Serikali kubadilisha Uongozi wa Hospitali ya Kitete Tabora kutokana na kutoa huduma duni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,853
12,089
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Molel ameonesha kutoridhishwa na utendaji kazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kitete - Tabora hivyo amesema watafanya mabadiliko makubwa ya Menejimenti kuanzia kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali na timu nzima inayosimamia Hospitali hiyo.

Amesema haiwezekani Rais Samia Suluhu Hassan atoe fedha na vifaa halafu Mtanzania akose Huduma bora kwa sababu ya menejimenti kushindwa kuisimamia Hospitali hiyo.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kushutukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete- Tabora , Dkt. Mollel amesema wameona mambo mengi ikiwemo suala la usimamizi mbovu wa mazingira kwani fedha zipo na vifaa vipo.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzia Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta fedha nyingi vifaa vipo, fedha zipo shida ni usimamizi wa mazingira kwamba mazingira hayasimamiwi, menejimenti imeshindwa kuisimamia Hospitali kwa maana usafi wa ndani na ubora wa Huduma kwa wananchi wanaofika katika hospitali hii," ameeleza Dkt.Mollel.

Pia soma:
- Hospitali ya Kitete (Tabora) haijatulipa posho zetu za Oktoba Madaktari Wanafunzi
 
Mwaka juzi Ultrasound iliibwa, na hakuna aliyekamatwa hata kwa tuhuma tu.
 
Back
Top Bottom