Rais Samia amteua Dkt. Ndungulile kugombea nafasi ya Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
44,685
51,550
Shirika la Afya Duniani WHO limeipendekeza Tanzania sanjali na Nchi zingine kuwa miongoni mwa Nchi ambazo zimepewa nafasi ya kuweka mgombea ambae anaweza kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika.

Rais Samia amependekeza kina la Dr. Faustine Ndungulile Kugombea Nafasi hiyo ambapo atachuana na wagombea wengine kutoka Mataifa ya Rwanda, Senegal,Ivory Coast na Niger.

Tayari Tanzania Ina kura 23 kutoka SADC na EAC huku kampeni zikiendekea.

Ikumbukwe hiki kitakuwa ni kipimo.kingine Cha Nguvu ya Ushawishi ya Rais Samia na Diplomasia ya Tanzania kwenye UGA wa Kimataifa.

Rais Samia amefanikisha Afcon, Rais wa IPU ,na Sasa ana kibarua Cha Kumfanya Dr.Ndungulile anapeperusha vyema bendera ya Tanzania.

====

My Take
Tanzania inatarajia kushinda nafasi hiyo kutokana na rekodi Bora zaidi kwenye swala la Afya ikiwemo Kupunguza vifo vya kina mama wajawazito Kwa 80%.
 
Kwa ushawishi na kukubalika kwa Rais wetu Daktari Samia Suluhu Hasssan naamini Tanzania tunakwenda kushinda kwa kishindo.

Halafu kwanini mada hii umeiweka kwenye jukwaa la historia.
 
Back
Top Bottom