Riport ya CAG na kikokotoo

Nsubhi

Senior Member
Jan 27, 2015
159
51
Kwenye report ya CAG imeonekana kuna mabilioni yamepotea kila secta lakini pia kuna mabilioni kwenye mifuko ya jamii wamekopeshana wafanyakazi wa mifuko ya jamii na mabilioni mengine serikali imekopa na haitaki kulipa.

Hivyo danadana zote hizi wanajua tatizo liko wapi hivyo wanaangalia mdhaifu (mfanyakazi) wao ili alipe deni lako kwa shuruti. Kwani katika hili hamna mfanyakazi mwenye akili nzuri anaweza kuli-support kwani halina faida kwa mfanyakazi ila machungu na kuongeza chuki dhidi ya serkali.

Kumekua na wabunge wa hovyo na hawajitambui kwasababu wanadai eti kikokotoo hiki kipya kinafaida kwa wastaafu na kama kina faida wao pia wabunge wanaenda kustaafu, swali hizo 250M wanazopewa zikatwe nao wapewe 33% yani 82.5M watakubali au hizi sheria wanatunga kwa ajili kuwa-fever yao siyo watanzania wote?

Ifike sehemu watanzania tuseme no. Laa hawa jamaa wanatengeneza tatizo ili mkuu wa majizi aje kusema hadharani tumetatua changamoto ya kikokotoo na vile wasivyo na uelewa walio wengi watampigia makofi na kusema kuupiga mwingi.

Hizi siasa zinazolenga kubinya masilahi yetu tena harari tuzikatae kabisa kwani zimelenga kutunyanyasa kisaikolojia na kiuchumi.
 
Kwa utafiti wangu tu mdogo na usio rasmi; nimegundua hakuna mstaafu anayekifurahia hiki kikokotoo kipya. Kila unayemuuliza, analalamika tu na kuilaani serikali kwa uonevu.

Kwa hiyo ni wazi serikali inawafanyia uhuni wastaafu kwa kuwadhulumu/kuwapangia matumizi ya fedha zao, kinyume kabisa cha utaratibu.
 
Back
Top Bottom