SoC03 Namna Teknolojia inavyoweza kuzuia Rushwa na kuongeza weledi kwa Jeshi la Polisi na Uhamiaji

Stories of Change - 2023 Competition

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
1,049
1,581
UTANGULIZI.
Jeshi la polisi na uhamiaji ni miongoni mwa vyombo vya dola ambavyo takwimu zinaonesha ndio vinavyoongoza kwa kukiuka maadili ya kazi kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani na askari wa doria ndio vinavyoongoza kwa vitendo vya rushwa, wakifuatiwa na askari wakawaida katika vituo vya polisi, jeshi la uhamiaji katika nyanja zote imeripotiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa kiwango kikubwa pia, kitu kinachopelekea ufanisi wa kazi na weledi wa kazi katika vyombo hivi kudhorota.

Kwa sasa rushwa ipo katika kila nyanja, kila taasisi kuanzia watu wa chini kabisa hadi wa juu kabisa, na katika tafiti zangu kadhaa nilizoweza kufanya kuhusu namna bora ya kuzuia na kupambana na rushwa, nimegundua kwamba hakuna njia moja mathubuti ya kukabiliana na rushwa bali, rushwa inaweza kudhibitiwa kwa mbinu tofauti kulingana na maeneo husika.

Si amini sana katika matumizi ya maafisa wa kuzuia na kupambana na rushwa kama nyenzo kuu ya kukabiliana na vitendo vya rushwa moja kwa moja nchini, maana wao nao ni binadamu na wanashawishika hivyo ni rahisi kwa mtu kupamba na rushwa na kula rushwa, na hili lipo wazi kabisa.

Imani yangu ipo katika teknolojia kwamba inaweza kudhibiti rushwa kulingana na maeneo. Hapa nitaelezea namna teknolojia itaweza kuzuia rushwa kwa askari wa usalama barabarani, askari wa doria sehemu mbalimbali kama mitaani, bandarini, majini, na viwanja vya ndege, pamoja na askari wa uhamiaji.

NAMNA TEKNOLOJIA IUNDWE NA IFANYE KAZI.
Kuwe na mfumo wa kiteknolojia ambao utakuwa na uwezo wa kurekodi matukio yote kwa kila askari awapo mazingira yake ya kazi kama vile barabarani, teknolojia hii itahusisha mfumo wa kompyuta, mtandao, na kifaa maalumu ambacho askari atakivaa kama kitambulisho "beji" katika sare yake ya kazi ama mavazi yake.

Kifaa hicho kiundwe kwa sensa za kamera ndogo ambazo zitakuwa na uwezo wa kurekodi matukio yote muhimu katika mfumo wa video zilizoambatana na sauti na picha pia, kiwe kidogo kama beji, ambacho kitasapoti mtandao kwa kutumia mfumo wa simu kadi ya kidijitali. Kifaa hiki kitachajiwa na kitakuwa na uwezo wa kuhifadhi nguvu ya umeme kwa muda wa saa 168, na pia kitakuwa na uwezo wa kugundua maeneo ambayo askari atakuwepo. Kifaa hiki pia kitakuwa na uwezo wa kupiga picha za papo kwa papo pale inapotokea kuna muingiliano wa mgusano baina ya mtu na mtu ili kuweza kubaini kwa urahisi sababu za mgusano huo kwa wakati huo.

Kila kifaa kitasajiliwa kwa mfumo wa kompyuta kwa jina la askari husika, na askari huyo ndiye atakuwa na jukumu la kukitunza kifaa hicho. Kifaa hiki hakitahitaji kuwashwa au kuzimwa na mtu isipokuwa kitajiwasha chenyewe pale tu askari anapo kipachika katika vazi lake tayari kwa kazi, na kitazima pale tu atakapokiondoa. Kitakuwa na swichi maalumu ambayo ni sensa maalumu.

Kwa kuwa askari wote wanafanya kazi kwa kuzingatia muda, basi ikitokea kikazima mfumo hautokuwa na mawasiliano na kifaa hicho, ila utaonesha vifaa vyote ambavyo havipo mtandaoni. Ikitokea kilizima muda wa kazi, basi askari anayekitumia kifaa hicho atawajibika kutoa sababu, maana hakitaweza kuwaka kama hakijavaliwa, na hakitaweza kuzima kama hakikuondolewa kwa nguvu.

Mfumo wa kompyuta utaonesha ubora wa utendaji kazi wa kifaa husika, ikiwemo kiwango cha nguvu ya umeme iliyopo. Pia utakuwa ukihifadhi matukio yote muhimu yanayorekodiwa na kila kifaa. Pia, kupitia mfumo huo, muongoza mfumo atakuwa na uwezo wa kufuatilia mwenendo kazi kwa kila kifaa, ikiwemo mazungumzo ya moja kwa moja.

Mfumo huu utakuwa chini ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na watashirikiana na Jeshi la Polisi katika kusimamia utekelezaji wake.

Iwe ni kosa kisheria kwa askari kutekeleza majukumu yake ya kazi pasipo kuwa na kifaa hicho, bila kujali wadhifa wake, na ikitokea hivyo, basi askari husika awajibike kisheria.

Mfumo itafungwa katika kila makao makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kikanda. Maofisa wa TAKUKURU watafanya kazi ya kupitia video kwa kila askari baada ya kuhitimisha muda wake wa kazi na kufanyia uchunguzi video na picha ambazo zimerekodiwa ili kugundua kama kuna viasharia vya kuomba rushwa ama kutoa rushwa kwa hatua zaidi.

Video na picha zilizorekodiwa hazitaweza kufutwa na mtu yeyote kwa ajili ya matumizi ya kisheria, na utengenezaji wa ripoti pale itakapohitajika.

FAIDA ZA KUTUMIA TEKNOLOJIA HII ILI KUONGEZA WELEDI NA UWAJIBIKAJI.
  • Inawafanya askari waogope kuomba rushwa ama kupokea rushwa.
  • Inasaidia kuongeza weledi kwa askari maana itakuwa ni vigumu kwake kujihusisha na vitendo ambavyo ni kinyume na maadili ya kazi yake.
  • Inachochea utendaji haki kwa watu wa kawaida
  • Itasaidia kupunguza majanga ambayo chanzo chake ni askari wapokea rushwa.
  • Itapunguza kuwa na wahamiaji haramu.
  • Itasaidia askari kutojihusisha na matendo ya kihalifu.
 
Back
Top Bottom