Nimekuwa mlemavu wa hisia za mapenzi

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,969
6,915
Kusema ule ukweli kabisa toka nimpe moyo dada mmoja akauvunja basi nahisi kabisa kuwa nimepata ulemavu wa kupenda tena.

Ni miaka mitatu sasa nimekosa hisia za kupenda na wala sioni dalili za kurudi kwa hisia hizo, Nimebaki na hisia za kutamani pekee… I feel fine niki-hit and run, Na hit yenyewe iwe nikiwa nimevaa mask ili mwanamke husika asinione akariri sura yangu

Baada ya broke up ile Nimefanikiwa ku-recover kwenye kila sector ya uchumi wangu binafsi, Afya na muonekano, Vitu ambavyo vinazidi kuchochea mvuto kwa warembo wengi ambao baadhi wamekuwa wakinijia waziwazi kutaka niwe nao ila kiukweli kabisa nimekuwa naishia kuwakataa waziwazi kwa kuwa hata kwa kuigiza nilishindwa kwa wale niliojaribu kuwapenda after kwanza… Sipendi kugandwa gandwa na kusongwa na mwanamke, Sipendi kuongea na simu kwa muda mrefu na mwanamke na pindi nikiona dalili hizo hutafuta jinsi ya kumkataa mwanamke huyo hadi hufika muda mwanamke huyo kunichoka na kuamua kutulia.

Kwa sasa nikigundua mwanamke fulani ameanza kuvutiwa na mimi naanza kumuepuka ili asipate attention yangu, Na ikitokea ametafuta njia hadi kunifikishia ujumbe wa yalio moyoni mwake basi huwa simfichi kumjuza kuwa sipo tayari ku-settle… kwa hili nina experience ya kuwa asilimia kubwa niliojaribu kuwakataa kwa njia hiyo walinitaka japo niwaguse tu ila katika hilo niligoma pia kwa kuhofia kuumiza hisia zao na lawama za baada ya tendo na kuwaacha so katika 10 basi wawili wa mwanzo ndo walifanikiwa kunishawishi nikawagusa before kila mtu ale hamsini zake.

Nimekuwa mtu ambae sipendi mahusiano kabisa na imefika muda nahisi mahusiano ya mapenzi ni utapeli fulani wa kurubuniana kihisia/unafiki. Naona wanawake wengi wazuri sehemu mbalimbali ila kusema ukweli hisia zangu hazijaona ambae anaweza ku-afford moyo wangu

Nimekuwa mtu ambae furaha yangu ni kujiboresha zaidi kwenye status na appearance yangu binafsi

Napenda the way ninavyoteka hisia za mabinti na kuwa mgumu kwao kunipata, Napenda kuwa attractive kama nilivyo and better than that alafu nisiwe affordable, Napenda kuumiza hisia zao kwa njia hiyo.

Hobby yangu ni mazoezi ya Gym/ Weight lifting na hasira niliyonayo kwa wanawake huzimalizia humo.

Sichukii wanawake ila sipendi wanavyojiona kwamba wanaweza kumpata mwanaume yoyote wamtakae wakati hawajanijaribu mimi

Lack of love emotion feels like peace of mind to me.

~YOFAV
 
Nikupe pole, wenzio tunakula wakileta na unakausha vilevile, akilalamika unamuuliza lini tumefunga ndoa mpaka niwe nakutaarifu mambo yangu, full stop.
 
Matter of different lifestyle, Good for you if you feel safe of that
Nikupe pole, wenzio tunakula wakileta na unakausha vilevile, akilalamika unamuuliza lini tumefunga ndoa mpaka niwe nakutaarifu mambo yangu, full stop.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom