana kwa kuwa sehemu ya mlolongo wa muendelezo wa damu ya kifalme kutoka koo ya Mbweha na tunakukaribisha nyumbani”Aliongea Latina
“Jamani … kwahio inamaana ninakwenda kuwa na mikia na masikio ..nakwenda kuwa jini wa Kimbweha?”
Aliongea kama vile muda wowote angekwenda kuangaua kilio , kwake ilikuwa haikubaliki kabisa kuamini kama yeye ni jini na anakwenda kuota mkia.
Latina na wenzake walitoa kicheko hawakutarajia Amina angekuwa hivyo na haraka sana walimwelezea Amina.
Ukweli ni kwamba Amina licha ya kwamba damu yake ya kibinadamu itapotea haikumaanisha kwamba anakwenda kuwa jini kamili hivyo hakukuwa na uwezekano wa yeye kuwa na umbo la Kimbweha.
Amina alijihisi kutulia sasa kwani hakutaka kujisumbua sana kama anakwenda kuwa sehemu ya koo ya majini.
Ukweli ni kwamba majini hao waliamini pengine kuna binadamu wengi ambao ni nusu majini lakini kutokana na kwamba hawana nguvu zozote za nishati ya mbingu na ardhi ingekuwa ngumu sana kuwagundua.
Amina alikuwa amegundulika kwasababu ya kuvuna nishati za mbngu na ardhi na kupelekea damu yake iliokuwa imelala kuamka.
Kitu kingine jamii zote za majini zinawadharau watu ambao wamezaliwa nusu nusu na kama sio Amina kuwa karibu na Roma wasingejisumbua hata kuja mpaka hapo.
Mara baada ya swala la Amina kupita habari zingine zilifatia ambazo zilihusisha ulimwengu wa majini watu.
Roma mara baada ya kusikia majini hao walishindwa na miungu watatu tu ambao ni Apollo, Artemis na Poseidon alishangaa mno.
Hata yeye pia aliweza kugundua uungu wa Hades ndani yake ulikuwa umeimarika sana lakini bado hakuweza kuelewa vizuri kanuni za anga kama ilivyokuwa kwa Hades mwenyewe , hivyo asingeweza kushinda majini wa levo ya maji ya kiroho kwa kutmia kanuni za anga kama walivyofanya Poseidon.
Sasa kitendo cha Apollo kuweza kumshinda hata Anjjiu na Chaopi ambao walikuwa wameshaipita radi ilimaansia uwezo wao ulikuwa umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana.
“Kama nilivyotarajia , inaonekana moyo wa Gaia ndio sababu kubwa”Aliwaza Roma lakini sasa mara baada ya kuwaza jambo lile ni kama wazo lingine lilichipuka katika ubongo wake.
“Moyo wa Gaia , Moyo wa Gaia!”
Wazo ambalo lilichipua ni kushuka kwa kiwango cha joto la dunia kwa haraka sana.
Na sasa anakuja kugundua tukio hilo linatokea katika wakati ambao Moyo wa Gaia unafufuka , Roma alijiuliza inamana sababu ya kushuka kwa joto kunasababishwa na moyo wa Gaia?.
Roma alikumbuka maneno ya Clark kwamba nishati ya jua ni kama vile inafyonzwa kabla ya kufika duniani hivyo mawazo yake ni kama moyo huo ndio unameza mionzi ya jua.
Ukweli ni kwamba Roma mwenyewe hakujua matumizi halisi ya moyo huo na namna ambavyo miungu inakwenda kufufua wenzao lakini alikuwa na uhakika kinachoendelea kina muunganiko na moyo huo.
Jambo hili kwa mara ya kwanza lilianza kumtia wasiwasi zaidi na zaidi na kujiuliza kama moyo huo utaendelea kumeza nishati ya jua nini kitatokea kwa binadamu na mimea.
Warembo wake walimshangaa pia mara baada ya kuonyesha mabadiliko.
“Hubby unawaza nini?”Aliuliza Dorisi kwa kumshitua Roma kwa kumpiga kwenye paja.
Roma mawazo yake yalirudi na palepale macho yake yalikutana na macho ya mke wake Edna .
Edna alimwangalia Roma akiwa katika hali ya utulivu kabisa lakini kuna hali ilikuwa ikionekana katika macho yake ambayo haikuwa ikielezeka na Roma alikuwa akihisi kabisa.
Lakini ni palepale aliondoa macho yake kwa Edna na kuwaambia wengine kwamba alikuwa sawa tu.
Mara baada ya kuwaza kwa muda palepale aliinua sura yake na kumwangalia Edna kwa mara nyingine.
“Babe wife , umewezaje kuwaua majini wote wa tano ndani ya dakika kadhaa tu licha ya kuwa na uwezo wa juu , unaweza kunielezea ilivyokuwa japo kidogo nikakuelewa?”Aliuliza Roma.
Wengine wote ni kama walisubiria Roma aulize swali hilo , walikuwa wakimuogopa kumuuliza kutokana na alivyokuwa siriasi na walijua pengine akiuliza Roma Edna anaweza kufunguka.
Unadhani ni siri gani ambayo Edna ameificha moyoni, Je Edna ni nani haswa?
Hatima ya Dunia ni nini?.
Zeus, Hera, Demeter na Dyonisus hii miungu ipo wapi?”
Yajayo Yanafurahisha.
Safi sana
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware

SEHEMU YA 748.
Edna alikuwa amekaa kwenye kiti chake kimapozi kabisa na mara baada ya kusikia swali hilo kutoka kwa Roma aliweza kuona sura zote zikimgeukia yeye na alinyanyua kikombe cha kahawa na kunywa kidogo na kisha akakiweka chini.
“Kama nilivyokwisha kusema , sikuwa nikielewa nini kinanitokea , nilichotaka ni kuwaua kwasababu walinikasirisha mara baada ya kumteka Lanlan , sijui nimewezaje lakini ni kama vile kuna sauti iliokuwa ikiongea na akili yangu na kuniambia niwagandishe ili iwe rahisi kuwafyeka na hata kumwambia Yezi anipatie upanga wake ni kama vile sio mimi nilie ongea , ilikuja tu nikafanya hivyo..”Aliongea Edna na sauti yake ilionyesha ni kwa kiasi gani alikuwa hadanganyi, haikuonyesha kama kuna siri ambayo alikuwa akificha , ukweli ni kwamba alionekana kama vile amechoka sana na kuonekana kutia huruma kwa namna ambavyo anaulizwa maswali , ni kama vile mgonjwa aliepoteza kumbuumbu akilazimishwa kukumbuka kitu.
Roma alimwangalia Edna kwa dakika kama moja hivi na kisha alivunja ukimya kwa kucheka.
“Usiwaze sana kuhusu hilo , kama huelewi nini kilikutokea haina haja ya kuumiza kichwa , kwangu kitu muhimu ni wewe na Lanlan kuwa salama basi”Aliongea Roma na palepale alisimama na kumwangalia Latina.
“Latina mkuu wa Dhehebu, majini kutoka ulimwengu usionekana wamejionyesha katika ulimwengu unaonekana na kuchokoza familia yangu ni muda wa mimi kulipa fidia lakini kabla ya kuondoka hapa nina ombi moja kwako”
“Mr Roma sio kwamba tunataka kwenda kinyume na maneno yetu au kwasababu sisi ni wakatili lakini kama tutavunja sheria ambazo zimewekwa karne na karne na kwenda kushambulia ulimwengu wa majini watu matatizo yatatupata sisi..”
“Umenielewa vibaya Mkuu wa Dhehebu , mimi ndio ninaenda mwenyewe ulimwengu wa majini watu ni kwamba tu ninahofia usalama wa familia yangu , ijapokuwa miungu ipo karibu itakuwa ni vizuri kama nyie wote wawili mtakuwepo hapa”
Aliongea Roma isitoshe kwasababu Latina alikuwa tayari katika levo ya kuipita radi na kumiliki mikia saba , uwezo wake wa kimapigano ulikuwa ni mkubwa mno na hakuna uwezekano wa kuzidiwa na majini jamii ya watu ndio maana Roma aliona ingekuwa salama zaidi kama atabakia hapo kisiwani kwa ajili ya kuipa ulinzi familia yake na hapo ndio hatokuwa na wasiwasi.
Hakukuwa na madhara kwa majini hao kuendelea kubakia hapo visiwani na ukweli ni kwamba walitamani pia kuangalia namna mazingira ya dunia yalivyo lakini kubwa zaidi kama watakubaliana na ombi la Roma ni kama wanatengeneza deni ambalo Roma atakuja kulilipa.
Na mara baada ya Latina kufikitia faida zote hizo moja kwa moja alimkubalia Roma kubakia hapo kisiwani kwa ajili ya kuilinda familia yake, yeye pamoja na majini wenzake Weni na Yunu huku wakimwambia Roma ahakikishe anazigeuza majivu miliki za majini hao lakini Roma aliona uwezo huo hana , kitu pekee ambacho anaweza kufanya ni kuua majini wengi na kisha kukimbia bila kupatwa na majeraha.
Mara baada ya kusikia Roma anakwenda kuwalipizia kisasi kwa kuchokozwa na majini warembo hao walikuwa ni waelewa juu ya hatari ambayo Roma anakwenda kujiingiza lakini hata hivyo hawakutaka kumzuia.
Ukweli ni kwamba ugomvi kati ya majini na Roma umefikia katika hatua mbaya sana kutokana na majini hao kupoteza washirika wao wengi na kama Roma hatofanya mashambulizi ya haraka wakiwa katika hali mbaya kama hio wanaweza kujijengea nguvu na ni swala la muda tu kuja tena kumchokoza hivyo muda sahihi wa kuvamia miliki hizo za majini ni wakati huo.
Mara baada ya matayarisho hatimae Roma aliaga na kuondoka lakini hata hivyo hakuelekea moja kwa moja katika ulimwengu wa majini.
Kabla ya kuanza safari yake alitafta watu wawili kwa kutumia simu lakini hakuna ambaye alikuwa akipatikana na hio ndio sababu ya kuchukua uelekeo mwingine na kufumba na kufumbua ilikuwa ni kama vile ametumbukia kwenye shimo la anga na alikuja kuibukia katika kilele juu ya safu za milima ya Alps upande wa Switzerland.
Upepo mkali uliokuwa ukivuma katika kilele hicho kilichofunikwa na barafu kubwa ilifanya hata wale watalii ambao wanapenda kukwea mlima kama sehemu ya utalii kuacha kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ya dunia.
Ilikuwa ni usiku wa manane na hakukuwa na dalili ya binadamu yoyote kuwepo katika mlima huo , ilikuwa ni kama vile shughuli za kitalii zimesitishwa kwa muda.
Roma palepale uso wake ulimbadilika na kuwa mweusi tii na aliweza kufungua ‘space seal’ na kufanya mawe makubwa yaliokuwa katika mlima huo kuanza kuporomokoka, ilikuwa ni kama vile kuna mlipuko unaotokea juu ya mlima huo.
Kitendo kile cha kutumia kanuni za anga kujaribu kuharibu mlima ilifanya milango minne ya anga kufunguka na sura za watu wanne kuonekana ambao ni Apollo , Artemis , Poseidon na Hermes.
Mara baada ya kumuona ni Hades walishajua Roma katumia kanuni za anga kujaribu kuwaita katika hilo eneo.
“Hades , it isn’t good to breach the treaty of god in the middle of night when there is no need to fight”Aliongea Hermes akimaanisha kwamba haina haja ya kuvunja sheria za mkataba wa miungu wakati huo wa usiku mnene ili hali hakuna haja ya kupigana.
“The gods treaty! , sidhani kama kuna haja ya kuwepo kwa hichi kitu kinachoitwa mkataba tena”Aliongea Roma mara baada ya kuwakagua mmoja mmoja.
“Hades unamaanisha nini kusema hivyo?”Aliuliza Artemis huku akiwa amekunja ndita.
“Malengo ya sheria za ’The gods treaty’ ni kuzuia majini kujitokeza katika ulimwengu unaonekana na kuanzisha vita na miungu ili kudumisha amani na usalama wa binadamu, lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ulitengenezwa kutokana na hali ilivyokuwa hapo zama za kale wakati kila pande ilikuwa ikitaka kubakia kuwa salama, lakini kwa sasa hali ni tofauti kwani tayari moyo wa Gaia unaendelea kufufuka na kufanya nguvu zenu kuongezeka maradufu na kama hii itaendelea inamaanisha kwamba miungu mtakuwa na nguvu kubwa kushinda hata majini na wavuna nishati za mbingu na ardhi na kutokana na jambo hili linaloenda kutokea, je kuna haja ya uwepo wa hiki kitu kinachoitwa ‘ the gods treaty’?, Apollo , Artemis na Poseiidon mnao uwezo wa kupigana na majini wakuu kutoka katika miliki tatu na kushinda mnadhani mimi ni mtu ambaye siwezi kuchanganua mambo? , Hermes wewe unaishi karibu na visiwa vyangu lakini hukujitokeza kwasababu ulikuwa na uhakika watatu pekee wanaweza kudili na kundi lote la majini, je nakosea?”
“Upo sahihi , lakini je kuna tatizo juu ya hilo? , mimi natokea katika ukoo wa wanywa damu hivyo mara nyingi mchana ndio wakati wangu wa kulala na usiku ndio wakati wa mawindo”Aliongea Hermes.
“Acha matani basi, hivi nyie mnaniona mimi ni mjinga eti? Majini watu wanaweza wasijue kiwango cha nguvu zenu lakini mimi pia nina uungu ndani yangu na wakati huu ambao nipo karibu yenu ninaweza kuona ni kwa namna gani mlivyokuwa na nguvu , kulingana na mapigano yaliotokea mapema ya leo majini wasingekuwa na uwezo wa kukimbia kama wote wanne mngejitokeza , mngekuwa na uwezo wa kuwaua wote lakini kwanini mkawaachia makusudi kabisa wakimbie?”Roma alianza kukosa uvumilivu na hasira alizionyesha waziwazi.
“Kwahio ndio unatulaumu , Hades familia yako kwa upande mwingine ipo salama shida iko wapi?””Aliongea Apollo huku akitingisha kichwa.
“Bado tu mnafanya maigizo mbele yangu , nilidhani sisi ni marafiki lakini inaonekana kuna kitu muhimu sana mnanificha , lazima kuna mpango mnauendeleza nyuma ya pazia ambao mimi si ujui”
“Hades stop making wild guesses , you are our companion”Aliongea Artemis akimwambia Roma aache kufanya makisio mabaya kwani yeye ni mwenzao.
“Mimi ni mwenzenu?, kama kweli mimi ni mwenzenu niambieni kwanini mpaka wakati huu nimeshindwa kuwasiliana na Aphrodite na Ares , kwanini hawapatikani hwani ni wapi wameenda?”
Miungu hio minne ilibakia kimya huku sura zao zikishindwa kusomeka ni kipi wana kiwaza.
Katika watu wawili ambao Roma Alijaribu kuwasiiliana nao kabla ya kuja hapo ni Christen na Ares na kwa hali isiokuwa ya kawaida wote hawapo hewani jambo ambalo sio la kawaida.
“Poseidon wewe unaishi Hawaii na mara nyingine upo Hongkong umbali ambao ni mrefu sana kuliko Urusi anapoishi Ares lakini wewe umefanikiwa kufika visiwa vya wafu mapema na Ares hajatokea , lazima kuna sababu kubwa kwa mtu mpenda vita kama Ares kutokujitokeza na kushiriki katika mapigano na hio ni kwasababu kuna kitu cha muhimu zaidi ambacho anafanyia kazi , je makisio yangu yapo sahihi?”Aliuliza Roma.
Kwa tabia ya Ares kupenda vita hakika isingekuwa rahisi kuvumilia kutokuja kupigana na majini.
“Tunaju vipi ni kipi kinaendelea katika maisha yao”Aliongea Poseidon kikauzu kabisa huku akimwangalia Roma usoni.
“Lazima wanachokifanya lazima kunahusiana na Moyo wa Gaia si ndio?”Wote kimya na kumfanya Roma kuendelea kuongea.
“Kabla ya hili kutokea nilikuwa nikijaribu kuwaza lakini nadhanni mpaka sasa nimeupata ukweli , kupotea kwa joto la dunia lazima kunasababishwa na kufufuka kwa Moyo wa Gaia , Wakati Athena alipoweza kuupata moyo huo kule Korea Apollo , Athena na Artemis mliweza kuongea kwa kutumia lugha yenu kwa njia ya kimawazo na inaonekana hili ni swala ambalo mlilitarajia”
“Hades we …”Apollo hakutaka kuona Roma anaumia na ndio maana alisita kumalizia sentensi yake na kufunga mdomo lakini kitendo kile kilimfanya Roma kucheka sio kicheko cha furaha bali kicheko cha uchungu.
“Haina haja ya kuwa na wasiwasi juu yangu hata kama hamtoniambia basi lazima itakuwa ni kwasababu ya Athena , sina uhakika ni jambo gani analipanga na sina uhakika na mnachokipanga lakini niwaonye tu msije kufanya jambo la kijinga la kuhatarisha usalama wa watu wangu wa karibu la sivyo siwezi kujizuia kuonyesha ukatili wangu”Aliongea Roma kibabe.
Macho yake yalikuwa yakionyesha nia ya kimauajji , ilikuwa ni kama vile ametawaliwa na pepo kwa namna ambavyo alikuwa akionekana.
Upepo uliendelea kuvuma huku kila mmoja akiwa kimya bila ya kuongea kitu lakini ni muda uleule Hermes alitoka angani na kuja kutua karibu na alipo Roma na kumwangalia usoni akiwa na tabasamu la kejeli.
“I believe in your words Hades , but remember what I told you that day , I know you don’t believe me but if my words come true one day , you’ll have to remember your words today .. that is somethig I’ m looking forward to”(Naamini katika maneno yako Hades lakini kumbuka nilichokuambia siku ile , najua huniamini lakini kama maneno yangu
yatakuja kuwa kweli siku moja utapaswa kukumbuka meneno yako ya leo .. hicho ni kitu ambacho natarajia…”)
Mara baada ya Hermes kuongea maneno hayo palepale alipotea kwa namna ya kutumbukia kwenye anga , maneno yake hayakuwa katika hali ya urafiki kabisa , yalikuwa ni kama vile yapo katika mtindo wa onyo kwamba kama maneno yake yatakuja kuwa kweli basi lazima Roma akumbuke maneno yake alioongea siku hio.
Roma macho yake yalionyesha ishara ya maumivu lakini yalipotea haraka sana na alionekana katika kuwaza.
Artemis na Apollo wao hawakuongea kitu na waliishia kuangaliana na kisha na wao wakapotea.
Ni Poseidon peke yake ambaye alikuwa amebakia na alimwangalia Roma machoni bila ya kukwepesha macho kwa namna ya kujiamini.
“Don’t think too highly of yourself young man , having a good temper is beneficial , but it is also dependent on the other party , sometimes complacency is foolishnes”
“Acha kujiona mwamba kijana , kuwa na utulivu kuna faida zake pia , lakini inategemea na upande mwingine , muda mwingine kuridhika sana ni ujinga”
Mara baada ya kuongea kauli hio na yeye pia alipotea katika giza totoro na kumuacha Roma nyuma akiwa amekunja ngumi na kung’ata meno kwa hasira kwa dakika kadhaa mpaka alipokuja kuvuta hewa nyingi na kupumua.
“Je kila ninachofanya ni kama ilivyotabiriwa na huyo mwanamke kama alivyosema Aphrodite juu ya unabii , ni kweli kesho yangu ya baadae imekwisha kuamuliwa , je kuna namna ya kubadilisha kesho yangu?, Kama ni hivyo si kila ninachokifanya ni kile alichokipanga , lakini kama kweli siwezi kuibadilisha kesho yangu ni kwa namna gani alitabiri nitakuja kufanya maamuzi yasiokuwa ni ya kutarajiwa?, hakuna wa kuniambia ni kipi ni sahihi na kipi sio sahihi na hii yote ni kutokana na uwezo wake ni mkubwa kuzidi wote na hawezi kusalitiwa , je ni kitu gani ana jaribu kukamilisha , nini kitatokea kama moyo wa Gaia utaendelea kunyonya nishati ya jua?”
Roma kichwa chake kilikuwa katika mawazo na kujiuliza maswali mengi,kuna mambo mengi ambayo hakuambiwa na ilikuwa ni kama kila anachokifanya tayari kilishakwisha kutegemewa na jambo hilo linamfanya kutokujua ni ipi njia sahihi ya kuchukua , anajiuliza je kuna uwezekano wa kubadilisha kile ambacho kitamtokea baadae lakini anakuwa katika hali ya kuchanganyikiwa na hio yote ni kutokana na kukosa majibu.
Ilikuwa ni kama kuna mkono ulioshikilia rimoti ambao ulikuwa ukimwendesha kama shushu lakini licha ya yote hayo hakuwa na namna ya kufanya chochote , hali hio ilikuwa ikimpelekea kujihisi ukichaa.
Watu ambao alihisi ndio marafiki zake walikuwa ni kama wageni machoni mwake.
“Au nilikuwa nikijidanganya mimi mwenyewe , hata hivyo siwezi kujilinganisha nao kwani wameishi muda mrefu na mimi kwao ni mtoto”Aliwaza Roma.
Ukweli ni kwamba Roma hakuwa na jinsi kwanzia alivyoweza kuachana na Hades wa zamani na maneno aliomwambia , maneno ambayo Aphrodite aliomwambia na maneno ambayo Hermes alimwambia ni kama yanaanza kutimia.
Aphrodite alimwambia kabisa Roma kwamba ikitokea siku ambayo Athena amepata jiwe lingine la kiuungu basi asije kumwamini hata yeye na kauli hio ilikuja kuthibitika katika wakati huo , miungu hio yote ilionekana tayari imekwisha kutengeneza ukuta wa undugu baina yao.
Roma alidumu kwa zaidi ya nusu saa akiwa katika hali ya kufikiria na mara baada ya kuona hakuwa na majibu aliamua kupotezea maswala hayo kwanza na kuamua kudili kwanza na majini ambao ndio kipaumbele chake kwa wakati huo.
Ngoja nikapunguze mawazo kwa kuua majini kwanza”Aliwaza Roma na palepale alipotea katika anga kwa spidi ya kupepesa macho.

















SEHEMU YA 749.
Hapo kale jumuia ya majini wa Hongmeng ndio ambao walikuwa na nguvu zaidi katika ulimwengu wote ule unaonekana na ule usionekana, nguvu yao ilitokana na kuwa na majini wengi ambao walikuwa levo za juu sana na kujitengenezea ushawishi kati ya binadamu.
Mara baada ya ujio wa viumbe kutoka sayari nyingine na kutokea kwa vita baina yao ndio wakati ambao Hongmeng ilipoteza ule utukufu wake licha ya kwamba mwishoni ni kama ilishinda vita hio kwa kufanikiwa kumkamata Zeus huku Athena yeye akikimbia lakini ki uhalisia ni kama vita hio haikuwa na mshindi ndio maana kukaja kutokea kwa kitu kinachoitwa The gods Treaty.
Mkataba ambao ulitokea kwasababu pande zote mbili zilihitaji kuishi , yaani Hongmeng walitamani kuendelea kuishi na miungu na wenyewe walitamani kuishi na kutokana na mahitajio yanayofanana ikawa sababu ya pamoja ya kutengeneza mkataba unaolinda pande zote.
Unachopaswa kujua wakati wa viumbe kutoka sayari nyingine wanatua duniani kulikuwepo na miliki nyingine za kijini kama vie Xia na Kekexil lakini majini wa miliki hizi hawakujihusisha na vita hivyo kutokana na kwamba hawakujali sana binadamu wala maswala ya dunia.
Vita baina ya miungu na majini iliipelekea
Hongmeng kupata hasara kubwa, hasara ambayo ilipelekea kupoteza kwa wanajeshi wao wenye uwezo wa juu wa nguvu za mbingu na ardhi na hali hio ya hasara moja kwa moja ilifanya miliki nyingine za kijini kuwa na nguvu kuliko Hongmeng..
Lakini hata hivyo mpaka leo hii licha ya kwamba miliki hii ilikuwa haina majini wenye nguvu kama vile miliki ya Kekexil na Xia lakini ndio miliki ambayo haikuwahi kushambuliwa na miliki nyingine.
Sio kwasababu miliki nyingine ilikuwa ikiogopa kuishambulia Hongmeng , ukweli ni kwamba miliki kama ya Xia itataka kuishambulia Hongmeng ikiwa nje ya eneo lake la miliki basi Xia itashinda lakini kama miliki ya Xia ikitaka kuishambulia Hongmeng ikiwa ndani ya eneo lake basi majini wa Xia watashindwa.
Sababu kubwa ya Xia kushindwa kuishambulia Hongmeng ikiwa katika eneo lake ni kwasababu miliki ya Hongmeng ilikuwa ikipatikana katika safu ya visiwa vinavyoelewa angani , visiwa ambavyo hulindwa na mfumo wa nguvu za maajabu za kijini zilizoasisiwa tokea zama hizo na majini waliokuwa na akili kubwa.
Ukiwa kilomita kadhaa kutokea miliki ya Xia utaona ni kama vitu kama vichuguu vinavyoelea angani huku vikichemka huku chini yake vikiwa vimefunikwa na mawingu makubwa kiasi kwamba huwezi kuona ardhi ya chini ilikuwa na nini.
Visiwa hivyo vilikuwa ni vya maajabu mno na vyenye kushangaza sana na kadri ambavyo unasogea karibu zaidi ndio utaweza kuona nguzo kubwa kama za mwanga wa njano hivi ambazo ni kama vile zimeshikilia visiwa hivyo ili vielee angani huku nguzo hizo zikitoa mng’ao flani wa herufi za kimaajabu ajabu.
Inasemekana kwamba hata majini wa Hongmeng wakati wanakuja ndani ya visiwa hivyo hawakujua ni kwa namna gani vilikuwepo vikielea angani au ni nani alihusika katika ujenzi wake , wanachoamini tu ni kwamba hapo enzi kulikuwa na majini wakuu wenye nguvu na maarifa mengi ndio waliohusika katika ujenzi wake.
Visiwa hivyo vilikuwa ni vingi lakini ambavyo vimejengwa katika kimo kinachotofautiana , kulingana na tamaduni za miliki hio kadri kisiwa kinavyoenda hewani ndio ambavyo hadhi yake huwa kubwa na ndio hukaliwa na wale majini wenye nguvu na vyeo vya hadhi.
Juu ya visiwa hivyo asili ilikuwa ni kama ilivyo kwa ardhi ya kawaida na ajabu ni kwamba katika kingo za visiwa hivyo kuna mito iliokuwa ikiteremsha maji kwenda chini huku chanzo chake kutoka juu ya kisiwa hakionekani.
Kisiwa cha mwisho kabisa kwenda juu kulikuwa na kisiwa kidogo sana ambacho kuna jengo ambalo lipo kwa umbo la Pyramidi ambapo limezingiwa na safu ya mwanga wa njano ambao huzunguka wakati wote.
Eneo la kisiwa hicho ndio husemekana kama eneo takatifu zaidi kwa miliki hio na Hongmeng wanaamini ndio misheni yao kulinda eneo hilo.
Inasemekana kwamba jengo hilo la Piramidi hutumika kama gereza na roho za majini pepo waliowahi kuwa na nguvu na kutaka kushambulia majini watu walifungiwa humo lakini pia roho ya Zeus na yenyewe imefungiwa ndani ya gereza hilo la kisiwa cha anga.
Gereza hilo mpaka leo hii majini pamoja na binadamu hawajui jina halisi wala teknolojia iliotumika kulitengeneza lakini wenyewe wakalipatia jina kama Gereza la Roho na Pepo .
Sasa mfumo wa uundwaji wa visiwa hivyo katika miliki ya Hongmeng ulikuwa ukiwalinda kwani ni kama vile kuna uzio ambao unawafanya majini wenye nia mbaya wanaotaka kufika katika miliki hio kufanya vita kushindwa kufanya chochote kabisa na hio ndio sababu inayoifanya miliki hio kutokushambuliwa kwa miaka mingi licha ya kujulikana kama moja ya miliki ambayo raia wake ni dhiafu sana.
Hakuna jini wala binadamu mwenye nguvu za kijinni ambae amefanikiwa kuipita Dhiki ya Radi katika miliki ya Hongmeng.
Inasemekana kama sio mfumo huo wa ki ulinzi wa visiwa hivyo vya anga isingekuwa rahisi kwa Zeus kushindwa vita, ukweli ni kwamba wakati wa Vita ,Zeus alitegwa na kuja mpaka kwenye ulimwengu huo wa majini watu na kuingia katika mtego wa safu hio ya ulinzi na ndipo alipoweza kukamatwa kirahisi kwa kushindwa kutumia kanuni za anga huku Athena yeye akikimbia.
Sasa imepita miaka mingi na majini ambao walihusika katika vita ya miungu walikwisha kufa na hata wale ambao walisimamia mkataba wa miungu na majini wenyewe wamekwisha kufa na waliobakia ni wale ambao ni kipya.
Katika historia, majini wa zama za kale walionekana kuwa na akili nyingi sana kuliko majini wa Zama za wakati huu na hii inapelekea mpaka leo hii majini wa zama hizi kujiuliza ulinzi wa miliki hio wa safu ya mwanga unafanya vipi kazi , au visiwa hivyo vinavyoelewa iliwezekanaje vikajengwa kwa mundo huo, wala nguzo ambazo zinaonekana kama ndio mhimili wa visiwa hivyo zimetokea wapi na chanzo cha nguvu yake ni nini.
Mpaka wakati huo majini hao hawakuwa na majibu ya maswali hayo na kitu pekee ambacho wanajua ni kwamba safu za mwanga ziliozokuwa zikizunguka kisiwa hicho ndio ulinzi wao , huku gereza la roho ndio misheni yao kubwa ya kulilinda ili wasiruhusu roho waliofungiwa kutoka.
Hakuna ukweli wowote kwamba ni kweli Zeus ameshikiliwa katika gereza hilo la piramidi . ukweli ni kwamba majini hao wanafanya makisio tu kulingana na historia au pengine kuna ukweli uliofichwa kuhusu wapi Zeus alipotelea.
Katika moja wapo ya kisiwa kikubwa zaidi kulikuwa na jiwe kuubwa jeupe ambalo limezungukwa na viti vya mawe vilivyochongwa katika mpangilio wa duara katika urefu unaotofautina na kufanya wale waliopo mbele kutowazibia wa nyuma, ni kama vile viti vya bar lakini chukulia kama vile vimetengenezwa na nguzo ya jiwe iliosindiliwa ardhini huku pale juu yake kuchongwa kwa mtindo wa kisahani na kumfanya ukaaji kuwa mzuri.
Vilikuwa vingi mno zaidi ya viti elfu moja ambavyo vimeachana kwa umbali maalumu.
Upande wa juu kabisa kulijengwa eneo la juu kidogo ambalo ilikuwa kama vile ni madhabahu au jukwaa na kwa mfano kama kuna mgeni au mtu anajadiliwa au kusomewa hukumu anapaswa kwenda kusimama juu ya jiwe kubwa ambalo lipo kama meza ya mviringo likiwa limeshikiliwa na nguzo mbili za mawe kwa chini.
Hakukuwa na mambo ya korido wala ngazi kwani majini wote pamoja na binadamu angalau uwezo wao ulikuwa si chini ya levo ya nafsi na kuwafanya wote kuwa na uwezo wa kupaa kwenda kukaa katika viti hivyo.
Mahali hapo ndio eneo ambalo majini pamoja na binadamu wenye nguvu za kijini hukusanyikia kwa ajili ya kikao cha jumla.
Sasa ikiwa ni kama lisaa moja nyuma hivi kabla ya Roma kukutana na miungu upande wa duniani katika miliki hio ya Hongmeng katika eneo hilo kulikuwa na kikao ambacho kinaendelea.
Kikao hichi kilihusisha mamia ya majini pamoja na binadamu ambao walikuwa na nguvu za kijini.
Unachopaswa kuelewa Hongmeng ni miliki ambayo ilikuwa na binadamu wengi ambao wananguvu za kijini na asilimia kubwa ya binadamu hao husalia Buddha, ijapokuwa walikuwepo wa dini nyingine lakini majini kwao dini ni Dhana sio imani na vitabu vya kidini kama vile Biblia na Quran wanatumia maandiko yake kama mbinu za kupandia levo tu
Siku za kawaida katika eneo hilo kungekuwa na majini angalau ishirini ambao hufanya kikao lakini siku hio kulikuwa na majini zaidi ya mia moja ambao walikuwa wamehudhuria kikao huku baadhi yao wakiwa sio majini wa miliki hio ya Hongmeng ikimaanisha kwamba ni wageni na walionekana kukaa katika meza hio iliokuwa katikati.
“Kutokana na ubini wako Nefi lazima utakuwa unawajua hawa waliopo mbele yetu , ni juzi tu hapa nimeweza kuingia daraja la mbingu hivyo sina uelewa wa kutosha, yupi hapo ni Anjiu, jini ambaye ameweza kupitia mapigo ya radi?”Alikuwa ni mwanaume aliekuwa pembeni ya jini aliefahamika kwa jina la Nefi , jini huyo hakuwa na uelewa na taarifa za miliki nyingine kwani sio muda mrefu aliweza kupanda daraja la mbingu.
Hongmeng majini na binadamu wapo katika madaraja mawili , daraja la kwanza ni la Ardhi ambapo hadhi yao ni ya chini na daraja linalofatia ni la Mbingu na hapa hadhi yako inaweza kuwa ya kati au ya juu.
Sasa anamuuliza Nefi kwamba hajui kati ya wageni waliokuwa mbele yao yupi ni jini Anjiu ambaye ameweza kuivuka dhiki ya radi.
Mara baada ya misheni yao ya kwenda kumshambulia Roma kukwama baada ya miungu
kuingilia viongozi wa miliki zote tatu yaani Panas , Kekexil na Xia walifanya safari ya kuelekea Hongmeng.
Dhumuni la kwenda Hongmeng ni ili kuungwa mkono katika vita yao ambayo haijaisha kati yao na binadamu anaefahamika kwa jina la Roma Ramoni.
Anjiu na wenzake walijua kabisa kutokana na hasara walioweza kuipata katika dunia kama Roma angefika katika miliki zao na kushambulia basi wasingeweza kumshinda na ndio maana waliona njia pekee ya kuweza kupona ni kuwashawishi Hongmeng kuungana nao.
“Kwani huwezi kuhisia nguvu zao, kuna haja ya kuuliza?”Alijibu Nefi huku akimwangalia Yozi alieuliza.
“Hehe …inatia aibu kukubali lakini ninakosa ujasiri wa kutumia uwezo wangu kuwatambua , Nefi je unaweza kuniambia wale wengine ni wakina nani , siwezi kuamini maneno ya wengine kama ninavyoamini ya kwako”
“Wale watatu wengine ni sehemu ya majini kumi wenye nguvu katika ulimwengu wetu , yule alievalia nguo za bluu ni mkuu wa miliki ya Kekexil ambaye amepewa jina jipya la kiungozi na sasa anafahamika kama Mkuu Menyu, yule wa nguo nyeupe yeye anafahamika kwa jina la Gefu ndio mkuu wa miliki ya Panas na yule mwingine ambae anaonekana mjeuri jeuri pale anafahaika kwa jina la Shozi kutoka miliki ya Panas pia”Aliongea Nefi akimwelezea Yozi ambaye hakuwa akitambua wageni waliofika katika miliki hio .
“Kwahio yule Shozi ni sehemu ya majini wenye nguvu , mbona yupo kimasikini masikini?”Aliuliza Yozi.
Katika ulimwengu wa majini haikumaanisha kwamba majini ambao wanaingia katika hesabu ya majini kumi ni kwamba ndio ambao walikuwa na nguvu kubwa sana bali ukweli ni kwamba wengine wanaweza kuwa na nguvu za kawaida lakini ushawishi wao na hadhi ukawa mkubwa.
Kwa mfano Gefu , Menyu na Anjiu walikuwa ni viongozi wa miliki sio kwasababu katika miliki zao ndio walikuwa na nguvu bali hadhi yao ndio iliwafanya kuwa na nguvu .
Sasa kwa upande wa Shozi yeye inasemekana sio mzaliwa kutokea miliki ya Panas bali ni kwamba mkuu wa miliki ya Panas iliopita alimwajiri katika miliki hio na kuwa katika kitengo cha Taisha.
Taisha ni majini wenye nguvu ambao huchukuliwa kama wanajeshi wa kitengo maalumu(Special force) ambao kazi yao kubwa ni kutoa ulinzi kwa miliki hivyo huyo Shozi alialikwa kama mwajiriwa kuwa katika miliki ya Panas na kuingizwa katika kitengo cha Taisha.
Kwanzia hapo ndio umaarufu wake katika miliki ya Panas ulikuwa mno na kutokana na kupendelea kuishi katika moja ya mlima ndani ya miliki hio basi kwanzia siku hio ndio mlima huo ukaja kufahamika kama mlima Shozi.
Uwezo wa nguvu za kijini wa Shozi ni mwishoni mwa maji ya upako na ndio ilimfanya kupewa heshima yake, ilikuwa ngumu kumjua alikuwa na uwezo mkubwa na ni mwenye kuheshimika kama vile Yozi alivyomwangalia ni kwasababu hakuvaa mavazi ambayo yalikuwa yakimpa utukufu bali alikuwa akivaa mavazi kama vile ni chokoraa.
“Huyo mzee tayari yupo kwenye levo ya maji ya kiroho lakini ni kama vile anakwenda kufa hivi karibuni”Aliwaza Yozi.
“Hebu jione ulivyo mjinga , unawezaje kumtafsiri mtu kutokana na muonekano wake , ijapokuwa Anjiu ameipita radi lakini hakuna uhakika kama atashinda kama atapambana na Shozi…. Kitendo cha Gefu kuja nae hapa Hongmeng basi lazima kuna jambo kubwa linaendelea”Aliongea Nefi.
“Nefi unamaanisha nini kuhusu hilo?”Aliuliza Yozi kwa mshangao lakini upande wa Nefi hakutaka kujibu swali lake.
Na minong’ono iliokuwa ikiendelea kati ya majini na binadamu wa Hongmeng wanaosubiria kikao kuanza ilikoma na kimya kikatawala.
Sababu ya ukimya wao ni kutokana na ujio wa majini ambao walikuwa na nguvu wanaokaribia ndani ya eneo hilo.
Kulingana na tamaduni za ki uongozi wa Hongmeng majini hao vyeo vyao ni vya Mbingu hadhi ya juu. “Hatimae wameweza kufika, nashangaa imekuwaje wakuu wa miliki zote tatu kuja Hongmeng na kutaka kuongea na viongozi wetu”
“Nadhani tutasikia sababu iliowaleta , hatujawahi kuwa na urafiki na miliki zingine za kijini , hivyo kulazimika kuja hapa lazima ni jambo kubwa limewaleta”
Baadhi ya majini waliongea wao kwa wao wakitaka kujua kilichowaleta Gefu , Anjiu , Menyu na Shozi katika miliki ya Hongmeng ni nini.
Ndani ya sekunde chache tu majini nane waliokuwa katika muonekano wa kizee na ujana walienda kutua kwenye eneo la madhabahu
Ijapokuwa kulikuwa na majini zaidi ya kumi na mbili wa Hongmeng ambao walikuwa katika daraja la mbingu hadhi ya juu , lakini ni wanne tu ambao walikuwa na nguvu kubwa na waliitwa Wakuu wanne wa hadhi.
Baada ya majini wa nne kufika katika eneo hilo la juu majini wengine wa nne waliongezeka kukamilisha idadi yao ya kumi na mbili.
Majini hao wote hawakuwa ni binadamu, walikuwa ni majini watu na walikuwa wakiheshimika mno na kila mmoja alikuwa kiongozi wa koo katika familia yake ndani ya miliki hio ya Hongmeng.
Hongmeng ni miliki ambayo haikuwa na mkuu mmoja wa miliki bali Hongmeng ni kama mkusanyiko wa koo za kijini na watu , koo hizi karibia zote zilikuwa na wawakilishi wao katika ulimwengu wa kawaida mathalani katika taifa la China ambao hufuata maagizo yao.
Kwa mfano katika ulimwengu wa kawaida katika taifa la China unaweza kukuta koo kama vile ya Shigao , sasa ukija katika miliki ya Hongmeng kunakuwepo na koo ya Shigao.
Hongmeng unaweza kuifananisha na freemason, au Illuminat au Zeros organisation katika ulimwengu wa kawaida na hii yote ni kutokana na kwamba ni jamii ya siri yenye nguvu ambayo ina ushawishi mkubwa wa kimadaraka katika ulimwengu wa kawaida.
Hii ndio maana Yan Buwen na marehemu Afande
Yang Gongming waliunda ushirikiano kwa kushawishiwa na Athena ili tu Yan Buwen awe na nguvu ambayo itamuwezesha kuunda siraha za kisayansi za kuishinda Hongmeng na kuweka kiongozi wanaemtaka wao.
Majini hao kumi na mbili wa cheo cha mbingu walikuwa wakiheshimika sana sio kwa majini tu lakini mpaka katika ulimwengu wa kawaida katika taifa la China hususani hao wanne.
Wanne hao ni Wucheni huyu ni mkuu wa koo ya
Yan , alikuwepo Yanyun huyu ni mkuu wa koo ya Yanyun na hawa ni majini ambao wanaamini katika dini ya Kibudha na mbinu zao za mafunzo ya kuvuna
nishati za mbingu na ardhi zimejikita katika mafundisho ya Kibuddha., wengine ni Umini na Shombeli kiongozi wa koo ya watumia mapanga.
Hao wote wa nne levo zao za nishati ya mbingu na ardhi ni mwishoni mwa maji ya kiroho.
“Kwanini mmefanya safari ya kuja visiwa vya anga.?”Aliongea yule aliefahamika kwa jina la Wucheni.
Gefu na wenzake walimwangalia Anjiu ambae alikuwa amefumba macho , kwasababu ndio pekee aliekuwa na nguvu kubwa walimwangalia kama kiongozi wa msafara huo.
“Nadhani hakuna haja ya kuuliza hilo swali , nina uhakika utakuwa unajua nini kimetuleta”Aliongea Anjiu mara baada ya kufumbua macho.
“Hehe… Anjjiu mkuu wa miliki ya Xia , sisi tutajua vipi kama wewe hutaki kutuambia”
Wakati huo alieongea ni kijana mdogo kabisa mchina ambaye alikuwa ameshikilia feni , huyo ndio ambaye alijulikana kwa jina la Umini, kwa muonekano wake wa ujana ni ngumu kusema kama alikuwa tayari na miaka mia moja na ushee.
“Ijapokuwa miliki zote tatu hazijawahi kuwa na maelewano mazuri na Hongmeng lakini bado zipo katika ulimwengu mmoja wa majini watu , kawaida lazima tuwe macho kwa kila kinachotokea katika huu ulimwengu , ni matarajio yangu kwamba Hongmeng mtakuwa na taarifa kwamba sisi miliki tatu zenye nguvu tuliungana na kutengeneza kikosi maalumu ambacho kilienda ulimwengu wa kawaida kumshambulia binadamu Roma Ramoni lakini tukaishia kushambuliwa na miungu watatu na kupoteza pambano…”
Maneno ya Anjiu yalisababisha gumzo ndani ya eneo hilo hususani kwa binadamu na majini wa kawaida ambao wamehudhuria kikao.
Kwasababub hawakuwa na vyeo vya kuweza kupata habari kwa haraka hivyo ilikuwa ni kama jambo jipya kwao.
Baadhi ya majini hao wa Hongmeng ambao walikuwa na taarifa kuhusu Roma Ramoni wote walijawa na wasiwasi.
“Amitabha…. Je hili linatuhusu vipi sisi kama Hongmeng?”Mkuu mwingine wa Hongmeng aliefahamika kwa jina la Yanyun aliongea.
“Haha.. kuna haja ya kujificha hata katika wakati kama huu , wakati nyie mkijua kinachoendela katika miliki zetu na sisi pia tunajua nini kinaendelea katika miliki yenu”Aliongea Anjiu na kisha akampatia ishara Gefu mkuu wa miliki ya Panas kuendelea.
“Kulingana na taarifa ambayo tumeipata Hongmeng mlikuwa mkitamani kuona ushirikiano wa faida baina ya Roma na China lakini alikataa na kisha akaua baadhi ya wajumbe wenu…”Aliongea
Aliongea kuchagua maneno ya kuongea , ukweli ni kwamba alijua licha kwa nje inaonekana ni kama China ndio wanataka kufanya ushirikiano na Roma lakini nyuma ya pazia sio China bali ni majini hao maana walichokuwa wakitaka kutoka kwa Roma ni mbinu yake ya mafunzo pamoja na vidonge.
“Kubwa zaidi ni kwamba kwasasa dunia inapitia hali ya kushuka kwa joto kwa kiwango cha juu sana na mpaka sasa ninapoongea baadhi ya maeneo ya Kaskazini mwa China hayakaliki na mimea mingi inanyauka ….. licha ya Chaopi kuwa na nguvu kubwa ya kijini katika levo ya kuipita radi lakini alishindwa kudhibiti miungu wote watatu yaani Apollo mungu wa jua, Artemis mungu wa mwezi na Poseidon mungu wa bahari, nadhani baadhi yenu hapa mnajua uwezo wa miungu hawa na mshawahi kuushuhudia hapo kabla lakini kilichotokea kinamaanisha kwamba miungu uwezo wao sio kama mliouzoea ..inaonekana hata kushuka kwa kiwango cha joto kunahusiana na kuongezeka kwao nguvu…”.
“Acha kuongea ujinga “Aliingilia maongezi yake bwana aliefahamika kwa jina la Shombeli, alikuwa na uchebe ambao ameusuka kabisa na alikuwa akiuchezea kila sekunde kana kwamba kuna hisia flani anazipata.
“Pointi yangu ni kwamba kama miungu hawa nguvu zao zitaendelea kuongezeka sio tu kwamba tutakuwa katika hatari lakini pia hali za binadamu zitaathirika kwa kiasi kikubwa na athari hizi zitagusa mpaka ulimwengu wetu”Aliongea Gefu bila kumzingatia Shombeli.
Kila mmoja alikaa kimya , hata kama kauli yake ilikuwa kinyume lakini hakuna ambaye aliweza kukanusha kauli yake.
“Viongozi , najua hamuwezi kuhisia chochote kwasababu hamjapata hasara kama tulioipata sisi lakini mnapaswa kujua kwamba sisi hatuna kinyongo na miungu na kinyongo chetu ni zidi ya Roma pekee lakini nyie kwa upande mwingine mmekuwa katika kutokuelewana vizuri na miungu na ni swala la muda tu kuja kuwashambulia na kulipiza kisasi cha kihistoria”
“Gefu unatutisha sio?”Wucheni aliongea huku akipandisha sauti.
“Hawatishi bali anajaribu kuwaelezea kwamba mkijifanyisha wajuaji mnaweza kuwa wa kwanza kufa kabla hata ya sisi”Aliingilia Anjiu.
“Umekosa adabu wewe, unasema tunajifanyisha? Anjiu usione kwamba tunakuoghopa kwasababu umeweza kupanda levo , pigana na sisi kama una ujeuri huo”Shombeli alifoka akionekana kutoridhishwa na maneno ya Anjiu na palepale hakuishia kufoka tu alitoa upanga wake unao wakawaka kwenye ala na kumnyooshea Anjiu akionekana kabisa yupo tayari kwa vita.
“Shombeli huu sio muda mzuri”Aliongea Wucheni akijaribu kumtuliza na kisha akawageukia majini waliokuwa wamehudhuria kikao hicho.
“Wote ambao mpo chini ya levo ya Mbingu ondokeni katika kisiwa cha anga”Aliongea.
Majini wengi walishangazwa na kauli ile kwani sio kawaida kwa majini hao wa levo ya chini kuondolewa katika kisiwa cha anga lakini licha ya hivyo hakuna ambaye alibakia na ndani ya muda mfupi walibakia majini wa levo ya mbingu.
“Kwahio mpo hapa kwa ajili ya kutafuta msaada?”Aliuliza.
Itaendelea kwanzia hapa katika sehemu ya 751 tuone yule aliekutana na Roma Dodoma ni nani.





SEHEMU YA 750.
NORTH POLE -Central Arctic Sea/Ncha ya kaskazini.
Katikae eneo pana la tambarare ya barafu na theluji tukio la kushangaza kubwa sana na la kuogopesha lilikuwa likichanua taratibu taratibu na kimya kimya bila ya sauti yoyote.
Ilikuwa ni mti mkubwa sana na wa kushangaza wa rangi ya dhahabu ambao ulikuwa umechomoza kutoka katika funiko ya barafu na kwenda moja kwa moja juu angani.
Mti huu mkubwa wa dhahabu matawi yake pekee tu yalikuwa yamechukua eneo kubwa la mzingo kwa zaidi ya hatua za mraba elfu moja huku shina lake pana sana likienda mpaka chini kabisa ya bahari ambapo mizizi yake ilikuwa imetambaa kuelekea pande sizizojulikana chini ya bahari hio ya Arctic.
Kivuli cha mti huo kilikuwa ni kikubwa mno takribani mita elfu kumi , ilikuwa ni kama vile turubai limetandazwa juu angani na kufanya mwanga wa jua usipite chini , matawi ya mti huo yalikuwa ni kama vile ni Dhahabu iliomulikwa na mwanga na kung’aa.
Majani yake yalikuwa makubwa mno zaidi ya ndege ya abiria huku yaking’aa kila dakika ambayo jua huyafiikia.
Katika mti huo sio kwa majani , matawi wala shina kila mahali kulikuwa na maandishi ambayo yalikuwa yakitoa mwanga na kufifia kwa namna ya kubipu.
Kuzunguka eneo la mti huo kilomita kadhaa kulikuwa na kitu kama karatasi la rangi ya njano kama uzio hivi ambapo lilikuwa kimezunguka na kutengeneza duana na kisha kwenda juu angani kwa kimo kikubwa mno.
Ukuta huo ukiachana na kazi yake ya ulinzi ulikuwa na kazi ya kukusanya mtiririsho wa nishati ya jua kufikia mti wa kimaajabu ambao husharabuu nishati yake mara moja.
Katikati ya kivuli cha mti huo kulikuwa na eneo ambalo linawaka waka na vivuli vya watu wawili vilikuwa vinaelea katika nusu anga chini ya shina la mti huo.
Walikuwa ni mwanaume na mwanamke ambao walikuwa wakimulikwa na mwanga wa dhahabu unaotoka katika mti huo kwa wakati mmoja na kama utaangalia kwa ukaribu utagundua kwamba licha ya kumulikwa na mwanga lakini pia kuna nguvu iliokuwa ikitoka katika vichwa vyao na kunyonywa na matawi ya mti huo wa kimaajabu.
Yaani ilikuwa kila mara baada ya nishati kutolewa katika mti huo kuwafikia kichwani na kuisharabu, nguvu nyingine inawatoka na kwenda kuuvaa mti huo Chini ya mti huo kutokea kwenye bahari ambako shina hupatikana nishati ambayo ilikuwa katika mfumo wa ukungu wa mwanga wa njano ilikuwa ikitoka kama vile ni mvuke na kusambaa angani kwa kiasi kikubwa mno.
Eneo lote hilo lilibadirika rangi kutoka ile rangi nyeupe ya barafu na theruji na kuwa rangi ya njano ya Dhahabu na kila kilichokuwa kikifanyika hapo hakikutoa sauti hata kidogo , kila kitu kilikuwa kikifanyika kimya kimya.
Wakati mti huo ukiendelea kunyonya nishati ya jua na kuibadilisha kwenda kuwa nishati nyingine ambayo inatokea chini ya bahari kwenye shina na kusambaa kama mvuke katika uso wa dunia hatimae waliweza kufika watu wengine wawili ndani ya eneo hilo ukiachana na wale ambao wapo.
Yule mwanamke na mwanaume ambao wote walikuwa wakibadilishana nguvu na mti huo waligeuka na kuangaliana , baada ya kuangalia
mwanaume na mwanamke waliovunja ukuta na kuingia wote walionyesha hali ya utulivu katika sura zao, kilichokuwa kikiendelea hapo hakikuwashangaza hata kidogo ilikuwa ni kama mti huo walishauona hapo kabla.
“You have worked hard Ares and Aphrodite , that bi*ch is mean by only letting the two of you help the ‘Mother Tree’ to recover , isn’t too tiringi…?”
“Mmefanya kazi kwa juhudi Ares na Aphrodite , yule Kahaba ni muonevu sana kuwaacha nyie wawili pekee kuusaidia ‘Mti Mama’ Kupona … si inachosha sana?”
Aliongea alikuwa ni mwanamke alievalia gauni la rangi ya kijani na alikuwa katika tabasamu lililojaa mapozi , mwanamke huyu alikuwa ni Rozu jini chotara kutoka miliki ya Panas.
Mwanamke na mwanaume ambao walikuwa waking’aa kama jua kutokana na kumulikwa na mwanga wa mti huo wa kimaajabu alikuwa ni Christen na Ares ambao Roma alikuwa akiwatafuta hewani hawapatikani.
“Baada ya kipindi kirefu sana hatimae kwa hiari yako mwenyewe umeamua kujitokeza , tulidhania utaendelea kuficha kichwa chako huku ukionyesha mkia wako huku ukimfanya Hermes kuwa msemaji wako,… Habari za miaka elfu tatu bila kuonana Hera”
Rozu alikuwa ni sehemu ya miungu , yaani viumbe kutoka sayari nyingine na jina lake halisi alikuwa ni Hera mungu wa mbingu.
“Sikupenda kujificha ni kwamba tu sipendeelei kuja huku ulimwengu wa kawaida lakini hali imebadilika sasa , sikutegemea huyo kichaa kufanikiwa kutumia moyo wa Gaia kuupanda upya Mti Mama”Aliongea Hera.
“Hera acha maigizo , sidhani kama ni kweli hupendi kujitokeza bali ukweli ni kwamba uliona ni ngumu kufanya mambo yako katika ulimwengu huu wa kawaida na kujificha”
“Kwanini unasema hivyo Aphrodite?”Aliongea akiwa ameelea hewani kama vile ni malaika na alijiegamiza kwenye jani la mti huo huku akinusa harufu yake.
“Kwanini usikubali tu kile ambacho ulikuwa ukifanya , Hephaestus ndio mtu pekee ambaye anaejua mkanda wangu unavyofanya kazi , unayoonekana na namna ya kuutengeneza hivyo moja kwa moja inamfanya yeye ndio katengeneza ule mkanda feki ulionekana nchini Tanzania. Mamlaka ya utengenezaji wa vitu feki anaipata moja kwa moja kutoka kwako , hivi unadhani hatukujua ni wewe mara baada ya kujiigiza ni Athena kwa kipindi kirefu kwa kutumia Sarafu feki na Ua la Blue
Orchid…”Aliongea na maneno yale yalimfanya Hera kushangaa kiasi baada ya siri yake kugundulika..
“Kwahio hii ndio topiki ambayo unaongelea .. ni aibu kwamba kila nilichofanya hakikufanikiwa lakini ninachoweza kulaumu ni mbinu yangu ya Ushirikina wa kinajimu kwa kushindwa kuwa na nguvu na kushindwa kutabiri matokeo”
“Ushirikina wa kinajimu!!?”Christen alishangaa na vilevile kwa Ares.
“Hera hio mbinu si ndio inayotumiwa na majini kufanya utabiri wa kinabii kama ilivyo Karama ya Athena ya unabii na Almanaki ya Hades wa zamani?, unataka kumaanisha kwamba jini aliefanya ule unabii kwa kutumia hio mbinu hakufariki?”
“Haha.. upo sahihi ..nilifikiria kwa kipindi kirefu sana kumshinda Athena kwa kila namna na ndio maana nilitafuta njia ya kuishinda Karama yake ya kinabii na juhudi zangu zilinichukua miaka elfu moja kuweza kukusanya vitabu vingi sana vya kihistoria katika kila miliki na koo za kijini ili kuweza kubobea katika Ushirikina wa kinajimu”
“Inamaana ulijificha katika ulimwengu wa majini kwa ajili tu ya kufunza hio mbinu , hakika uvulimivu wako ni wa viwango lakini kwa bahati mbaya ni kwamba wewe sio mtu sahihi kuweza kumshinda Athena kwa namna yoyote , hata Almanaki ya Hades wa zamani haifui dafu mbele ya Nguvu ya Karama ya kinabii aliokuwa nayo Athena”
“Haha.. hilo natambua lakini sio mbaya kwani mpaka sasa ninachoona Athena unabii wake siku zote haujawahi kuwa sahihi kwa asiliimia mia moja , hii inamaanisha kwamba siku moja mbeleni mambo yanaweza kuwa tofauti nje na matarajio yake kitu ambacho kinanitekenya mno..”Aliongea Hera.
“Kwahio hampo hapa kwa ajili ya kuingilia hili si ndio?”Aliuliza Christen kwa wasiwasi.
“Hey Aphrodite unawaza nini?,Hata kama hatumpendi Athena haimaannisi kwamba hatutaki kufufuka kwa ndugu zetu , huu ni Mti Mama na hatutaki kutokuwa na heshima mbele ya Gaia , Mama wa asili yetu”Aliongea Hermes.
“Mpo nyie wawili tu , itachukua muda mrefu sana mpaka kuurudisha huu mti katika hali yake ya kawaida na kuanza hatua ya kubadili hali ya kidunia
, kwanini Poseidon na Apollo hawajaja kuwasaidia?”Aliuliza Hera.
Christen aliishia kutoa pumzi ya ahueni mara baada ya kujua hao wawili hawajafika hapo kwa ajili ye kuleta matatizo bali wamekuja kuangalia kile kinachoendelea.
“Kulingana na makadirio ya uasili wake , Athena anatumaini kukusanya baadhi ya nguvu za kiuungu ambazo zimesambaa katika mifupa ya miili ambayo roho zilipotea na baadhi ya mabaki ya kale ya kiuungu na kuamsha baadhi ya nafsi kwanza , baadae kwa kujumlisha miungu wote kumi na moja tutakuwa na uwezo wa kuiamsha nguvu ya damu ya Titan ili kuamsha asili kamili ya Mti Mama. Lakini Athena alifanya utafiti na kugundua kwamba dunia ina utofauti sana na Mars lakini hata hivyo amegundua katika kiini cha dunia kuna uwepo wa madini yanayofanana na yale ya sayari yetu ambayo yatakuwa na uwezo wa kuamsha damu ya asili yetu, ili mradi muda uliopangwa kutimia , roho zilizopotea zitarudi kuwa na nguvu yake na damu yetu itaanza kufanya kazi upya na kadri dunia inavyopitia mabadiliko ndio asili yetu itakavyoanza hatua za kuweza kumudu mazingira ya dunia , ndio maana mpaka sasa ameachana na zile Clones zilizotoka katika damu ya Hades , isitoshe uungu wao sio mkamilifu hivyo kufanya iwe ngumu sana kutumika , kazi yetu mimi na Ares ni kuhakikisha tunausaidia huu Mti Mama kuweza kutengeneza mazingira ya kidunia ili kuamsha nafsi za wenzetu kwanza pamoja na mazingira ambayo uzao upya utamudu hali ya hewa , majukumu yetu sio makubwa sana haina haja ya kupata msaada”
“Vizuri , inaonekana kabisa Athena amefanya makosa katika mahesabu yake na unabii wake pia sidhani kama utaweza kutimia, kubwa zaidi ni tatizo alilokuwa nalo yeye mwenyewe … hehe”
“Lakini anachotaka kitokee ndio hiki mnachoona kwa macho yenu kinakaribia kutimia”Aliongea Christen lakini Hera alipotezea na kuanza kuangalia mazingita ya eneo hilo hususani barafu iliokuwa imezidi kujiongeza kwa mbali.
“Sikuwahi kuwaza kama Mti wa Uzazi utafanikiwa kukua na kustawi katika mazingira ya dunia lakini kwa ninachoona hapa ni kwamba kama kiini cha dunia kikaathiriwa na huu mti , sidhani kaa athari zitakazotokea ni dunia kupoteza joto tu …ni rahisi kutabiri binadamu ku… kuweni tu makini”
“Hey ….binadamu na majini ni viumbe ambavyo asili yao ni majongoo wanaotambaa wa hadhi ya chini kabisa na kama kipindi kile sio kutelekeza miili yetu majini na binadamu wasingeweza kutuletea ukinzani na tungekuwa tushawafuta katika uso wa dunia , kinachokwenda kutokea ni utawala mpya uliochelewa kwa miaka elfu ishirini”Aliongea Hermes akiwa amepamba uso wake na tabasamu lililojaa uovu.
“Kama kilichowaleta ni kuangalia mnaweza kuondoka mti upo salama kwani kuna uzio tayari wa ulinzi”Aliongea Christen akiwa katika hali ya kukasirika huku akionyesha hali ya huzuni kwenye macho yake kutokana na kauli ya Hermes.
“Najua una hasira na nilichokufanyia lakini sina pakwenda kwasasa , nadhani itakuwa vizuri kama nitaendelea kupumzika hapa hapa .. ijapokuwa binadamu wa kawaida hawezi kufika hapa lakini kama mtu mwenye nguvu za kijini au majni wenyewe kufika hapa na uwepo wangu hamtokuwa na wasiwasi kuendelea kuuhudumia mti wetu wa uzao katika hali ya utlivu”
“Haina haja kama kweli watakuja itanifanya kupunguza uchomvu wangu kwa kupambana nao”Aliongea Ares.
“Muda huu naamini Roma tayari ashaenda ulimwengu wa majini watu kwanini usiende na kuangaia kinachoendelea?”Aliongea Hermes
“Haina haja tena , mpaka sasa vita hio imekwisha kufeli , Hades anatembea kwenye hatua alizoandaliwa na Athena katika mipango yake”Aliongea akimaanisha kwamba Roma kwenda kuua majini ni mpango wa Athena , pengine ili kutoweza kuingiliana na hicho kinachofanyika hapo.
Mara baada ya kuongea kauli hio alikwenda kutua juu ya jani la mti huo wa kimaajabu ambalo lilianza kunesa nesa na ajabu ni kamba lile jani pana lilijikunja kidogo kana kwamba linampa nafasi Hera kulala bila kupata shida.
Ares na Aphrodite waliangaliana na wote kwa pamoja waliishia kutingisha vichwa vyao kwa namna ya kusikitika.
Mother Tree ni mti ambao unahistoria yake ambayo tutaiona mbele lakini kinachofanyika hapo ni kwamba unanyonya nishati ya jua na kuipeleka chini kwenye mizizi na baada ya hapo inageuza nishati hio na kudhalisha nishati nyingine ambayo inasambaa katika uso wa dunia.
Hivyo kwa lugha nyepesi sio tu kwamba dunia inapitia hatua za kushuka kwa hali ya joto bali nguvu ya nishati ambayo inasambaa kutoka katika mti huo ina athari zake.
Je ni kwanini Hera alikuwa akijifanyisha kuwa Athena , kama kweli alikuwa akijifanyisha ni vitu gani aliweza kufanya na akafanikiwa na vipi alifanya akafeli.
Almanaki ni sawa na Kalenda , ndio ambayo wanaitumia Ant- Illuminat kutabiri matokeo yajayo hivyo ni sawa na kusema ni Kalenda ya kinabii ambayo mmiliki wake ni Hades wa Zamani.
Sasa Athena na yeye ana karama yake ya kinabii hivyo inatuonyesha kitu kimoja kwamba pengine kuna utofauti kati ya unabii uliokuwa katika Kalenda ya Hades na unabii wa Athena.
Tukumbuke kwamba wakati Athena akianzisha mipango yake na Hades na yeye alianzisha mipango yake ya kwenda kinyume na mipango ya Athena je nani atashinda tusichoke kuendelea kufatilia bado vipande hamsini tu kukamilisha mwishoni utashangaa.
MWISHO WA SEASON YA 25.










*****
Good and clear
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware

SEHEMU YA 748.
Edna alikuwa amekaa kwenye kiti chake kimapozi kabisa na mara baada ya kusikia swali hilo kutoka kwa Roma aliweza kuona sura zote zikimgeukia yeye na alinyanyua kikombe cha kahawa na kunywa kidogo na kisha akakiweka chini.
“Kama nilivyokwisha kusema , sikuwa nikielewa nini kinanitokea , nilichotaka ni kuwaua kwasababu walinikasirisha mara baada ya kumteka Lanlan , sijui nimewezaje lakini ni kama vile kuna sauti iliokuwa ikiongea na akili yangu na kuniambia niwagandishe ili iwe rahisi kuwafyeka na hata kumwambia Yezi anipatie upanga wake ni kama vile sio mimi nilie ongea , ilikuja tu nikafanya hivyo..”Aliongea Edna na sauti yake ilionyesha ni kwa kiasi gani alikuwa hadanganyi, haikuonyesha kama kuna siri ambayo alikuwa akificha , ukweli ni kwamba alionekana kama vile amechoka sana na kuonekana kutia huruma kwa namna ambavyo anaulizwa maswali , ni kama vile mgonjwa aliepoteza kumbuumbu akilazimishwa kukumbuka kitu.
Roma alimwangalia Edna kwa dakika kama moja hivi na kisha alivunja ukimya kwa kucheka.
“Usiwaze sana kuhusu hilo , kama huelewi nini kilikutokea haina haja ya kuumiza kichwa , kwangu kitu muhimu ni wewe na Lanlan kuwa salama basi”Aliongea Roma na palepale alisimama na kumwangalia Latina.
“Latina mkuu wa Dhehebu, majini kutoka ulimwengu usionekana wamejionyesha katika ulimwengu unaonekana na kuchokoza familia yangu ni muda wa mimi kulipa fidia lakini kabla ya kuondoka hapa nina ombi moja kwako”
“Mr Roma sio kwamba tunataka kwenda kinyume na maneno yetu au kwasababu sisi ni wakatili lakini kama tutavunja sheria ambazo zimewekwa karne na karne na kwenda kushambulia ulimwengu wa majini watu matatizo yatatupata sisi..”
“Umenielewa vibaya Mkuu wa Dhehebu , mimi ndio ninaenda mwenyewe ulimwengu wa majini watu ni kwamba tu ninahofia usalama wa familia yangu , ijapokuwa miungu ipo karibu itakuwa ni vizuri kama nyie wote wawili mtakuwepo hapa”
Aliongea Roma isitoshe kwasababu Latina alikuwa tayari katika levo ya kuipita radi na kumiliki mikia saba , uwezo wake wa kimapigano ulikuwa ni mkubwa mno na hakuna uwezekano wa kuzidiwa na majini jamii ya watu ndio maana Roma aliona ingekuwa salama zaidi kama atabakia hapo kisiwani kwa ajili ya kuipa ulinzi familia yake na hapo ndio hatokuwa na wasiwasi.
Hakukuwa na madhara kwa majini hao kuendelea kubakia hapo visiwani na ukweli ni kwamba walitamani pia kuangalia namna mazingira ya dunia yalivyo lakini kubwa zaidi kama watakubaliana na ombi la Roma ni kama wanatengeneza deni ambalo Roma atakuja kulilipa.
Na mara baada ya Latina kufikitia faida zote hizo moja kwa moja alimkubalia Roma kubakia hapo kisiwani kwa ajili ya kuilinda familia yake, yeye pamoja na majini wenzake Weni na Yunu huku wakimwambia Roma ahakikishe anazigeuza majivu miliki za majini hao lakini Roma aliona uwezo huo hana , kitu pekee ambacho anaweza kufanya ni kuua majini wengi na kisha kukimbia bila kupatwa na majeraha.
Mara baada ya kusikia Roma anakwenda kuwalipizia kisasi kwa kuchokozwa na majini warembo hao walikuwa ni waelewa juu ya hatari ambayo Roma anakwenda kujiingiza lakini hata hivyo hawakutaka kumzuia.
Ukweli ni kwamba ugomvi kati ya majini na Roma umefikia katika hatua mbaya sana kutokana na majini hao kupoteza washirika wao wengi na kama Roma hatofanya mashambulizi ya haraka wakiwa katika hali mbaya kama hio wanaweza kujijengea nguvu na ni swala la muda tu kuja tena kumchokoza hivyo muda sahihi wa kuvamia miliki hizo za majini ni wakati huo.
Mara baada ya matayarisho hatimae Roma aliaga na kuondoka lakini hata hivyo hakuelekea moja kwa moja katika ulimwengu wa majini.
Kabla ya kuanza safari yake alitafta watu wawili kwa kutumia simu lakini hakuna ambaye alikuwa akipatikana na hio ndio sababu ya kuchukua uelekeo mwingine na kufumba na kufumbua ilikuwa ni kama vile ametumbukia kwenye shimo la anga na alikuja kuibukia katika kilele juu ya safu za milima ya Alps upande wa Switzerland.
Upepo mkali uliokuwa ukivuma katika kilele hicho kilichofunikwa na barafu kubwa ilifanya hata wale watalii ambao wanapenda kukwea mlima kama sehemu ya utalii kuacha kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ya dunia.
Ilikuwa ni usiku wa manane na hakukuwa na dalili ya binadamu yoyote kuwepo katika mlima huo , ilikuwa ni kama vile shughuli za kitalii zimesitishwa kwa muda.
Roma palepale uso wake ulimbadilika na kuwa mweusi tii na aliweza kufungua ‘space seal’ na kufanya mawe makubwa yaliokuwa katika mlima huo kuanza kuporomokoka, ilikuwa ni kama vile kuna mlipuko unaotokea juu ya mlima huo.
Kitendo kile cha kutumia kanuni za anga kujaribu kuharibu mlima ilifanya milango minne ya anga kufunguka na sura za watu wanne kuonekana ambao ni Apollo , Artemis , Poseidon na Hermes.
Mara baada ya kumuona ni Hades walishajua Roma katumia kanuni za anga kujaribu kuwaita katika hilo eneo.
“Hades , it isn’t good to breach the treaty of god in the middle of night when there is no need to fight”Aliongea Hermes akimaanisha kwamba haina haja ya kuvunja sheria za mkataba wa miungu wakati huo wa usiku mnene ili hali hakuna haja ya kupigana.
“The gods treaty! , sidhani kama kuna haja ya kuwepo kwa hichi kitu kinachoitwa mkataba tena”Aliongea Roma mara baada ya kuwakagua mmoja mmoja.
“Hades unamaanisha nini kusema hivyo?”Aliuliza Artemis huku akiwa amekunja ndita.
“Malengo ya sheria za ’The gods treaty’ ni kuzuia majini kujitokeza katika ulimwengu unaonekana na kuanzisha vita na miungu ili kudumisha amani na usalama wa binadamu, lakini ukweli ni kwamba mkataba huu ulitengenezwa kutokana na hali ilivyokuwa hapo zama za kale wakati kila pande ilikuwa ikitaka kubakia kuwa salama, lakini kwa sasa hali ni tofauti kwani tayari moyo wa Gaia unaendelea kufufuka na kufanya nguvu zenu kuongezeka maradufu na kama hii itaendelea inamaanisha kwamba miungu mtakuwa na nguvu kubwa kushinda hata majini na wavuna nishati za mbingu na ardhi na kutokana na jambo hili linaloenda kutokea, je kuna haja ya uwepo wa hiki kitu kinachoitwa ‘ the gods treaty’?, Apollo , Artemis na Poseiidon mnao uwezo wa kupigana na majini wakuu kutoka katika miliki tatu na kushinda mnadhani mimi ni mtu ambaye siwezi kuchanganua mambo? , Hermes wewe unaishi karibu na visiwa vyangu lakini hukujitokeza kwasababu ulikuwa na uhakika watatu pekee wanaweza kudili na kundi lote la majini, je nakosea?”
“Upo sahihi , lakini je kuna tatizo juu ya hilo? , mimi natokea katika ukoo wa wanywa damu hivyo mara nyingi mchana ndio wakati wangu wa kulala na usiku ndio wakati wa mawindo”Aliongea Hermes.
“Acha matani basi, hivi nyie mnaniona mimi ni mjinga eti? Majini watu wanaweza wasijue kiwango cha nguvu zenu lakini mimi pia nina uungu ndani yangu na wakati huu ambao nipo karibu yenu ninaweza kuona ni kwa namna gani mlivyokuwa na nguvu , kulingana na mapigano yaliotokea mapema ya leo majini wasingekuwa na uwezo wa kukimbia kama wote wanne mngejitokeza , mngekuwa na uwezo wa kuwaua wote lakini kwanini mkawaachia makusudi kabisa wakimbie?”Roma alianza kukosa uvumilivu na hasira alizionyesha waziwazi.
“Kwahio ndio unatulaumu , Hades familia yako kwa upande mwingine ipo salama shida iko wapi?””Aliongea Apollo huku akitingisha kichwa.
“Bado tu mnafanya maigizo mbele yangu , nilidhani sisi ni marafiki lakini inaonekana kuna kitu muhimu sana mnanificha , lazima kuna mpango mnauendeleza nyuma ya pazia ambao mimi si ujui”
“Hades stop making wild guesses , you are our companion”Aliongea Artemis akimwambia Roma aache kufanya makisio mabaya kwani yeye ni mwenzao.
“Mimi ni mwenzenu?, kama kweli mimi ni mwenzenu niambieni kwanini mpaka wakati huu nimeshindwa kuwasiliana na Aphrodite na Ares , kwanini hawapatikani hwani ni wapi wameenda?”
Miungu hio minne ilibakia kimya huku sura zao zikishindwa kusomeka ni kipi wana kiwaza.
Katika watu wawili ambao Roma Alijaribu kuwasiiliana nao kabla ya kuja hapo ni Christen na Ares na kwa hali isiokuwa ya kawaida wote hawapo hewani jambo ambalo sio la kawaida.
“Poseidon wewe unaishi Hawaii na mara nyingine upo Hongkong umbali ambao ni mrefu sana kuliko Urusi anapoishi Ares lakini wewe umefanikiwa kufika visiwa vya wafu mapema na Ares hajatokea , lazima kuna sababu kubwa kwa mtu mpenda vita kama Ares kutokujitokeza na kushiriki katika mapigano na hio ni kwasababu kuna kitu cha muhimu zaidi ambacho anafanyia kazi , je makisio yangu yapo sahihi?”Aliuliza Roma.
Kwa tabia ya Ares kupenda vita hakika isingekuwa rahisi kuvumilia kutokuja kupigana na majini.
“Tunaju vipi ni kipi kinaendelea katika maisha yao”Aliongea Poseidon kikauzu kabisa huku akimwangalia Roma usoni.
“Lazima wanachokifanya lazima kunahusiana na Moyo wa Gaia si ndio?”Wote kimya na kumfanya Roma kuendelea kuongea.
“Kabla ya hili kutokea nilikuwa nikijaribu kuwaza lakini nadhanni mpaka sasa nimeupata ukweli , kupotea kwa joto la dunia lazima kunasababishwa na kufufuka kwa Moyo wa Gaia , Wakati Athena alipoweza kuupata moyo huo kule Korea Apollo , Athena na Artemis mliweza kuongea kwa kutumia lugha yenu kwa njia ya kimawazo na inaonekana hili ni swala ambalo mlilitarajia”
“Hades we …”Apollo hakutaka kuona Roma anaumia na ndio maana alisita kumalizia sentensi yake na kufunga mdomo lakini kitendo kile kilimfanya Roma kucheka sio kicheko cha furaha bali kicheko cha uchungu.
“Haina haja ya kuwa na wasiwasi juu yangu hata kama hamtoniambia basi lazima itakuwa ni kwasababu ya Athena , sina uhakika ni jambo gani analipanga na sina uhakika na mnachokipanga lakini niwaonye tu msije kufanya jambo la kijinga la kuhatarisha usalama wa watu wangu wa karibu la sivyo siwezi kujizuia kuonyesha ukatili wangu”Aliongea Roma kibabe.
Macho yake yalikuwa yakionyesha nia ya kimauajji , ilikuwa ni kama vile ametawaliwa na pepo kwa namna ambavyo alikuwa akionekana.
Upepo uliendelea kuvuma huku kila mmoja akiwa kimya bila ya kuongea kitu lakini ni muda uleule Hermes alitoka angani na kuja kutua karibu na alipo Roma na kumwangalia usoni akiwa na tabasamu la kejeli.
“I believe in your words Hades , but remember what I told you that day , I know you don’t believe me but if my words come true one day , you’ll have to remember your words today .. that is somethig I’ m looking forward to”(Naamini katika maneno yako Hades lakini kumbuka nilichokuambia siku ile , najua huniamini lakini kama maneno yangu
yatakuja kuwa kweli siku moja utapaswa kukumbuka meneno yako ya leo .. hicho ni kitu ambacho natarajia…”)
Mara baada ya Hermes kuongea maneno hayo palepale alipotea kwa namna ya kutumbukia kwenye anga , maneno yake hayakuwa katika hali ya urafiki kabisa , yalikuwa ni kama vile yapo katika mtindo wa onyo kwamba kama maneno yake yatakuja kuwa kweli basi lazima Roma akumbuke maneno yake alioongea siku hio.
Roma macho yake yalionyesha ishara ya maumivu lakini yalipotea haraka sana na alionekana katika kuwaza.
Artemis na Apollo wao hawakuongea kitu na waliishia kuangaliana na kisha na wao wakapotea.
Ni Poseidon peke yake ambaye alikuwa amebakia na alimwangalia Roma machoni bila ya kukwepesha macho kwa namna ya kujiamini.
“Don’t think too highly of yourself young man , having a good temper is beneficial , but it is also dependent on the other party , sometimes complacency is foolishnes”
“Acha kujiona mwamba kijana , kuwa na utulivu kuna faida zake pia , lakini inategemea na upande mwingine , muda mwingine kuridhika sana ni ujinga”
Mara baada ya kuongea kauli hio na yeye pia alipotea katika giza totoro na kumuacha Roma nyuma akiwa amekunja ngumi na kung’ata meno kwa hasira kwa dakika kadhaa mpaka alipokuja kuvuta hewa nyingi na kupumua.
“Je kila ninachofanya ni kama ilivyotabiriwa na huyo mwanamke kama alivyosema Aphrodite juu ya unabii , ni kweli kesho yangu ya baadae imekwisha kuamuliwa , je kuna namna ya kubadilisha kesho yangu?, Kama ni hivyo si kila ninachokifanya ni kile alichokipanga , lakini kama kweli siwezi kuibadilisha kesho yangu ni kwa namna gani alitabiri nitakuja kufanya maamuzi yasiokuwa ni ya kutarajiwa?, hakuna wa kuniambia ni kipi ni sahihi na kipi sio sahihi na hii yote ni kutokana na uwezo wake ni mkubwa kuzidi wote na hawezi kusalitiwa , je ni kitu gani ana jaribu kukamilisha , nini kitatokea kama moyo wa Gaia utaendelea kunyonya nishati ya jua?”
Roma kichwa chake kilikuwa katika mawazo na kujiuliza maswali mengi,kuna mambo mengi ambayo hakuambiwa na ilikuwa ni kama kila anachokifanya tayari kilishakwisha kutegemewa na jambo hilo linamfanya kutokujua ni ipi njia sahihi ya kuchukua , anajiuliza je kuna uwezekano wa kubadilisha kile ambacho kitamtokea baadae lakini anakuwa katika hali ya kuchanganyikiwa na hio yote ni kutokana na kukosa majibu.
Ilikuwa ni kama kuna mkono ulioshikilia rimoti ambao ulikuwa ukimwendesha kama shushu lakini licha ya yote hayo hakuwa na namna ya kufanya chochote , hali hio ilikuwa ikimpelekea kujihisi ukichaa.
Watu ambao alihisi ndio marafiki zake walikuwa ni kama wageni machoni mwake.
“Au nilikuwa nikijidanganya mimi mwenyewe , hata hivyo siwezi kujilinganisha nao kwani wameishi muda mrefu na mimi kwao ni mtoto”Aliwaza Roma.
Ukweli ni kwamba Roma hakuwa na jinsi kwanzia alivyoweza kuachana na Hades wa zamani na maneno aliomwambia , maneno ambayo Aphrodite aliomwambia na maneno ambayo Hermes alimwambia ni kama yanaanza kutimia.
Aphrodite alimwambia kabisa Roma kwamba ikitokea siku ambayo Athena amepata jiwe lingine la kiuungu basi asije kumwamini hata yeye na kauli hio ilikuja kuthibitika katika wakati huo , miungu hio yote ilionekana tayari imekwisha kutengeneza ukuta wa undugu baina yao.
Roma alidumu kwa zaidi ya nusu saa akiwa katika hali ya kufikiria na mara baada ya kuona hakuwa na majibu aliamua kupotezea maswala hayo kwanza na kuamua kudili kwanza na majini ambao ndio kipaumbele chake kwa wakati huo.
Ngoja nikapunguze mawazo kwa kuua majini kwanza”Aliwaza Roma na palepale alipotea katika anga kwa spidi ya kupepesa macho.

















SEHEMU YA 749.
Hapo kale jumuia ya majini wa Hongmeng ndio ambao walikuwa na nguvu zaidi katika ulimwengu wote ule unaonekana na ule usionekana, nguvu yao ilitokana na kuwa na majini wengi ambao walikuwa levo za juu sana na kujitengenezea ushawishi kati ya binadamu.
Mara baada ya ujio wa viumbe kutoka sayari nyingine na kutokea kwa vita baina yao ndio wakati ambao Hongmeng ilipoteza ule utukufu wake licha ya kwamba mwishoni ni kama ilishinda vita hio kwa kufanikiwa kumkamata Zeus huku Athena yeye akikimbia lakini ki uhalisia ni kama vita hio haikuwa na mshindi ndio maana kukaja kutokea kwa kitu kinachoitwa The gods Treaty.
Mkataba ambao ulitokea kwasababu pande zote mbili zilihitaji kuishi , yaani Hongmeng walitamani kuendelea kuishi na miungu na wenyewe walitamani kuishi na kutokana na mahitajio yanayofanana ikawa sababu ya pamoja ya kutengeneza mkataba unaolinda pande zote.
Unachopaswa kujua wakati wa viumbe kutoka sayari nyingine wanatua duniani kulikuwepo na miliki nyingine za kijini kama vie Xia na Kekexil lakini majini wa miliki hizi hawakujihusisha na vita hivyo kutokana na kwamba hawakujali sana binadamu wala maswala ya dunia.
Vita baina ya miungu na majini iliipelekea
Hongmeng kupata hasara kubwa, hasara ambayo ilipelekea kupoteza kwa wanajeshi wao wenye uwezo wa juu wa nguvu za mbingu na ardhi na hali hio ya hasara moja kwa moja ilifanya miliki nyingine za kijini kuwa na nguvu kuliko Hongmeng..
Lakini hata hivyo mpaka leo hii licha ya kwamba miliki hii ilikuwa haina majini wenye nguvu kama vile miliki ya Kekexil na Xia lakini ndio miliki ambayo haikuwahi kushambuliwa na miliki nyingine.
Sio kwasababu miliki nyingine ilikuwa ikiogopa kuishambulia Hongmeng , ukweli ni kwamba miliki kama ya Xia itataka kuishambulia Hongmeng ikiwa nje ya eneo lake la miliki basi Xia itashinda lakini kama miliki ya Xia ikitaka kuishambulia Hongmeng ikiwa ndani ya eneo lake basi majini wa Xia watashindwa.
Sababu kubwa ya Xia kushindwa kuishambulia Hongmeng ikiwa katika eneo lake ni kwasababu miliki ya Hongmeng ilikuwa ikipatikana katika safu ya visiwa vinavyoelewa angani , visiwa ambavyo hulindwa na mfumo wa nguvu za maajabu za kijini zilizoasisiwa tokea zama hizo na majini waliokuwa na akili kubwa.
Ukiwa kilomita kadhaa kutokea miliki ya Xia utaona ni kama vitu kama vichuguu vinavyoelea angani huku vikichemka huku chini yake vikiwa vimefunikwa na mawingu makubwa kiasi kwamba huwezi kuona ardhi ya chini ilikuwa na nini.
Visiwa hivyo vilikuwa ni vya maajabu mno na vyenye kushangaza sana na kadri ambavyo unasogea karibu zaidi ndio utaweza kuona nguzo kubwa kama za mwanga wa njano hivi ambazo ni kama vile zimeshikilia visiwa hivyo ili vielee angani huku nguzo hizo zikitoa mng’ao flani wa herufi za kimaajabu ajabu.
Inasemekana kwamba hata majini wa Hongmeng wakati wanakuja ndani ya visiwa hivyo hawakujua ni kwa namna gani vilikuwepo vikielea angani au ni nani alihusika katika ujenzi wake , wanachoamini tu ni kwamba hapo enzi kulikuwa na majini wakuu wenye nguvu na maarifa mengi ndio waliohusika katika ujenzi wake.
Visiwa hivyo vilikuwa ni vingi lakini ambavyo vimejengwa katika kimo kinachotofautiana , kulingana na tamaduni za miliki hio kadri kisiwa kinavyoenda hewani ndio ambavyo hadhi yake huwa kubwa na ndio hukaliwa na wale majini wenye nguvu na vyeo vya hadhi.
Juu ya visiwa hivyo asili ilikuwa ni kama ilivyo kwa ardhi ya kawaida na ajabu ni kwamba katika kingo za visiwa hivyo kuna mito iliokuwa ikiteremsha maji kwenda chini huku chanzo chake kutoka juu ya kisiwa hakionekani.
Kisiwa cha mwisho kabisa kwenda juu kulikuwa na kisiwa kidogo sana ambacho kuna jengo ambalo lipo kwa umbo la Pyramidi ambapo limezingiwa na safu ya mwanga wa njano ambao huzunguka wakati wote.
Eneo la kisiwa hicho ndio husemekana kama eneo takatifu zaidi kwa miliki hio na Hongmeng wanaamini ndio misheni yao kulinda eneo hilo.
Inasemekana kwamba jengo hilo la Piramidi hutumika kama gereza na roho za majini pepo waliowahi kuwa na nguvu na kutaka kushambulia majini watu walifungiwa humo lakini pia roho ya Zeus na yenyewe imefungiwa ndani ya gereza hilo la kisiwa cha anga.
Gereza hilo mpaka leo hii majini pamoja na binadamu hawajui jina halisi wala teknolojia iliotumika kulitengeneza lakini wenyewe wakalipatia jina kama Gereza la Roho na Pepo .
Sasa mfumo wa uundwaji wa visiwa hivyo katika miliki ya Hongmeng ulikuwa ukiwalinda kwani ni kama vile kuna uzio ambao unawafanya majini wenye nia mbaya wanaotaka kufika katika miliki hio kufanya vita kushindwa kufanya chochote kabisa na hio ndio sababu inayoifanya miliki hio kutokushambuliwa kwa miaka mingi licha ya kujulikana kama moja ya miliki ambayo raia wake ni dhiafu sana.
Hakuna jini wala binadamu mwenye nguvu za kijinni ambae amefanikiwa kuipita Dhiki ya Radi katika miliki ya Hongmeng.
Inasemekana kama sio mfumo huo wa ki ulinzi wa visiwa hivyo vya anga isingekuwa rahisi kwa Zeus kushindwa vita, ukweli ni kwamba wakati wa Vita ,Zeus alitegwa na kuja mpaka kwenye ulimwengu huo wa majini watu na kuingia katika mtego wa safu hio ya ulinzi na ndipo alipoweza kukamatwa kirahisi kwa kushindwa kutumia kanuni za anga huku Athena yeye akikimbia.
Sasa imepita miaka mingi na majini ambao walihusika katika vita ya miungu walikwisha kufa na hata wale ambao walisimamia mkataba wa miungu na majini wenyewe wamekwisha kufa na waliobakia ni wale ambao ni kipya.
Katika historia, majini wa zama za kale walionekana kuwa na akili nyingi sana kuliko majini wa Zama za wakati huu na hii inapelekea mpaka leo hii majini wa zama hizi kujiuliza ulinzi wa miliki hio wa safu ya mwanga unafanya vipi kazi , au visiwa hivyo vinavyoelewa iliwezekanaje vikajengwa kwa mundo huo, wala nguzo ambazo zinaonekana kama ndio mhimili wa visiwa hivyo zimetokea wapi na chanzo cha nguvu yake ni nini.
Mpaka wakati huo majini hao hawakuwa na majibu ya maswali hayo na kitu pekee ambacho wanajua ni kwamba safu za mwanga ziliozokuwa zikizunguka kisiwa hicho ndio ulinzi wao , huku gereza la roho ndio misheni yao kubwa ya kulilinda ili wasiruhusu roho waliofungiwa kutoka.
Hakuna ukweli wowote kwamba ni kweli Zeus ameshikiliwa katika gereza hilo la piramidi . ukweli ni kwamba majini hao wanafanya makisio tu kulingana na historia au pengine kuna ukweli uliofichwa kuhusu wapi Zeus alipotelea.
Katika moja wapo ya kisiwa kikubwa zaidi kulikuwa na jiwe kuubwa jeupe ambalo limezungukwa na viti vya mawe vilivyochongwa katika mpangilio wa duara katika urefu unaotofautina na kufanya wale waliopo mbele kutowazibia wa nyuma, ni kama vile viti vya bar lakini chukulia kama vile vimetengenezwa na nguzo ya jiwe iliosindiliwa ardhini huku pale juu yake kuchongwa kwa mtindo wa kisahani na kumfanya ukaaji kuwa mzuri.
Vilikuwa vingi mno zaidi ya viti elfu moja ambavyo vimeachana kwa umbali maalumu.
Upande wa juu kabisa kulijengwa eneo la juu kidogo ambalo ilikuwa kama vile ni madhabahu au jukwaa na kwa mfano kama kuna mgeni au mtu anajadiliwa au kusomewa hukumu anapaswa kwenda kusimama juu ya jiwe kubwa ambalo lipo kama meza ya mviringo likiwa limeshikiliwa na nguzo mbili za mawe kwa chini.
Hakukuwa na mambo ya korido wala ngazi kwani majini wote pamoja na binadamu angalau uwezo wao ulikuwa si chini ya levo ya nafsi na kuwafanya wote kuwa na uwezo wa kupaa kwenda kukaa katika viti hivyo.
Mahali hapo ndio eneo ambalo majini pamoja na binadamu wenye nguvu za kijini hukusanyikia kwa ajili ya kikao cha jumla.
Sasa ikiwa ni kama lisaa moja nyuma hivi kabla ya Roma kukutana na miungu upande wa duniani katika miliki hio ya Hongmeng katika eneo hilo kulikuwa na kikao ambacho kinaendelea.
Kikao hichi kilihusisha mamia ya majini pamoja na binadamu ambao walikuwa na nguvu za kijini.
Unachopaswa kuelewa Hongmeng ni miliki ambayo ilikuwa na binadamu wengi ambao wananguvu za kijini na asilimia kubwa ya binadamu hao husalia Buddha, ijapokuwa walikuwepo wa dini nyingine lakini majini kwao dini ni Dhana sio imani na vitabu vya kidini kama vile Biblia na Quran wanatumia maandiko yake kama mbinu za kupandia levo tu
Siku za kawaida katika eneo hilo kungekuwa na majini angalau ishirini ambao hufanya kikao lakini siku hio kulikuwa na majini zaidi ya mia moja ambao walikuwa wamehudhuria kikao huku baadhi yao wakiwa sio majini wa miliki hio ya Hongmeng ikimaanisha kwamba ni wageni na walionekana kukaa katika meza hio iliokuwa katikati.
“Kutokana na ubini wako Nefi lazima utakuwa unawajua hawa waliopo mbele yetu , ni juzi tu hapa nimeweza kuingia daraja la mbingu hivyo sina uelewa wa kutosha, yupi hapo ni Anjiu, jini ambaye ameweza kupitia mapigo ya radi?”Alikuwa ni mwanaume aliekuwa pembeni ya jini aliefahamika kwa jina la Nefi , jini huyo hakuwa na uelewa na taarifa za miliki nyingine kwani sio muda mrefu aliweza kupanda daraja la mbingu.
Hongmeng majini na binadamu wapo katika madaraja mawili , daraja la kwanza ni la Ardhi ambapo hadhi yao ni ya chini na daraja linalofatia ni la Mbingu na hapa hadhi yako inaweza kuwa ya kati au ya juu.
Sasa anamuuliza Nefi kwamba hajui kati ya wageni waliokuwa mbele yao yupi ni jini Anjiu ambaye ameweza kuivuka dhiki ya radi.
Mara baada ya misheni yao ya kwenda kumshambulia Roma kukwama baada ya miungu
kuingilia viongozi wa miliki zote tatu yaani Panas , Kekexil na Xia walifanya safari ya kuelekea Hongmeng.
Dhumuni la kwenda Hongmeng ni ili kuungwa mkono katika vita yao ambayo haijaisha kati yao na binadamu anaefahamika kwa jina la Roma Ramoni.
Anjiu na wenzake walijua kabisa kutokana na hasara walioweza kuipata katika dunia kama Roma angefika katika miliki zao na kushambulia basi wasingeweza kumshinda na ndio maana waliona njia pekee ya kuweza kupona ni kuwashawishi Hongmeng kuungana nao.
“Kwani huwezi kuhisia nguvu zao, kuna haja ya kuuliza?”Alijibu Nefi huku akimwangalia Yozi alieuliza.
“Hehe …inatia aibu kukubali lakini ninakosa ujasiri wa kutumia uwezo wangu kuwatambua , Nefi je unaweza kuniambia wale wengine ni wakina nani , siwezi kuamini maneno ya wengine kama ninavyoamini ya kwako”
“Wale watatu wengine ni sehemu ya majini kumi wenye nguvu katika ulimwengu wetu , yule alievalia nguo za bluu ni mkuu wa miliki ya Kekexil ambaye amepewa jina jipya la kiungozi na sasa anafahamika kama Mkuu Menyu, yule wa nguo nyeupe yeye anafahamika kwa jina la Gefu ndio mkuu wa miliki ya Panas na yule mwingine ambae anaonekana mjeuri jeuri pale anafahaika kwa jina la Shozi kutoka miliki ya Panas pia”Aliongea Nefi akimwelezea Yozi ambaye hakuwa akitambua wageni waliofika katika miliki hio .
“Kwahio yule Shozi ni sehemu ya majini wenye nguvu , mbona yupo kimasikini masikini?”Aliuliza Yozi.
Katika ulimwengu wa majini haikumaanisha kwamba majini ambao wanaingia katika hesabu ya majini kumi ni kwamba ndio ambao walikuwa na nguvu kubwa sana bali ukweli ni kwamba wengine wanaweza kuwa na nguvu za kawaida lakini ushawishi wao na hadhi ukawa mkubwa.
Kwa mfano Gefu , Menyu na Anjiu walikuwa ni viongozi wa miliki sio kwasababu katika miliki zao ndio walikuwa na nguvu bali hadhi yao ndio iliwafanya kuwa na nguvu .
Sasa kwa upande wa Shozi yeye inasemekana sio mzaliwa kutokea miliki ya Panas bali ni kwamba mkuu wa miliki ya Panas iliopita alimwajiri katika miliki hio na kuwa katika kitengo cha Taisha.
Taisha ni majini wenye nguvu ambao huchukuliwa kama wanajeshi wa kitengo maalumu(Special force) ambao kazi yao kubwa ni kutoa ulinzi kwa miliki hivyo huyo Shozi alialikwa kama mwajiriwa kuwa katika miliki ya Panas na kuingizwa katika kitengo cha Taisha.
Kwanzia hapo ndio umaarufu wake katika miliki ya Panas ulikuwa mno na kutokana na kupendelea kuishi katika moja ya mlima ndani ya miliki hio basi kwanzia siku hio ndio mlima huo ukaja kufahamika kama mlima Shozi.
Uwezo wa nguvu za kijini wa Shozi ni mwishoni mwa maji ya upako na ndio ilimfanya kupewa heshima yake, ilikuwa ngumu kumjua alikuwa na uwezo mkubwa na ni mwenye kuheshimika kama vile Yozi alivyomwangalia ni kwasababu hakuvaa mavazi ambayo yalikuwa yakimpa utukufu bali alikuwa akivaa mavazi kama vile ni chokoraa.
“Huyo mzee tayari yupo kwenye levo ya maji ya kiroho lakini ni kama vile anakwenda kufa hivi karibuni”Aliwaza Yozi.
“Hebu jione ulivyo mjinga , unawezaje kumtafsiri mtu kutokana na muonekano wake , ijapokuwa Anjiu ameipita radi lakini hakuna uhakika kama atashinda kama atapambana na Shozi…. Kitendo cha Gefu kuja nae hapa Hongmeng basi lazima kuna jambo kubwa linaendelea”Aliongea Nefi.
“Nefi unamaanisha nini kuhusu hilo?”Aliuliza Yozi kwa mshangao lakini upande wa Nefi hakutaka kujibu swali lake.
Na minong’ono iliokuwa ikiendelea kati ya majini na binadamu wa Hongmeng wanaosubiria kikao kuanza ilikoma na kimya kikatawala.
Sababu ya ukimya wao ni kutokana na ujio wa majini ambao walikuwa na nguvu wanaokaribia ndani ya eneo hilo.
Kulingana na tamaduni za ki uongozi wa Hongmeng majini hao vyeo vyao ni vya Mbingu hadhi ya juu. “Hatimae wameweza kufika, nashangaa imekuwaje wakuu wa miliki zote tatu kuja Hongmeng na kutaka kuongea na viongozi wetu”
“Nadhani tutasikia sababu iliowaleta , hatujawahi kuwa na urafiki na miliki zingine za kijini , hivyo kulazimika kuja hapa lazima ni jambo kubwa limewaleta”
Baadhi ya majini waliongea wao kwa wao wakitaka kujua kilichowaleta Gefu , Anjiu , Menyu na Shozi katika miliki ya Hongmeng ni nini.
Ndani ya sekunde chache tu majini nane waliokuwa katika muonekano wa kizee na ujana walienda kutua kwenye eneo la madhabahu
Ijapokuwa kulikuwa na majini zaidi ya kumi na mbili wa Hongmeng ambao walikuwa katika daraja la mbingu hadhi ya juu , lakini ni wanne tu ambao walikuwa na nguvu kubwa na waliitwa Wakuu wanne wa hadhi.
Baada ya majini wa nne kufika katika eneo hilo la juu majini wengine wa nne waliongezeka kukamilisha idadi yao ya kumi na mbili.
Majini hao wote hawakuwa ni binadamu, walikuwa ni majini watu na walikuwa wakiheshimika mno na kila mmoja alikuwa kiongozi wa koo katika familia yake ndani ya miliki hio ya Hongmeng.
Hongmeng ni miliki ambayo haikuwa na mkuu mmoja wa miliki bali Hongmeng ni kama mkusanyiko wa koo za kijini na watu , koo hizi karibia zote zilikuwa na wawakilishi wao katika ulimwengu wa kawaida mathalani katika taifa la China ambao hufuata maagizo yao.
Kwa mfano katika ulimwengu wa kawaida katika taifa la China unaweza kukuta koo kama vile ya Shigao , sasa ukija katika miliki ya Hongmeng kunakuwepo na koo ya Shigao.
Hongmeng unaweza kuifananisha na freemason, au Illuminat au Zeros organisation katika ulimwengu wa kawaida na hii yote ni kutokana na kwamba ni jamii ya siri yenye nguvu ambayo ina ushawishi mkubwa wa kimadaraka katika ulimwengu wa kawaida.
Hii ndio maana Yan Buwen na marehemu Afande
Yang Gongming waliunda ushirikiano kwa kushawishiwa na Athena ili tu Yan Buwen awe na nguvu ambayo itamuwezesha kuunda siraha za kisayansi za kuishinda Hongmeng na kuweka kiongozi wanaemtaka wao.
Majini hao kumi na mbili wa cheo cha mbingu walikuwa wakiheshimika sana sio kwa majini tu lakini mpaka katika ulimwengu wa kawaida katika taifa la China hususani hao wanne.
Wanne hao ni Wucheni huyu ni mkuu wa koo ya
Yan , alikuwepo Yanyun huyu ni mkuu wa koo ya Yanyun na hawa ni majini ambao wanaamini katika dini ya Kibudha na mbinu zao za mafunzo ya kuvuna
nishati za mbingu na ardhi zimejikita katika mafundisho ya Kibuddha., wengine ni Umini na Shombeli kiongozi wa koo ya watumia mapanga.
Hao wote wa nne levo zao za nishati ya mbingu na ardhi ni mwishoni mwa maji ya kiroho.
“Kwanini mmefanya safari ya kuja visiwa vya anga.?”Aliongea yule aliefahamika kwa jina la Wucheni.
Gefu na wenzake walimwangalia Anjiu ambae alikuwa amefumba macho , kwasababu ndio pekee aliekuwa na nguvu kubwa walimwangalia kama kiongozi wa msafara huo.
“Nadhani hakuna haja ya kuuliza hilo swali , nina uhakika utakuwa unajua nini kimetuleta”Aliongea Anjiu mara baada ya kufumbua macho.
“Hehe… Anjjiu mkuu wa miliki ya Xia , sisi tutajua vipi kama wewe hutaki kutuambia”
Wakati huo alieongea ni kijana mdogo kabisa mchina ambaye alikuwa ameshikilia feni , huyo ndio ambaye alijulikana kwa jina la Umini, kwa muonekano wake wa ujana ni ngumu kusema kama alikuwa tayari na miaka mia moja na ushee.
“Ijapokuwa miliki zote tatu hazijawahi kuwa na maelewano mazuri na Hongmeng lakini bado zipo katika ulimwengu mmoja wa majini watu , kawaida lazima tuwe macho kwa kila kinachotokea katika huu ulimwengu , ni matarajio yangu kwamba Hongmeng mtakuwa na taarifa kwamba sisi miliki tatu zenye nguvu tuliungana na kutengeneza kikosi maalumu ambacho kilienda ulimwengu wa kawaida kumshambulia binadamu Roma Ramoni lakini tukaishia kushambuliwa na miungu watatu na kupoteza pambano…”
Maneno ya Anjiu yalisababisha gumzo ndani ya eneo hilo hususani kwa binadamu na majini wa kawaida ambao wamehudhuria kikao.
Kwasababub hawakuwa na vyeo vya kuweza kupata habari kwa haraka hivyo ilikuwa ni kama jambo jipya kwao.
Baadhi ya majini hao wa Hongmeng ambao walikuwa na taarifa kuhusu Roma Ramoni wote walijawa na wasiwasi.
“Amitabha…. Je hili linatuhusu vipi sisi kama Hongmeng?”Mkuu mwingine wa Hongmeng aliefahamika kwa jina la Yanyun aliongea.
“Haha.. kuna haja ya kujificha hata katika wakati kama huu , wakati nyie mkijua kinachoendela katika miliki zetu na sisi pia tunajua nini kinaendelea katika miliki yenu”Aliongea Anjiu na kisha akampatia ishara Gefu mkuu wa miliki ya Panas kuendelea.
“Kulingana na taarifa ambayo tumeipata Hongmeng mlikuwa mkitamani kuona ushirikiano wa faida baina ya Roma na China lakini alikataa na kisha akaua baadhi ya wajumbe wenu…”Aliongea
Aliongea kuchagua maneno ya kuongea , ukweli ni kwamba alijua licha kwa nje inaonekana ni kama China ndio wanataka kufanya ushirikiano na Roma lakini nyuma ya pazia sio China bali ni majini hao maana walichokuwa wakitaka kutoka kwa Roma ni mbinu yake ya mafunzo pamoja na vidonge.
“Kubwa zaidi ni kwamba kwasasa dunia inapitia hali ya kushuka kwa joto kwa kiwango cha juu sana na mpaka sasa ninapoongea baadhi ya maeneo ya Kaskazini mwa China hayakaliki na mimea mingi inanyauka ….. licha ya Chaopi kuwa na nguvu kubwa ya kijini katika levo ya kuipita radi lakini alishindwa kudhibiti miungu wote watatu yaani Apollo mungu wa jua, Artemis mungu wa mwezi na Poseidon mungu wa bahari, nadhani baadhi yenu hapa mnajua uwezo wa miungu hawa na mshawahi kuushuhudia hapo kabla lakini kilichotokea kinamaanisha kwamba miungu uwezo wao sio kama mliouzoea ..inaonekana hata kushuka kwa kiwango cha joto kunahusiana na kuongezeka kwao nguvu…”.
“Acha kuongea ujinga “Aliingilia maongezi yake bwana aliefahamika kwa jina la Shombeli, alikuwa na uchebe ambao ameusuka kabisa na alikuwa akiuchezea kila sekunde kana kwamba kuna hisia flani anazipata.
“Pointi yangu ni kwamba kama miungu hawa nguvu zao zitaendelea kuongezeka sio tu kwamba tutakuwa katika hatari lakini pia hali za binadamu zitaathirika kwa kiasi kikubwa na athari hizi zitagusa mpaka ulimwengu wetu”Aliongea Gefu bila kumzingatia Shombeli.
Kila mmoja alikaa kimya , hata kama kauli yake ilikuwa kinyume lakini hakuna ambaye aliweza kukanusha kauli yake.
“Viongozi , najua hamuwezi kuhisia chochote kwasababu hamjapata hasara kama tulioipata sisi lakini mnapaswa kujua kwamba sisi hatuna kinyongo na miungu na kinyongo chetu ni zidi ya Roma pekee lakini nyie kwa upande mwingine mmekuwa katika kutokuelewana vizuri na miungu na ni swala la muda tu kuja kuwashambulia na kulipiza kisasi cha kihistoria”
“Gefu unatutisha sio?”Wucheni aliongea huku akipandisha sauti.
“Hawatishi bali anajaribu kuwaelezea kwamba mkijifanyisha wajuaji mnaweza kuwa wa kwanza kufa kabla hata ya sisi”Aliingilia Anjiu.
“Umekosa adabu wewe, unasema tunajifanyisha? Anjiu usione kwamba tunakuoghopa kwasababu umeweza kupanda levo , pigana na sisi kama una ujeuri huo”Shombeli alifoka akionekana kutoridhishwa na maneno ya Anjiu na palepale hakuishia kufoka tu alitoa upanga wake unao wakawaka kwenye ala na kumnyooshea Anjiu akionekana kabisa yupo tayari kwa vita.
“Shombeli huu sio muda mzuri”Aliongea Wucheni akijaribu kumtuliza na kisha akawageukia majini waliokuwa wamehudhuria kikao hicho.
“Wote ambao mpo chini ya levo ya Mbingu ondokeni katika kisiwa cha anga”Aliongea.
Majini wengi walishangazwa na kauli ile kwani sio kawaida kwa majini hao wa levo ya chini kuondolewa katika kisiwa cha anga lakini licha ya hivyo hakuna ambaye alibakia na ndani ya muda mfupi walibakia majini wa levo ya mbingu.
“Kwahio mpo hapa kwa ajili ya kutafuta msaada?”Aliuliza.
Itaendelea kwanzia hapa katika sehemu ya 751 tuone yule aliekutana na Roma Dodoma ni nani.





SEHEMU YA 750.
NORTH POLE -Central Arctic Sea/Ncha ya kaskazini.
Katikae eneo pana la tambarare ya barafu na theluji tukio la kushangaza kubwa sana na la kuogopesha lilikuwa likichanua taratibu taratibu na kimya kimya bila ya sauti yoyote.
Ilikuwa ni mti mkubwa sana na wa kushangaza wa rangi ya dhahabu ambao ulikuwa umechomoza kutoka katika funiko ya barafu na kwenda moja kwa moja juu angani.
Mti huu mkubwa wa dhahabu matawi yake pekee tu yalikuwa yamechukua eneo kubwa la mzingo kwa zaidi ya hatua za mraba elfu moja huku shina lake pana sana likienda mpaka chini kabisa ya bahari ambapo mizizi yake ilikuwa imetambaa kuelekea pande sizizojulikana chini ya bahari hio ya Arctic.
Kivuli cha mti huo kilikuwa ni kikubwa mno takribani mita elfu kumi , ilikuwa ni kama vile turubai limetandazwa juu angani na kufanya mwanga wa jua usipite chini , matawi ya mti huo yalikuwa ni kama vile ni Dhahabu iliomulikwa na mwanga na kung’aa.
Majani yake yalikuwa makubwa mno zaidi ya ndege ya abiria huku yaking’aa kila dakika ambayo jua huyafiikia.
Katika mti huo sio kwa majani , matawi wala shina kila mahali kulikuwa na maandishi ambayo yalikuwa yakitoa mwanga na kufifia kwa namna ya kubipu.
Kuzunguka eneo la mti huo kilomita kadhaa kulikuwa na kitu kama karatasi la rangi ya njano kama uzio hivi ambapo lilikuwa kimezunguka na kutengeneza duana na kisha kwenda juu angani kwa kimo kikubwa mno.
Ukuta huo ukiachana na kazi yake ya ulinzi ulikuwa na kazi ya kukusanya mtiririsho wa nishati ya jua kufikia mti wa kimaajabu ambao husharabuu nishati yake mara moja.
Katikati ya kivuli cha mti huo kulikuwa na eneo ambalo linawaka waka na vivuli vya watu wawili vilikuwa vinaelea katika nusu anga chini ya shina la mti huo.
Walikuwa ni mwanaume na mwanamke ambao walikuwa wakimulikwa na mwanga wa dhahabu unaotoka katika mti huo kwa wakati mmoja na kama utaangalia kwa ukaribu utagundua kwamba licha ya kumulikwa na mwanga lakini pia kuna nguvu iliokuwa ikitoka katika vichwa vyao na kunyonywa na matawi ya mti huo wa kimaajabu.
Yaani ilikuwa kila mara baada ya nishati kutolewa katika mti huo kuwafikia kichwani na kuisharabu, nguvu nyingine inawatoka na kwenda kuuvaa mti huo Chini ya mti huo kutokea kwenye bahari ambako shina hupatikana nishati ambayo ilikuwa katika mfumo wa ukungu wa mwanga wa njano ilikuwa ikitoka kama vile ni mvuke na kusambaa angani kwa kiasi kikubwa mno.
Eneo lote hilo lilibadirika rangi kutoka ile rangi nyeupe ya barafu na theruji na kuwa rangi ya njano ya Dhahabu na kila kilichokuwa kikifanyika hapo hakikutoa sauti hata kidogo , kila kitu kilikuwa kikifanyika kimya kimya.
Wakati mti huo ukiendelea kunyonya nishati ya jua na kuibadilisha kwenda kuwa nishati nyingine ambayo inatokea chini ya bahari kwenye shina na kusambaa kama mvuke katika uso wa dunia hatimae waliweza kufika watu wengine wawili ndani ya eneo hilo ukiachana na wale ambao wapo.
Yule mwanamke na mwanaume ambao wote walikuwa wakibadilishana nguvu na mti huo waligeuka na kuangaliana , baada ya kuangalia
mwanaume na mwanamke waliovunja ukuta na kuingia wote walionyesha hali ya utulivu katika sura zao, kilichokuwa kikiendelea hapo hakikuwashangaza hata kidogo ilikuwa ni kama mti huo walishauona hapo kabla.
“You have worked hard Ares and Aphrodite , that bi*ch is mean by only letting the two of you help the ‘Mother Tree’ to recover , isn’t too tiringi…?”
“Mmefanya kazi kwa juhudi Ares na Aphrodite , yule Kahaba ni muonevu sana kuwaacha nyie wawili pekee kuusaidia ‘Mti Mama’ Kupona … si inachosha sana?”
Aliongea alikuwa ni mwanamke alievalia gauni la rangi ya kijani na alikuwa katika tabasamu lililojaa mapozi , mwanamke huyu alikuwa ni Rozu jini chotara kutoka miliki ya Panas.
Mwanamke na mwanaume ambao walikuwa waking’aa kama jua kutokana na kumulikwa na mwanga wa mti huo wa kimaajabu alikuwa ni Christen na Ares ambao Roma alikuwa akiwatafuta hewani hawapatikani.
“Baada ya kipindi kirefu sana hatimae kwa hiari yako mwenyewe umeamua kujitokeza , tulidhania utaendelea kuficha kichwa chako huku ukionyesha mkia wako huku ukimfanya Hermes kuwa msemaji wako,… Habari za miaka elfu tatu bila kuonana Hera”
Rozu alikuwa ni sehemu ya miungu , yaani viumbe kutoka sayari nyingine na jina lake halisi alikuwa ni Hera mungu wa mbingu.
“Sikupenda kujificha ni kwamba tu sipendeelei kuja huku ulimwengu wa kawaida lakini hali imebadilika sasa , sikutegemea huyo kichaa kufanikiwa kutumia moyo wa Gaia kuupanda upya Mti Mama”Aliongea Hera.
“Hera acha maigizo , sidhani kama ni kweli hupendi kujitokeza bali ukweli ni kwamba uliona ni ngumu kufanya mambo yako katika ulimwengu huu wa kawaida na kujificha”
“Kwanini unasema hivyo Aphrodite?”Aliongea akiwa ameelea hewani kama vile ni malaika na alijiegamiza kwenye jani la mti huo huku akinusa harufu yake.
“Kwanini usikubali tu kile ambacho ulikuwa ukifanya , Hephaestus ndio mtu pekee ambaye anaejua mkanda wangu unavyofanya kazi , unayoonekana na namna ya kuutengeneza hivyo moja kwa moja inamfanya yeye ndio katengeneza ule mkanda feki ulionekana nchini Tanzania. Mamlaka ya utengenezaji wa vitu feki anaipata moja kwa moja kutoka kwako , hivi unadhani hatukujua ni wewe mara baada ya kujiigiza ni Athena kwa kipindi kirefu kwa kutumia Sarafu feki na Ua la Blue
Orchid…”Aliongea na maneno yale yalimfanya Hera kushangaa kiasi baada ya siri yake kugundulika..
“Kwahio hii ndio topiki ambayo unaongelea .. ni aibu kwamba kila nilichofanya hakikufanikiwa lakini ninachoweza kulaumu ni mbinu yangu ya Ushirikina wa kinajimu kwa kushindwa kuwa na nguvu na kushindwa kutabiri matokeo”
“Ushirikina wa kinajimu!!?”Christen alishangaa na vilevile kwa Ares.
“Hera hio mbinu si ndio inayotumiwa na majini kufanya utabiri wa kinabii kama ilivyo Karama ya Athena ya unabii na Almanaki ya Hades wa zamani?, unataka kumaanisha kwamba jini aliefanya ule unabii kwa kutumia hio mbinu hakufariki?”
“Haha.. upo sahihi ..nilifikiria kwa kipindi kirefu sana kumshinda Athena kwa kila namna na ndio maana nilitafuta njia ya kuishinda Karama yake ya kinabii na juhudi zangu zilinichukua miaka elfu moja kuweza kukusanya vitabu vingi sana vya kihistoria katika kila miliki na koo za kijini ili kuweza kubobea katika Ushirikina wa kinajimu”
“Inamaana ulijificha katika ulimwengu wa majini kwa ajili tu ya kufunza hio mbinu , hakika uvulimivu wako ni wa viwango lakini kwa bahati mbaya ni kwamba wewe sio mtu sahihi kuweza kumshinda Athena kwa namna yoyote , hata Almanaki ya Hades wa zamani haifui dafu mbele ya Nguvu ya Karama ya kinabii aliokuwa nayo Athena”
“Haha.. hilo natambua lakini sio mbaya kwani mpaka sasa ninachoona Athena unabii wake siku zote haujawahi kuwa sahihi kwa asiliimia mia moja , hii inamaanisha kwamba siku moja mbeleni mambo yanaweza kuwa tofauti nje na matarajio yake kitu ambacho kinanitekenya mno..”Aliongea Hera.
“Kwahio hampo hapa kwa ajili ya kuingilia hili si ndio?”Aliuliza Christen kwa wasiwasi.
“Hey Aphrodite unawaza nini?,Hata kama hatumpendi Athena haimaannisi kwamba hatutaki kufufuka kwa ndugu zetu , huu ni Mti Mama na hatutaki kutokuwa na heshima mbele ya Gaia , Mama wa asili yetu”Aliongea Hermes.
“Mpo nyie wawili tu , itachukua muda mrefu sana mpaka kuurudisha huu mti katika hali yake ya kawaida na kuanza hatua ya kubadili hali ya kidunia
, kwanini Poseidon na Apollo hawajaja kuwasaidia?”Aliuliza Hera.
Christen aliishia kutoa pumzi ya ahueni mara baada ya kujua hao wawili hawajafika hapo kwa ajili ye kuleta matatizo bali wamekuja kuangalia kile kinachoendelea.
“Kulingana na makadirio ya uasili wake , Athena anatumaini kukusanya baadhi ya nguvu za kiuungu ambazo zimesambaa katika mifupa ya miili ambayo roho zilipotea na baadhi ya mabaki ya kale ya kiuungu na kuamsha baadhi ya nafsi kwanza , baadae kwa kujumlisha miungu wote kumi na moja tutakuwa na uwezo wa kuiamsha nguvu ya damu ya Titan ili kuamsha asili kamili ya Mti Mama. Lakini Athena alifanya utafiti na kugundua kwamba dunia ina utofauti sana na Mars lakini hata hivyo amegundua katika kiini cha dunia kuna uwepo wa madini yanayofanana na yale ya sayari yetu ambayo yatakuwa na uwezo wa kuamsha damu ya asili yetu, ili mradi muda uliopangwa kutimia , roho zilizopotea zitarudi kuwa na nguvu yake na damu yetu itaanza kufanya kazi upya na kadri dunia inavyopitia mabadiliko ndio asili yetu itakavyoanza hatua za kuweza kumudu mazingira ya dunia , ndio maana mpaka sasa ameachana na zile Clones zilizotoka katika damu ya Hades , isitoshe uungu wao sio mkamilifu hivyo kufanya iwe ngumu sana kutumika , kazi yetu mimi na Ares ni kuhakikisha tunausaidia huu Mti Mama kuweza kutengeneza mazingira ya kidunia ili kuamsha nafsi za wenzetu kwanza pamoja na mazingira ambayo uzao upya utamudu hali ya hewa , majukumu yetu sio makubwa sana haina haja ya kupata msaada”
“Vizuri , inaonekana kabisa Athena amefanya makosa katika mahesabu yake na unabii wake pia sidhani kama utaweza kutimia, kubwa zaidi ni tatizo alilokuwa nalo yeye mwenyewe … hehe”
“Lakini anachotaka kitokee ndio hiki mnachoona kwa macho yenu kinakaribia kutimia”Aliongea Christen lakini Hera alipotezea na kuanza kuangalia mazingita ya eneo hilo hususani barafu iliokuwa imezidi kujiongeza kwa mbali.
“Sikuwahi kuwaza kama Mti wa Uzazi utafanikiwa kukua na kustawi katika mazingira ya dunia lakini kwa ninachoona hapa ni kwamba kama kiini cha dunia kikaathiriwa na huu mti , sidhani kaa athari zitakazotokea ni dunia kupoteza joto tu …ni rahisi kutabiri binadamu ku… kuweni tu makini”
“Hey ….binadamu na majini ni viumbe ambavyo asili yao ni majongoo wanaotambaa wa hadhi ya chini kabisa na kama kipindi kile sio kutelekeza miili yetu majini na binadamu wasingeweza kutuletea ukinzani na tungekuwa tushawafuta katika uso wa dunia , kinachokwenda kutokea ni utawala mpya uliochelewa kwa miaka elfu ishirini”Aliongea Hermes akiwa amepamba uso wake na tabasamu lililojaa uovu.
“Kama kilichowaleta ni kuangalia mnaweza kuondoka mti upo salama kwani kuna uzio tayari wa ulinzi”Aliongea Christen akiwa katika hali ya kukasirika huku akionyesha hali ya huzuni kwenye macho yake kutokana na kauli ya Hermes.
“Najua una hasira na nilichokufanyia lakini sina pakwenda kwasasa , nadhani itakuwa vizuri kama nitaendelea kupumzika hapa hapa .. ijapokuwa binadamu wa kawaida hawezi kufika hapa lakini kama mtu mwenye nguvu za kijini au majni wenyewe kufika hapa na uwepo wangu hamtokuwa na wasiwasi kuendelea kuuhudumia mti wetu wa uzao katika hali ya utlivu”
“Haina haja kama kweli watakuja itanifanya kupunguza uchomvu wangu kwa kupambana nao”Aliongea Ares.
“Muda huu naamini Roma tayari ashaenda ulimwengu wa majini watu kwanini usiende na kuangaia kinachoendelea?”Aliongea Hermes
“Haina haja tena , mpaka sasa vita hio imekwisha kufeli , Hades anatembea kwenye hatua alizoandaliwa na Athena katika mipango yake”Aliongea akimaanisha kwamba Roma kwenda kuua majini ni mpango wa Athena , pengine ili kutoweza kuingiliana na hicho kinachofanyika hapo.
Mara baada ya kuongea kauli hio alikwenda kutua juu ya jani la mti huo wa kimaajabu ambalo lilianza kunesa nesa na ajabu ni kamba lile jani pana lilijikunja kidogo kana kwamba linampa nafasi Hera kulala bila kupata shida.
Ares na Aphrodite waliangaliana na wote kwa pamoja waliishia kutingisha vichwa vyao kwa namna ya kusikitika.
Mother Tree ni mti ambao unahistoria yake ambayo tutaiona mbele lakini kinachofanyika hapo ni kwamba unanyonya nishati ya jua na kuipeleka chini kwenye mizizi na baada ya hapo inageuza nishati hio na kudhalisha nishati nyingine ambayo inasambaa katika uso wa dunia.
Hivyo kwa lugha nyepesi sio tu kwamba dunia inapitia hatua za kushuka kwa hali ya joto bali nguvu ya nishati ambayo inasambaa kutoka katika mti huo ina athari zake.
Je ni kwanini Hera alikuwa akijifanyisha kuwa Athena , kama kweli alikuwa akijifanyisha ni vitu gani aliweza kufanya na akafanikiwa na vipi alifanya akafeli.
Almanaki ni sawa na Kalenda , ndio ambayo wanaitumia Ant- Illuminat kutabiri matokeo yajayo hivyo ni sawa na kusema ni Kalenda ya kinabii ambayo mmiliki wake ni Hades wa Zamani.
Sasa Athena na yeye ana karama yake ya kinabii hivyo inatuonyesha kitu kimoja kwamba pengine kuna utofauti kati ya unabii uliokuwa katika Kalenda ya Hades na unabii wa Athena.
Tukumbuke kwamba wakati Athena akianzisha mipango yake na Hades na yeye alianzisha mipango yake ya kwenda kinyume na mipango ya Athena je nani atashinda tusichoke kuendelea kufatilia bado vipande hamsini tu kukamilisha mwishoni utashangaa.
MWISHO WA SEASON YA 25.










*****
 
NILIMHDANIA KAHABA KUUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware

SEHEMU YA 751.
Mkuu wa miliki ya Panas, Gefu mara baada ya kuulizwa na viongozi wa Hongmeng kama wapo hapo kwa ajili ya kuomba msaada alitabasamu na kisha akawaangalia wenzake na kukubaliana kwa macho kisha akawageukia.
“Kiongozi mkuu ni kama nilivyosema , mnadhani Hongmeng peke yake inao uwezo wa kushindana na miungu wakati sisi miliki nyingine tumeshindwa , sio kwamba nadharau uwezo wa wakuu wa Hongmeng lakini kaka yangu Anjiu na baba yake wote kwa pamoja wapo katika levo ya kuipita dhiki ya radi na hakuna jini yoyote ambae anauwezo wa kuwashinda hapa Hongmeng lakini wao wameshindwa kuwadhibiti miungu”
“Ninakiri kwamba ni kweli Anjiu uwezo wake ni mkubwa kuliko wa kwetu lakini mnapaswa kutambua kwamba sisi tunalindwa na safu ya ulinzi wa mababu zetu , hawawezi kutufanya chochote kama tutakuwa ndani ya miliki yetu , walishajaribu kuingia huku miaka mingi iliopita na wakaambulia kushinidwa”
“Kiongozi mkuu nadhani uache maigizo , kwasababu umeshawaondoa watu wako wa daraja la chini ongea sababu yako’
“Oh , inaonekana unajua mengi kuhusu sisi?”Aliongea Wucheni huku akipepesa macho kulia na kushoto.
“Kwasababu safu yenu ya ulinzi ilitengenezwa na mababu wa enzi hizo waliokuwa na akili kubwa ni kweli kwamba nguvu yake ya ulinzi ni kubwa kama sio hivyo isingeweza kushikilia roho za majini waovu ndani ya gereza lenu la Roho kwa miaka mingi , lakini je naweza kusema au wewe unaweza kusema mnao uwezo wa kuutumia ulinzi huo , je mnajua namna ulinzi huo unavyofanya kazi?, kwa kile ambacho nakijua mimi ni kwamba majini wa miliki yako wanasema wao ndio wanaosapoti ulinzi huo kwa kuingiza nguvu yao ya mbingu na ardhi , lakini ukweli ni kwamba inaonekana safu hii ya ki ulinzi imetengenezwa kuvuna yenyewe nishati za mbingu na ardhi na hakukuwa na haja ya kuiongezea nguvu”
“Sidhani kama ni sahihi kwa wewe kufanya makisio yako juu ya maswala yetu ya ndani”Aliongea Wucheni.
“Ni kweli , lakini matumaini yetu ni nyie kuweza kujua namna ya kuendesha safu yenu ya ulinzi na kujilinda zidi ya miungu lakini kulingana na hali ilivyo inaonekana kabisa hamuwezi kwani hamjui busara iliopo nyuma ya ulinzi huo”
Wale majini wanne ambao ni viongozi wote walikaa kimya wakimwangalia Gefu ambaye alikuwa akiongea.
Ukweli ni kwamba walikuwa wakijua sana namna nguvu ya miungu ilivyo mara baada ya kuwachakaza majini hao huko katika ulimwengu wa binadamu.
Sasa kama miungu wote kumi na moja watashambulia miliki ya kijini hawatoweza kujilinda na ni hakika kwamba watashindwa.
Katika swala la nguvu haikujalisha miungu ilikuwa upande wa dunia inayoonekana lakini kama nguvu zao zikirudi kikamilifu ilimaanisha kwamba lazima wangetaka kujipima uwezo na washindani sahihi ni hao majini , isitoshe pia miungu hio ina kinyongo na majini kwa muda mrefu.
Ilikuwa ni swala la muda tu kurudia kile ambacho walitaka kufanya miaka mingi iliopita mara baada ya kutua katika uso wa dunia.
“Mwisho wa yote inaonekana kabisa mlichokijia hapa sio sisi kuwasaidia bali mnatafuta kura ya pamoja ili walinzi wa umoja wa majini kuchukua hatua”Aliongea Yanyun na ilikuwa ni kama vile amepatia kile ambacho Gefu na wenzake wamekijia hapo Hongmeng.
Ijapokuwa ni kweli kwamba kulikuwa na umoja wa ki ulinzi wa pamoja wa majini ulioundwa maiaka mingi iliopita lakini miliki nyingi za kijini hazijawahi kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na jini mkuu namba moja ambaye ndio kiongozi wa umoja huo.
Hivyo Gefu na wenzake walikuwa wakijua kwamba mkuu wa umoja wa majini lazima atakuwa na mawasiliano na Hongmeng ndio maana wakafika hapo.
Hawakuenda Hongmeng kwa ajili ya kuomba msaada wa kivita ukweli ni kwamba Hongmeng ni miliki dhaifu ambayo isingekuwa na mchango mkubwa kumshambulia Roma.
Inaaminika kwamba mkuu namba moja wa umoja wa majini ndio jini ambaye ana nguvu kubwa za kijini na ambaye ameishi muda mrefu sana hivyo kama yeye na wajumbe wake wa ulinzi wa baraza la umoja huo wataingia katika vita na Roma ni hakika kwamba Roma asingeweza kushinda kwa namna yoyote ile.
Jini mwenye nguvu ambaye alikutana na Roma jijini Dodoma ndio ambae anazungumziwa hapo , ndio jini ambaye anadumisha muungano wa pamoja wa ki ulinzi wa ulimwengu wa kijini na wa kibinadamu.
Haikuwa sheria ya ‘The Gods treaty’ tu ambayo ilikuwa ikiwazuia majini kutoka katika ulimwengu wa kawaida na kufanya fujo , ukweli ni kwamba mkataba huo wa The gods treaty ulikuwa ni wa maslahi wa pande mbili tu na binadamu kwa namna moja ama nyingine hanufaiki kwa namna yoyote na mkataba huo.
Mkataba huo ulikuwa ukiwapa ruhusa miungu kushughulika na majini wote wanaovuka mipaka na kujitokeza katika ulimwengu wa kawaida lakini hakukuwa na kipengele cha moja kwa moja ambacho kilikuwa kikisema kwamba majini wakiua binadamu miungu inapaswa kuchukua hatua.
Umoja wa muungano wa pamoja wa ki ulinzi ndio ambao ulikuwa na sheria ya moja kwa moja ya kuwazuia majini au viumbe wote wenye nguvu za mbingu na ardhi kushambulia binadamu ambao hawana uwezo wa nguvu hizo au kutoka katika ulimwengu na kutaka kutawala binadamu hio ndio sheria ambayo ilikuwepo mara baada ya vita kati ya majiini pepo, binadamu na majini watu.
Hivyo mkuu namba moja alikuwa akiishi katika ulimwengu wa kawaida na kazi yake kubwa ni kulinda mpaka wa kisheria kati ya majini na binadamu lakini wakati huo huo akiwa na jukumu la kulinda miliki za kijini pale tu itakapotokea hatari ambayo majini hawawezi kuizuia wenyewe.
Sasa miliki hizi za Panas , Kekexil na Xia zilitaka kuwaamsha wajumbe wa muungano wa pamoja wa ki ulinzi wakiongozwa na mkuu namba moja mwenyewe wa umoja huo wa majini kumchukulia Roma hatua.
“Kama hichi ndio kilichowaleta basi hatuwezi kuwasaidia , ukweli ni kwamba hatuwezi kukutana nao pale tunapohitaji na hata sura zao hatuzijui kwani hawajawahi kujionyesha “Aliongea Shombeli.
“Najua pia hatuwezi kukutana nao , lakini ukweli ni kwamba lazima watakuwa wanajua kile kinachoendelea , kama wajumbe wa ulinzi wa pamoja watakataa kutusaidia sidhani kama pia wanaweza kuisadia miliki yenu pale itakapokuwa hatarini , hivyo kwasasa ni sawa na kusema wote tupo kwenye tatizo moja , taarifa za siri ambazo tunazo mpaka sasa Roma ameshakutana na mkuu wa umoja mara baada ya kutibua amani ndani ya familia ya Sharif sehemu ya wafuasi wa majini pepo kutoka miliki ya Braki, mnadhani hii tafsiri yake ni nini?”
Kauli yake ilibadili hali ya hewa palepale hakuna ambaye aliamini kama kweli Roma alikuwa amekwisha kukutana na mkuu wa umoja sehemu ya wajumbe wa ulinzi.
Ukweli ni kwamba mara nyingi umoja huo haujawahi kuamulia majini hao cha kufanya , ni umoja ambao haujawahi kuingilia maswala ya majini na binadamu na hata pale inapotokea migogoro hawajitokezi mpaka waone kuna ulazima.
Kuna uwezekano mkuu wa umoja alikutana na Roma kumpa onyo kutokana na kuchokoza miliki ya Braki , miliki ya majini pepo , majini ambao ni hatari kama wataingia katika ulimwengu wa binadamu.
Tokea siku nyingi Hongmeng ilitaka kusafiri kwenda Afrika kumshambulia Roma lakini ukweli sio kwamba walishindwa au sheria ilikuwa ikiwazuia kufanya hivyo ila ni kwamba walikuwa wakimuogopa Roma.
Hata pale taarifa zilipowafikia hivi majuzi mara baada kutuma mjumbe wao kuja ulimwengu wa kawaida kutoa msimamo wao na Roma kumuondolea nguvu za kijini hawakuwa na cha kufanya licha ya kwamba walitafsiri kitendo hicho kama uchokozi wa wazi ambao Roma ameufanya.
“Kwasasa haiwezekani kuwasiliana na mkuu wa umoja na wajumbe wake wa ulinzi , kama kweli wangekuwa tayari kutusaidia wangekuwa washafanya wenyewe bila ya kutafutwa , hata kama miliki zetu zote zitaingia kwenye matatizo nina wasiwasi wanaweza wasijali , wanachokilinda wao sio majini bali ni asili ya usalama wa ulimwengu”Aliongea Umini.
“Umini wewe ndio ambae ushawahi kukutana na mkuu wa umoja unakadiria vipi uwezo wake?”Aliuliza Wucheni.
“Sina uhakika lakini kulingana na mkandamizo wa msisimko anaozalisha inaonekana ana uwezo mkubwa kuliko hata Anjiu , watu ambao hawajionyeshi kama wao sidhani kama kuna mmoja kati yetu anaweza kushindana nao”Kauli yake iliwashangaza na kuwaogopesha.
Ukweli ni kwamba hata huyo Umini aliwahi kukutana na mkuu wa umoja wakati wa kupewa msisitizo wa kimaagizo.
“Wajumbe wote wa ulinzi wa pamoja hawajawahi kujitokeza mpaka sasa kwasababu hawapo tayari kutusaidia , hatuwezi kukaa na kusubiria na lazima tupambanie maisha yetu , wazee kwasasa tunayofursa , tunaweza kumuua Roma kama ataingia kwa mara nyingine katika ulimwengu wa majini ili mradi tu Hongmeng mtatoa ushirikiano wenu kwetu , kama mtaendelea kusita sita na kukataa kutoa msaada mtakuwa mmechelewa kutuomba msamaha mara baada ya Roma kuja kuwashambulia , mkumbuke tu kwammba balozi wenu Xuan Jizi alifanyiwa kitendo cha aibu sana na Roma Ramoni hii inamaanisha Roma ameshatangaza vita yake na Hongmeng”
Kikao kilikuwa ni cha moto na adui namba moja ambaye alikuwa akizungumziwa ni Roma , ukweli ni kwamba hawakuwa na habari hata na miungu kuwa na nguvu kubwa kwa wakati huo , hofu yao kubwa ilikuwa ni Roma kuja kuwashambulia.
Kutokana na kutokuwa na uhakika juu ya kutokea kwa viongozi wa umoja wa majini, Hongmeng kabla ya kukubaliana na miliki nyingine waliona kwanza wakae wao kwa wao wajadiliane na wakishafikia maamuzi watawapatia msimamo wao.
Hivyo wakuu hao wa miliki walipelekwa katika kisiwa cha maua ya Lotus kwa ajili ya mapumziko wakisubiria maamuzi.
“Kwanini hawa vikongwe bado tu wanasita sita , Roma tayari amekwisha kuua balozi wao hivyo moja kwa moja ametangaza vita nao lakini bado tu wanaamini Roma hawezi kuwashambulia , kama tutaendelea kuruhusu Roma uwezo wake kuongezeka Hongmeng ushawishi wao katika dunia utashuka kwa viwango”
“Hey! Menyu huna haja ya kuwa na wasiwasi si bora ufuruhie zako kwani ndio kwanza umeweza kupata cheo cha ukuu wa miliki ya Kekexi?”
“Menui kifo kilikuwa kikimtafuta , nani angedhania kifo chake kitatokea katika ulimwengu wa binadamu , hii nafasi nilistahili kwa muda mrefu haina haja ya kuwa na furaha kwani ni haki yangu”Aliongea Menyu kijeuri na kumfanya Gefu na Anjjiu kuangaliana na kisha walicheka.
Ukweli ni kwamba Anjiu alikuwa akimkubali sana Menyui kuliko kaka yake Menui na ni marafiki wa muda mrefu na ndio ambaye alimpasha habari juu ya kuwekewa sumu ya Taouwu.
Mara baada ya Menui mkuu wa miliki ya Kekexil kuuliwa na Apollo moja kwa moja nafasi yake ilirithiwa na Menyu ambae ni mdogo wake , pengine kungekuwa na mgogoro nani arithi nafasi yake lakini kutokana na vifo vya Mohena na Mohi kiti hicho cha uongozi kilikuwa wazi na moja kwa moja nafasi ikamwangukia Menyu kwa urahisi kabisa.
Yalipita kama masaa kadhaa hivi wakati wakuu wa Hongmeng wakjjadiliana huku upande wa wageni waliokuja kuomba ushirika wakiwa katika eneo la mapumziko.
Mkuu wa kikosi cha ulinzi wa mipaka alifika katika nyumba ambayo anaishi Nefi mtendaji wa shughuli za miliki , bwana huyo alionekana kuwa na taarifa ya haraka ambayo mkuu wake anapaswa kuifahamu.
“Mkuu kuna mvamizi ambae amejeruhiwa sana yupo nje ya uzio , nini tunapaswa kufanya?”Aliongea yule mkuu wa vikosi vya ulinzi wa mipaka mara baada ya kumfikia Nefi.
“Mzamiaji!! , mmegundua anatokea wapi na kwanini amejeruhiwa?”
“Amesema anataka kuonana kwa haraka na kaka yake mkubwa ili kumpa taarifa ya kinachotokea katika miliki yao , ni mdogo wake Gefu mkuu wa miliki ya Panas lakini amepoteza fahamu hivyo tumeshindwa namna ya kudili nae”
“Nipelekeni kwa huyo mtu haraka”Aliongea Nefi mara baada ya kuwaza jambo.
Dakika chache tu Nefi aliweza kuchukuliwa mpaka seheu ya wazi ambayo ni mpakani mwa Hongmeng na kukuta majini wawili ambao wanalinda mtu ambaye amejeruhiwa.
Mtu huyo alikuwa ni wa ngozi nyeusi lakini mweupe na alikuwa amelala ardhini akiwa na sura iliokuwa ikionyesha ni kwa kiasi gani yupo kwenye maumivu.
Nefi ni moja ya majini ambao walikuwa na taarifa nyingi sana kuhusiana na miliki karibia zote na alikuwa akijua baadhi ya majini waiopo katika nafasi za uongozi wa juu katika miliki zote hivyo mara baada ya kumchunguza majeruhi huo palepale aliweza kumjua jina lake , alikuwa ni Gegu Master namba tatu kutoka miliki ya Panas.
“Gegu nini kimekutokea?”Aliuliza Nefi mara baada ya kumfikia yule majeruhi kwa haraka sana.
“Haraka … haraka ..”Aliongea na palepale aliinua mkono wake na kumshika Nefi kwa nguvu huku akiongea kwa shida.
“Mwambie kaka … Roma … Roma anaua watu wetu .. mwambie amevamia Panas”Aliongea kwa shida lakini taarifa yake ilieleweka.
Nefi na baadhi ya majini wa Hongmeng walishangazwa na kauli ile , walikuwa wakijua ndio Roma na Panas hakukuwa na maelewano mazunri lakini hawakutegemea angevamia miliki ya Panas mapema hivyo na kuanza kushambulia.
Mara baada ya kuona Gegu angepoteza maisha kama asingemfanyia huduma ya kwanza palepale alitoa kidonge cha daraja la kati ambacho kazi yake ni kuponya , ijapokuwa kilikuwa cha thamani lakini kwa wakati huo aliona ndio njia pekee ya kumuokoa Gegu.
Baada ya kumuwekea mdomonni alimsaidia kumponyesha na nguvu zake za kijini na hatimae majeraha yake yalipona na kumpa nafasi ya kuanza kukusanya nguvu za nishati ya mbingu na ardhi ili kurejewa na uwezo wake
Ndani ya sekude tu nguvu zake zilirudi na angalu macho yake yalirudi katika hali ya uhai.
“Nitakupeleka katika kisiwa cha anga kwa ajili ya kuonana na baba na wengine”Aliongea Nefi.
Nefi baba yake alikuwa ni Wucheni mkuu wa hadhi ya juu kabisa katika miliki hio ya Hongmeng.
“Nyie wengine nendeni mkatoe taarifa kwa mkuu wa miliki ya Panas haraka”Alitoa maagizo kwa wale wengine .
Katika dakika hio hali ya wasiwasi iliwafunika kila mmoja na raia hao wa Hongmeng walikimbia kwenda kutoa taarifa kwa haraka sana
Mara baada ya Nefi kumfikisha Gegu juu ya kisiwa moja kwa moja alienda mpaka katika eneo la mkutano unapofanyikia na aliweza kugundua tayari Anjiu na wenzake wamekwisha kufika.
Gefu mara baada ya kuona hali aliokuwa nayo Gegu macho yake yalisinyaa huku hasira ikianza kumvaa na haraka sana aliuliza kile kilichotokea.
Gegu ambaye alikuwa akihema kwa nguvu kama mbwa aliekimbia maili nyingi alielezea kila kilichotokea.
Ilionekana lisaa limoja lililopita Roma aliweza kuvamia miliki ya Panas , mara baada ya kugunduika na walinzi ni adui hakuwachelewesha na kuanza kuwashambulia , anasema ni kama vile anga linatema moto ambao ulikuwa ukiunguza makazi yao.
Gegu ambaye aliponea chupuchupu ndio aliweza kukimbia kuja katika miliki ya Hongmeng kwa ajili ya kutoa taarifa.
Anasema kama sio kusaidiwa na walinzi wa miliki waliokuwa katika levo ya maji ya upako na pamoja na Dhana asingeweza kukimbia kwani Roma alikuwa akimshambulia kwa kasi.
“Pumbavu!! , Kwannini Roma kutushambulia sisi Panas kwanza?”Aliongea Gefu kwa hasira huku akijizuia hata kuwazia kile ambacho kinaendelea wakati huo katika miliki yake.
“Gefu unamaanisha nini , kwahio ulitaka aanze kutushambulia sisi Kekexi kwanza?”Aliongea Menyu kwa jazba.
“Ndio ninachomaanisha kwanini asingeanza na nyie”
“Wewe mwanaharamu!!!”
“Inatosha , huu sio muda wa kulumbana , Roma ameenda miliki ya Panas kwasababu moja tu miliki ya Panas ipo katika bara la Afrika sehemu ambayo ipo karibu na Ulaya tofauti na miliki zetu ambazo kimahesabu ni kama zipo katika bara la Asia”Aliongea Anjiu.
“Nin!!”
Gefu na Menyu walishangaa lakini waliona alikuwa sahihi , ukweli ni kwamba kwa njia ya mkato inachukua dakika tano kamili kutoka Tanzania kuingia katika miliki ya Panas.
Lakini swali bado liliibuka katika kichwa cha Gefu , Roma amejuaje njia ya kuingia katika miliki yao maana kuna mahesabu ambayo wanatumia katika kufungua mlango unaoteganisha ulimwengu wa binadamu na miliki yao.
“Viongozi bado tu mtanzamo wenu ni wa kujijengea ukuta.?”Aliuliza Anjiu.
“Roma tayari amechagua kushambulia Panas kwanza kwasababu hakutaka usumbufu na miliki zetu za Xia na Kekexil na hii inaonyesha nia yake ni kushamblia miliki zote , hajali hata ni chuki ya namna gani anaitengeneza kwa kutushambulia , je bado mnaamini ataiacha na miliki ya Hongmeng au mnaamini mtaweza kumdhibiti baada ya miliki zetu kushambuiwa , mkumbuke kwamba ana Dhana ya Cauldron na roho ya Chaosi iliopo ndani yake inaweza kumeza nguvu ya aina yoyote ile na kadri anavyozidi kumeza nguvu za majini wengi ndio anavyozidi kuongezeka nguvu”
Viongozi wa Hongmeng wote walionyesha hali ya wasiwasi wao kwenye macho mara baada ya Anjiu kumaliza kauli hio.
Gefu palepale ni kama wazo lilimwingia na alimgeukia Gegu na kumuuliza swali.
“Gegu dada yetu wa tatu yupo wapi , je ndio anapambana na Roma muda huu?”Aliuliza akimaanisha Rozu.
“Hapana… Dada wa tatu hajaonekana na haijulikani ni wapi alipo , ki ufupi ni kwamba kapotea”Aliongea Gegu.
Hawakujua siku zote Rozu hakuwa mwenzao , alikuwa katika miliki za kijini kwa ajili ya kujipatia nguvu ya unabii maarufu kama Darubini ya Kichawi ya unajimu ambayo ingemsaidia kujua maisha ya mbele yapoje kupitia unabii ili kuweza kumshinda Athena na Hades.
“Okey , ili kutenda haki na kuondoa hii roho ya uovu, nitatupilia mbali unafiki wangu na kuungana na Wabobezi wa miliki zote tatu kumuua huyu shetani Roma Ramoni’Aliongea Wucheni.
Kauli hio ilimfurahisa Anjiu na wenzake na alijua sasa wana nafasi kubwa ya kumdhibiti Roma kama wataunganisha nguvu.
“Kama ndio tumekubaliana, basi bado hatujachelewa tutaita Wabobezi wote na kuianza safari ya kuelekeaPanas”Aliongea Anjiu.
“Amitabbha , awamu hii huyu mzee wenu hata ambatana na nyie , nitaungana na walinzi wa mipaka ili kutengeneza safu ya ulinzi wa jini pepo KingKong ili kuilinda Hongmeng , mniwie radhi”Aliongea Yanyun.
“Usiwe na wasiwasi tunaelewa”Aliongea
Ijapokuwa Yanyun hakuungana nao lakini bado Hongmeng walikuwa na wataalamu watatu wa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi lakini pia waliunganisha nguvu na majini wote ambao walikuwa katika daraja la mbingu.



SEHEMU YA 752.
PANAS
Yale majengo ya kisasa ambayo yalikuwa yameenda hewani , yaliokuwa yamejengwa kwa msingi imara yaliikuwa yamekatwa katikati huku mengine yakidondoka kwanzia chini kabisa kwenye msingi na kutengeneza kifusi.
Moto mkubwa uliokua ukiwaka katika kila pande ya makao makuu ya miliki hio ya Panas ulikuwa ukizidi kuongezeka katika kila kona huku ukivuka mpaka kwenye msitu uliokuwa karibu na eneo hilo.
Anguko la mikili ya Panas lilikuwa likikaribia muda wowore na kubakia katika historia.
Walinzi na majini wa Panas walikuwa wamepata majeraha makubwa mno na ni wachache sana ambao walikuwa wamefanikiwa kukimbia.
Damu iliotengeneza mfereji ilikuwa ikitiririika kuelekea katika mto uliopita katikati ya jiji la miliki hio na kufanya maji yake kubadilika rangi, ilikuwa ni vigumu kabisa kuelezea namna eneo hilo lilivyokuwa mwanzo kutokana na uharibifu uliotokea.
Hali ilikuwa ikitisha kweli kweli , kulikuwa na miguu pamoja na vichwa vilivyoachana na miili vimesambaa katika kila kona ya eneo hilo , ilikuwa ni ngumu kuona maiti ya jini ikiwa na viungo vyore.
Panas ilikuwa na majini wengi lakini maiti zao zilikuwa chache ikimaanisha kwamba asilimia kubwa ya majini hao walikuwa wamekwisha kuungua na wengine wamemezwa na chungu .
Ijapokuwa muda mfupi ujao eneo hilo lingefunikwa na nguvu ya giza kutokana na kuzama kwa jua lakini ilionekana kama vile ndio kwanza imefika mchana.
Roma alikuwa amesimama katikati ya mbingu na ardhi , macho yake yalikuwa sio ya ubinadamu kabisa , ilikuwa ni kama vile kuna roho abayo imemvaa kwa wakati huo.
Nguvu ya chungu kilichokuwa kikizunguka na kutoa makelele kilimeza nguvu ya upepo ndani ya eneo hilo.
Baada ya kuchinja na kuvunja vunja majini wengi mpaka wakati huo alikuwa amemeza nguvu za majini waliovuka levo ya dhiki wengu sana , kwa kujumlisha na uwezo wake wa mapigo mengi ya radi ilikuwa ni swala la muda tu kuingia katika levo nyingine.
Ukweli hakupata ukinzani wowote mara baada ya kuanza mashambuizi yake , alitegemea pengine Panas ingekuwa na nguvu kuliko Kekexil au Xia lakini hakuna jini yoyote ambaye alikuwa levo zake na kwake aliwaona kama viumbe dhaifu sana.
Wakati huo ni kama uwezo wake umeongezeka maradufu mara baada ya kufyonza nguvu za majini hao.
Dhana ya Chaos Cauldron na yenyewe haikuwa nyuma katika kujiimarisha nguvu kwa kumeza majini.
Chungu hicho kadri kilivyokuwa kikimeza ndio kilivyotengeneza mzingo mkubwa wa kani mvutano.
Mpaka dakika hio ni majini wawili tu wa miliki ya Panas ambao walikuwa wamesimama upande wa kulia na kushoto kwake wakijaribu kupambana nae.
Roma mpango wake ulikuwa ni kuimaliza kabisa miliki ya Panas na kuifutilia mbali , ukweli sio Panas tu alikuwa na mpango wa kumaliza majini wote na kuwatufilia mbali ili aweze kuishi kwa utulivu na amani.
“Wewe mhalifu , umeamsha hio roho ya kishetani na sasa inakwenda kumaliza ulimwengu , hakika lazima utakufa”Aliongea Gezi , mzee mmoja jini chotara ambaye alikuwa ni moja ya wazee wa umri mrefu ndani ya miliki hio , alikuwa na madirio ya umri wa miaka mia tatu na ushee, muda huo alikuwa akitema damu, huku mkononi akiwa ameshikilia siraha ya Dhahabu iliokuwa katika umbo la koni , alikuwa katika levo ya kati ya maji ya kiroho na Dhana hio ilionekana alikuwa akitumia kwa ajili ya kujilinda.
Ilikuwa ni Dhana ya kati ambapo katika elimu ya majini Dhana hio ilikuwa imebeba roho ya jini pepo aliekuwa na nguvu kubwa aliefahamika kwa jina la Tanywi.
Moja ya nguvu ya siraha hio ni kwamba ilikuwa na uwezo wa kubusti uwezo wa mtumiaji kwa kukusanya kiwango cha ziada cha nguvu ya kijini katika mazingira , lakini sio hivyo tu ilikuwa pia na uwezo wa wa kurahisisha mtiririko wa nguvu hizo kutoka katika senta ya hifadhi ya nishati.
Ilikuwa na uwezo wa kuzuia mashambulizi makubwa na hata kama ikishindwa kutokana na ukubwa wa shambulizi ilikuwa na uwezo wa kupunguza kasi ya mashambulizi.
Sasa ilionekana ndio ambayo iliweza kumlinda mzee huyo na kutokufa katika muda huo maana ilikuwa imetengeza uzio wa rangi ya Dhahabu wa mzingo wa futi kumi na iliweza kumlinda Geyu pamoja na Gezi kwa wakati mmoja.
Lakini wazee hao wote wawili hawakuwa na uwezo wa kujilinda muda mrefu kwani nguvu ya Roma ilikuwa kubwa mno na hawakuonyesha hali ya utulivu , ilikuwa ni kama muda wowote wangeweza kukumbwa na kifo kabla ya msaada wa majini wengine kufika.
”Hata kama nisingeacha kuwaua nyie mngekuja na kutaka kuua familia yangu , haya yote yanayowatokea yametokana na uchokozi wenu”
Roma hakuwa katika mudi kabisa ya kuwasikiliza wala kuwaonea huruma, alikuwa tayari amekwisha kufanya maamuzi ya kuangamiza miliki zote za kijini ,hakujali ni damu kiasi gani angekwenda kumwaga lakini kwasababu asipo fanya hivyo wangemrudia wao basi hakuona haja ya kuwasamehe.
Ilikuwa ni ukichaa lakini ndio mbinu pekee ambayo ni ya moja kwa moja aliona inaweza kumsaidia kuliko kumalizana na majini hao kwa njia ya kidiplomasia.
Chungu cha machafuko kiliendelea kushindana na ngao ile ya wale majini na dakika chache tu hatimae ngao ile iliweza kutengeneza upenyo.
Kutokana na wote wawili walikuwa wakiendesha ile Dhana ili kujumlisha nguvu yao mwanamke aliefahamika kwa ina la Geyu alitema damu mara baada ya ngao hio kutengeneza ufa.
“Geyuu…!!”Gezi alipiga yowe lakini kabla hata hajaiitikia Roma alikuwa ashatuma mashambulizi zaidi ya kumi katika ule upenyo.
Licha ya kwamba waliunganisha nguvu zao lakini uwezo wao bado ulikuwa ni wa chini sana kulinganisha na wa Roma na hata hivyo ilikuwa ni ujasiri na ujuzi wa aina yake ambao wametumia kuweza kumihili mashambulizi ya Roma mpaka wakati huo ili kusubiria msaada.
Kitendo cha kutuma shambulizi ilimtengenezea Roma mwanya mwingine wa kutuma mashambulizi ya moto wa Zambarau na kumshambulia yule mwanamke.
“Ni mwaka wa elfu kumi sasa mpaka kuanzishwa kwa miliki ya Panas , je leo ndio anguko lake”Aliwaza Gezi huku akimwangalia mwenzake namna pumzi inayyoachana na mwili.
Gezi alikuwa akijua kabisa miliki yao ilikuwa na wataalamu wa juu tu wabobezi lakini mpaka muda huo hawakuwa wamejitokeza na moja kwa moja alijua pengine walishajua hawana uwezo wa kushindana na Roma hivyo wakaamua kukimbia.
Alijua hata kama vita hio iishe muda huo ni ngumu sana Panas kurejea katika ukuu wake waliokuwa nao mwanzo kwani hasara ilikuwa ni kubwa mno ambayo haikuwahi kutokea wala kuwaziwa itakuja kuikumba miliki hio.
Roma upande wake aliona kuendelea kuwaangalia majini hao wakijificha chini ya ngao aliona ni swala la kupoteza muda na palepale alikipa kazi chungu na kiliwasogelea kwa kasi na kuwanza kuwavuta katika kila pande.
Gezi alijitahidi kushindana na kasi ya mvutano huo lakini alishindwa hata kusogea , upande wa Geyu yeye alikuwa amekwisha kujeruhiwa muda mrefu hivyo alikosa uwezo wa kuhimili nguvu ya mvutano na aliamua kujitoa tu kafara na kugeuka kuwa chakula.
Gezi aliishia kutoa machozi ya damu mara baada ya kushuhudia kifo cha rafiki yake wa muda mrefu.
Muda uleule wakati Roma akijiandaa kummeza na Gezi ghafla tu vitu kama mawe yaliokuwa meuzi yalirushwa kuelekea upande wake kwa spidi kubwa kama vile ni vimondo.
Roma palepale sura ilijikunja mara baada ya kuweza kuhisi ujio wa kundi kubwa la majini wanaomsogelea.
“Naona wamekuja kuongeza nguvu , vizuri wamenirahisishia kazi ya kwenda kuwatafuta”Aliwaza Roma.
Mara baada ya kugeuka aligeuza nguvu zake za kijini na kuwa kama vile ni shuka na kuyakinga yale mashambulizi yote.
Dakika hio hio Anjiu , Gefu na Wucheni walijitokeza mmoja baada ya mwingine huku wakifuatiwa na kundi kubwa la majini kutoka miliki ya Xia , Kekexil na Hongmeng.
Wale majini watu ambao Roma alikuwa akiwasubiria kwa muda mrefu kujitokeza hatimae walikuwa mbele yake.
Gefu chozi la maumivu lilimtoka mara baada ya kuona makao makuu ya miliki yake yalikuwa yameharibika kwa kiwango ambacho hakivumiliki na palepale hasira zilimvaa na nia ya kumuua Roma iliongezeka kwa zaidi ya mara elfu moja.
“Huyu moto ni katiri mno , inaonekana kama vile ametawaliwa na roho ya Chaos na kugeuka kuwa muuaji”Aliongea Shombeli.
“Nguvu ya huyu binadamu sio ya kawaida kabisa , ndio kwanza ana miaka ishirini hivi , inasikitisha kwamba ameruhusu shetani amtawale , kama tukishindwa kumuua leo hii hakika atakuja kuwa tatizo kubwa kwetu”Aliongea Menyu.
Muda huo Gezi aliweza kufanikiwa kukimbia kwenda upande wa wenzake na kuanza kuelezea hali ilivyo kwa mkuu wake.
Kwa maelezo ya Gezi ni kwamba mpaka wakati huo Roma amekwisha kuua majini wengi sana ikiwemo viongozi watatu wa juu sana na taarifa hio ilizidi kumkasirisha sana kiasi kwamba alitamani hata kutema damu.
Kitu ambacho kilimshangaza ni namna uzio wa kuingia katika makao makuu hayo ulivyovunjwa.
Roma aliangalia mamia ya majini hao ambao asilimia kubwa wote walikuwa ni wale wabobezi na walionekana kuwa na ari kubwa ya kutaka kumuua , hakuna hata mmoja aliekuwa akimwangalia kwa macho mazuri.
“Haina haja ya kuongea ujinga , haijalishi ni maamuzi gani ninachukua lakini hamna haki ya kutafsiri matendo yangu watu kama nyie mnaojitafutia umaarufu kupitia migongo ya wengine , Mungu anaangalia kila maamuzi mnayochukua na kila hatua mnayopiga na kilichotokea siku ya leo ni kutokana na tamaa zenu , mimi Roma Ramoni muwakilishi wa binadamu dhamiri yangu ni ya wazi , angalau mimi sikatati pale ninapoua mtu wala ninapofanya makosa , ninachotaka sasa hivi ni kuwaueni wote na damu yenu kusafisha ulimwengu huu wa majini , kama uwezo mnao pambaneni na mimi vinginevyo msinilaumu kwa kutowapa nafasi ya kuonyesha uwezo wenu , nataka kuona ni kipi mnachoweza kunifanya leo hii”
“Wewe kibinadamu hakika una majigambo sijapata ona , hivi unaamini una nguvu kubwa kuweza kupambana na majini mia moja kwa wakati mmoja ,pengie leo hii ningekupa tu adhabu kwa kuzingatia asili yako lakini ulichokifanya leo hakisameheki”
Roma alishangazwa na kali ya Wucheni kusema maswala ya asili lakini hakutaka kujua anamaanisha nini maana alikuwa mvivu wa kufikiria.
Wucheni palepale alisogea mbele na mwili wake wote ni kama vile umefunikwa na gamba lingine la ngozi huku nguvu za kijini zikimtoka kama vile ni ukungu wa asubuhi na ghafla tu siraha ndefu sana ilitokea katika mikono yake.
Siraha hio ilikuwa ni nyeusi tupu na rangi ya bluu huku ikiwa na michoro ya kustaajabisha ya kikale iliokuwa imechorwa , ilikuwa ni mwishoni katika makali ndio kulikuwa na rangi ya bluu bahari.
Siraha hio ilikuwa kubwa kwa futi kama kumi hivi na ilikuwa na upana mkubwa mno , ilikuwa ni siraha kubwa mno ya kimaajabu lakini mbele ya jini huyo haikuonekana kama siraha nzito kuishikilia.
“Wucheni kiongozi wa hadhi naona namna ambavyo upo siriasi mara baada tu ya kufika ushatoa huo upanga wa kimilenia”
“Lazima nifanye hivyo ninaeshindana nae hapa tayari ashaivuka radi na anatumia Dhana ya kihistoria ya Chaos Cauldron , ijapokuwa siraha yangu ilitumiwa na jini aliekuwa na nguvu na imejaa r nguvu ya roho ya kukatisha tamaa lakini bado haina nguvu kama Cauldron”
“Ni ngumu kutabiri pia , hapa kuna damu nyingi imemwagika na chanzo cha nguvu ya upanga huo ni damu , nadhani nguvu yake itaongezeka kwa kasi”
“Lakini kiongozi uwezo wake…”
“Kwanini unajaribu kukadiria uwezo wa adui yetu?”Aliongea Shombeli akimkatisha moja ya majini kutoka Hongmeng ambaye alikuwa akitaka kuongea..
“Siraha ya uungu wa Nebula!!”
Shombeli aliongea kwa nguvu na palepale nguvu zake za kijini ni kama zilikuwa zikijikusanya na kufumba na kufumbua siraha ya rangi iliweza kutokea mbele yake .
Dhana hio ilikuwa ni ya kimaajabu ya daraja la kati la kimaajabu na mashambulizi yake ni yale ya kutokutabirika , kutokana na uwezo wake wa kutumia siraha basi nguvu yake haikuwa ya kupuuzwa.
Kulikuwa na Dhana ya upanga mweusi na kushoto kulikuwa na siraha ya kinebula , majini wengine na wenyewe hawakuzubaa walikusanya kila walichokuwa nacho na kumzingira Roma.
Anjiu na Gefu pia waliungana pia pamoja na wafuasi wao kwa ajili ya kushambulia , ilionekana hawakuwa na sababu ya kushambulia mmoja mmoja bali wote walitaka kufanya mashambulizi.
Roma macho yake yalisinyaa na palepale hisia zake zilimwambia pengine hao majini wamekuja na mbinu ya kutaka kummaliza mapema na kama atakurupuka kushambulia mmoja wapo anaweza kuzidiwa hivyo alisubiri kuona wanachokipanga na kuangaia namna ya kuwadhibiti mmoja baada ya mwingine.
“Nafsi pepo kutoka Kaskazini, Shibe mmiliki wa barafu”
“Utupu wa mzimu katika anga ya Nebula!!”
Ule upanga wa Wucheni ulifyatuka kwenda agani na kugeuza chini na kuanza kutengeneza mapanga mengi na kumshukia Roma kama mishale.
Silaha ya kiuungu ya Nebula ilitengeneza kitu kama shimo ambalo halina hewa ndani yake na kumshukia Roma na kumuweka kati.
Roma alishangazwa na namna ambavyo Wucheni na Shombeli walivyokuwa spidi ya kufanya mashambulizi.
Dakika ileile kulitokea boma la barafu kubwa ambalo lilikuwa ikijjijenga kwenda juu , kitendo kile kilimfanya Roma kukumbuka aina hio ya ngao na mawazo yake yalimrudisha kwa mtu aliemshambulia kule Australia.
Palepale akili yake ilimwambia mtu ambaye aliemshambulia akiwa kule Arnhem Australia akiwa katika vazi la Mask pengine ni Wucheni jini wa miliki ya Hongmeng.





SEHEMU YA 753.
Roma hakuwa na uhakika pengine labda amuulize yeye mwenyewe , maana siku ile alikuwa amevalia Mask lakini nywele zake zilikuwa tofauti kidogo siku hio hivyo hakuwa na majibu sahihi kama mtu aliemshambulia wakati akitafuta miti shamba ni huyo huyo Wucheni.
Roma hakuwa na muda wa kuwaza kwani aliona ni kama vile anatengenezewa gereza la kukamatiwa katikati.
Roma pia hakutaka kuttubutu kuruhsu nguvu ya mashambulizi ya siraha ile ya Nebula kumfikia na palepale alitumia Chungu kukinga mashambulizi yote , ijapokuwa chungu kilikuwa kipipitia mapigo ya nguvu hio lakini kutokana na udhibiti wake aliweza kukinga mashambulizi yote mawili ya Wucheni na Shombeli.
Hakukuwa na ubishi majini hao wanne walikuwa ndio mhimili wa Hongmeng kutokana na uwezo wao na ili kuhakikisha wanashinda pambano walitumia uchawi wa kilevi na kufawafanya majini hata wale wa levo ya chini kuingiwa na hali ya kujiamini na hofu ya kifo iliwatoweka.
“Roho usie na mipaka ,Vifungo vva kuzimu”Aliongea Shombeli
Wakati ule Roma alipokuwa akitaka kufanya shambulizi kuvunja boma la barafu lisilioelezeka , zile panga za nguvu za kijini ambazo zilitumwa na Wucheni kumshambulia hazikumffikia moja kwa moja bali zilikuwa zikizunguka hewani na kutengeneza mfumo wa ajabu mno.
Roma palepale alijua nini kinatokea , ilionekana zile panga zilikuwa zikifyonza nguvu ya damu ya majini iliokuwa imemwagika katika ardhi ili kujiongezea nguvu.
Roma palepale aliona ashambulie panga zile kabla hazijaendelea kujikusanyia nguvu zaidi na zaidi lakini sasa ile anataka kufanya mashabulizi zilifyatuka kwa namna ya kutawanyika na kisha zilielekea kwenda ardhini kwa kasi kubwa mno.
Ilikuwa ni kitendo cha sekunde tu zile panga zote ziliungana na kutengeneza mkuki mmoja wa nishati ya mbingu na ardhi na kumsogelea Roma kama mshale kwa spidi kubwa mno
“Bang , Bang , Bang!!”
Ile siraha iliokuwa kama mkuki kabla haijamkaribia Roma kulitokea mlipuko na kufumba na kufumbua kulitokea mapanga marefu mengi zaidi ya nishati na kuungana kwa namna ya kipekee na kutengeneza kitu kama kijumba hivi ambacho kilimfanya Roma kuwa ndani yake kama vile ni kijumba cha mbwa.
Ilionekana ni gereza la nishati ya mbingu na Ardhi ambalo siraha zile imetengneza kwa ajili ya kumkamata Roma.
Roma alishangazwa na uwezo wa kimaajubu aliokuwa nao Shombeli na Wucheni , ulikuwa ni uwezo wa kichawi ambao aliweza kuuona katika vitabu mara baada ya kutembelea dhehebu la Tang kule China milima ya Shushan.
Lakini licha ya kumtengeneza gereza lile la visu lakini bado nguvu yake haikuwa kubwa zaidi kumzingira Roma.
Roma mwili wake ulikuwa umemezwa na roho ya hasira , ya vifo na uozo, ilikuwa ni kama vile visu vile vilikuwa vimepakwa sumu ya nyoka.
Visu vilizid kuungana katika gereza lile kwa kasi kumzingira Roma lakini hata hivyo bado kigereza hicho kilikuwa dhaifu kuhimili moto wa rangi ya zambarau.
Ilimtumia Roma sekunde tu kujinasua katika gereza la visu na alichokuwa akitaka ni kuweza kupitisha mashambulizi yake katika boma ya barafu aliotengeneza Wucheni lakini ni kama alikuwa akisubiriwa kwani ile Dhana yake ya Lindi(Abyss) ilikuwa ikikusanya nguvu za giza kutoka katika kila pande na kuifanya kuwa hatari zaidi na zaidi.
“Hii ni…”
Roma macho yake yalisinyaa kutokana na uelewa wa nguvu za giza , Roma uwezo wake wa kuhisi roho ya kimizimu ulikuwa ni mkubwa mno kuliko mwanzo.
Sasa kilichokuwa kikifanyika ni kwamba wale majini ambao walionekana kufariki roho zao bado hazikuwa zimekimbia mbali zilikuwa zikizunguka ndani ya eneo hilo na ile siraha ya Wucheni ndio ilikuwa ikikusanya nguvu za roho hio na kutengeneza lindi kubwa la makali(ferrocius)kutoka katika hio Dhana.
“Haha… wewe pia ni shetani, unatuhubutu vipi kuniambia mimi nikichaa niliepotoka wakati siraha yako hio ya maajabu imefanikiwa kukusanya roho za hao majini waliokwisha kufa , hata kama hao majini wamekwisha kufa bado hawawezi kukupatia nguvu kubwa ya kushindana na mimi”
Aliongea Roma na palepale alifyatuka kuelekea chini ya ardhi ikiwa kama vile anafanya mawasiliano ya anga na ardhi na palepale aligeuza nguvu zake za kijini na kuwa donge la moto wa nguvu ya giza na kisha alimsogelea Wucheni kwa spidi kwa kutaka kumshambulia nalo.
“Pepo barafu wa Kaskazini , mvua ya mishale barafu,visosi mia moja vya barafu kutoka madhabahu ya Shibe!!”
Wucheni ambaye alikuwa juu ya Roma alifyatua ile siraha yake na ilitokea vitu kama mishale ya midogo ya barafu na kumvaa huku vitu kama vile ni visahani vya barafu vilienda kumvaa Roma kwa spidi kubwa.
Ilionekana Wucheni alikuwa ametumia nguvu kubwa kumshambulia Roma lakini ukweli ni kwamba Roma alikuwa na nguvu kubwa mno kuweza kujeruhiwa na shambulio la namna hio.
Mpango wa Shombeli na Wucheni ni kumkamata Roma ili asiweze kutumia nguvu zake za kijini na kisha Anjiu na wenzake waanze kumshamblia lakini kila namna ambavo walikuwa wakifanya ilikuwa ngumu kwao kumkamata na mashambulizi ya namna yoyote ile.
Walitumia mbinu lakini hawakuweza kumfanya Roma chochote kwani kila mtego waliokuwa wakijaribu kumkamata nao ulishindikana kabisa.
Baada ya kuona wameshindwa Gefu alimpa ishara Shozi aingie na yeye kazini kutekeleza mpango wao.
Wucheni roho ilikuwa ikimtoka , kitu pekee ambacho waliweza kufanikisha ni kumfanya Roma kutokufanya mashambulizi kwani walikuwa wakishambulia kwa spidi kubwa.
Sasa mara baada ya Shozi kuingia kazini kitu cha kwanza kabisa alichokifanya kilimshangaza Roma kwani alianza kutokwa na damu kama vile ni mgonjwa wa Ebola kwani damu ilitoka katika kila tundu la kichwa chake.
Sijapambana nae lakini ashaanza kutoa damu kila tundu , anajaribu kufanya nini?”Aliwaza Roma akiwa kwenye mshangao lakini ni ndani ya muda uleule aliweza kukisia kinachokwenda kutokea , ilionekana kuna mbinu ya kimaajabu ambayo ili kuamka lazima atumie damu yake.
Roma alipata wazo mara baada ya kuona hakuwa akitema damu tu bali kulikuwa na vitu kama vile ni vijisumari vidogo vidogo ambavyo mara baada a damu kukauka nguvu ya ajabu ilianza kusambaa , ilikuwa ni msisimko wa nguvu ya ajabu mno na ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua lilitokea fuvu la kiumbe cha ajabu katika mkono wa Shozi ambalo limetapakaa damu.
Ilikuwa ni dakika ileile Roma sasa alweza kujua alichokuwa akifanya mara baada ya vile vitu kuongezeka ukubwa , misumari ile ilikuwa jumla yake ni tisa
Shozi mwili ulikuwa ukimtetemeka mno na damu kuzidi kumtoka na ilikuwa ni ndani ya sekunde chache tu yalitokea mafuvu tisa .
Roma hakutaka kujiluliza mara mbilimbili mara baada ya kuona ile misumali ya skeletoni inamsogelea kwa kasi kubwa mno huku ikizalisha nguvu ya ajabu.
Lakini sasa Roma alijua pengine inakwenda kumshambulia lakini mara baada ya kumkaribia ilitawanyika katika umbali wa futi kama kumi na mbili hivi na kufumba na kufumbua ile misumari tisa ya mifupa iliungana na yale mafuvu na kutengeneza umbo la Dimenssion tatu.
Ilikuwa ni kufumba na kufumbua Roma alijikuta akiwa ndani ya boksi la damu , ilionekana dhamira ya shambulizi lile sio kwa ajili ya kumshambulia bali kumkamata.
Roma aliishia kukunja ndita kwani hakutemgemea tukio la namna hio , ilionekana majini walikuwa na vitu vingi mno vya kuonyesha kabla ya pambano kuisha.
Roma hakutaka kulembesha alijua hakuna namna anaweza kufungiwa katia mtego wa namna hio na palepale aliandaa bomu la nguvu za mbingu na ardhi na kujaribu kulipua lile boksi.
“Boom!!
Mara baada ya mlipuko mkubwa wa kuumiza masikio kutokea Roma alijikuta akilia ndani kwa ndani mara baada ya kuhisi maumivu makali sana.
Roma alihihisi ni kama vile yupo kwenye chumba ambacho kuta zake zote zimejengwa kwa vioo vya kujiangalia na kila anachokifanya ni kama vile kinamrudia.
Yaani lile shambulizi lake lilidunda katika kuta na kisha likamrudia yeye mwenyewe na kumuunguza.
“What the hell!!!”
Roma alipiga yowe mara baada ya kuuguzwa na moto wa rangi ya zambarau ambao alitumia kushambulia
Roma aliishia kusambaratisha moto ule ili usimuunguze bahati nzuri ni kwamba hakuogopa moto wa namna hio kutokana na mbinu yake ya adiko
Mara baada ya kuona ni kama Roma anajishambulia mwenyewe baada ya kuingia katika mtego waliomwandalia majinii hao walianza kuangua kicheko kikubwa mno na wote walionyesha ishra kwamba wanakwenda kushinda hilo pambano.
“Wewe mtoto Roma hivi unadhani hakuna mtu ambaye anaweza kupambana na wewe , , yaani unakuja kwenye ulimwengu wa majini kwa ajii ya kushindana na sisi wabobezi wa nishati za mbingu na ardhi , ni majigambo ya namna gani hayo kutuchukuliwa kiwepesi namna hio”Aliongea Menyu.
“Hakika Shozi unastahili kupewa sifa ya uti wa mgongo wa usalama wa miliki ya Panas”Aliongea Umini akimsifia Shozi.
“Hey! .. khoo ..koho”
Shozi alishia kucheka lakini alionekana kupaliwa na kikohozi mfululizo na kulikuwa na damu iliokuwa ikimtoka pembeni kwenye midomo.
Uso wake ulikuwa umepauka sana lakini alizidi kubadilika na kuwa kama mti mkavu na nguvu yake ya kijini ilionekana kupungua kwa kiasi kikubwa.
“Gefu awamu hii uliniambia nije na nishafanya ulichoniambia , kwasasa nishakuwa dhaifu tayari hivyo unapaswa kunilinda , isitokee baadhi ya wahalifu wakatumia udhaifu wangu kunishambulia”a
“Usiwe na waswasi Shozi, leo hii hawa wote waliokuwa mbele yako wapo hapa kwa ajili ya kushuhudia kifo cha Roma Ramoni na wewe ni muokozi wetu”Aliongea Gefu
Shozi aliishia kucheka na alisema hivyo ili kila mmoja kuweza kusikia ili kama ikitokea yoyote kumshambulia ili moja kwa moja iwe ni aibu kwake.
Ilikuwa ni wakati huo macho yao yote yalikuwa yakimwangalia Roma aliekuwa kwenye boksi la damu , Roma alikuwa akitumia kila mbinu ili kujitoa katika mtego wa boksi ambalo amewekewa , alijaribu hata kuvuta boksi hilo na Cauldron lakini kila alivyokuwa akijaribu kushambulia mapigo yalimrudia yeye mwenyewe kitendo ambacho kilimfanya kupata majeraha makubwa ambayo ameyasababisha yeye mwenyewe.
Ilikuwa kwa bahati nguvu ya andiko la urejesho wa azimio lilikuwa na spidi ya kumponya.
Roma alijaribu kutumia upanga kushambulia ukuta wa kingo za boksi lile na alikuja kugundua kila alivyokuwa akishambulia kuna vitu kama vile vipele vya damu vivyokuwa vikisambaaa katika mwili wake na kisha hugeuka na kuwa kama vipele vyeusi na kupasuka kisha kufutika.
Roma alijiuliza au ni tindikali lakini mara baada ya kuangalia kwa umakini aliweza kugundua kwamba ukuta huo ulikuwa ukiongezeka nguvu kutokana na kwamba ile damu ambayo ilikuwa ikigusana na mwili wake ilikuwa ikinyonya nguvu yake kwa kukausha damu.
Roma alijua kama ataendelea na mbinu hio hio hawezi kuondoka hapo kwani kadri atakavyokuwa anashambulia ukuta huo basi ndio nguvu zake zitakvyokuwa zinaisha na ukuta kuzidi kuimariaka.
“Kijana usihangaike sana , nitakufanya ufe kwa amani , hio ni Dhana ya misumari tisa ya mfupa wa Dragoni na mafuvu yake, ijapokuwa ni Dhana ya daraja la kati lakini ilitengenezwa na mababu zetu wa enzi hizo kwa ajili ya kukamata majini pepo wenye levo kubwa kufikia levo ya kuidhibiti radi pale wanapokiuka sheria
Hii dhana ya kimajabu inafanya kazi kwa kunyonya damu ya mzee wa miaka mia tatu na kila inapotumika itatumia kiasi kikubwa cha damu lakini inao uwezo wa kufukuza na kukamata adui , ukishakamatwa na mtego wake kazi yake ni kunyonya damu kila mara inapokutana na nguvu za kijini , ijapokuwa uwezo wangu sio mkubwa sana lakini unatosha kabisa kukukamata mtu kama wewe ambaye umekwisha kuipita dhiki ya radi, haijalishi Chaos Cauldron ina nguvu namna gani lakini hakiwezi kuvunja huo mtego”
Roma mara baada ya kusikia maelezo hayo aliishia kuchukia , ilionekana majini wa enzi hizo walikuwa na juhudi kubwa katika kushambulia wenzao waliokuwa levo za juu mpaka kuunda Dhana hio.
Lakini alijiuliza kama Dhana hio ni ya zama za kale imewezaje kufika katika mikono ya Shozi.
Ukweli ni kwamba hio Dhana ilikuwa mali binafsi ya Shozi na sio ya Panas na kabla ya kuja katika miliki hio alikuwa nayo tayari haiikueleweka aliipata vipi lakini ilikuwa na nguvu kubwa mno.
Shida kubwa ni kwamba Dhana hio ili kuendelea kuwa na nguvu lazima inyonye damu na kwasababu hio Shozi alikuwa ameua majini wengi sana kwa ajili ya kulisha hio Dhana.
Ilikuwa ni Dhana hai ya kijini ambayo ina tabia kama za Vampire bila damu haifanyi kazi na inalishwa damu hio kila baada ya siku therathini katika kipindi cha mwaka mzima , uzuri ni kwamba damu haijalishi hio ina nguvu za mbingu ili mradi iwe ni damu tu lakini damu ya jini mwenye nguvu kubwa ndio faida huwa kubwa.
Kama ilivyokuwa kwa Dhana ya Cauldron kutaka kumvaa Roma basi dhana hio pia ilikuwa ikimfanya Shozi kukonda kwani ilikuwa ikifyonza damu yake kila siku na ndio maana ngozi yake ilionekana kuwa kavu na kuwa kama vile amechakaa.
Roma hakutaka kuamini kirahisi maneno ya Shozi hivyo alijaribu kuita nguvu za kijini kushambulia boksi hilo ili kuchoropoka.
“Mnasubiri nini , ili kumzuia kabisa asipate nafasi ya kutoka kwanini msiunganishe nguvu zenu za kijini katika misumari yangu ili tumkaushe damu na kumuua kwa haraka “Aliongea Shozi.
Anjiu na wenzake mara baada ya kusikia kauli hio hawakutaka kuzubaa na kila mmoja alishikilia msumari wake wa Dragoni katika kila fuvu na kisha wakapitisha nguvu zao za kijini ili kuongezea nguvu Roma asiweze kuchoropoka.
Kadri walivyokuwa wakilisha nguvu ile misumali ya skeleton lile boksi lilizidi kukorea rangi na kuwa la damu tupu na kumfanya Roma kutokuonekana kwa nje.
Roma hakujua nguvu ya boksi hilo mara ya kwanza lakini hatimae sasa alijua nini kinafanyika , kwani ngozi yake ilianza kuota vipele vyeusi vingi sana kwa kasi kubwa na nguvu zake za kijini ni kama vile zinapungua kila mara baada ya vipele hivyo kupasuka na kukauka.
“Pumbavu kabisa inaonekana huu ndio ulikuwa mpango wao tokea mwanzo ndio maana wakakusanya majini wengi namna hio”
Aliwaza Roma na pale karibia majini yote waliunganisha nguvu zao na kuzichaneli katika ile misumari na kadri walivyokuwa wakifanya hivyo lile boksi lilizidi kuwa jekundu kama vile karatasi ambalo limeloa damu na kuta zake kuzidi kuwa pana.
Roma vipele vilizidi kumtoka na vilikuwa vikitoka kwa awamu na kisha vinapasuka na damu inapotea na kisha jeraha linapona na vinaota tena kwa kasi kubwa huku akihisi maumivu makali mno.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA .

MTUNZI SINGANOJR.

Mono no aware

SEHEMU YA 754.
Roma aliishia kukunja sura akiwa ndani ya Kizimba(Cage) amekunja ngumi kwa hasira huku akiwa kimya wakati vipele vikienelea kuota katika mwili wake na kunyauka kwa kasi.
Wakati Roma akionekana kama vile amejikatia tamaa kabisa majini wale walishangilia na kuridhika kabisa.
“Haha..ulikuwa na maringo sana lakini sasa hivi umekuwa mpole kama mbwa , unaonaje ukipiga magoti na kuomba msamaha?”Aliongea Menyu mkuu wa miliki ya Kekexil huku akicheka kicheko cha furaha.
“Nadhani anaogopa sana hapo kiasi cha kushindwa kuongea chochote , ndani ya lisaa limoja na nusu huyu shetani atakuwa amekwisha kufa”Aliongea Gefu akiwa katika hali ya kutabasamu
“Uhai wa raia wa Panas zaidi ya elfu moja umepotea katika mikono yako hivyo ni damu yako inakwenda kulipia deni”Aliendelea kuongea.
“Haina haja ya kupoteza maneno yetu , tumuueni kwa nguvu zetu zote ili kusitokee tatizo kabisa”Aliongea Anjiu.
Majini hao hatimae walikaa kimya lakini hakuna ambaye alijali kwani asilimia mia moja wote walikuwa wakitaka kuona kifo cha Roma.
Dhana ya fuvu la misumari tisa ya mfupa wa Dragon iliendana na jina lake , majini hao katika vitabu vyao walisoma na kuelewa kwamba ambao washawahi kutumia Dhana hio wengi wao wamekwisha kufa kutokana na kunyonywa damu.
Ukweli ni kwamba hata kwa Shozi ambaye alikuwa mdhibiti wa Dhana hio, kama akifanikiwa kumkamata Roma katika kizimba hicho cha damu baada ya hapo kuna uwezekano mdogo sana wa kuendelea kuishi muda mrefu , hio Dhana athari yake kubwa ni kupunguza urefu wa maisha kutokana na kwamba inanyonya uhai kupitia damu.
Roma alikuwa amesimama katikati ya boksi hilo , chungu chake cha maafa kilikuwa pia kipo ndani kikielea katika kichwa chake, ule ukali wa chungu hicho ulionekana kupungua kabisa.
Dakika iliofuata baada ya Roma kunyanyua kichwa chake uso wake haukuonyesha ishara yoyote ya wasiwasi lakini viashiria vya kukata tamaa vilionekana kwa mbali.
“Inanishangaza kuona bado unao uwezo wa kutumia huo mkono…”
Majini hao waliokuwa wamezunguka kizimba hicho cha gereza la damu hawakumwelewa Roma anachomaanisha na walioamini anaongea ujinga.
Roma mara baada ya kuwaza kwa dakika kadhaa palepale aliweka kila alichokuwa amekishikilia katika hifadhi ya pete na kisha mkono wake mmoja wa kulia alibadilisiha nishati za mbingu na ardhi kwa kutengeneza moto wa rangi ya zambaranu na mwingine akatengeneza moto wa rangi ya bluu na madonge yale ya moto yalizidi kuongezeka ukubwa kadri sekunde zilivyokuwa zikisonga.
“Dogo bado tu unahangaika , unachokitafanya ndio kitakuua mapema”Aliongea Umini.
Roma alimpotezea kabisa na wakati moto ule ukiwa unawaka katikam mikono yake alifanya kitu kama vile anapiga makofi ili kuunganisha ule moto kwa pamoja.
“BOOM!!
Moto wa rangi ya Zambarau na wa bluu uligongana na kusababisha kishindo cha aina yake , ilikuwa ni kama vile aina hizo mbili za nishati zilikuwa zikiumana na kujaribu kumezana kwa wakati mmoja.
Ilichukua sekunde kadhaa tu kama vile kemikali zimeungana hatimae kulitokea matokeo mengine kabisa ambayo ni ya kimaajabu mno.
Roma mikono yake ilikuwa ikitetemeka kwa nguvu kama vile inaungua na alitumia nguvu ambayo sio ya kawaida kujaribu kuhakikisha nguvu hizo mbili za moto zinaungana ili kutengeneza kitu kingine.
“Buzz. Buzzz, Buzzz!!!!”
Ilikuwa ni cheche za umeme ambazo zilitoa sauti flani hivi kama ile ambayo inasikika wakati wa mafundi wakichomelea chuma na umeme lakini yenye sauti kubwa mno.
Mwanga wa ajabu uliweza kutokea pia katikati ya viganja vya mikono ya Roma na kuna kitu ambacho ni kama vile kinafutuka kana kwamba muda wowote kinakwenda kulipuka.
“Hicho ... hicho ni……!!!!!”
Anjiu ndio aliekuwa wa kwanza kuhamaki mara baada ya kuhisi kitu cha ajabu , macho yake yalikuwa yamepanuka kiasi kwamba yanataka kumchomoka.
Wucheni na wenzake pia walianza kuhisi nguvu ya ajabu ikitoka katika eneo ambalo amesimama Roma , ilikuwa ni nguvu ambayo hawakuwahi kuihisia katika maisha yao yote na ilionekana nguvu ile ilikuwa ikianza kula ukuta wa kizimba cha damu.
Mwanga uliokuwa ukionekana katikati ya mikono ya Roma ulizidi kuongezeka na kuzidi kuwa na nguvu sekunde hadi sekunde.
“Hehe.. hahaha simaanishi ,,, kila kitu kilichopo chini ya nguvu ya radi ya mapigo mengi , moto wa mbingu na maji ya kiroho hayana nguvu.. dah .. ninashauku .. kama nguvu ya radi ya mapigo tisa athari zake zilivyo”
Roma alikuwa akibwabwaja mwenyewe maneno ambayo hayakuwa yakieleweka ilionekana ni kama vile kuna ufunuo anaupata.
Palepale aliinua sura yake juu kama vile anaangalia anga huku akitunisha kifua na ghafla tu mikono yake ilijiachia.
“Hey!!”
Ghafla tu shoti ya radi ya mwanga wa bluu na zambarau ilitoka katika mikono yake na kutengeneza umbo kama la mkuki uliopinda pinda huku ukitoa cheche.
Mwanga wake ulikuwa ni mkali mno na ndani ya sekunde tu Roma alikuwa amefunikwa na mwanga ule na sehemu aliosimama ilionekana kama vile ni jua la rangi ya bluu zambarau na ngurumo kubwa ilianza kugonga na mwanga ulikuwa ukizidi kuongezeka na kuwa mkubwa sekunde hadi sekunde.
Upande wa Roma alikuwa akiendelea kuzalisha moto wa bluu na wa zambarau katika mikono yake na kuunganisha kwa spidi kubwa na kadri alivyokuwa akifanya hivyo ni kama yeye mwenyewe anageuka na kuwa nishati ya ajabu vile.
Ndani ya sekunde chache tu kile kizimba cha damu kilibadilika rangi na kufunikwa na mwanga na ngurumo za radi zilizidi kuongezeka na shoti za rangi ya urujuani zilianza kutoka.
“Haiwezekani … radi ya Zambarau!!!?”
Gefu ndio aliekuwa wa kwanza kuhamaki , huku majini wengine wakiwa ni kama hawaamini kile ambacho wanakiona mbele yao.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba moto wa bluu unatokana na mapigo tisa ya radi yaani kwa lugha nyepesi ile nguvu ambayo unaipata baada ya kupitia mapigo tisa ya radi ndio inakufanya kuweza kudhibiti moto wa bluu , upande mwingine mapito tisini na tisa yanakupa uwezo wa kutengeneza moto wa zambarau.
Sasa kwa haraka haraka Roma ni kama ameunganisha nguvu ya radi ya mapigo tisini na tisa na nguvu ya radi ya mapigo tisa na kufanikiwa kudhibiti radi ya rangi ya urujuani(Violet).
Sasa majini walishangaa mara baada ya kuona Roma amegeuza moto wa bluu na wa zambarau kutengeneza radi ya zambarau.
Shozi ambaye ndio alikuwa akidhibiti kizimba cha misumari na mafuvu tisa ya mfupa wa Dragoni alianza kutetemeka kwa maumivu ,ilikuwa ni kama vile mwili wake unakwenda kupasuka kutokana na presha kubwa iliokuwa ikimwingia.
“Haraka ongezeeni nguvu ya nishati za mbingu kuimalisha ulinzi , anataka kujinasua!”Aliongea Shozi kwa kubweka.
Haikujalisha aliongea kwa sauti kubwa namna gani lakini majini hao mioyo yao ilikuwa imetingishika kabisa na kukosa ujasiri.
Moja ya udhaifu wa majini ni radi(Wenyewe wanaita moto wa mbingu) , wanaiogopa radi kuliko kitu chochote kile na ndio adhabu yao kubwa ambayo ukiipita wanakupa heshima.
Kile kizimba kilishindwa kumnyonya Roma damu tena na sekunde baada ya sekunde kilikuwa kikipoteza nguvu.
Anjiu macho yake yalionyesha hali ya kusita kulikokithiri , alikuwa pia ni jini ambaye amepitia mapigo ya radi hivyo swali liliibuka kwanini Roma kuwa na mwili wenye utimamu wa namna hio mpaka kufanikiwa kuidhibiti radi , alishakuwa katika mshangao kwa uwezo wake wa kudhibiti moto wa bluu , Wa zambarau na maji ya kiroho lakini wakati huo amefanikiwa pia kuidhibiti radi ya rangi ya urujuani.
Alijiambia hapana haiwezekani sio ujuzi pekee wa Roma katika kung’amua siri za mafunzo ya mbingu za ardhi na mbingu tu , pengine ametawaliwa na nguvu ya roho ya andiko la Urejesho.
Kadri alivyokuwa akiwaza ndio namna ambavyo alizidi kuwa na hasira , alijiambia kwanini sio yeye mwenye kumiliki mbinu hio ya andiko la urejesho wa azimio, kwanini ashindwe na binadamu ambaye amejifunza utamaduni wao.
Yeye ni jini kikamilifu kwanini ashindwe na binadamu ambaye hana damu ya kijini.
Pengine Roma angeangua kicheko kama angejua kile ambacho Anjiu alikuwa akiwaza , mbinu hio ya mafunzo ilikuwa amepatiwa ndio lakini hakuwa akiwaza watu wanavyoichukulia wala kuamini uwezo wake.
“Kama nilivyotarajjia , ijapokuwa hichi kizimba chenu kinaweza kuwa kama gereza kwa jini mwenye kuipita radi lakini ni ngumu kuhimili shambulizi la radi ya Urujuani ambayo hata jini ambaye amepitia mapigo elfu moja anaogopa”Aliongea Roma.
Aliangalia kizimba hicho ambacho tayari kilikuwa kikitetema na alijitingisha kidogo tu radi ile ya Zambarau ilitoka kama vile ni mshale na mara baada ya kugusana na kingo za kizimba kile kilipasuka na kuharibu kabisa ile Dhana.
Roma ni kama vile hakuwa na uwezo wa kudhibiti uwezo wake na kama angejua nguvu ya radi hio ilikuwa na nguvu namna hio asingetumia kiharibu Dhana hio kwani angeipata huenda ingekuwa na matumizi kwake hapo baadae.
Lawama alizipeleka kwa jini Shozi kwa kutokuwa na nguvu za kutosha za nishati ya mbingu na ardhi ndio maana shambulizi lake moja limeharibu Dhana hio.
Shozi mara baada ya Dhana yake kuharibiwa ilikuwa ni kama moyo wake ndani umepasuka na alitema damu nyingi sana na uso wake ulikuwa mweupe kama vile ni karatasi kutokana na kukosa damu na hakuendelea hata kusalia katika anga kwani alidondoka chini kama kifusi akiwa katika hali ya kukata tamaa kabisa.
Dhana ya misumari na mafuvu tisa ya mfupa wa dragoni ndio uikuwa ni kiini cha uhai wake na kitendo cha kuharibiwa na pigo la radi ya bluu zambarau haikuwa tu nguvu zake za kijini kumpotea lakini pia kifo kilimpata .
Hatimae Roma alikuwa amechoropoka kwa mara nyingine katika mtego wao wa kizimba cha damu na sasa alirudi na kusimama katikati ya mbingu na ardhi, kwa jinsi mwili wake ulivokuwa ukipumua ni kama kila sehemu ya mwili wake kulikuwa na moyo unaosukuma damu.
Roma sasa alikuwa ameijua siri ya radi ya zambarau , yaani alikuwa kama ule mnara wa kuingia katika ulimwengu wa majini pepo , radi na Roma ilikuwa ni kitu kimoja.
Anjiu na majini wenzake wote walionyesha hali ya hofu katika macho yao , walikuwa wamemzingira kwa umbali mrefu sana na hakuna ambaye aliweza kuthubutu kusogea karibu hata kwa nchi moja , wote walikuwa wakiogopa nguvu ya radi iliokuwa ikimtoka Roma.
Radi ilikuwa na uwezo wa kuharibu sio mwili tu bali mpaka roho na nafsi na kupotea katika anga.
“Inaonekana tayari umekwisha kufanikiwa kubobea katika kuidhibiti radi ya Zambarau ?”Aliongea Anjiu , ijapokuwa alikuwa kwa mbali lakini sauti yake ilikuwa ikisikika kwa ukaribu.
Roma alinyanyua mkono wake mmoja na ile anafungua kiganja ilikuwa ni kama vile kuna mnyororo wa radi unamtoka na kwenda angani na kutengneza kitu kama upinde.
“Kama ilivyokuwa siku ile nilivyoficha kete yangu ya ushindi leo pia ni hivyo hivyo , kama ningekuambia nimeweza kugundua siri ya kuidibiti radi ya zambarau ungenichokoza?”Aliongea Roma akiwa katika hali ya utani.
Ukweli ni kwamba ile siku mara baada ya kufanikiwa kuinyonya nguvu ambayo Chaos alikuwa ameificha aliweza kugundua mambo mawili matatu namna ya kudbiti radi , alichokuwa amekosa tu ni changamoto ya kufungua mawazo yake.
Ili kupanda levo Roma alikuwa akihitaji changamoto na ndio maana aikuwa akizitafuta sana , wakati majini wakiwaza kumuua Roma yeye alikuwa akichukulia changamoto hizo kama mbinu ya kufungua mawazo yake na hio ndio siri kubwa ambayo ipo katika nguvu ya andiko la Urejesho.
Andiko la Urejesho ni kama njia ya kupokea maono na ili iweze kukupatia maono lazima ukidhi vigezo vya kimazingira ambavyo ni kuwa katika changamoto , pale linapotokea giza kubwa la changamoto mbele yako ndio maono yanapotokea.
Yaani utofauti wa mbinu nyingi za majini wanazojifunza katika kupanda levo na kuvuna zaidi na zaidi nishati ya mbingu na ardhi ni kufanya mazoezi kila siku na kutamka maneno maalumu lakini kuhusu andiko la urejesho ni kama vile ni ahadi ambayo Mungu amemuwekea binadamu kwamba pale ambapo utakuwa katika changamoto atamletea maono ya kutatua changamoto hio.
Unapaswa kuelewa andiko la urejesho wa azimio jina hilo sio jina lake bali ni jina ambalo Roma aliamua kuliita , mwalimu wake ambaye alimfundisha kuhusu mbinu hio alimwambia aipatie jina analotaka yeye na ndio jina la Andiko la urejesho wa Azimio lilipozaliwa.
Sasa siku ambayo Anjiu alipitia dhiki ya Radi upaande wa Roma iikuwa ni kama vile maono yalimjia na kuona radi ambayo alikuwa akipitia Anjiu ilikuwa na rangi mbili yaani rangi ya bluu na Zambarau hivyo moja kwa moja Roma aliamini pengine ni muunganiko wa elementi za moto wa bluu na elementi za moto wa zambarau na matokeo yake yalikuwa ni kama vile alivyokuwa amewaza.
Roma hatimae alikuja kuelewa pengine kinachomtokea katika maisha yake ni mambo yaliopangwa na Mungu tokea mbali , hakuwahi kuamini sana katika Mungu lakini kila kinachomtokea kilikuwa katika fumbo la namna yake na njia ambazo anapitia ni kama vile zimekwisha kuandaliwa.
Ukweli ni kwamba katika sheria za kikanuni za matokeo ya radi katika rangi tofauti tofauti ukizungumzia radi ya urujuani ni matokeo ya muunganiko wa elementi zinazozalisha mwanga wa bluu na zambarau ki ufupi ni kanuni zilezle za kisayansi .
Bila shaka haikuwa kama vile unafanya majaribio ya kikemikali kwamba lazima kutokee makosa kwanza mpaka unapofikia mafanikio.
Mbinu za mbingu na ardhi zilikuwa ni za tofauti kidogo , ufunuo ukishakutokea na ukaufahamu basi ukiufanyia kazi matokeo yake ni sahihi na namna ya kupata maono ni kujua asili ya dunia ilivyo , kila kitu kipo kwa sababu kiwe na uhai kisiwe na uhai , kila tukio la asili linatokea kwa sababu na hio ndio njia rahisi ambayo ilimuwezesha kupata ufunuo.
Sasa Roma kutokana na uzoefu wake wa kijamii ulimwambia kwamba asili ya moyo wa kiumbe chenye utashi siku zote ni Dhambi kwanza kabla ya kupitia utakaso na ndio maana hakutaka kuambia mtu yoyote kwamba ameweza kufanikiwa kujua siri iliopo katika kuidhibiti radi.










SEHEMU YA 755.
Roma sasa alikuwa na hali ya kujiamini na alijiambia akishaingia katika levo ya mapigo ya radi elfu moja atakuwa na uwezo wa kutumia moto wa bluu na elementi za moto mweusi na kufanikiwa kutengeneza radi ya mapigo elfu moja.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba Roma ameweza kudhibiti radi ya mapigo tisini na tisa , hii haikumaanisha kwamba Roma anaweza kutengeneza mapigo tisini na tisa lakini katika kanuni za nguvu za mbingu na ardhi inamaanisha kwamba anao uwezo wa kutengeneza radi yenye nguvu mara 9 katika awamu 11 na ndio hutokea hesabu ya 99.
Nishati za nguvu ya radi zinaenda katika kanuni hii tatu mara tatu , tisa mara kumi na moja , tisa mara mia na kumi na moja na kuendelea.
Maana yake ni kwamba unaweza ukapigwa na awamu tatu za radi yenye nguvu sawa ya mapigo matatu ambapo moja kwa moja utakuwa umepitia mapigo tisa , au unaweza kupigwa na mapigo kumi na moja yenye ujazo wa nguvu ya mapigo tisa hivyo kimahesabu utakuwa umepigwa na mapigo tisini na tisa au mapigo mia moja kumi na moja hapo utakuwa na uwezo wa kupigwa na mapigo mia tisa tisini na tisa , kanuni hii inabadilika lakini majawabu yanakuwa yanafanana, inategemea sana namna anga lilivyokasirika na mbinu yako ya mafunzo kwa mfano Anjiu na Rozu wao walipitia mapigo matatu tu ambayo ni sawa na mapigo tisa lakini kwa Roma alipitia awau tisa na awamu tisini na tisa katika mnara
Kila pigo lina rangi yake , asilimia kubwa ya mapigo tisa rangi yao ni bluu , tisini na tisa ni zambarau na kuendelea.
Roma sasa mara baada ya kuangalia majini waliokuwa mbele yake , aliona kabisa hana cha kuogopa licha ya kwamba walihesabika kama wabobevu wa nguvu za mbingu na ardhi katika ulimwengu huo.
“Nilikuwa nikipasha mwili joto na nishamaliza sasa , ni muda wa kuanza kazi..”
Mara baada ya kuongea kauli hio alitengeneza wimbi kubwa la radi ambazo shoti zake ziligawanyika na kuwa kama mishale midogo na kuwarushia wale majini.
Ngurumo iliosikika ni kama vile dunia imegongana na sayari nyingine na kabla hata majini hao wa Hongmeng na miliki nyingine masikio yao hayajatafsiri sauti hio walikwisha kufikitwa tayari na boriti za radi na kuwayeyusha.
Kwa Roma lilikuwa pigo la kawaida tu lakini athari zake hazikuwa za kawaida kwani majini waliokuwa katika levo za maji ya kawaida wote walipotea.
Majini wote ambao wamekwisha kuijua nguvu ya radi ya zambarau walijua namna ilivyokuwa ni hatari kuguswa na radi hio ukiwa hujajiandaa , hata Anjiu mwenyewe ambaye alikuwa na uwezo wa juu alitumia chungu cha Roma kuweza kuipita radi.
“Kimbieni!”
Sauti ilisikika kusikojulikana kama vile ni ya binadamu , meza ilikuwa imepinduliwa kibabe na kitu pekee ambacho majini hao waliona ni aidha kukwepa au kukimbia na sio kufanya mashambulizi.
Majini wa levo za chini waliosalimika walikimbia kwa kutawanyika lakini Anjiu , Gefu, Wucheni walikuwa wamebakia.
“Mnataka kukimbia , kukimbia kwenda wapi?”Aliwaza Roma akiwaangalia majini hao wa levo ya majji ya kiroho.
“Nyie vipi mbona hamkimbii kama wenzenu?, nimetoa kionjo tu show yenyewe haijaanza”
“Mh Tukimbie! ,unataka tukimbie kwenda wapi , unataka turudi katika miliki zetu ili utufuate huko huko ukaondoe mizizi ya vizazi vyetu kama ulivyofanya hapa Panas”Aliongea Menyu katika uchungu mkubwa na Roma hakukataa kwani ndio alichokuwa akiwaza.
“Hujakosea , isitoshe kama mnataka nianze kuwatafuta mmoja baada ya mwingine ni usumbufu ni kheri kama kutakuwa na mmoja wenu ambaye atakuwa ananielekeza njia”
“Ni kweli unataka kuua majini wote? , Roma kwa nguvu zako unaweza kutawala dunia nzima wewe mwenyewe na hatutanii katika hili… hatuwezi kukuchokoza tena kama utatuacha tuondoke leo hii .. au kama huridhiki na hivyo sisi kama miliki ya Panas tupo tayari kuwa chini yako , itakuwa ni kutuambia tu unachokitaka na sisi tutakutimizia”Aliongea Gefu akiwa na tabasamu pana kwenye uso wake.
“Ndio bro Roma , tunaomba msamaha kwa kukuchokoza , Mungu anatutaka kuishi maisha mazuri na nia yako ya kimauaji ni kubwa mno na inaenda kinyume na sheria za ulimwengu , sasa hakuna haja ya kuuana sisi kwa sisi kwanini unataka kwenda mbali namna hio?”Aliongea Umini.
“Sio wewe ambaye ulikuwa ukitaka kuniua muda huu , sasa nipo katika nafasi ya kukuua ndio unaniambia huo ujinga , kwasababu mmeamua kubakia na kufa basi sina haja ya kuwachelewesha”Aliongea Roma na palepale radi ya zambarau ilianza kumzingira katika mwili wake kwa namna ya ajabu kabisa na haikuwashambulia moja kwa moja bali ilichomoza na kwenda kugongana na wingu.
Wakati huo wingu kubwa juu angani lilikuwa likizunguka kwa kasi mno katika usawa aliosimama Roma na cheche za moto kugongana zilikuwa zikionekana.
Anga kati ya mbingu na ardhi lilikuwa giza tupu likiwa limefunikwa na ngurumo za radi sauti ilikuwa kubwa kana kwamba Mungu amaemua kuharibu sayari nzima.
Katika mabadiliko ya spidi ambayo ilikuwa ikionekana kwa macho ya kibinadamu , mawingu ya ngurumo yalitengeneza kizingia kikubwa ambacho kilizngira mzingo wa maili mia moja , katika maeneo mengi mbali na miliki hio kulikuwa na Dhoruba kubwa ya upepo.
Sasa katikati ya kizingia hicho ndio mahali ambapo Roma alikuwa amesimama , ilionekana alikuwa akiivuta radi kutoka juu kuja chini , haikuwa uwezo wakudhibiti radi tu lakini alikuwa na uwezo wa kuyasuguanisha mawingu kwa moto wa bluu na zambarau kutengeneza radi.
“Hivi bado tunaweza kusema huyu ni binadamu kweli…!”’Majini waliokuwa wakitetemeka kwa hofu wakiwa hawaaini kile wanachokiona waliongea , kilichokuwa mbele yao ilikuwa ni zaidi ya uhalisia wa kiumbe binadamu.
“Kulingana na vitabu vyetu, majini wa enzi hizo walikuwa na uwezo zaidi ya huo, hivyo nguvu hio ni nusu ya nguvu zao”Aliongea Shombeli.
Ubaridi wa maji ya mvua uligonga uso wa Anjiu na aliishia kukunja ngumi tu huku macho yake yakiwa yamejaa husda.
“Andiko la urejesho wa Azimio …hii ni mbinu ya namna gani, kuna siri gani iliopo nyuma yake?”
Anjiu ambaye alikuwa na tamaa kubwa ya kupanda levo mara baada ya kuhisi nguvu ya ajabu iliokuwa ikiongezeka kila sekunde na namna ambavyo Roma analizungusha wingu na kufanya linavyotaka alijikuta akishindwa hata kujua ni hisia gani anazipata.
Roma alikuwa katika levo za juu kabisa na kwa wakati huo hakuwafikiria majini hao kama washindani wake , moyo wake ulikuwa ukiimba wimbo wa; ‘Athena njoo nikushikishe adabu’.
Roma alijiua pengine hisia anazozipata hata Athena alikuwa amezipata kwa muda mrefu sana , pengine Athena hakuwa akiigiza kuwa na ukiburi na ukauzu , vile vitu ambavyo watu wengi walikuwa wakiviona vya thamani kwake havikuwa vya thamani na hisia hizo ndio alizokuwa nazo Roma.
Ni kama vile mtu mzima kutokuvutiwa na midoli ya kuchezea watoto basi ilikuwa ni kama yeye vile kutokuvutiwa na vitu kama vile pesa na madaraka , Roma hakuwa hata na tamaa tena ya kuua viumbe dhaifu tena.
Roma alikuwa na uwelewa na hisia hizo mwanzoni lakini katika nguvu ya namna hio aliweza kufikiria kama vile alivyokuwa akifikiria Athena,
Mabadiliko ya kimtazamo na kiakili ilikuwa ni hatua ya ukuaji kwake ambao ulimpa hali ya kujiamini , Roma sasa alijiambia hawezi tena kuogopa yule mkuu wa umoja wa majini aliekutana nae Dodoma tena.
Mambo mengi alikuwa akiyafikiria katika kichwa chake na alikuwa ameshasahau kuna kundi la majini chini yake ambao linasubiria hukumu yake.
Katika wakati huo Roma sasa alikuwa katika hali ya utulivu kabisa na macho yake hayakuonekana kama yale ya fujo tena kama alvyoweza kuingia katika ulimwengu huo , ilikuwa ni kama vile amebatizwa na kuwa kiumbe kipya.
Roma alikiwa amesimama juu angani alinyanyua mkono wake na kunyoosha kidole upande wa aliposimama Menyu na wenzake.
“Boom!!”
Kitendo cha kunyossha kidole ni kama ishara ya kuruhusu pigo kwani wingu lililokuwa likizunguka juu yake lilishusha radi na kwenda kupiga katika eneo lile alilonyooshea kidole.
Ijapokuwa radi hio haikuwa kubwa kama ya mapigo tisa lakini ilikuwa na nguvu kubwa mno ya kugeuza majini wa nne wa levo ya maji ya kiroho kuwa majivu.
Anjiu na wenzake waliweza kukwepa shambulizi lile lakini ile wanakuja kumgeukia Menyu na baadhi ya majini walikuwa wamebadlika na kuwa moto wa rangi ya bluu na roho zao na nafsi zao ziliunguzwa .
Ijapokuwa walijua hawakuwa saizi ya Roma tena lakini walishangazwa na uwezo wake wa kuua majini wa levo ya kati ya maji kwa pigo moja tu.
BOOM!!
Radi nyingine ilishuka bila hata ya tahadhari , na awamu hio wazee wakuu wa miliki ya Xia walishambuliwa na kuuliwa palepale.
Roma alihisi ni kama vile ameanza kutumia radi miaka mingi iliopita namna ilivyokuwa rahisi kushambulia, moto huo wa mbingu aliweza kuita kama vile akili yake imetawaliwa na mdudu ambaye anawezesha hayo yote.
Gefu na wenzake waliona kabisa hali sio nzuri kwao kabisa na alipanga kuchukua baadhi ya watu wake kukimbia , hata kama angeamua kucheza kamari lakini ni kheri kuishi kwa muda mrefu kidogo kuliko asili yao kufutwa.
“Tawanyikeni , jiokoeni”Aliongea na baadhi ya wazee wa miliki ya Panas mara baada ya kusikia kauli hio walianza kukimbia kuelekea pande tofauti tofauti.
Roma hakuwaangalia kabisa na palepale aliita moto wa mbingu na kisha kunyoosha vidole upande wao na palepale walishukiwa na mashambulizi na kumezwa ndani ya sekunde ikiwemo Gefu mwenyewe.
Majini wote wa miliki ya Panas walipotea na kilichoweza kubakia ni Dhana ya kiuungu ya mkuki peke yake , ilikuwa ni dhana ya kilijendi hivyo haikuharibika kirahisi.
Ikawa Roma amekwisha kuua mkuu wa miliki ya Panas na mkuu wamiliki ya Kekexil.
Katika kifo cha Gefu hakuna jini ambaye alikuwa hata na habari ni wapi Dhana yake ya kiuungu ilipokuwa imedondikea.
Anjiu aliishia kung’ata meno yake na katika hali kama hio aliamua kuita pepo lake la ndani la kijeshi na mwili wake wote ulifunikwa na nguvu ya moto wa ndege wa dhahabu wa miguu mitatu.
“Msikimbie ni vizuri kupigana nae kuliko kushambuliwa wakati wa kukimbia , sidhani kama anao uwezo wa kuhimili uharibifu wake mwenyewe kwa kutuua wengi namna hii’
“Anjiu upo huru kufa mwenyewe , wewe ndio umetuleta katika hali hatarishi namna hii”Umini alitoa alimwangushia lawama kwa hasira , huyu kijana wa miaka mia mbili hatimae alijua kwamba tayari kifo kinamuita.
Kinyume chake Wucheni na Shombeli na wenzake wote walikuwa katika muoenekano wa utulivu kabisa , ni kama wamejiandaa kufa kimya kimya.
Roma aliweza kuoneysha kejeli katika macho yake na wakati kama huo alichopata kuona kati ya majini hao ni Anju peke yake ambaye alikuwa na muonekano wa kishujaa.
Mbele ya israeli mtoa roho Anjiu alikuwa bado akionyesha hali ya kujiamnni , ni kama hakutaka kufa kama muoga bali alitaka kufa kama mwanajeshi.
Pengine hio ndio sababu ya kumfanya Anjiu kuwa maarufu katika ulimwengu wa majini , Roma alijiambia kama sio Anjiu mwenyewe kutaka kumchokoza pengine angeweza kumfanya kuwa rafiki yake kwani kuna vitu vingi wanafanana.
Ni dakika kadhaa wakati Roma akijiandaa kumalizana na Wucheni hatimae aliweza kuhisi nguvu za majini zikisogea katika eneo hilo huku akisikia sauti ikimwita.
“Master Roma naomba usimuue mjomba tafadhari ,, usimuue”
Roma aliweza kuijua sauti hio kutokea mbali , ni kama vile alishawahi kuisikia na kufumba na kufumbua aliweza kuona wanawake wawili pamoja na mwanaume mmoja wakisogea katika eneo hilo.
“Bi Zenzhei!!”
Roma alishangaa mara baada ya kumuona ni Zenzhei , ijapokuwa Zenzhei alikuwa amebadilika na kuwa msichana lakini Roma alikuwa akimtambua kwani alionana nae wakati akiwa anaondoka.
Lakini alishangaa Zenzhei kusema mjomba wake asiuliwe



SEHEMU YA 756.
Roma mara baada ya kumjua Zenzhei alionyesha hali ya kuwa na furaha , ukweli licha ya kwamba alikuwa ni msichana lakini hakujizuia kumuita bibi.
Watu aliokuwa ameambata nao ni Nefi pamoja na Yiyu ambao ni watoto wa Wucheni.
Zenzhei mara baada ya kusikia Roma akimuita Bibi , Zenzhei alishindwa kujizuia na kutokwa na machozi ya furaha neno bibi lilikuwa na maana kubwa kwake , ilimaanisha Roma alikuwa akimheshimu.
“Master Roma siamini kama kukutana kwetu kutakuwa kwa namna hii , mambo yanaendaje nyumbani Tanzania?”Aliuliza Zenzhei.
“Mambo kwanini yasiwe shwari wakati nipo , nina vitu vizuri kwa ajili ya yule mzee na umri wake kwasasa sio tatizo, usiwe na wasiwasi kabisa”Aliongea Roma akiwa katika tabasamu la furaha kumuona Zenzhei kwa mara nyingine.
“Ndio , nimesahau kama tayari unao uwezo wa kutengeza vidonge”
Baada ya kumuona Zenzhei anamsogelea Roma , Nefi na Yiyu walienda kwa baba yao wakiwa katika hali ya wasiwasi.
“Zenzhei usimsogelee atakuuwa huyo”Wucheni alibweka lakini Zenzhei aligeuza sura yake na kumtingisha kichwa mjomba ake na kisha akamgeukia Roma.
“Mr Roma Zenzhei anajua kwamba Hongmeng wamefanya makosa , nilipofika nilipata kujua ukweli wa mambo menginyuma ya vifo vya wazazi wangu kutoka kwa mjomba Wucheni na nimejua ni maamuzi gani ambayo nilipaswa kufanya muda mrefu juu ya kisasi changu , Mjomba ana makosa ndo lakini bado ana majukumu makubwa , najua nakosa aibu kukuomba hili kulingana tulivyokubaliana lakini naomba unikubalie hili ombi moja , muache aondoke ..nimeweza kusikia kutoka kwa baadhi ya wenzetu waliokimbia hapa kwamba tayari unao uwezo wa kudhibiti radi , hata kama Hongmeng wanatamani kukuchokoza hawatothubutu kwani wanajua unao uwezo mkubwa tayari”
Majini wa Hongmeng wote walikuwa kimya na walikuwa na taarifa ya Zenzhei kuishi katika taifa la Tanzania tokea akiwa mdogo hivyo ni kama ni raia wa Tanzania.
Lakini hawakuwa wakijua kama wakati Roma anaingia katika levo ya nafsi mara baada ya kukamilisha mzunguko wa Andiko la urejesho msaada mkubwa aliupata kutoka kwa Zenzhei.
Kutokana na kujua hayo Shombeli , Umini na wengne walijua pengine kuna tumaini la kubakia hai kwa kumtegemea Zenzhei.
“Acha kumbembeleza , hata kama watoto wangu na mabinti zangu watakufa hawawezi kukupigia magoti , mimi Wucheni ijapokuwa siwezi kujiita shujaa lakini sio mjinga ambae ninaweza kuishi kwa kuchekwa na kuomba kuhurumiwa”Aliongea Wucheni akionyesha hali ya kujisikia vibaya kwa Zenzhei kumuombea msamaha kwa Roma.
“Bi Zenzhei huna haja ya kunibembeleza , kama unataka nimuachie mjomba wao nitamuacha , sitaki kukuona ukinibembeleza”Aliongea Roma akimwangalia Zenzhei ambaye alikuwa na muonekano wa kinyeyekevu.
Majini wote ambao walikuwa hawampendi Roma walishangaa mara baada ya kuona Roma kweli alikuwa akijali maneno ya Zenzhei.
“Usishangae sana , wewe kwangu ni mwanafamilia na umekuwa mkarimu kwangu kwa muda mrefu sana na bado sijalipa yale yote ambayo umeyafanya kwa familia yetu , ijapokuwa mjomba wako alitaka kuniua lakini bila shaka nitamuacha aende lakini hii itakuwa ni mara yake ya mwisho kumpa nafasi nyingine , awamu nyingine akinichokoza ajue kwamba ndio mwisho wa uvumiivu wangu”
“Binadamu ulielaaniwa wewe acha kunibebesha uovu , hata kama nitakufa mimi na uzee wangu huu huwezi kunisingizia vitu ambavyo sijafanya , ni lini nikataka kukuua?”Aliongea Wuchen.
“Kwahio unataka kusema sio wewe uliekuja Australia katika nyika ya Arnhem na kutaka kuniua?”
“Australia!!. , unaongea nini?, Lini nikaja Australia na kutaka kukuua miii?”Aliongea Wucheni akiwa katika hali ya kushangaa.
“Roma! Baba yangu siku zote ni mtu mwema asie tayari kuvunja sheria , kama kweli alitaka kukuua unadhani ungeweza kumshinda wakati huo?”Aliongea Nefi.
“Nilishambuliwa na mtu aliekuwa amevalia Mask ya chuma na kutaka mbinu yangu ya mafunzo , mtu huyo alikuwa na uwezo wa kutumia kinga ya boma la barafu na kuita pepo wa kikaskazini , vipepeo wa kufikirika na mbingu nyingine , mtu huyo uwezo wake wa kijini ulikuwa mkubwa mno , kama sio Wucheni je ni nani kama sio mmoja wenu ndani ya miliki yenu?”
Mara baada ya kuongea kauli hio wazee hao wa Hongmeng walijikuta wakishangaa , ilikuwa haiwezekani Roma kumsingizia mtu kwasababu alikuwa na uwezo wa kumuua mtu yoyote ambae hakuwa akimfurahisha.
Dakika ileile macho yao yote yaliokuwa katika hali ya hasira yalimgeukia Anjiu.
“Anjiu unathubutu vipi kutumia mbinu ya familia yangu kujifanyisha ni mimi katika kufanya uovu wa namna hio , una moyo uliojaa hila, je ulikuwa ukinitafutia matatizo kati ya Roma na miliki yetu?”
“Nini , Anjiu!?, kwanini Anjiu aweze kutumia mbinu yenu?”
“Mr Roma mjomba hajahusika kabisa na kinachoendeea ni kama kilichoitokea familia yangu , kuna baadhi ya majini wa jamii yetu walijua siri ya mbinu yetu ya mafunzo lakini walikufa wote na mpaka sasa aliebakia katika ulimwengu wetu ni Anjiu pekee , alijua mbinu yetu kwa njia ya kumhadaa kimapenzi binamu yangu Yiyu ndio maana mpake leo hii kuna ugomvi mkubwa baina yao”
“Ushachelewa kufahamu hili, vyovyote vile lazima unapaswa kujiona mwenye bahati , nilitumia hii mbinu kwa ajili ya kukugombanisha na Hongmeng lakinni inasikitisha kwamba hukuchukua hatua na badala yake ukaja katika miliki yangu na kuanzisha vurugu, nadhani nilikosea mahesabu yangu”
“Kama ni hivyo wakati nilipokuwa kwenye Dhehebu la Tang , mtu ambaye alikuwa akiwatala kiakili wale wazee jr wewe pia?, je ambaye alijaribu kumtumia Tang luyi kwa kumleta binti wewe pia unahusika?”
“Ndio ni mimi, usisahau ilikuwa rahisi sana mimi kukuua wakati ule na usione inaweza kuwa rahisi kuniua leo hii”
“Kama ni hivyo basi utakuwa unamjua binti wa damu wa Tang Luyi, hivyo sema binti yake yupo wapi?”
Tang Luyi ni Master yake na Magdalena kutokea milima ya Shushan katika ngome ya Tang sasa siku ile Roma alivyoenda katika ile ngome alikuta wazee wote wakiwa katika kutawaliwa kimawazo na kutaka kumshambulia.
“Kwanini nikuambie?”Hali ya muonekano ya Anjiu ilibadilika.
“Haijalishi kama hutaki kujibu, hivyo nitakuuliza tena swali lingine, Je umejuaje nilikuwa nikitumia mbinu ya Andiko la Urejesho , je swala hili linahusiana na mtu ambaye alikuwa akimfukuza Master wangu Tang Chi na kutaka kumuua?”Aliuliza Roma.
Ukweli ni kwamba Roma alikuwa akijiuliza swali la namna hio kwa muda mrefu na kukosa majibu na hio yote ni kukosa mtu wa kumuuliza , hata alivyokutana na Tang Chi kwenye ulimwengu wa majini pepo hakumpa habari juu ya ubini wa adui ambaye alikuwa akimfukuza.
Kitu kingine ni kwamba asilimia ya majini wote ambao wapo katika ulimwengu wa majini watu hawakuwa na uelewa na mbinu hio aliokuwa akitumia , jambo ambalo lilimfahamisha kwamba hawakuwa wakijua mbinu ya andiko la Urejesho ni mara baada ya kukuta karatasi lenye andiko linalofanana na kwake japo majina tofauti.
Hivyo moja kwa moja lazima kuna mtu ambaye aliwaambia majini kwamba Roma anatumia mbinu ya Andiko , mbinu ya kijini ambayo hawaiujui ndio maana miliki zote zilikuwa zikihitaji kupata mbinu hio.
“Kama nikijibu maswali yako je utaniacha hai?”
“Huna jinsi zaidi ya kujibu maswali yangu au ufe , usifikiri pepo lako la ndani linaweza kudili na mimi awamu hii , ninao uwezo wa kukuua na radi kabla hata hajafanya shambulizi”
Anjiu mara baada ya kusikia maneno hayo aling’ata meno kwa hasira na kisha alimwangalia Roma na sura iliokuwa ikicheza cheza kwa hasira.
“Kama ni hivyo basi jibu langu ni kwamba sijui chochote, nasema hivi kwasababu mtu ambaye aliniambia kuhusu mbinu yako alikuwa ni wa ajabu sana haieleweki alikuwa ni mwanamke au mwanaume lakini nilichoweza kukuta ni barua katika meza yangu nyakati za usiku ambayo imeachwa na mtu huyo , sikujua hata kama kuna mtu aliingia katika ofisi yangu , kutokea siku hio huyo mtu alionekana sio wa kawaida hivyo sikumuwazia sana … kuhusu swala la kumfukuza Master wako na kutaka kumuua sijui hata kama una master wa jina hilo , hivyo sina majibu unayotaka na unaweza kuamini unachotaka”
Haikujalisha Roma alisikiaje jibu hilo lakini alihisi ni kama vile ni ujinga lakini kwa kumwangalia Anjiu haikuonekana alikuwa akidanganya
Mara baada ya kuona Roma yupo kwenye mawazo kila mmoja aliona hakuwa na nia tena ya kuendelea kuua na hatimae waliweza kupata ahueni ya kupumua.
Shombeli na Umini waliangaliana na kisha walipeana ishara ya maelewano na kwa haraka sana waliondoka na kundi la majini wa miliki ya Hongmeng.
Roma hakujali hata kuwafukuzia , mpaka wakati huo alikuwa na uwezo wa kuua jini yoyote kwa muda wowote anao taka laikini aliona kabisa kuua majini hao hakuna faida kubwa kwake
Iwe ni kwa kuua sana au kuua kidogo kwake hakukuwa na utofauti wa aina yoyote zaidi ya kujisumbua tu.
“Hakuna siku niliodhalilika kama leo , sijawahi kupitia huu uzoefu , umeniumiza na kisha ukachukua Dhana yangu , nipo tayari kufa nikipigana kuliko kukimbia ninakataa kushindwa lakini mimi Wucheni nachagua kuishi leo hii kwa ajili ya familia yangu .. mimi Wucheni nina deni la uhai kutoka kwako na kwanzia leo hii natangaza Hongmeng haitokuja kuwa na uadui na wewe kama ili mradi nitaendeea kuwa hai”Roma mara baada ya kusikia maneno hayo almwangalia Wucheni na palepale alijikuta akiangua kicheko.
“Sawa mzee , ndio uondoke wakati huu ambao nimekuruhusu na sitaki uchukulie mimi kukuacha hai ni kama deni , kama nilivyosema mwanzo nimekusamehe wewe na watu wako kwa ajili ya Bi Zenzhei , viumbe kama nyie ni swala la mimi kujiuliza kama niwaue au niwaache hai hivyo usijifanyishe kama utakuja kuwa na manufaa kwangu , kwangu muwe maadui msiwe maadui kwangu haibadilishi kitu kwanni mtabakia kuwa viumbe dhaifu mbele yangu”
Maneno yale ya Roma yalitaka kumfanya Wucheni kubadilika na kuonyesha hasira zake lakini mtoto wake Nefi na Yiyu walikuwa na hofu mno ya Roma kuwachukulia hatua.
“Zenzhei alimwangalia Roma na kisha akamwangalia Anjiu lakini kwa jinsi alivyokuwa akimwangalia Roma hakuonyesha aina yoyote ya hofu.
“Mr Roma nadhani sina haja ya kuwa na wasiwasi tena kwa mafanikio yako naamini yule mtu alifanya chaguzi sahihi , kwa mara nyingine niseme asante sana kwa ukarimu wako wa leo”
“Bibi kama upo tayari unaweza kurudi Tanzania na nitahakikisha hakuna anaeweza kukurudisha katika huu uimwengu wakifanya hivyo naua wote”
Zenzhei alifurahishwa na maneno yake , alikuwa na muonekano wa kijana na kwa Roma ni kama vile alikuwa akilinganga nae umri licha ya kwamba alikuwa akimwita bibi na aliishia kutingisha kichwa tu na palepale aliondoka kwa kupotea.
Sasa aliebaki alikuwa ni Anjiu peke yake , sio kwamba hakutaka kuondoka lakini alijua Roma anaweza kuwaacha wote waondoke lakini yeye asimruhusu
“Kusema ukweli sina uhakika kama ulichoongea ni ukweli kwasababu ya hilo najikuta nakuona wa hatari sana , kama unachochote unachotaka kuongea ongea kabla ya kifo chako”
“Nishajua unakwenda kuniua muda mrefu hivyo sogea tupambane , ijapokuwa nafasi yangu ya kushinda ni ndogo lakini siwezi kufa”
Mara baada ya kuongea hivyo aliita pepo lake la ndani na palepale ni kama vile kivuli cha mtu kinamtoka na kusimama mbele yake , kilikuwa ni kivuli kinacholingana kila kitu na yeye na kufumba na kufumbua kivuli kile kilimsogelea Roma kwa kasi.
Roma alikuwa tayari amekwisha kujindaa na aliita chungu cha maaafa na kwenda kugongana na kwa ana na lile pepo.
Lakini kwa nguvu ya Chaos ilivyokuwa kubwa ilikuwa ni mchezo wa kitoto sana kwa pepo wa namna hio kuweza kushindana na chaos kwani palepale mara baada ya kukaribiana na mdomo wa chungu lilipuka. Kama bomu.
Roma aliishia kupiga yowe kwenye moyo wake , ilionekana Anjiu hakuwa na nia ya kutumia pepo hilo kushambulia bali alilitoa kafara na kulitumia kama bomu la moshi.
Pepo la namna hio hata kama lilipuke ilikuwa ni swala la muda tu kwa Anjiu kulirudisha licha ya kwamba inaweza kumgharimu nguvu nyingi za mbingu na ardhi.
Sasa mara baada ya mlipuko ule wa pepo ambao ulitengeneza wingu Anjiu alitumia nafasi hio kukimbia lakini Roma ni kama alitegemea anachotaka kufanya na hakuwa na mpango wa kumuacha akimbie kizemba namna hio.
Uelekeo aliochukua Anjiu ilikuwa ni kuelekea katika miliki ya Xia na ilionekana alikuwa akitaka kuita wasaidizi wake
Ijapokuwa Roma alikuwa na spidi kubwa lakini spidi ya majini haikuwa ya kawaida hawakuwa wakipotea bali walikuwa wakisafiri kwa kasi mno kiasi kwaba wanaonekana kama wanapotea na ndani ya sekunde tu Anjiu alikuwa maili nyingi sana akiwa amemuacha Roma na hio ilimfanya Roma kutokuweza kuita radi kumshambulia tena.
Kilichomshangaza Roma ni uwezo wa Anjiu kukimbia huku akiacha kinga nyuma za barafu kama maboma
Ilimchukua Roma dakika kama tano kuweza kumfikia Anjiu lakini ile anataka kumzuia kwa mbele na kumshambulia na pigo la radi ghafla tu alihisi msisimko wa nguvu za kijini ukiongezeka kwa kuwasogelea na kufumba na kufumbua walitokeza majini waliokuwa katika kundi kutoka katika miliki ya Xia wakiongozwa na msichana mdogo Xiao .
“Mnafanya nini hapa?”Anjiu alikuwa amekasirika mno mara baada ya kumuona binti yake Xiao.
Roma alitaka kutumia ile nafasi kuwashambulia na pigo moja la radi na kuwaua lakini mara baada ya kumuona Xiao alisita.
Msichana huyo nusu jini nusu binadamu alimpa Roma ugumu wa kumshabulia , pengine ni kutokana na kwamba Rufi alikuwa na deni nae na yeye pia alikuwa amemshuku zaidi ya mara mbili.
“Baba wewe unaweza kuondoka , mimi binti yako nitamzuia huyu mtu mbaya”Aliongea Xiao na kisauti chake cha kuumiza masikio na palepale alisogea mbele ya Roma na kumkinga baba yake.
“Wewe mhalifu mkubwa niue sasa kama uwezo huo unao , hujatosheka kunichokoza mara kibao lakini na sasa hivi unataka kumuua baba yangu, dhamiri haikusuti?”
Roma aliguswa na maneno ya Xiao , yalikuwa ni kama vile ni shambulizi la radi , ijapokuwa alikuwa na uwezo wa kuua majini kwa kufikiria tu lakini alijikuta akiwa mzito sana kumuuiza huyo mrembo.
“Sogea pembeni , Mimi na Rufi tuna deni kwako ndio , lakini kinachotokea hapa ni kati yangu na baba yako , kama nisipomuua leo hii ataniua mimi”
“Unaongea ujinga, kama kweli una deni kwangu kwanini unataka kumua baba yangu , hii ndio namna ya kulipa hilo deni?”
“Hili ni tofauti..”
“Ni tofauti kivipi?”
Anjiu macho yake yaliongezeka ukubwa , palepale aligundua Roma alikuwa akimjali sana binti yake.
Kama ingekuwa ni zamani angemtumia Xiao kama mateka ili kumzuia Roma asimuue lakini tokea siku ambayo alirudi kutoka katika ulimwengu wa kawaida alianza kumchukulia kama binti yake kipenzi.
Siku hio ndio Anjiu aliweza kumjua Roma vizuri , alikuwa ni katili ambaye anao uwezo wa kuua miliki karibia zote hivyo alijua mtu wa aina hio anaweza kumuua hata kama atakubali kutokumuua kwa ajili ya binti yake
Anjiu hakutaka kumuona binti yake akijihatarisha kwa ajii ya kumuokoa.
Kuna vitu nadhani alisahau kuvijua kuhusu Roma , ukweli ni kwamba alijua kama Roma hakuwa akimjali Xiao basi mpaka wakati huo angekuwa ashawaua yeye na binti yake na kuwageuza majivu.
Roma hakuwa bado amefanya maamuzi , alikuwa akiwaza namna ya kutokumdhuru Xiao lakini amuue Anjiu kwani ni tishio kwa usalama wake na watu wake.
Mara baada ya kuona Roma anawaza wale majini wengine walianza kumbembeleza Anjiu kuondoka lakini yeye aliwafaokea kwa kumruhusu Xiao kuja nao.
“Mkuu tulikuwa na wasiwasi juu yako , taarifa za vita imesambaa katika miliki zote za majini , mkuu aliepita bado hajapona tutafanya nini kama na wewe tutakupoteza”
“Baba ondoka , nitamzuia asikudhuru , huyu nanamdai fadhila hivyo siwezi kumruhusu kukudhuru”
Xiao aliacha kumwangalia baba yange na alikuwa akijaribu kumsukuma Roma kurudi nyuma bila ya hofu yoyote , pengine ni hisia zake za kimapenzi ndio zinamfanya kutokumuogopa Roma.
Anjiu alitaka kumzuia Xiao lakini wazo lilimwingia , alijiambia kama ataendelea kumshikilia si nitangia katika mtego wa Roma labda anapanga kumtumia kama mateka ili kunikamata.
Kutokana na mawazo hayo alishindwa kuchukua maamuzi ya kukikimbia.
Ukweli ni kwamba Roma hakuwa hata na mpango wa kumtega Anjiu,alikuwa na uwezo wa kutokumdhuru Xiao na kisha kumuua Anjiu lakini matendo ya Xiao yalimfanya kutokuchukua hatua yoyote.
Xiao alienda mbali na kumshikilia Roma kiuno kwa kupitisha mikono kwa mbele ili kumzuia asisogee , vitendo hivyo vilimfanya Roma kushangaa na kuishia kucheka kwani vilikuwa vya kitoto sana
Licha ya kwamba uwezo wake ulishafikia levo ya nafsi lakini bado matendo yake yalikuwa kama ya msichana mdogo.
Upande wa Anjiu alikuwa na wasiwasi mno kwa kuogopa Roma kumuua binti yake.
“Baba kimbia basi”
Aliongea Xiao akiamini kwa namna alimvyomshikilia Roma hawezi kuchoropoka.
“Haka kajinga kanadhani Roma hawezi kuniua kwa kufanya vile”Aliwaza Anjiu.
Roma palepae alitoa tabasamu la kifedhuli na alimgeuza Xiao kama karatasi na kumshikilia na kwapa la mkono na kabla hata hajaleta ukinzani alikuwa tayari ashamzimisha.
Roma mpango wake ulikuwa ni mwepesi , alijua kama ataondoka na kurudi nae anaweza kumjua vizuri Xiao ni nani na kama ni mtoto wa Tang Luyi angempeleka kwa mama yake lakini pia asingekuwa na wasiwasi kuivamia Xia na kuisambaratisha.
Anjiu hakuweza kumuokoa binti yake na aliamua kukimbia huku akiamini Roma hawezi kumdhuru.
Upande wa Roma alikuwa mzito mno kumuacha Anjiu akimbie na alijaribu kumshambulia kwa kumrushia shoti za radi na mkono mmoja lakini kwasababu alikuwa amembeba Xiao alishindwa kubomoa ngao yake ya kijini ya barafu.
Roma aliweza kukiri ngao ya barafu ya pepo wa kaskazini ilikuwa sio ya kawaida kabisa , ilikuwa na nguvu mno kwani iliweza kumsaidia Anjiu kutoroka.
Lakini licha ya kwamba Roma hakuweza kumpata Anjiu na shambulizi lake lakini wale majini waliofika hapo waliweza kupatwa na mashambulizi hayo na kupoteza maisha.
Roma hakutaka kumwangalia tu akipotea katika macho ake na aliamua kumfukuzia kwa nyuma kwa kasi kubwa huku akiwa bado amembeba Xiao.
Anjiu alichukua uelekeo wa Kaskazini mashariki na alikuwa na spidi ya kasi mno lakini Roma licha ya kumfukuzia kwa kasi hakuwa na wasiwasi wa kumpata.
Roma alijiambbia hata kama asipomkata Anjiu miliki yake anaifahamu hivyo angeenda Xia na kuilipua na aone kama hatojitokeza.
Wakati Roma akiwa nyuma anaendelea kumfukuzia Anjiu alihisi kitu kisichokuwa cha kawaida kimeamka , ilikuwa ni kama vile kuna kitu kinataka kumtoka katika mwili wake , Roma mara baada ya kujichunguza alikuja kugundua ni kitu ambacho kilikuwa ndani ya hifadhi yake ya pete na jambo lile lilimshangaza sana.
Kabla hata hajagundua ni kitu gani hicho baada ya kufungua hifadhi hio kivuli cheusi kilitoka kwa kasi na kumvaa , kivuli hicho kilikuwa na nguvu ya giza , na kimejaa roho ya ukichaa , kifo na baadhi ya hisia hasi ambazo hazikuwa zikielezeka.
“Ni ile Hazina ya majini pepo!!!”
Roma alishangaa mno kwani ilikuwa ndio mara ya kwanza hazina hio ikawa hai na kutoka katika hifadhi bila ya ridhaa yake.
Kubwa zaidi ni kwamba hajawahi kujua kazi ya hazina hio ni nini na tokea mwanzo hakuweza kuhisi kama ilikuwa na nguvu zozote zile.
“Kwanini ghafla tu imeamua kuzalisha nguvu ya ajabu ya namna hii ya giza?”
Roma alijiuliza na kabla hata hajapata majibu kivuli kile kilichokuwa kimemzingita kiligeuka na kuwa kama vile ni kizingia au kimbunga na kuanza kumzunguka kwa kasi mno huku kikielekea juu angani zaidi na zaidi huku ncha yake juu kabisa kukiwa na ile hazina nyeusi.
Msuguano wa nisahti za mbingu na ardhi na nishati za hazina ile ziliongezeka kwa kiasi kikubwa na kuanza kumsukuma Roma kwenda juu angani , ilikuwa ni kama vile alikuwa amefungwa kamba kiunoni na kulazimishwa kwenda juu kwa kuvutwa.
Nguvu ilikuwa ni kubwa mno na Roma hakuweza kujinasua kwa kadri alivyokuwa akijitahidi , alijaribu kutumia chungu cha maafa kuweza kumeza nguvu inayotokaana ile hazina lakini alishindwa kabisa , alijaribu uwezo wake wote wa nguvu za kijini katika levo ya radi lakini pia ilishindikana na alijikuta akitoa macho.
“Hii nguvu ya hazina mbona kama inanyonya nguvu zangu?”
Roma aligeuza macho yake juu angani na palepale aliona katika anga ni kama vile kuna shimo kubwa jeusi ambalo anga yake ilikuwa ikichemka kana kwamba ni mafuta meusi yanayochemswa na moto mkali.
Roma kutokana na uwezo wake wa kuelewa kanuni za anga aligundua kilichokuwa juu yake ni Lango(Portal) la shimo ambalo ndio lilikuwa likimvuta.
Ilikuwa ni ndani ya sekunde tu ilikuwa ni kama alivyowaza kwani akiwa amemshikilia Xiao aliweza kutumbukia katika lile shimo refu na hakujua hata kinachomtokea ni kitu gani , kila kitu kwake kilikuwa cha maajabu.
Roma alijiuliza au pengne Hazina hio haikuwa na uwezo wa kuzalisha nguvu yoyote bali kazi yake ilikuwa ni kuamsha malango ya anga.
Kilichokuwa kimemtokea ni kama vile alivyovutwa na mnara na kupelekwa katika ulimwengu wa majini pepo na ndio kitu cha namna hio hio ndio kilichokuwa kikimtokea tofauti tu ni kwamba alijihisi ni kama vile anatumbukia kwenye shimo lefu la giza huku akishindwa kujizuia.
Roma mara baada ya kutumbukia mzima mzima katika shimo hilo ndio sasa anakumbuka kwenye mikono yake alikuwa memshikilia Xiao.
“Ni kitu gani hichi kinanitokea , kwanini nina bahati mbaya namna hii , au majini pepo waliniwekea mtego , au hii hazina yao ilikuwa ni ufunguo wa kuteleport kwenda ulimwengu mwingine , kama ningejua ningerudisha hazina yao mara moja”
Roma alianza kujilaumu wakati akiwa ndani ya giza totoro asijue ni wapi anaelekea , alichokuwa akijua tu ni kwamba nguvu inayomvuta ilikuwa ni kubwa sana kiasi kwamba hawezi kufanya lolote.
Anjiu ambaye alikuwa akikimbia kwa kasi kuokoa maisha yake hakujua ni kipi ambacho kinamtokea Roma na mara baada ya kuhisi nguvu ya ajabu alijiuliza au kuna mbinu nyingine Roma anajaribu kufanya ili kumuua.
Kitendo cha kugeuka nyuma aliona kitu kama duara nyeusi ambalo linapungua ukubwa kwa namna ya kusinyaa na ilikuwa ni kwa haraka sana kidoti kile cheusi kilipotea na hakuhisi tena msisimko wa nguvu za Roma wala za binti yake Xiao.
Ilikuwa ni kama vile Roma na Xiao walikuwa wamepotea katika anga jembamba , aliishia kukunja ndita na alirudi kwa kasi nyuma na kujaribu kumtafuta Roma , alijaribu kutumia nguvu zake za kijini za utambuzi ili kumuona binti yake lakini hakukuwa na dalili yoyote.
Roma kapotelea wapi au ndio mpango wa Athena kumpoteza Roma kukamilisha mambo yake.
Hatima ya Lekcha na Aoiline ni nini.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI :SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 758.

Anjiu mara baada ya kujiuliza kwa dakika kadhaa ni kama sasa alikuwa anapata uelewa ni kitu gani kimetokea.
“Jicho la Anga!!!’
Mara baada ya kuangalia eneo ambalo yupo ni kati ya mpaka wa miliki ya Xia na Panas na ndio eneo ambalo jicho la anga hufunguka alipata wazo hilo, ijapokuwa muonekano wa jicho hilo hutofautiana kila linapofunguka lakini ilikuwa ni sehemu hio , sasa alijiuliza je kile kidoti cheusi alichoona angani ndio lango la jicho la anga lakini kwanini lifunguke wakati huo ilihali tarehe ya kufunguka kwake ilikuwa mwakani.
Hakukuwa na ishara ya furaha katika macho ya Anjiu wakati akijaribu kuchunguza eneo hilo na aliishia kuonyesha hali ya wasiwasi na majonzi.
*****
Anga lilikuwa ni la kijivu huku ukungu wa ajabu ukiwa umetanda katika kila kona.
Ni ulimwengu ambao ni kama umetelekezwa uliojaa ukiwa na ukale , ardhi ambayo haikuwa na dalili ya mti ilikuwa imetawaliwa na harufu mbaya sana ya uozo huku ardhi yake ikiwa ni ya rangi ya kahawia iliokolea iliokuwa na chembechembe za mchanga mwekundu.
Hewa ilikuwa na unyevunyevu kiasi kidogo sana na mara moja moja upepo wa nishati ya nguvu hasi ilikuwa ikizingira katika eneo hilo.
Kulikuwa na vilio vya ajabu na min’gako ambayo ilikuwa ikisikika kutokea pande zote lakini ukisikia sauti upande huu na ukigeuza macho na kuangalia inatokea wapi sauti ile hukoma mara moja.
Eneo hilo lilikuwa ni nusu kuzimu , iijapokuwa kulikuwa na mwanga usiokuwa na chanzo cha jua lakini bado ilionekana kama vile ni alfajiri.
Wakati huo Roma alionekana akiwa amesimama katika ulimwengu huo ambao hakuwa akijua ni ulimwengu gani akiwa amempakata Xiao ambaye bado hakuwa katika fahamu zake.
Kitu pekee ambacho Roma aliona ni unafuu katika eneo hilo ni kwamba uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi haukuwa umepungua kama wakati alivyongia katika ulimwengu wa majini pepo.
Ijapokuwa nguvu ya giza ilikuwa kubwa mno kuliko katika ulimwengu wa kawaida lakini bado haikuwa imemuathiri.
Lakini licha ya Roma kuona uwezo wake anao lakini ilikuwa salama kukiita chungu chake cha maafa na kukifanya kielee juu ya kichwa chake kama kinga ya ulinzi.
Katika mazingira kama hayo ambayo kuna nguvu ya giza kubwa kitu pekee ambacho kinaweza kupambana na nguvu hizo ni chungu hicho ambacho asili yake pia ni nguvu za giza.
Kutokana na uwepo wa ukungu mzito Roma alijaribu kutumia uwezo wake wa utambuzi kupima eneo hilo na aligundua ni eneo ambalo lilikuwa na ukubwa mpana sana ambao alishindwa kujua mwisho wake.
Hakuweza kuona mbali zaidi kwani ilikuwa ni kama juu angani kuna tabaka ambalo linamfanya nguvu zake za kijini kutokufanya kazi na hata kanuni za anga hazikumfanya kwenda juu angani zaidi , ilionekana kabisa hazikuwa zikifanya kazi na alijua lazima anga hilo limefungwa.
Lakini hisia za Roma zilimwambia pengine bado yupo ndani ya anga la dunia isingekuwa ni hivyo asingeweza kutumia uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi.
Roma aliamua kutoka katika eneo hilo na kujaribu kusafiri kwa umbali wa kilomita kadhaa kwenda mbele na alikuja kutua katika ardhi ambayo ilionekana kama vile ni ya kijangwa yenye mchanga mwembamba sana na mlima uliochakaa ambao haukuwa na miti.
Kitu kingine alichoweza kugundua ni uwepo wa mifupa mikubwa sana ya wanyama , ilikuwa ni mifupa isiokuwa ya kawaida kama vile ya wanyama ambao wamepotea katika dunia au waliaminika kuwepo na wakapotea lakini pia aliweza kuona baadhi ya Dhana ambazo zilionekana kukatika hivyo kukosa matumizi.
Roma mara baada ya kutembea kwa muda hatimae alipata wazo ambalo hakuwa na uhakika nalo.
Alikumbuka wakati alipokuwa katika miliki ya Kekexil majini watu walikuwa wakijiandaa mwakani kuingia katika jicho la anga na pengine eneo hilo alipo ndio jicho lenyewe la anga.
Tabia za ulimwengu huo ni kunyonya kiasi kikubwa cha nguvu zake za kijini na kitendo cha kuona Dhana na siraha mbalimbali pamoja na mifupa ya majini pepo waliokufa aliona tabia hizo zinalingana na kile walichosema.
Kuhusu namna alivyoweza kufika katika ulimwengu huo yote hayo yalichangizwa na hazina ya majini pepo kutoka Braki ambayo ilikuwa chini ya familia ya mzee Sharif.
Kokoto ile bado alikuwa nayo lakini katika wakati huo ilionekana kutokuwa na nguvu ya aina yoyote , ilikuwa imebakia katika hali yake ileile ya mwanzo ya kikokoto.
Roma alijaribu kuifanyia mizengwe ya namna nyingi lakini haikuonyesha kutoa nguvu ya aina yoyote na alijikuta akikosa cha kufanya na kuamua kuirudisha katika hifadhi yake.
Kitu kingine ambacho kilimshangaza Roma ni kwamba alishindwa kuhisi roho za nguvu za majini pepo , kinadharia ilitakiwa roho hizo ziwepo kulingana na namna majini walivyokuwa wakiuita ulimwengu huo , lakini amesafiri kwa zaidi ya kilomita mia moja lakini hajahisi nguvu yoyote ya kiumbe hai iwe ni ya kishetani au ya kawaida.
Ulimwengu huo ulikuwa ni mkubwa mno na ilikuwa ngumu hata kujua uelekeo , Roma alikuwa hata hajui alikuwa katika eneo gani ndani ya huo ulimwengu na kilichomshangaza ni kwamba ardhi yake ilikuwa haina viumbe hai wa namna yoyote , lakini hata hivyo aliamini lazima kuna viumbe wanaoishi hapo kama ni hivyo kwanini bado anavuta pumzi kama kawaida , kwanini kuna uwepo wa oksijeni.
“Nini kitatokea kama nitaishia kukwama katika ulimwengu huu , nini kitatokea kwa familia yangu na Lanlan?”
Roma wasiwasi ulianza kumvaa kutokana na kutokujua namna ya kurudi katika ulimwengu wa kawaida na aliishia kulaani majini pepo wa Braki kwa kutokuchukua hazina yao lakini hata hivo aliona anapaswa kuwa na utulivu lazima angepata njia.
Katika wakati huo wa mawazo hatimae Xiao na yeye alishituka kutoka kwenye usingizi na kuanza kuangaza kwa mshituko katika ulimwengu ambao alikuwepo na mara baada ya kuona sura ya Roma imempakata alijikuta akipiga ukulele.
Roma alijua ni hali ya kawaida kwani alikuwa amerejewa na kumbukumbu hivyo alimwacha atulie yeye mwenyewe , na aliishia kumaka na kisha kuanza kuongea maneno yasioeleweka mpaka akaja kutulia.
“Ushamaliza?”Roma aliuliza akiwa katika sura ambayo haikuwa na furaha wala huzuni.
Xiao aliishia kukohoa kwani koo lake lilikuwa linauma kutokana na kupiga yowe, na mara baada ya fahamu zake kuweza kutafsri harufu aliokuwa akinusa aliishia kujaribu kuziba pua kwani ni kama vile anga linatoa mashuzi lakini angalau alikuwa amekwisha kutulia.
Roma aliishia kuvuta pumzi ya ahueni na alijiambia angalau wapo wawili na wanaweza kuibua wazo la kujitoa katika huo ulimwengu..hivyo aliamua kumwelezea Xiao namna ambavyo wamefika katika eneo hilo.
Xiao mara baada ya kusikia baba yake alikuwa hai alifurahi lakini muda huo wasiwasi ulianza kumvaa mara baada ya kusikia kuna uwezekano wapo ndani ya ulimwengu wa jicho la anga.
Akiwa ameshikilia Roma alianza kumsindilia ngumi za lawama na kumlaumu kumleta huku bila kujua namna ya kurudi.
“Acha kunipigia makelele hujichukii tu?, tayari ushakuwa mtu mzima lakini bado unajifanyisha kama mtoto ..nipigie makelele uone kama sitokuacha mwenyewe”
Xiao alishangazwa na kufokewa na Roma lakini alinywea haraka na kuangalia chini.
“Sawa nimetulia , naomba usiniache mwenyewe…”Aliongea na palepale akaanza kuangua kilio cha kwikwi jambo ambalo lilimshangaza Roma.
“Unalia nini sasa , sijasema nataka kukutelekeza nimekuambia utulie , kama ningetaka kufanya hivyo ningekuwa nishafanya muda mrefu , usilie na ongea kawaida tu”Roma alikuwa sio mvumilivu mbele ya machozi ya mwanamke.
Ukweli ni kwamba muda mwingine alijiona sijui ni mwenye bahati ya namna gani , kila anapoingia katika eneo nje ya hiyari yake lazima awe na mwanamke , wakati alipokuwa katika ulimwengu wa majini pepo alikuwa na Sophia na sasa wapo katika ulimwengu wa jicho la Anga yupo na Xiao.
“Mh.. ba.. Roma najua unanijali sana na huwezi kunitelekeza hehe…”Xiao kilio chake kilikuwa cha kinafiki tu ili kumuona Roma atamwangalia vipi , ukweli alishajua hakuna namna Roma anaweza kumtelekeza , ilikuwa ni mbinu za kike tu.
Mabadiliko ya mrembo huyo yalimfanya Roma kukosa usemi , tokea siku ambayo amekutana nae mpaka wakati huo tabia yake haikuwa imebadilika.
“Kwasasa sijui vizuri huu ulimwengu ulivyo hivyo inatupasa kuuelewa kidogo kidogo , nifuate kwa adabu na nitahakikisha unatoka ukiwa salama , sina ombi lolote kwako hivyo usiniletee matatizo tu , sawa?”
“Sawa nitakuwa mwema”
Mara baada ya kuona alikuwa na mtu mwenye nguvu kama Roma hakuwaza kuondoka kwa haraka katika ulimwengu huo wala hakuona hofu ya aina yoyote ile.
Alikuwa na furaha ili mradi tu hawawezi kukwama katika ulimwengu huo.
Ukweli ni kwamba asingekuwa na msaada mkubwa kwa Roma kwani hakuwa mwenye kutamani sana kuvuna nishati za mbingu na ardhi , xiao ni wasichana ambao walijifuza kwa ajili ya kudumisha muonekano wao na kuishi maisha marefu.
Roma mara baada ya kuona utulivu wa msichana huyo alijiuliza au alikuwa amemsahau baba yake , maana hakuuliza chochote.
Kutokan na kwamba Roma alikuwa akitafuta kitu chochote cha kumfanya kuelewa ulimwengu huo hivyo alijitahidi kujibu baadhi ya maswali huku wakiwa wanazurura.
Katika safari yao hio aliweza kupata Dhana ya daraja la juu pamoja na andiko ambalo lugha yake licha ya kwamba hakuilewa vizuri lakini aliona linaweza kuwa la muhimu kwake.
Upande wa mrembo Xiao alikuwa akichunguza kila Dhana aliokuwa akiona , baadhi hakuzipenda lakini nyingine zilimfurahisha na alifurahia safari hio kwani kwake alichukulia kama vile ni safari ya kitalii ya kusaka hazina.
Baada ya muda mrefu sana Roma alikuja kugundua anga linazidi kuwa giza , ijapokuwa hakukuwa na mwanga mkali mwanzoni lakini kadri saa zilivyokuwa zikiongezeka ndio giza lilivyokuwa likiongezeka na walijua lazima kuna nyakati za usiku na mchana hata katika ulimwengu huo,
Sasa wakati ambapo giza hilo lilivyokuwa likiongezeka hali ya nguvu za giza na msisimko wa ajabu ulizidi kukithiri na palepale ni kama Roma anapata uelewa kwamba au viumbe wa ulimwengu huo mchana wanalala na giza likiingia ndio wanaamka.
Roma alikuwa sahihi katika makisio yake , kwani mara baada ya giza kuwa kubwa ni kama miguu yao imeshikiliwa na kani ya mvutano na ilikuwa ngumu sana kupiga hatua na kama sio uwezo wao wa nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi ingekuwa ngumu kusonga mbele.
Roma aliamua kuachia nguvu zake za kijini na kuzifanya zimuongoze katika kutambua hatari katika mzingo wa kilomita kumi lakini mara baada ya kitendo hicho palepale sura yake ilijikunja.
Xiao mara baada ya kubadilika kwa muonekano wa Roma alionyesha wasiwasi na kumuuliza Roma nini tatizo.
“Roma kwanini una mabadiliko?”
“Simama mkabala na mimi na hakikisha sio umbali wa hatua tatu , unaelewa”Aliongea Roma kwa namna ya tahadhari.
Wakati msichana huyo akiwa katika hali ya mshangao wa maneno yake aliweza kuona vitu ambavyo vinawasogelea na alijikuta akipatwa na hali ya kupaniki.
“Ni viumbe gani hao , wanaonekana kuwa wengi wanatusogelea”Aliongea Xiao kwa hofu .
Wakati akiongea kauli hio vitu kama moshi mweusi ulianza kujikusanya kutoka katika pande zote na kusogelea katika eneo walipo huku vikitengeneza maumbo ya ajabu.
Mara baada ya kuangalia kwa umakini katika moshi ule ungeweza kuona viumbe vya ajabu sana ambavyo vinasura ya ukali vilivyokuwa vikiwasogelea.
Baadhi ya viumbe hao walikuwa wameshikilia vitu kama mifupa ya kibinadamu na wengine walionekana kuwa na mifupa ambayo haikueleweka wanyama wake .
Kwa msichana kama Xiao ambaye nyoka tu inamtisha katika wakati huo mkojo ulitaka kumtoka.
Chungu cha maafa kilianza kunesa nesa na kuonyesha kustuka na kudhalisha kiwango kikubwa cha nguvu ya giza ambayo ilizingira eneo kubwa katika muundo wa duara.
Chungu hicho kwa namna kilivyokuwa kikicheza cheza ni kama vile kilikuwa katika furaha ya kunasa uwepo wa viumbe wa namna hio.
Ijapokuwa roho ya mnyama huyo alikuwa akiitawala lakini kwa namna fulani bado ufahamu wake alikuwa upo katika akili ya Roma.
Chaos alionekana kutokuweza kumtawala Roma kiakili lakini ilikuwa ni kama vile anasubiria muda nuafaka wa kujiimarisha na kisha kumteka Roma na kutumia mwili wake.
Kabla Roma hajajua hali ilivyo hatimae roho wa giza walimsogelea karibu zaidi na zaidi wakielea kutoka kilomita kadhaa kutoka walipo.
Ghafl tu ilikuwa ni kama vile ni kimbunga cheusi ambacho kilikuwa kinaendesha zile roho kuwasogelea na tofauti na kusinyaa kwa kile kiwingu cheusi kilikuwa kikipanuka na kuwa kama wingu jeusi.
Roma aliweza kugundua kwamba roho hao wa kishetani hawakuwa na nguvu kubwa kutokana na kwamba walikosa miili, haijalishi wakati wakiwa na miili walikuwa na nguvu namna gani lakini kwa wakati huo walikuwa dhaifu mbele ya viumbe wenye miili.
Mwili ndio unafanya mtu kuhifadhi nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi na ndio huo huo unaomfanya jini kuweza kupanda levo za dhiki na mengineyo , ukiwa jini katika roho au pepo moja kwa moja unakosa ile sifa ya kuweza kuhifadhi nguvu za nishati ya mbingu na ardhi hivyo athari zako zinakuwa ni za kiroho zaidi tofuati na kuwa za kimwili.
Roma kwa haraka haraka aliweza kujua roho hizo za kishetani kama ni kupima uwezo wao kwa kufananisha na namna nguvu za anga zinavyopimwa basi ni majini ambao watakuwa katika levo ya maji meupe hivyo ni dhaifu sana kuwa tishio kwa Roma.
Kitu kingine ambacho Roma aligundua ni kwamba hizo roho hazikuwa na akili ya namna yoyote na zilikuwa zikitembea kwa kutuia utashi tu wa kihisia na zilianza kuzingira kwa mbali kama vile zilikuwa makini katika kumsogelea.
Roma aliona pengine sio kwasababu roho hao waovu wanamuogopa , ukweli ni kwamba majini wengi ambao waliingia katika ulimwengu huo wa jicho la Anga mara nyingi wanakuwa katika levo ya maji ya kiroho hivyo ilimaanisha kwamba viumbe au roho walizokutana nazo katika ulimwengu huo waliweza kuzimudu.
“Hizi roho zinaonekana zinaogopa roho ya Chaos”Ijapokuwa Chaos alikuwa amepoteza mwili wake lakini ukali wake na nguvu zake hazikujificha.
Kama ilivyo katika ulimwengu wa wanyama , wale wanyama wadogo wadogo walikuwa wakiogopa wale wanyama wakubwa ndio ilivyokuwa kwa roho hizo.
Lakini licha ya hivyo hawakutaka kupotezea tageti yao , ilionekana walikuwa wakitafuta namna ya kushindana na roho hio ili kumvamia Roma na Xiao.
Roa mara baada ya kuona roho hao wa kishetani wanamwangalia kwa macho ya tamaa aliamua kumalizana nao kwa kuruhusu chungu kuwameza , lakini wale roho mara baada ya kuhisi nguvu ya roho ya mnyama ya mvuto wote walianza kukimbia lakini hata hivyo chungu hicho kilikuwa na uwezo mkubwa hivyo roho hao hawakufanikiwa kukimbia.
Ilikuwa ni kama vile moshi mweusi unatoka angani na kuingia katika chungu kile wale roho wote walimezwa na mng’ako wa chngu hicho uliongezeka kadri ilivyokuwa ikimeza hao roho.
Roma aliweza kuhisi nguvu ya ajabu ikiingia katika mwili wake na kufanya senta za nguvu zake za kijini kusinyaa na kupanuka kwa wakati mmoja.
Roma alionekana kufurahi , kilichomfurahishwa ni kwamba ijapokuwa hizo roho hazikuwa katika miili ya kibinadamu lakini chungu chake kilikuwa na uwezo wa kubadiisha nishati yao ya kiovu na kuwa nishati safi na kumwingia Roma na kumfanya nguvu zake kuongezeka.
Roho wale wa giza walikuwa wengi mno na walijaribu kukimbia katika mvuto wa chungu lakini walishindwa kutoka katika mvutano wa roho ya mnyama.
Xiao ambaye alikuwa akiona tukio zima aliishia kuvuta hewa ya amani na kugundua roho hao wa kishetani hawakuwa na uwezo wa kuwasogelea lakini alishangaa kuona Roma alikuwa na tabasamu la ajabu katika uso wake.
Lakini hata hivyo alijua Roma asingejali maoni yake , kwa akili ya kawaida alijua ni nini ambacho Roma anafanya , alijua kabisa anajilisha na nguvu za hayo mapepo.
Ijapokuwa roho na mapepo katika ulimwengu huo walikuwa wengi lakini haikumaanisha kwamba wote wangemsogelea Roma na kumshambulia hivyo idadi ya waliokuwa wakifyonzwa na chungu ilizidi kupungua.
Roma alikuwa akihisi kabisa uwezo wake unaongezeka , kimahesabu kwasababu alikuwa tayari katika levo ya radi ya mapigo tisini na tisa kwa nguvu hizo aliokuwa akipata ni kama nguvu ya ziada tu.
Sasa mara baada ya kuona hakukuwa na roho na pepo nyingine za kumeza walianza kujiandaa kuelekea eneo lingine ili kutafuta mapepo mengine ili kuyanyonya , kwake ni kama ardhi hio ya ulimwengu wa jicho la anga wa mapepo na roho ilikuwa ni kama nchi ya ahadi ya maziwa na asali.
Ijapokuwa hakujua bado namna ya kutoka lakini sio mbaya kama ataendelea kuongeza nguvu zake.alijiambia pengine anaweza kupanda hata levo akiwa ndani ya ulimwengu huo.
Wakati wakijiandaa kuondoka mara aliweza kuhisi mkandamizo wa nguvu ya ajabu , ilikuwa ni nguvu kubwa kuliko wale mapepo wa mwanzo ikiwasogelea kutokea mbali.
“Wewe ni nani unaethubutu kuua watu wangu?”
Sauti iliokuwa kama ya kishetani iliweza kuzifikia ngoma za masikio yake kutoka mbali , ilikuwa sauti kubwa ilioweza kusambaa karibia eneo lote.
Sauti hio ilimshangaza Roma kwani mapepo hayo ya awamu hayo yalikuwa na maumbo ya ajabu lakini mpangilio wa kibinadamu kama vile ni mizuka.
Roma mara baada ya kuangalia kwa umakini aligundua lazima sauti ile ilitoka kwa kiumbe ambaye alikuwa na mwili mkubwa na alieenda hewani mno kwa mita kama nne hivi.
Alikuwa akitisha pamoja na wenzake na alikuwa amevalia mavazi machakavu kama ya ngozi ya mnyama huku akiwa amejifunga na vito flani kama goroli katia mikono yake.
Alikuwa ameambatana na roho nyingine ambazo zilikuwa na maumbo ya kibinadamu lakini sura mbaya zilizokuwa katika mavazi ya kufanana na ilionekana walikuwa ni walinzi.
Roma macho yake yalisinyaa mara baada ya kugundua Mzuka huo ulikuwa na nguvu kulingana na jini ambaye yupo levo ya radi ya mapigo tisini na tisa na walinzi wawili waliokuwa wakimlinda walikuwa katika levo inayolingana na radi ya mapigo tisa na wengine ni sawa na levo ya maji ya kiroho.
Roma alishangaa na kujiambia pengine ndio maana walionekana kuwa na akili.
Unapaswa kuelewa kwamba kila kiumbe ambacho kinapatikana katika ulimwengu huo wa jicho la anga ni viumbe ambao walikufa na roho zao zikaja kuishi katika huo ulimwengu.
Sasa Roma anashangaa kuona mizuka hio kuwa na nguvu kubwa namna hio mara baada ya kufa.
Roma mara baada ya kukumbuka ulimwengu wa jangwa tenganifu ulikuwa na umri zaidi ya miaka elfu hamsini hivyo na ulimwengu huo utakuwa na miaka mingi na kama kweli roho za majini wanaokufa walikuwa wakikimbilia katika ulimwengu huo basi kutakuwa na roho ambazo zilikufa zikiwa katika levo ya kudhibiti radi na kuweza kupitia levo za dhiki ya radi elfu moja.
Wakati Roma akiwa haongei ule Mzuka mkubwa wa kipepo ulisogelea Chaos Caulrdon na macho yake ya kipepo yalikuwa katika hali ya mshangao kama vile hakutegemea kuona kitu kama hicho.
“Hii ni Chaos Cauldron , wewe ni nani mpaka kumiliki Dhana hii ya kilijendi ya Kale?”Aliongea kwa sauti kubwa na nzito sana.
Sauti hio ilikuwa na mwangi na ilikuwa ni kama vile upo katika shamba kubwa la migomba na ujaribu kuongea kwa sauti, lakini licha ya hivyo sauti yake haikuwa ya kuogofya bali ilionekana kuwa ya heshima mbele ya Chungu cha Chaos.


SEHEMU YA 759.
Roma alishangazwa na ukarimu ule, mwanzoni alikuwa akiwaza kama anaweza kushinda kama ataishambulia hio mizuka lakini ilionekana haikuwa na mapngo wa kumshambulia.
“Nyie ni wakina nani na kwani kumiliki Chaos Cauldron ndio nini?”Aliuliza Roma.
“Mimi ndio ‘Mramu’ wa miliki hii naitwa Uramu Hantu ,nimekuja hapa mara baada ya kugundua kundi kubwa la mapepo limepotea , nadhani utakuwa umewameza na hii Dhana ya Chaos Cauldron”
Uramu maana yake ni cheo cha Lord au Bwana katika lugha ya kihangaria na Hantu ni neno pepo au mzuka katika lugha ya Kimalay.
Sasa Roma mara baada ya kusikia neno Uramu na Hantu alishangazwa na majina hayo lakini kitu ambacho hakuwa akifahamu ni kwamba hilo sio jina lake halisi wakati akiwa hai ila ni jina la kutambulisha jamii yake , majini mara nyingi wanakuwa na majina ambayo yanaendana na tabia zao.
“Kwahio umekuja kulipiza kisasi ?”Aliuiza Roma akiwa hana ishara ya hofu kabisa.
Lakini sasa ghafla tu ule mzuka uliangua kicheko kikubwa na kadri ulivyokuwa ukicheka ndio ulivyokuwa ukitisha zaidi na zaidi kwasababu sura yake ilikuwa ni kama lijiskeleton.
“Umenielewa vibaya , waliokufa ni kundi la wasio na faida kwangu na kuna mapepo wengi sana hapa , kwanini nishindane na wewe kwa ajili yao?”
Roma aliona wasiwasi mara baada ya kumuona pengine Uramu Hantu anamuoopa , sasa alijuliza pengine anachomuogopea sio uwezo wake kwani ni kama vile wanalingana ki uwezo lakini pia alikuwa na kundi la watu wake ambao wana uwezo hivyo ilipaswa wasimuogope.
“Au wanadhani mimi ni moja wapo ya wakuu wa enzi hizo kutokana na kumiliki chungu cha maafa?”Aliwaza Roma.
“Nimefika hapa katika ulimwengu wa jicho la anga kwa ajali mbaya na sitaki kugombana na yeyote hivyo usiwe na wasiwasi”
“Je naweza kujua ni ajali gani imekupata?”Uramu Hantu aliuliza huku akionyesha wasiwasi wake.
“Kulingana na maarifa yangu jicho la Anga linafunguka huko katika ulimwengu wa nje kila baada ya karne moja na huu sio muda bado , hivyo imekuwaje ukaingia huku?”Roma aliona kwasababu anauliza maswali anaweza kumjibu lakini lazima na yeye ajibiwe.
“Nitakupa majibu lakini unapaswa kunijibu mimi kwanza”
Uramu Hantu alishangaa lakini palepale alitoa kicheko kidogo na kuonyesha kukubali.
Mapepo hayo ya kijini pengine yamekwisha kufa muda mrefu lakini yaliendelea kuwa hai kutokana na kuendelea kung’ang’ania uwezo wao..
Uramu Hantu alijibu maswali ya Roma yote kwani hakuwa na sababu ya kumficha.
Ilionekana kwamba ulimwengu huo wa jicho la anga ulikuwepo tokea enzi na enzi na kuhusu alieutengeneza haifahamiki lakini kinachofahamika ni kwamba alieugundua ni jini aliekuwa na nguvu kubwa aliefahamika kwa jina la Demok wa enzi hizo.
Ni nafasi katika anga ambayo inajitegemea kabisa kama ilivyokwa ulimwengu wa jangwa tenganifu.
Anasema kwamba wakati wa vita Demok mara baada ya kugundua uwepo wa hilo eneo aliwatega majini pepo wa kishetani ambao walikuwa ni maadui zao na kuwaingiza katika ulimwengu huo na kufanya maamuzi ya kiharibifu kwa kujilipua yeye mwenyewe na kutokana na kitendo hicho majini pepo jamii ya mashetani wa anga waliishia kufa kwani alikuwa ni kama bomu.
Sasa kitendo cha majini wale kufa roho zao hazikufariki bali miili yao ilikuwa ndio iliharibika , sasa wakati roho hizo zilipokuwa zikijaribu kutoka katika ulimwengu huo kwenda ulimwengu wa nje ilishindikana na kwanzia hapo ndio ikawa makazi yao.
Sasa anasema ambacho kinaonekana katika anga ya majini watu kila baada ya miaka mia moja sio mlango bali ni kama ufa ambao huruhusu majini hao kuingia katika ulimwengu huo.
“Nikueleze ukweli tu kwamba tokea niingie katika huu ulimwengu sijawahi kuona roho yoyote inatoweka , huu ni ulimwengu ambao naweza kusema hauna mipaka na haijalishi unaweza kusafiri kwenda umbali kiasi gani lakini tukio la ajabu ni kwamba utaishia kurudi palepale ulipotokea”
Roma alishangaa sana na ndio maana aliona ni kama vile ni ulimwengu usiokuwa na mwisho.
“Umesema kwamba ufa huo hutokea katika kila miaka mia moja , lakini si kuna majini watu wanaingia wakati huo kwa ajili ya kujitafutia hazina na Dhana , kwanini usitumie nafasi hio kutoka kwani uwezo wako ni mkubwa?”
“Kama niivyosema mwanzo hakuna uwezekano wa kutoka katika huu ulimwengu kwasababu moja, kila mara ufa unapojitegneneza kiwango cha nishati hasi ambayo ndio kama chanzo cha nguvu yetu hupungua kwa kiwango kikubwa sana hivyo hutufanya kuwa dhaifu na tunakuwa kama tupo kwenye usingizi mzito , kabla ya ufa kutokea tunachofanya ni kujificha kwanza katika mashimo ili tusije kushambuoliwa na majini watu wanaokuja , hata kama wasipokuja hata kama twende katika ufa hio kuna nguvu kubwa ya chanya ambayo tukiisogelea hatuwezi kuihimili na tunaishia kupotea”Aliongea.
Nguvu hasi inamaanisha nguvu ya giza au nguvu ya kipepo na nguvu chanya ndio nguvu ya nuru au nguvu ya Kimungu.
Ulimwengu wa kawaida upo katika uwiano wa nguvu hasi na nguvu chanya ndio maana viumbe wanaishi katika mchanganyiko lakini katika ulimwengu huo wa jicho la Anga nguvu hasi ambayo ni ya giza ndio kubwa zaidi.
Sasa Roma ndio anajua kumbe ndio maana majini watu walikuwa wakija katika jicho hilo na kutoka bila shida yoyote , ilionekna nguvu ya mapepo hao ilikuwa ni dhiafu mno katika wakati wa kujitengenza kwa ufa ndio maana walishindwa kutoka.
Walijua hata kama wanaweza kutoka katika ulimwengu huo hawawezi kuishi katika nishati ya jua ambayo ina kiwnago kikubwa cha nishati chanya.
Ukweli ni kwamba kama wasingekuwa katika ulimwengu huo ambao ulikuwa na hali ya hewa tofauti na dunia wangekufa muda mrefu.
Roma zamu yake aliongea kila kitu na alimuonyesha Uramu Hantu ile hazina ya familia ya Sharifu na kumuuliza kama ashawahi kuona mahali.
Lakini mapepo hayo hayakuweza kuigundua kazi ya hio hazina lakini walifurahi mara baada ya kujua ni kitu ambacho kiliachwa na watangulzi wao.
“Hiki kitu kinashangaza hakina nguvu yoyote na sijawahi kuona na hata malighafi iliotumika kutengenezea siijui”Aliongea Uramu.
“Kwasababu umekuwa katika huu ulimwengu kwa muda mrefu lazima utakuwa umekutana na majini pepo , je naweza kupata taarifa yoyote kutoka kwake?” Roma mara baada ya kuuliza Uramu alionyesha ishara za hasira.
“Ingawa sikuwa katika levo ya juu ya mapigo elfu moja wakati nafariki lakini wakati huo sikuwa na kinyongo na koo ya majini pepo…”Aliendelea kuongea na Roma aliweza kujua alikuwa ni jini pepo wa kishetani yaani wale majini ambao huzaliwa wakiwa kama wanyama wa kutisha.
“Je nawezaje kutoka katika huu ulimwengu?”Aliuliza Roma kwa shauku.
“Njjia ya kutoka ni moja tu , inakupasa kusubiri mpaka mwaka unaofuatia wakati wa kutokea kwa ufa , isitoshe wote mna miili na una nguvu kubwa hivyo utaweza kutoka bila shida , kama hutojali unaweza kukaribia nyumbani kwangu na kuchukua hifadhi kwa muda”Aliongea
******
MIEZI MIWILI BAADAE
Katika nyumba iliojengwa kwa mawe iliokuwa katikati ya kisiwa kikubwa ndani ya fungu la visiwa hivyo vva wafu , moto ulikuwa ukiwaka kwa hasira kutokana na kuni kuwa kavu na cheche za moto zilikuwa zikionekana zikiruka ndani ya jiko katika eneo hilo la sebuleni.
Tv ya nch 83 ya teknolojia ya Oled iliokuwa imetundikwa ukutani ilikuwa ikionyesha taarifa ya habari za kimataifa kwa kile kinachoendelea ulimwenguni hususani katika mataifa ambayo yapo upande wa Kaskazini mwa dunia.
Chaneli hio ilikuwa ni kama vile imechagua kuonyesha kile kinachoendelea katika nchi kubwa kubwa kama China na Japani na baadhi ya mataifa mengine katika mabara husika.
Katika runinga hio alionekana mwandishi wa habari ambaye anaripoti kutoka katika aneo la tukio ambaye amevalia koti kubwa lililomfunika kutoka juu hadi chini , lipsi zake zilikuwa za zambarau kutokana na baridi kali na alikuwa ni mwanamke, alikuwa amesimama akinyooshea kidole upande wa bandari kubwa ya kusafirishia mzigo kaskazini mwa China.
Theluji ilikuwa ikidondoka kwa kasi mno kama vile ni mvua na kufunika ardhi yote kiasi cha kuifanya ardhi ni kama imefunikwa na zuria pana jeupe.
“Kama mnavyo ona , maji yote kuja katika bandari hii yameganda , hii bandari haijawahi kuganda katika historia yake yote lakini katika nyuzi joto -37oC maji yamegeuka na kuwa barafu , meli zimekwama kufika katika bandari na wafanyakazi wameshaondoka muda mrefu, kulingana na serikali ya China wameshaanza kuingia makubaliano na nchi kumi na moja zilizopo katika bara la Afrika upande wa kusini kwa ajili ya kuhifadhi raia huku taratibu nyingine za kuokoa binadamu zikiendelea…”
Aliekuwa akiangalia Tv ni Bi Wema na alikuwa amejifunika na Blanket kubwa ambalo alikuwa akijifunika vizuri kila sekunde na alijaribu kubadilisha chaneli na karibia chaneli zote za kisimbuzi lakini zilikuwa zikitangaza habari zinazofanana , yote hayo ni kile kinachoendelea katika dunia.
Watu katika mataifa mengi walikuwa katika hali ya taharuki kwa kile kinachotokea duniani.
Bi Wema mara baada ya kuona hakuna chaneli inayoonyesha tamthilia aliishia kuzima na kumgeukia Sui na Rufi.
“Yaani nimebadilisha chaneli zote habari zinafanana tu , dunia ipo katika taharuki sijui ni kitu gani kinaendelea usiku nakosa hata usingizi”
“Mama si uachane kuangalia habari naona zinakuongezea wasiwasi tu , ni kama kinachoendelea hapa Mediterranian ni swala la muda tu na bahari yetu kuganda”
“Ndio kwanza ni mwezi wa saba kwenda wa nane huu lakini hali ipo hivi , kama ikiendelea watu ambao watapoteza maisha kutokana na baridi watakuwa wengi sana.. Mwenyezi Mungu ukoa watu wako”
Sui ambaye alikuwa kimya muda wote alitaka kuongea neno lakini muonekano wake ulionekana kubadilika.
“Wamerudi”Aliongea
Muda uleule mlango ulifunguliwa na kufanya upepo wa baridi kuingia ndani na kumfanya Bi Wema na Rufi kutetemeka.
Wanawake warembo waliokuwa wamevalia ‘trench Coats’ waliingia , alikuwa ni Edna , Amina na wengine wote na miili yao ilikuwa imefunikwa na kiasi cha theluji..
“Naona huko nje mvua ya theluji imeanza , ona ulivyojaa chembe theluji“Aliongea Bi Wema akijaribu kumpangusa Edna kichwa chake
Kwa kuangalia kwa nje tu ungeweza kuona namna miti ilivyokuwa imenyauka , kila kitu kilikuwa cha kutisha.
“Nje hakuna theluji Bi Wema , tumepitia China ndio kuna theluji ya kutisha”Aliongea Edna.
“Oh! ,,, nikajua ni huko nje , hebu kaeni kwanza mniambie habari za Tanzania’Aliongea Bi Wema kwa shauku.
Siku chache zilizopita warembo hao walisafiri kwenda Tanzania kuona hali ilivyo na baada ya hapo wakaelekea katika maeneo ya China na Japani kujaribu kumtafuta Roma.
Upande wa Edna , Neema Luwazo na Amina walikuwa na makampuni mengi tu ambayo yana wafanyakazi wengi ,yaan Vexto, Kanani Group na Maple zote
Kutokana na kwamba wao ndio viongozi wa juu wa makampuni hayo hawakuwa na sababu ya kujitokeza mara kwa mara kazini hivyo walienda kwa ajili ya kazi ambazo ziliihitaji uwepo wao.
Ukweli ni kwamba wote walirudi kutokana na biashara yao ya Real Estate na hio ni kutokana na kwamba matajiri wengi walikuwa wakitoka mataifa ya Kaskazini mwa dunia na kuja katika nchi za Ikweta ambazo baridi yake ilikuwa chiin.
Serikali ya Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimekubali kupokea baadhi ya raia kutoka katika mataifa makubwa ikiwemo China , Japani na Marekani na hawa raia ambao wanakuja walihitaji sehemu za kuishi na makampuni makubwa ambayo yanamiliki mahoteli na Apartment ilikuwa ndio biashara sasa kwa wakati huo ambayo ilikuwa na thamani kubwa.
Sasa Edna , Neema na Amina ni moja ya wamiliki wa kampuni hizo ambazo zinamiliki biashara za kukarimu watu , wakati Neema yeye akiwa na mahoteli karibia nchi nzima na Afrika mashariki na kati yote upande wa Edna yeye alikuwa na Apartment za kutosha katika kila nchi na baadhi ya hoteli na projekti za ujenzi wa hoteli nyingi katika nchi ya Afrika mashariki yote na kati yote ulikuwa ukiendelea.
Hivyo ilikuwa ni swala la kuchangamkia fursa , Amina yeye kampuni yake pia ilikuwa ikijihusisha na mahoteli pamoja na vyakula hivyo pia ni kama amepitiwa na upepo wa fursa.
Sasa mara baada ya kusaini mikataba mingi ya ujenzi moja kwa moja wote walienda Hongkong kwa ajili ya kusaini mikataba na makampuni ambayo inasafirisha raia kuja nchi za hali ya joto na baada ya hapo walielekea Beijing China kwa ajili ya misheni maalumu.
Ijapokuwa joto lilikuwa likishuka kwa kasi katika mwambao wa kaskazini lakini nchi ambazo zilikuwa katika mwambao wa kusini na ikweta na baadhi ya nchi za Afrika nyingi zilikuwa bado hazijapitia hali ya baridi kali na mazingira yake bado yalikuwa mazuri kwa kusapoti maisha ya viumbe hai.
Yaani kwa siku kadhaa baadhi ya nchi nyingi zilizokuwa katika bara la Afrika na baadhi ya nchi za Amerika ya kusini zimegeuka kuwa nchi ambazo nyumba na ardhi zimekuwa za thamani kuliko hata dhahabu.
Changamoto kubwa ambayo inaikumba dunia ni swala la usafirishaji , baadhi ya bahari nyingi zilikuwa zimeganda na reli nazo hazikuruhusu treni kupita hivyo usafirishaji wa chakula kuwa mgumu mno na hii inasababisha serikali nyingi kufanya juhudi kubwa kuzia uhalifu.
Ijapokuwa maeneo ambayo bado yapo salama ni mengi lakini maeneo hayo kilimo chake kilikuwa hakitoshelezi watu wote , kwa mfano nchi kama Tanzania haijitoshelezi katika kilimo chake , sasa kwa wingi wa watu ambao wanaingia nchini inafanya nchi kukosa chakula.
“Nasikia nusu ya nchi za China , Urusi na Japani zimeganda na matajiri wengi wanakimbilia nchi ambazo zipo katika mstari wa ikweta na baadhi ya maeneo ya kusini na hali ikiendelea hivi na maeneo ya kusini pia joto lake linaweza kufikia nyuzi sifuri “Aliongea Rose
“Sasa nini kitatokea jamani, kama hali hii itaendelea watu wengi watakufa”Aliuliza Bi Wema.
“Wasiwasi wangu ni kwamba kama watu hawatokufa kwa baridi bali watakufa kwa njaaa au kupigana wao kwa wao mpaka kufa , katika maeneo mengi maduka ambayo yalikuwa chini ya uendeshaji binafsi yanaendeshwa na wanajeshi wa kiserikali ili kuzuia uhalifu lakini bado haitoshi , kiwango cha uhalifu kimeongezeka sana ,imekuwa bahati kwa nchi nyingi za Afrika hali sio mbaya lakini bara la Asia na Ulaya ndio kwenye hali mbaya zaidi lakini hili linaweza kuwa swala la muda tu”Aliongea Magdalena
Hali ilikuwa mbaya wale wa imani kali wanatangaza ni wakati wa kiama huku baadhi ya watumishi kutoka Afrika wanasema abara ya Asia , Ulaya na Amerika ya Kaskazini yanaadhibiwa kutokana na kufanya dhambi sana ikiwemo kuruhusu ndoa za jinsia moja.
Ki ufupi kila mtu alikuwa akiongea lake na wale ambao hawakuwa wakiamini uwepo wa Mungu walikuwa wakikimbilia makanisani na msikitini.
“Vipi wakwe zako , Blandina na Mzee Kweka?hujaenda kuwasalimia?”Bi Wema alimuuliza Edna.
“Nimeenda na wapo salama mama na babu wote wapo Dar Mzee anasema baridi Iringa imezidi, sijawaeleza chochote kuhusu Roma”Aliongea Edna kinyonge.
“Tukiachana na hayo vipi kuhusu Mr hakuna taarifa yoyote ambayo mmeweza kuipata?”Aliuliza Bi Wema.
Ijapokuwa walienda China kibiashra lakini pia walienda kwa misheni ya kuweza kujua Roma yupo wapi , ukweli ni kwamba kitu ambacho Roma hakuwa akijua ni kwamba muda ulivyokuwaukihesabika katika ulimwengu ule aliopo ulikuwa ni tofauti katika ulimwengu wa kawaida.
“Tumefanikiwa kwenda China na kuonana na mkuu wa jeshi la kitengo cha Iron Flame Brigade kwa msaada wa serikali ya Tanzania na tumeweza kuonana na Jenerali Cai Yuncheng ambaye alituunganisha na mjumbe wa Hongmeng , na taarifa zinasema kwamba Anjiu ndio ambaye alipambana na Roma mara ya mwisho na taarifa za chini ni kwamba hakukuwa na uwezekano wa Hubby kushindwa na jini Anjiu lakini Anjiu yupo hai na yeye kapotea”Aliongea Mage
‘Hongmeng na wenyewe wanasema wapo na wasiwasi na wanatafuta msaada wa Roma kwani Anjiu ashaanza kushambulia miliki zote na kutaka ziwe chini yake na kutokana na Hongmeng kupoteza watu wao wengi hofu yao ni kwamba akimaliza miliki nyingine anaweza akaja kwao pia”Aliongea Magdalena.
“Ni shetani yule lazima kuna mbinu ametumia kumuumiza mpenzi wetu , lakini uhakika wangu ni kwamba Roma atarudi”Aliongea Rufi
Na warembo hao wote walilazimisha tabasamu , ijapokuwa walikuwa wakitamani kuona Roma anarudi akiwa salama lakini hawakuwa na uelewa alikuwa kaenda wapi , mtu pekee ambae anaweza kuwaambia mahali alipo Roma ni jini Anjiu lakini wasingeweza kwenda ulimwengu wa majini na kumuuliza.
“Kwasasa haina haja ya kuwa na wasiwasi , kitu pekee tunachoweza kufanya ni kumuanini na kumsubiri arudi.. Bi Wema simuoni bini yangu Lanlan kakimbilia wapi?”Aliongea Edna mara baada ya kuwatuliza na ndio wakati ambao alimkumbuka binti yake.
“Wale dada zetu wameenda kutembelea baadhi ya nchi kadhaa za karibu na kama unavyojua Lanlan ametokea kuwapenda sana hivyo walimchukua na kuondoka nae , wameniambia nisikuambie maana ungekataa , niliamni atakuwa salama akiwa nao hivyo nimekubali waondoke nae tu”Alijibu Bi Wema lakini sura ya Edna ilijikunja.
Usikose ni ya moto sana ijayo.
ITAENDELEA KESHO AU JUMAMOSI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom