Profesa Ndakidemi kuipa Milioni 5 familia iliyopoteza watu wanne kwenye mafuriko Moshi

Jun 20, 2023
71
83
Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini (ccm),Profesa Patrick Ndakidemi ameahidi kutoa shilingi Milioni tano familia iliyopoteza watu wanne ambao walifari Dunia baada ya nyumba yao kuangukiwa na kifusi baada ya mvua kubwa Iliyonyesha usiku wa April 25 Mwaka huu .

Mvua hiyo ambayo ilileta uharibifu mkubwa Katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Kilimanjaro ilisababisha mafuriko ambayo yaliharibu Mali za watu zikiwamo nyumba ,mifugo,vyakula.

Profesa Ndakidemi alitoa ahadi hiyo wakati wa mazishi ya watu hao Katika kata ya Kimochi jimboni humo.

Alisema kiasi hicho cha fedha kitatumika kuwarejeshea makazi yao baada ya nyumba Yao kuanguka na kukosa makazi.

Katika mazishi hayo,Profesa Ndakidemi alitoa ubani wa shilingi laki tano kwa familia hiyo huku akitoa tani mbili za mahidi kwa wananchi wa Kata za Mabogini na Arusha chini ambazo ziliathiriwa na mafuriko hayo.
Zaidi ya watu 4,000 wameripotiwa kuathiriwa na mafuriko hayo yaliyosabishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Mbali na hao zaidi ya Kaya 906 zimeathiriwa na mafuriko hayo huku watu sita wakiripotiwa kufariki dunia kutokana na mvua hizo.

Hiyo ni kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Zephania Sumaye April 29,2024 Mjini Mosh wakati akipokea Misaada ya kijamii kutoka kwa msamalia mmoja kwa ajili ya wahanga wa mafuriko hayo waliopatiwa hifadhi kwenye shule ya Sekondari ya kutwa ya Lucy Lameck.

Akipokea misaada hiyo Sumaye alisema wahanga hao wa mafuriko wana uhaba mkubwa wa chakula ,huku wengi wakiwa hawana malazi huku akimpongeza msamalia huyo kwa moyo wake wa kujitolea kwa kuwasaidia wahanga hao wa mafuriko ikiwemo Magodoro, Unga , Mafuta, Mchele, Sabuni, Taulo za kike , Kalamu, Madaftari pamoja na Mikungu ya ndizi.

Mafuriko hayo yalisababisha mto Rau kujaa huku kingo za Daraja la Otieno lililopo Kata ya Msaranga kusombwa na Maji na kusababisha baadhi ya nyumba kusombwq na Maji huku maji mengi yakiingiq ndani ya makazi ya watu na kusababisha uharibifu wa vitu vingi vya ndani vikiwamo vyakula.
 
Back
Top Bottom